Ufafanuzi: Je, kuna Majimbo yatashindwa kujiendesha kwenye mfumo wa Majimbo?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
SWALI NI: JE, MFUMO WA MAJIMBO UTALETA UKABILA NA KUFANYA BAADHI YA SEHEMU TANZANIA KUTOKUWA NA MAENDELEO?

Amani iwe nanyi wadau!

Leo napenda kuwajibu wana CCM wanaosema mfumo wa Majimbo utachochea ukabila na kusababisha baadhi ya maeneo kutokuwa na maendeleo,

Ukweli ni kuwa kamwe mfumo wa majimbo hautaleta ukabila na kamwe hautoleta kudumaa kwa maendeleo kwenye baadhi ya sehemu kama propaganda za CCM zinavyosema! Hii ni kwa sababu zifuatazo;

1. Jimbo la Kati- Mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora na Morogoro.
Mikoa hii ina utajiri mkubwa wa mazao kama Tumbaku, Zabibu, Alizeti, Karanga, Asali na Mtama, Mpunga,Ndizi na Mahindi(vya mkoa wa Morogoro) Haya mazao tukipata viongozi wenye akili sio hawa wa CCM yataendelezwa vizuri na kuingiza mapato makubwa kwenye jimbo hili la kati.

Kuna uhitaji mkubwa sana wa Karanga na Asali kwenye masoko ya Asia na Ulaya. Haya mazao yakiendelezwa kisasa na kibiashara jimbo hili litanyanyuka mno kiuchumi. Hata viwanda vya mvinyo tu Dodoma vikiendelezwa na kutangazwa vizuri na mvinyo ukitengenezwa mzuri mapato

Pia kwenye jimbo hili kuna maliasili mbalimbali za wanyama kutokana na mapori ya akiba kama swagaswaga, manyoni na mapori ya Tabora ambayo pia yana tembo wengi na mbao nyingi. Hivi vitu vikiendelezwa na kutangazwa vizuri vitakuwa source kubwa ya mapato kutokana na uwindaji na utalii. Haya pia ni mapato makubwa sana.

Mkoa wa Morogoro una mbuga za wanyama kama mikumi, udzungwa na nyingine nyingi ambazo pia zitaleta mapato ya utalii.

Pia Kuna madini Kama dhahabu mikoa ya Tabora na Singida na Morogoro ambayo yakiendelezwa vizuri yataketa mapato makubwa sana kwenye maeneo haya. Hapo sijaweka biashara za mifugo, wanyama na viwanda ambavyo navyo vipo na vitakuwepo kwenye jimbo hili.

Kwa hiyo dhana ya Jimbo la Kati kuwa masikini si kweli.

2. Jimbo la Mashariki- Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani
Jimbo hili chanzo kikuu cha Maputo kitakuwa Bandari, Viwanda na Biashara. Kodi nyingi itakusannywa kutoka maeneo haya na kwa kweli itaendeleza kweli jimbo hili.

3. Jimbo la Kusini- Mikoa ya LINDI, Mtwara na Ruvuma
Jimbo hili lina utajiri mkubwa wa gesi na mazao ya korosho na mbaazi bila kusahau viwanda, bandari na uvuvi. - Hili jimbo litakuwa na na mapato makubwa sana ambayo yatajenga shule bora, hospitali, madawa, kujenga barabara nzuri na makazi bora.

Pia jimbo hili litakuwa na mapato ya utalii kutokana na hifadhi ya Selous na mapori ya akiba ya mkoa wa Ruvuma.

4. Jimbo la Nyanda za Juu kusini- Mikoa ya Iringa, Njombe,Songwe na Mbeya
Jimbo hili ndo mzalishaji mkuu wa chakula kinacholisha Tanzania, Afrika ya kati na Afrika mashariki. Kilimo na Biashara ya Chakula kitaingiza mapato makubwa sana kwenye jimbo hili. Biashara pia ya mbao na utalii kutokana na hifadhi za kipengele, Ruaha, Kitulo na Rungwe vitaingiza mapato makubwa sana kwenye jimbo hili.

Mipaka ya Zambia na Malawi pia itaingiza mapato makubwa kutokana na biashara bila kusahau viwanda na kilimo cha mashamba makubwa ya mpunga, maparachichi, nyanya, chai na miti.

5. Jimbo la Magharibi- Mikoa ya Katavi, Rukwa, Kigoma na Kagera- Mikoa hii ina utajili wa kilimo hasa cha mazao ya mahindi, tumbaku, mawese, miwa pamoja na miti pia. Pia ina uvuvi wa maziwa ya Tanganyika na Victoria.

Mikoa hii pia ina utalii wa mbuga za wanyama kama hifadhi za Gombe, Kimisi, Katavi, Mto Maragarasi pamoja na biashara kubwa na kodi katika mipaka ya nchi za Congo( Bandari) , Burundi, Rwanda na Uganda! Itoshe tu kusema kuwa jimbo hili pia litakuwa na mapato mengi sana ambayo yataboresha miondombinu ya barabara, hospitali , mashule na huduma za Maji safi na salama!!

6. Jimbo la Kaskazini- Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Mara.
Jimbo hili litakuwa na na chanjo kikuu cha mapato ambacho ni utalii na pia madini ya mikoa ya Arusha, Manyara na Mara. Utalii wa mbuga za kilimanjaro, Ngorongoro, Serengeti na Manyara utaingiza pesa nyingi sana za kuboresha miondombinu na huduma za msingi

Biashara pia na kodi kwenye mipaka ya Kenya kwa sehemu za holili,Silali na Arusha italeta mapato mengi Sana. Na hapa hujaweka kilimo cha ndizi, tangawizi na mifugo bila kusahau viwanda.

7. Jimbo la Kanda ya Ziwa (Victoria)- Mikoa ya Simiyu, Geita, Shinyanga na Mwanza.
Jimbo hili ndo kitovu cha madini Tanzania. Pia lina mbuga na mapori ya akiba mengi bila kusahau viwanda na biashara ambavyo vitaingiza napata mengi sana na kuleta impact kubwa sana kwenye uchumi. Uvuvi pia utaleta mapato mengi sana.

Dhana ya ukabila haiwezi kupata nguvu kwenye mfumo huu kwa sababu Kuna mchanganyo mkubwa wa makabila kwenye majimbo haya!

Pia chini ya mfumo huu kila mwananchi atawajibika kufanya kazi halali na kujituma kwa sababu atajua bila kufanya kazi hawezi endelea na sehemu yake haiwezi kufanya vizuri katika huduma za msingi.

Chini ya mfumo huu pia hakutakuwa na unyanyasaji wa wananchi kwa sababu wananchi watakuwa wanajua kuwa Mapato yao ndio yatakayowaletea maendeleo!

Viongozi pia watawajibika moja kwa moja kwa wananchi na kamwe hawatofuja mali kwa wananchi wala kuwagawa kwa misingi ya kikabila au kichama kwenye maendeleo.
 
Mkuu katika uchambuzi wako kuna mikoa umeiacha haina jimbo lolote. Au yenyewe tutaigawa kwa ndugu zao upande wa pili wa ziwa??😅😅😅😂( joke)

Ongezea nyama
 
Mkuu katika uchambuzi wako kuna mikoa umeiacha haina jimbo lolote. Au yenyewe tutaigawa kwa ndugu zao upande wa pili wa ziwa??😅😅😅😂( joke)

Ongezea nyama
Nimeacha mikoa gani ndugu?😂😂😂
 
NaAWAKUMBUSHA TU WAKUU.

Tanzania ni moja kati ya The Poorest Countries in the World (NCHI MASIKINI ZAIDI DUNIANI) inashika nafasi ya 8 kutoka chini. ( Focus economy 2019- 23)
MIAKA 60 YA UHURU.

CCM imetufikisha hapa
 
Toa sababu ya kupingana na hii Sera Ndugu. Tuelezane kwa hoja?

Usije ukawa tu na hofu ya kutokuwepo kwa vyeo vya uRc, Udc, Ras na Das hivyo unaogopa kukosa cheo
Nchi zenye sera hii zimejikuta zikikuza ile tabia ya watu kujitambulisha kwa majimbo yao na hivyo utaifa unakuwa shakani.

Ni rahisi sana watu kupata sababu za kuchukiana kuliko zile za kutaka kuwa kitu kimoja.

Mnapokubaliana kwamba udhaifu wa kila mmoja wenu unamezwa na umoja wenu maana yale ni rahisi hata huo udhaifu kupatiwa suluhisho ndani ya kuamini kwenu kwamba mpo salama mnapokuwa ni wamoja.
 
Nchi zenye sera hii zimejikuta zikikuza ile tabia ya watu kujitambulisha kwa majimbo yao na hivyo utaifa unakuwa shakani.

Ni rahisi sana watu kupata sababu za kuchukiana kuliko zile za kutaka kuwa kitu kimoja.

Mnapokubaliana kwamba udhaifu wa kila mmoja wenu unamezwa na umoja wenu maana yale ni rahisi hata huo udhaifu kupatiwa suluhisho ndani ya kuamini kwenu kwamba mpo salama mnapokuwa na wamoja.
Tuanzie China na Marekani na hata Ujerumani nani anajitambulisha kwa jimbo lake??

Kwa miaka karibu 60 sasahivi mbona huo mfumo wenu haujaleta matokeo yeyote chanya???
Juzi tu Mama Ndalichako kasema kwa Magufuli sehemu yake watu wanakunywa Maji ya matope. Nyie hela yote ya kigoma inajenga Dar alafu kigoma wanakunywa Maji ya matope mnaona ni sawa???
 
Tupe mfano wa nchi ambako kuna majimbo yaliyoshindwa kujiendesha - Msumbiji, Marekani, Japan, Congo DRC nk? Mipaka ya majimbo itatengezwa upya. Siyo lazima iwe kama mikoa ilivyo sasa.
 
Tuanzie China na Marekani na hata Ujerumani nani anajitambulisha kwa jimbo lake??
MIsingi ya hao uliowataja ni tofauti na ya kwetu, Wajerumani na Wamarekani ni watawala wenye historia fulani iliyowalazimisha wakubaliane na hali zao.

Tazama vipindi vya tv za China utaona wanavyosisitiza katika umoja. Tazama vikao vyao kila mwaka vinavyoongozwa na rais wao utaelewa maana ya umoja.

Nyerere aliua uchifu kwa makusudi ili tuwe kitu kimoja, Nigeria wanajitambulisha kwa majimbo na uchifu tazama jamii yao ilivyojaa hulka za kubaguana.
 
Tanzania haina majimbo kwa sasa. Mipaka ya majimbo haijulikani. Kwa hiyo kusema kuna majimbo yatashindwa kujiendesha ni utabiri usiokuwa na msingi.
Hujaelewa hoja yangu!! Hapa ninajibu hoja za wana CCM kuwa sera ya majimbo haitafanikiwa kwa sababu Kuna majimbo yatashindwa kujiendesha???

Alafu kuna issue yeyote juu la suala la mpaka??? Kwani tukiamua sasa tukitengeneza sheria na kutambua utawala wa majimbo na kusema mikoa hii itakuwa jimbo hili, mikoa hii jimbo hili kuna tatizo lolote????
 
MIsingi ya hao uliowataja ni tofauti na ya kwetu, Wajerumani na Wamarekani ni watawala wenye historia fulani iliyowalazimisha wakubaliane na hali zao.

Tazama vipindi vya tv za China utaona wanavyosisitiza katika umoja. Tazama vikao vyao kila mwaka vinavyoongozwa na rais wao utaelewa maana ya umoja.

Nyerere aliua uchifu kwa makusudi ili tuwe kitu kimoja, Nigeria wanajitambulisha kwa majimbo na uchifu tazama jamii yao ilivyojaa hulka za kubaguana.
Kwani kuna shida gani hapa kwetu??? Majimbo ya kinigeria yanakaliwa ana kabila moja tu na hii ni misingi ya divide and rule ya waingereza. Majimbo yetu yatakuwa na makabila tofauti tena jimbo moja hadi makabila 4 au 5 sasa shida iko wapi????

Alafu kumbuka mfumo wa utawala wa majimbo unaopendekezwa na Chadema hauendi kwenye misingi ya Mila desturi au makabila Kama kurudisha uchief. WAO wanamaanisha mfumo wa kiutawala na wa kiuchumi. Sasa hoja yako hapa haina mashiko
 
Back
Top Bottom