Wabunge CCM iringa waingiwa kiwewe!

Martoism

Member
May 31, 2012
36
21
Ni saa chache tu zimepita tangu Mkt wa Taifa Chadema na Kiongozi wa upinzani Bungeni ambaye pia ni mbunge wa hai Mh, Freeman Mbowe kuutangazia uma wa watanzania kuwa atatua mkoani Iringa na makamanda wa vuguvugu la mabadiliko almaarufu "Movement for Change M4C" kuwatia nuru ya mapambazuko na mwangaza wa utajiri walioukalia kwa mda mrefu chini ya viongozi wa CCM akiwamo spika wa bunge Anna Makinda, Prof Msola, Lukuvi, Deo Sanga - ''Jaa people'' na wengine ambao kwa taarifa zinazozagaa mitaani wamejiapisha na kuwaagiza makatibu wa chama chao kuhakisha nguvu ya M4C inadhoofishwa hata kwa nguvu ya dola na ndumba ili waendele kutawala . Najua unaweza kujiuliza Iringa ina nini? kwa kifupi tu niwaambie Iringa ni mkoa wenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka , ina mbuga kubwa na ya pili barani Africa yaani Ruaha National Park, vivutio vya utali kama kalenga na isimila , mikunjo (ox-bow lakes) ya "The great Ruaha River unaotiririsha maji throughout a year, mazao ya misitu kutoka Sao hill forest , migodi mikubwa ya makaa ya mawe, kilimo cha chai kisichokuwa na mfano barani Africa, viwanda vikubwa east and centra Africa kama Mufindi paper mills na Chai Bora lakini pamoja na utajiri wote huo bado Iringa ina harufu ya umaskini wa kutisha huku ikisifiwa kutoa mayaya wengi wanaofanya kazi miji na majiji mashuhuri kama Dar-es -Saalamu na kwingineko je mwanaJF mwenzangu M4C waende au Wasinde Iringa?
 
Hakuna mkoa amabo M4C haitafika hivyo kwenda ni lazima cha msingi ni mipango na muda muafaka.
 
Ukistaajabu ya musa utaona ya ccmagamba Sao hill huuza nguzo za umeme kenya lkn Tz inanunua Afrika kusini,Mpm ni kiwanda cha pili kwa ukubwa duniani kwa kuzalisha makaratasi lakini kina milikiwa na kuwafaidisha Wakenya na zaidi ya yote Sao hill imekinyima kijiji cha Nyololo kibali cha kuvuna mbao qb 500 japo kijiji hiki hapa Mufindi ndo Mabingwa wa kuzima moto Misituni na badala yake kapewa Lukuvi,niamini mimi hii ndo shukrani ya Magamba hapa bila M4c hakana Maisha
 
London vipi M4C. Lema alifikia hoteli au nyumbani kwa Mbowe alipokuwa huko?

"Mkombozi" wa Mwaafrika anatowa hela Tanzania anapeleka kwenda kununuwa nyumba London na Dubai ili tu na yeye akiongea aweze kusema "pale nyumbani kwangu London" au "pale nyumbani kwangu Dubai".

Miafrika ndivyo Ilivyo - NN
 
London vipi M4C. Lema alifikia hoteli au nyumbani kwa Mbowe alipokuwa huko?

"Mkombozi" wa Mwaafrika anatowa hela Tanzania anapeleka kwenda kununuwa nyumba London na Dubai ili tu na yeye akiongea aweze kusema "pale nyumbani kwangu London" au "pale nyumbani kwangu Dubai".

Miafrika ndivyo Ilivyo - NN

Waliweka pesa swiss ni kina nani?mbona hamwasemi wazirudishe?
 
[kikwete kila kukicha anapanda pipa kutalii anaogopa majukumu ya serikali dhaifu na chama goigoi kwi kwi kwi
 
kawaulize wakina riziwani na nyumba zao dubai m4c ikiingia madarakani tutahoji walipata wapi pesa hizo?
 
wasiwe na wacwac kabisa hata waloge au watumie nguvu za dola lazima chadema watue huko tu na watu lazima washaurike na kuvua magamba na kuvaa magwanda
 
London vipi M4C. Lema alifikia hoteli au nyumbani kwa Mbowe alipokuwa huko?

"Mkombozi" wa Mwaafrika anatowa hela Tanzania anapeleka kwenda kununuwa nyumba London na Dubai ili tu na yeye akiongea aweze kusema "pale nyumbani kwangu London" au "pale nyumbani kwangu Dubai".

Miafrika ndivyo Ilivyo - NN

Sawa kabisa miafrika ikiongozwa na CCM na kushabikiwa na wewe.
 
karibuni iringa kwetu ingawa sipo huko kwa sasa lakini naimini ngome ya mkwawa alipigwa mjerumani ccm itaona ,,,vijana wameiva kisiasa iringa ndio chachu na mwanzo wa kusini all the best cdm ....
 
Siku mbowe atasema anaenda kwimba mwanza nitajisikia faraja sana .kuna muhindi mmoja anaitwa mansoor anaishi mjini ila ni mbunge wa kwimba sijawahi msikia akiwatetea hata mara moja
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom