Uchaguzi 2020 Sauti ya Umma (SAU): Ilani ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
1600022944414.png
YALIYOMO;
1. UTANGULIZI
2. VIPAUMBELE VYA SERIKALI YA SAUTI YA UMMA(SAU)
3. AFYA
4. ELIMU
5. MAJI
6. KILIMO MIFUGO NA UVUVI
7. MALI ASILI
8. MIUNDO MBINU
9. VIWANDA NA BIASHARA
10. SANAA UTAMADUNI NA MICHEZO

Kwanza Kabisa Nimshukuru Mwenyezi Mungu Kwa Kutuongoza Na Kutusimamia Katika Safari Na Njia Mbalimbali Za Kuweza Kufanikisha Upatikanaji Wa Ilani Hii
Pili Kwa Niaba Ya Kamati Kuu Ya Chama Cha Sauti Ya Umma - SAU Tunawashukuru Viongozi Wetu Wote Katika Nafasi Mbalimbali Za Uongozi Ndani Ya Chama, Wanachama Wetu Wote,Wananchi Mbalimbali Wenye Vyama Na Wasiokuwa Na Vyama Tanzania Bara Na Visiwani Na Wote Waliotoa Maoni Yao Ambayo Ndio Kiini Cha Kupatikana Ilani Hii.

Mwisho Lakini Sio Kwa Umuhimu ,Niwashukuru Wajumbe Wote Wa Kamati Kuu Ya Chama Cha Sauti Ya Umma – SAU Kwa Kutumia Muda Wao Vema Katika Kukusanya Maoni Kutoka Katika Makundi Mbalimbali Na Mtu Mmoja Mmoja Na Kisha Kufanikisha Kupatikana Ilani Hii Ambayo Itakwenda Kuwa Mwongoza Katika Uchaguzi Mkuu Wa 2020 Na Kipindi Cha Miaka Mitano Ya Chama Cha Sauti Ya Umma Kushika Dola Kuanzia 2020 – 2025, Kama Watanzania Watatupa Kura Nyingi Zitakazo Tuwezesha Kupata Ushindi.

Majalio Kyara
KATIBU MKUU
CHAMA CHA SAUTI YA UMMA (SAU)

UTANGULIZI

Ndugu Mtanzania Karibu Sana Uisome Kwa Kina Na Kuitafakari Ilani Hii Ya CHAMA CHA SAUTI YA UMMA - SAU, Kwa Ajili Ya Uchaguzi Mkuu Wa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania ,Rais Wa Zanzibar ,Wabunge ,Wawakilishi Na Madiwani Kwa Mwaka 2020.Ilani Imefafanua Ni Jinsi Gani Chama Cha Sauti Ya Umma Kitakavyo Kuhudumia Mtanzania Endapo Utakipa Mamlaka Ya Kushika Dola Kwa Kuwapa Wagombea Wake Kura Nyingi Za Ndio Katika Uchaguzi mkuu Wa Mwaka 2020.
Nia Kubwa Ya Chama Cha Sauti Ya Umma (Sau) Ni Kumkomboa Mtanzania Kuanzia Wa Hali Ya Chini Kabisa Kiuchumi Na Kuondosha Kabisa Maadui Watano Yaani; Ujinga , Umasikini , Rushwa Na Ufisadi , Maradhi Na Ukosefu Wa Ajira Katika Kipindi Cha 2020-2025.

SAU Tunalengo La Kutengeneza Ajira Mpya Milioni Tisa(9,000,000) Katika Kipindi Cha Miaka Mitano Yaani Ajira Milioni Moja Na Laki Nane (1,800,000) Kwa Kila Mwaka. Lakini Pia Tutajikita Katika Kutambua Usawa Na Kuwawezesha Vijana , Wanawake Na Watu Wenye Ulemavu. Pamoja Na Hayo Ni Lazima Kuhakikisha Tunailinda Vema Amani Ya Nchi Yetu Ambayo Ni Kati Ya Urithi Mzuri Na Mkubwa Sana Tulioachiwa Na Mababu Zetu.Tunasema Sau Kwa Mabadiliko Makubwa Zaidi Ya Haraka Zaidi Na Yatakayo Mlenga Kila Mtanzania Kuanzia Wa Hali Ya Chini Hadi Juu.Iamini Sau Mkombozi Wa Kweli ,Twende Na Sau Tanzania Itasonga Mbele Zaidi.

Dhamira Ya Chama Cha Sauti Ya Umma (Sau) Ni Kuwa Na Tanzania Yenye Siasa Safi , Uongozi Bora, Uchumi Shirikishi Usio Tegemezi Utakao Kwenda Sambamba Na Kukua Kwa Uchumi Wa Jamii Nzima Tena Kwa Uwazi. Kwa Kuwa Sau Inataka Ahadi Zake Kwa Jamii Zitekelezwe, Mchakato Wa Katiba Mpya Utarejeshwa Ili Jamii Iweze Kutuadhibu Pindi Tutakapo Kwenda Kinyume Na Ahadi Zetu (Ilani Hii). Kila Mtanzania Lazima Ale Na Kufaidi Matunda Ya Mti Tanzania.

VIPAUMBELE VYA CHAMA CHA SAUTI YA UMMA – SAU
a) Afya
b) Elimu
c) Kilimo na viwanda

AFYA.
Afya Ndio Msingi Wa Kila Kitu, Kama Huna Afya Bora Hutoweza Kuzalisha Na Kuchangia Katika Uchumi Wa Taifa.Taifa Lenye Watu Wenye Afya Bora Ni Taifa Tajiri (A Health Nation Is A Wealthy Nation). Bado Hali Ya Utoaji Wa Huduma Za Afya Nchi Sio ya Kurizisha
 Sehemu za kupata matibabu ni chache hivyo kusababisha wananchi kusafiri mwendo mrefu kwa ajili ya kupata matibabu
 Hakuna uhakika wa matibabu kwa kushindwa kulipia gharama
 Upatikanaji wa dawa sio mzuri
 Upungufu mkubwa wa wataalam hasa vijijini.

Chama Cha Sauti Ya Umma –Sau Kitahakikisha Kila Mtanzania Anapata matibabu bure, Ili Kuwa Na Uhakika Wa Matibabu Pindi Atakapoumwa.Hii Itaenda Sambamba Na Uwepo Wa Zahanati Katika Kila Kijiji/Mtaa Kituo Cha Afya Kwa Kila Kata Ambacho Kitaweza Kutoa Huduma Kamili Ya Mama Na Mtoto , Hospitali Kwa Kila Wilaya.Na Hospitali Sita Za Rufaa Kikanda zenye kitengo cha kushughulikia magonjwa ya kansa. Kwa kutambua na kunufaika na ukuwaji wa TEHAMA, Utumiaji Wa matibabu kimtandao “Telemedicine” Utatumika.

Ufadhili Mkubwa Utatolewa Kwa Wanafunzi Wa Masomo Ya Sayansi Ili Kuvutia Wanafunzi Wengi Zaidi Ambao Watawezesha Kupata Wataalam Wengi Zaidi Wa Afya
Mishahara Mizuri Na Mazingira Mazuri Zaidi Kwa Wataalam wa afya Watakaotoa Huduma Zao Vijijini Kuliko Wale Walio Mijini .Kwa Kutambua Fani Ya Uuguzi Ni Wito Punguzo Maalum Litatolewa Kwa Wauguzi Katika Manunuzi Ya Mahitaji Yao Ya Msingi Kama Vyakula,Vifaa Vya Majumbani,Vyombo Vya Usafiri N.K

Teknolojia InaKuwa Na Kubadilika Kila Siku Vitendea Kazi Vitakuwepo Kwa Wingi Na Zinavyoendana Na Utaalam Wa Kisasa.Pia Mafunzo Endelevu Yatafadhiliwa Ambayo Yatawezesha Kutoa Matibabu Ya Kisasa Na Kuondosha Kabisa Matibabu Nje Ya Nchi.lakini pia kuvutia wagojwa kutoka nchi mbalimbali kuja kutibiwa Nchini Hivyo Sekta Hii Nayo Kuanza Kuchangia Katika Pato La Taifa.

Ili kuhakikisha Jamii Inakuwa Na Afya Bora Kila Wakati ,Wataalam Wa Lishe Watatumika Zaidi Kuwaelimisha Wananchi Jinsi Ya Kula Mlo Bora Wenye Uiano Yaani Vitamin ,Protein ,Wanga,Madini N.K. hii itasaidia pindi ikitokea gonjwa kama covid-19,watanzania tuzidi kuushangaza ulimwengu pia kujenga miili yenye uwezo mkubwa wakupambana na maadui (maradhi). Mfumo Maalum Utawekwa Kwa Ajili Ya Kuwahudumia Watoto Yatima Na Wasiojiweza Au Waliotelekezwa.Haya Yote Serikali Yetu Itashirikiana Vema Sana Pamoja Na Taasisi Binafsi Na Zile Za Kidini.

Vifaa Vya Kuwasidia Watu Wenye Ulemavu Kama Viti Vya Matairi,Mashine Kwa Ajili Ya Kuandikia Nukta Nundu, Fimbo Za Kutembelea Kwa Wasioona Na Mafuta Kwa Wenye Ulemavu Wa Ngozi(Albino) Vitatolewa Bure Kabisa Kwa Wahitaji Wote.

Kutoa Elimu Na Vifaa Kwa Ajili Ya Kujikinga Na Magonjwa Kama ,Ukimwi Na Kutokomeza Kabisa Maambukizi Kutoka Kwa Mama Kwenda Kwa Mtoto. Chama Cha Sauti Ya Umma –Sau Tunasema Hatuta Pambana Kwa Kusambaza Vyandarua Ambavyo Vina Msaidia Mtu Pindi Awapo Kitandani Tu, Bali Tutapuliza Dawa( Viuatilifu) Nchi Nzima Ilikuua Wadudu Na Mazalia Yote Ya Mbu Hivyo Kutokomeza Kabisa Ugonjwa Wa Malaria Nchini Tanzania.

Tutatengeneza Mpango Wa Siku 450 Kuhakikisha Mama Mjamzito Anapata Virutubisho Bora Kuanzia Kwenye Ujauzito Wake Hadi Miezi Sita Baada Ya Kujifungua. Lengo Ni Kuwa Na Watoto Wenye Kinga Nzuri, Afya Bora Na Kunyonyeshwa Maziwa Bora Ya Mama Katika Kipindi Cha Miezi Sita Ya Mwanzo.Hivyo Kupata Watoto Wenye Kinga Na Afya Bora Na Kuchangia Katika Kuondosha kabisa Vifo Vya Watoto Chini Ya Miaka Mitano. Sau Tunataka Wauguzi Waheshimiwe Kama Walivyokuwa Wanaheshimiwa Waalimu Miaka Ya Nyuma.

HIFADHI YA JAMII
Hifadhi Ya Jamii Ni Jambo Mtambuka Sana.Serikali Ya Chama Cha Sauti Ya Umma Itatengeneza Mfumo Ambao Kila Mtanzania Hasa Walio Jiajiri Katika Kilimo Na Uvuvi ,Atakuwa Anajiwekea Akiba Na Serikali Itamchangia Asilimia 90% Ya Akiba Aliyojiwekea .Hii Itawavutia Wananchi Wengi Zaidi Kujiwekea Akiba Ya Baadae Na Itakuza Akiba Ya Nchi Na Uchumi Kukua Zaidi.

ELIMU
Chama Cha Sauti Ya Umma – Sau Tunaamini Baada Ya Kuhakikisha Mtanzania Ana Afya Bora, Elimu Bora Ndio Msingi Wa Maendeleo Ya Taifa Letu. Tuta Wekeza Sana Katika Elimu Bora Ili Kupata Wataalam Bora Watakaosaidia Katika Kukamilisha Mipango Mbalimbali Ya Maendeleo Ya Taifa.

Uhaba Wa Walimu Na Vifaa Vya Kujifunzia Ni Kati Ya Changamoto Kuu Katika Elimu,Lakini Pia Mazingira Mazuri Ya Kujifunzia Kama Maabara,Madarasa ,Madawati Na Vyoo.

Sau Kwa Kutambua Kwamba Kuwa Na Uwiano Mzuri Kati Ya Wanafunzi Na Mwalimu Ni Kiashiria Cha Kupata Elimu bora.Tutahakikisha tunatoa ajira mpya kwa walimu lengo ni kupata Walimu Wakutosha Ambao Ni Mahiri. Na kufikia Uwiano Wa Wanafunzi 20-29 Kwa Mwalimu.

Kwa Kuwa Elimu Ya Awali Ndio Msingi Wa Elimu Tutahakikisha Elimu Ya Awali Kwa Watoto (Chekechea) Ina Boreshwa Na Kuzingatiwa.Masomo Ya Hisabati, Sayansi Na Tehama Yatapewa Kipaumbele Zaidi.

Tutapunguza Miaka Ya Kusoma Masomo Ya Msingi Na Mwanafunzi Kujikita Moja Kwa Moja Kwenye Kile Ambacho Atakwenda Nacho Mpaka Chuo Kikuu Na Baadae Kujiajiri Au Kuajiriwa Kwa Fani Hiyo.Hii Itasaidia Zaidi Kumudu Ushindani Katika Soko La Ajira Na Wanafunzi Kuelewa Na Kupenda Anachofundishwa Sio Kufundisha Kwa Ajili Ya Kufanya Mtihani.

Kuhakisha Kila Mtanzania Anafika Hadi Hatua Ya Elimu Ya Chuo Bila Malipo. Yaani Chuo Cha Ufundi Stadi , Chuo Cha Ufundi Mchundo , Au Chuo Kikuu. Hivyo Kusaidia Kupata Wataalam Wengi Zaidi Wa Fani Mbalimbali. Lengo Kila Mtanzania Kwa Uwezo Na Elimu Yake Aweze Kuchangia Katika Pato La Taifa Kwa Kuajiriwa Au Kujiajiri.
Sau Itahakikisha Maslahi Ya Waalimu Yana Zingatiwa Na Wanapata Mazingira Bora Ya Kufundishia Na Vitendea Kazi Kama Vitabu, Vifaa Vya Maabara Na Kemikali.Pia Madai Yote Ya Walimu Yatalipwa. Kila Mwalimu Kumpatia Kompyuta Ili Watumie Tehama Zaidi Katika Kufundisha Na Kuandaa Vipindi Vya Masomo Mbalimbali.

MAJI
Maji Ni Uhai Na Maji Ni Kitu Muhimu Katika Uhai Wa Viumbe Hai Umuhimu Wa Raslimali Hii Nyeti Unatokana Na Kukosa Kwake Mbadala.
Kwa Kutambua Hili Serikali Ya Sau Itajikita Na Kuhakikisha Kila Mwananchi Anapata Maji Safi Na Salama Ya Kutosha Tena Bila Gharama
Yaani Maji Safi Na Salama Bure Kwa Kila Mtanzania.

Kwa Kuwa Shida Ya Maji Itakuwa Imeisha Hivyo Mama Na Dada Zetu Waliokuwa Wanakesha Katika Foleni Za Maji Sasa Watakuwa Na Muda Mzuri Na Mwing Zaidi Wakushiriki Katika Kuchangia Uchumi Wa Familia Zao Na Kwa Nchi.Pia Sau Tutazingatia Na Kushirikisha Wananchi Katika Kulinda Vyanzo Vya Maji Na Utekelezaji Wa Miradi Mablimbali Ya Maji Mijini Na Vijijini.

Serikali Ya SAU Tutajenga Mabwawa Makubwa Yatayowezesha Kuvunwa Na Kukusanywa Kwa Maji Ya Mvua Ambayo Yatatumika Kwa Binadamu, Mifugo Na Kilimo Cha Umwagiliaji Badala Ya Maji Yote Kuishia Baharini.

Miradi Mbalimbali Ya Maji Itaanzisha Ili Kumaliza Kabisa Kwa Asilimia Mia Moja (100%) Tatizo La Maji Nchini

MAJI TAKA
Kutengeneza Miundo Mbinu Ya Kukusanya Maji Taka Kisha Kuyatumia Maji Taka Katika Shughuli Mbalimbali Kama Umwagiliaji, Usafishaji Mazingira N.K

ARDHI NYUMBA NA MAKAZI
Upimajiwa Ardhi Umesuasua Na Kupelekea Kutokea Dhuluma Na Kesi Nyingi Ambazo Hazikupaswa Kutokea.Wakati Mwingine Watendaji Wa Wizara Husika Wanakuwa Chanzo Cha Gomvi Hizo.

Serikali Ya CHAMA CHA SAUTI YA UMMA –SAU Itahakikisha Kila Ardhi Ya Tanzania Inapimwa, Inamilikishwa Na Kulipiwa Kodi. Hii Itaondoa Ugomvi Na Kuongeza Pato Kwa Taifa. Pia Ambao Hawana Matumizi Ya Ardhi Hawatakubali Kukaanayo Pasipo Izalisha.

Kurekebisha Wizara Ya Ardhi Na Kuweka Watumishi Waadilifu Ili Kuondoa Malalamiko Na Dhuluma Za Ardhi Kwa Wananchi Mbalimbali.Na Wizara Hii Itakuwa Chini Ya Rais.

Kutumia Vyema Ardhi Kubwa Tuliojaliwa Kwa Kuhusisha Wawekezaji Wakubwa Wa Ndani Na Nje Ya Nchi, Katika Kilimo Na Viwanda Ili Ajira Nyingi Zaidi Zipatikane Na Uuzaji Mkubwa Wa Bidhaa Nje Ya Nchi.

Kodi Ya Majengo Kwa Nyumba Za Makazi Itafutwa Kabisa Na Kutokuruhusu Ujenzi Wa Maduka Ya Biashara Katika Maeneo Ya Makazi.Sehemu Maalamu Zitatengwa Badala Ya Kila Mwenye Nyumba Kujaza Frame Za Maduka Mbele Ya Nyumba Yake.

Vikundi Vya Walemavu Na Kina Mama Vicoba Vitapewa Ardhi Bure Ili Wawekeze Katika Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Majengo Kama Hostel N.K
Kupunguza Gharama Za Vifaa Vya Ujenzi

Nyumba Bora 200,000(Laki Mbili) Za Makazi Vijijini Zitajengwa Katika Kipindi Cha Miaka 5,Kwa Kushirikiana Na Tanzania Building Agency(Tba),Taasisi Za Fedha Na Viwanda Vya Vifaa Vya Ujenzi.Tutaanzishwa Kampeni Maalum Vijijini Ya Nipe Mazao Au Mfugo Nikupe Nyumba Bora Katika Eneo Lako. Lengo Ni Kuhakikisha Watanzania Wanaishi Maisha Bora

KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
KILIMO

Chanzo Kikuu Cha Ukuaji Wa Uchumi Wa Nchi Yetu Na Nchi Nyingine Za Afrika Ni Chakula.Kwa Kuwa SAU Tunataka Uhuru Wa Kiuchumi Uendelee Katika Nchi Yetu Ni Lazima Tuanze Na Chakula.

Katika Nchi Yetu Kilimo Ni Sekta Ambayo Wananchi Wengi Wameajiriwa ,Wamejiajiri Au Wanajishughulisha Nayo.Lakini Hakichangii Kwa Ukubwa Huo Katika Ukuaji Wa Uchumi.Changamoto Ni Nyingi Ikiwemo Kutegemea Kilimo Cha Asili,Upatikanaji Mbovu Wa Pembejeo Za Kilimo Hususani Mbegu Bora, Mbolea Na Viuatilifu. Bei Kubwa Za Pembejeo, Utegemezi Wa Madalali Katika Masoko N.K

Serikali Ya CHAMA CHA SAUTI YA UMMA Itajikita Zaidi Katika Kuhamasisha Kilimo Hai Nchini.Kilimo Cha Kutumia Mbolea Za Kemikali Si Salama Sana Na Kina Athari Nyingi Kwa Mazingira, Kina Haribu Ardhi,Upotevu Wa Viumbe Hai,Ukosefu Wa Maji,Ikolojia Na Athari Nyingine Nyingi Lakini Pia Kina Ongeza Ukosefu Wa Chakula Katika Nchi Zinazoendelea.

Kilimo Hai Kitasaidia Kuimarisha Usalama Na Uhakika Wa Chakula Lakini Pia Uhifadhi Wa Mazingira Na Kuhimili Mabadiliko Ya Tabia Nchi.Hii Itasaidia Kuwa Na Kilimo Endelevu.Tena Chenye Gharama Nafuu Hivyo Kuwa Mkombozi Wa Kweli Kwa Mkulima.

Chama Cha Sauti Ya Umma (SAU) Kupitia TADB (Tanzania Agriculture Development Bank) Kitatoa Mikopo Ya Gharama Nafuu Na Ya Muda Mrefu Kwa Vikundi Vya Wakulima Hasa Vijana,Wanawake Na Walemavu Wanaolima Zaidi Ya Ekari 30 Kwa Ajili Ya Kukuza Kilimo Chao Au Kununua Zana Za Kilimo Za Kisasa, Pembejeo, Ujenzi Wa Maghala,Ujenzi Wa Viwanda Vya Kusindika Na Kuongeza Thamani Ya Mazao Ya Kilimo ,Uvuvi Na Mifugo.

Kila Ardhi Ya Tanzania Lazima Iendelezwe Na Izalishe, Mwiko Kuwa Na Mashamba Makubwa Yasiozalisha.Mashamba Yote Yasioendelezwa Yatagaiwa Kwa Wananchi Wenyeji Wenye Nia Ya Kuyaendeleza .

Kutenga Maeneo Maalum Ya Wakulima Tofauti Na Yale Ya Wafugaji Kushirikiana Na Sekta Binafsi Katika Kupanua Na Kuongeza Viwanda Vya Mbolea Ya Kupandia (DAP) Na Mbolea Ya Kukuzia(UREA) Ili Zipatikane Kwa Wingi Na Kuchagiza Katika Kushusha Bei Elekezi Ya Mbole Kwa Muuzaji Wa Rejareja(Muuzaji Wa Mwisho) Kama Ilivyo Kanuni Za Mbolea Za Mwaka 2011kupitia The Fertilizer(Amendment) Regulations, 2017.

Kuvutia Uwekezaji Katika Viwanda Vya Kusindika Mazao Kama Nyanya Na Mengineyo, Ili Ziweze Kupatikana Kwa Wingi,Bei Nzuri Na Kwa Wakati Wote Kwa Ajili Ya Matumizi Ya Ndani Ya Nchi Na Uuzwaji Nje Ya Nchi.

Mbegu Bora, Mbolea Na Viuatilifu Bora Kwa Wakulima Zifike Kwa Wakati Serikali Ya SAU Tutajikita Katika Kilimo Cha Kisasa Kisichotegemea Mvua .Tutajenga Mabwawa 70 Makubwa Yatakayo Hudumia Zaidi Ya Ekari Million Moja Na Laki Nne(1,400,000) Za Kilimo Cha Kisasa Cha Umwagiliaji.Mabwawa Haya Yatatumika Pia Katika Uvuvi Ambao Tutapata Tani 28,000 Za Samaki Kwa Mwaka, Hivyo Kupunguza Utegemezi Wa Samaki Kutoka Vyanzo Vya Asili.

Kilimo Katika Maeneo Haya Kitahusisha Wananchi Wa Eneo Husika Na Wawekezaji Wakubwa Katika Kilimo Duniani, Ambao Kwa Upatikanaji/Uwepo Wa Maji Haya Utawavutia Kuja Kulima Tanzania Hivyo Nchi Yetu Kuwa Na Chakula Kingi Cha Kutosheleza Mahitaji Ya Nchi Na Ziada Kwa Ajili Ya Kuuza Nje Ya Nchi.

Kukuza Na Kutoa Elimu Ya Kilimo Cha Mboga Mboga,Matunda,Viungo Na Maua Kwa Wananchi Waishio Katika Maeneo Yafaayo Kilimo Hicho Na Kuhimiza Kilimo Hai (Organic Farming)

Uwekezaji Katika Vituo Vya Utafiti Wa Kilimo Ili Kupata Mbegu Mpya Bora Za Mazao Mbalimbali Na Kusaidia Katika Ongezeko La Uzalishaji Wa Mazao. Kuongeza Viwanda Vya Uzalishaji Mbegu Za Asili Lengo Ni Kuhakikisha Asilimia 99% Ya Mbegu Zinatoka Nchini.Mbegu Nyingi Za Kisasa Zinazotengenezwa Na Viwanda Vya Nje Zina Gharama Kubwa Lakini Zinahitaji Matunzo Sana Mbolea, Viutilifu Na Madawa Ili Kumea Lakini Pia Huwezi Kupata Mbegu Kutoka Katika Mazao Uliyo Vuna

Hivyo Kusababisha Mkulima Kununua Mbegu Na Mbolea Kila Msimu Jambo Ambalo Linakwenda Kumuangamiza Mkulima Lakini Pia Tunaweza Kuja Kuwa Na Ukoloni Wa Chakula(Food Colonialism).

Sau Tunataka Kurejesha Mbegu Zetu Za Asili. Kufufua,Kujenga,Kuongeza Na Kuboresha Kilimo Cha Mazao Ya Biashara Kama Mkonge,Kahawa,Pamba , Karafuu,Chai,Alzeti,Miwa N.K Pamoja Na Kuinua Kilimo Cha Nazi. Malengo Haya Yatasaidia Kuongeza Sana Pato La Taifa Kwa Uuzwaji Mkubwa Wa Chakula Nje Ya Nchi Na Kuwa Na Chakula Cha Kutosheleza Nchini.

MIFUGO
Tanzania Ni Nchi Yenye Mifugo Mingi Takwimu Zinaonyesha Kuna Ng’ombe Zaidi Ya Million30, Mbuzi 18milioni, Kondoo 5milioni, Nguruwe 2milioni Na Kuku 74milioni.Idadi Hii Ya Mifugo Inaonyesha Zahiri Kwamba Asilimia Kubwa Ya Watanzania Ni Wafugaji. Sekta Hii Bado Haijaweza Kumkomboa Vema Mwananchi Hasa Kutokana Na
 Garama Kubwa Za Malisho Kwa Sababu Uzalishaji Wa Chakula Cha Mifugo Ni Mdogo Sana.
 Vifo Vingi Vinavyosababisha Na Uwepo Wa Majosho Yasiyotosheleza Hivyo Kushindwa Kukabiliana Na Magonjwa Yanayoenezwa Na Kupe.
 Wataalam Wa Kutoa Huduma Ya Uhimilishaji Wa Ng’ombe Kwa Ajili Ya Kuboresha Koosafu Ni Wachache.

Ili Kupunguza Garama Ya Malisho Serikali Ya Chama Cha Sauti Ya Umma – SAU Itahimiza Kilimo Cha Malisho Ya Mifugo Yaliyo Bora Yatakayo Patikana Kwa Wingi Na Kwa Garama Nafuu Kwani Malisho Ndio Mkombozi Wa Mfugaji. Wafugaji Watapata Mafunzo Ya Ufugaji Bora Kupitia Kwa Maafisa Ugani.

Kilimo Kilichozoeleka Cha Malisho Kwa Kutumia Udogo Kitahimizwa Kwa Kutolewa Elimu Juu Ya Kuboresha Na Jinsi Ya Kuhifadhi Malisho Kwa Ajili Ya Kutumika Kipindi Cha Ukame.Pia Madarasa Ya Kilimo Cha Kisasa Kisichotumia Udongo Kama Hydroponic Fodder Na Azolla Yatatolewa Na Kuwasihi Wafugaji Kutumia Aina Hizi Za Kilimo Kwani Kinahitaji Eneo Dogo Ambalo Litatoa Malisho Mengi.

Mfano Azolla Ikilimwa Katika Bwawa Lenye Mita Za Mraba Kumi Na Sita (16) Ndani Ya Siku Tatu Utavuna Kilo Kumi Na Sita Za Malisho Na Utaendelea Kuvuna Kila Baada Ya Siku Mbili. Vivyo Hivyo Hydroponic Fodder Katika Eneo La Mita Za Mraba 150 Utavuna Tani Moja Ya Malisho Kila Siku. Ng’ombe Mmoja Anakula Kilo Kumi, Hivyo Malisho Ya Tani Moja Yanatosha Kulisha Ng’ombe 100 Kwa Siku.

Tutaongeza Idadi Majosho Na Kufikia 600 Ifikapo 2025 Malambo Zaidi Kuongezwa Ili Kufikia 3600 Kutoka Takribani Malambo 2000 Yaliopo Sasa
Uzalishaji Na Usindikaji Wa Maziwa Na Kutoza Kodi Kubwa Sana Kwa Maziwa Yanayoingia Kutoka Nje Ya Nchi.Lengo Ikiwa Ni Kupunguza Uingizwaji Wa Maziwa Kutoka Nje Ili Kulinda Soka La Maziwa Ya Ndani Ya Nchi.

Kufufua na Kujenga Viwanda Vya Ngozi Sambasamba Na Kutoa Elimu Jinsi Ya Kuboresha Zao La Ngozi. Kwa Kutambua Umuhimu Wa Masoko Serikali Ya Sau Itahakikisha Inapiga Marufuku Uingizwaji Wowote Wa Nyama Na Mifugo Kutoka Nje Ya Nchi Na Kuwatafutia Wafugaji Masoko Ya Uhakika, Ili Mfugaji Afuge Huku Akiwa Na Uhakiki Wa Soko.

Kuboresha Minada Ya Mifugo

UVUVI
Uvuvi Ni Sekta Muhimu Katika Upatikanaji Samaki Na Mazao Yake,Sekta Hii Inauwezo Mkubwa Wa Kupanua Wigo Wa Ajira Kwa Vijana Na Kuongeza Kipato Kwa Jamii.Bado Ushirikishwaji Wadau Wa Ufugaji Sio Wakurizisha .Kukosekana Kwa Mitaji Ili Kuweza Kuvua Kisasa Na Matumizi Mabaya Ya Uvuaji Kama Wavu Zisizostahili Ni Kati Ya Changamoto Katika Uvuvi.

Lengo La Serikali Ya SAU Ni Kuwashirikisha Wadau Ili Kuongeza Uzalishaji Kutoka Tani 50,000 Za Samaki Zinazokadiriwa Kuvunwa Kwa Sasa Hadi Tani 150,000 Kwa Mwaka.

Kuongeza Idadi Ya Vizimba Vya Kufugia Samaki Katika Ziwa Nyasa, Tanganyika Na Victoria Kutoka 408 Zilivyopo Hivi Sasa Hadi Kufikia 1009 Ifikapo Mwaka 2025
Ujenzi Wa Bandari Ya Uvuvi Katika Pwani Ya Tanzania Eneo La Bagamoyo Katika Mkoa Wa Pwani Na Mkoa Wa Mtwara Itakayowezesha Meli Kubwa Za Uvuvi Kupakia Na Kupakua Mazao Ya Uvuvi Hivyo Kutengeneza Ajira Na Kuvutia Katika Uwekezaji Wa Viwanda Vya Kuchakata Samaki Na Kuongeza Thamani Ya Mazao Ya Uvuvi.
Unuaji Wa Meli Kubwa Za Uvuvi Katika Bahari Kuu Na Kwenye Maziwa Ili Kuwa Na Uvuaji Mkubwa Utakaoleta Kitoweo Bora Na Kwa Wingi.

MALI ASILI
UTALII

Ketenga Pesa Kwa Ajili Ya Kufanya Tafiti Mbalimbali Za Mambo Ya Kale Ili Yaingie Katika Vivutio Vya Utalii. Kuongeza Idadi Ya Vyumba Vya Kulala Wageni Katika Sekta Ya Utalii Vya Madaraja Mbalimbali Kuhimiza Utalii Wa Ndani Ili Watanzania Wenyewe Tuwe Miongoni Mwa Mabalozi Huru Wa Utalii Wanchi Yetu Kote Duniani.

MADINI
NISHATI GESI NA MAFUTA

Tunayo Gesi Asilia Nyingi Iliyopatikana Katika Nchi Yetu. SAU Tunasema Ni Wakati Sasa Wakuhakikisha Bei Ya Nishati Kama Gesi Inapungua Na Kusambazwa Kwa Ajili Ya Matumizi Ya Majumbani Na Viwandani. Hii Itasaidia Kupunguza Matumizi Ya Misitu Kwa Kuni Na Mkaa Serikali Ya SAU Itaendeleza Zaidi Utafiti Wa Mafuta Na Gesi Na Kushusha Garama Za Nishati Ya Umeme Ili Kulinda Misuti

Kufadhili Elimu Kwa Vijana Wetu Ambao Wanasomea Taaluma Hii. Lengo Ni Kupata Wataalam Wengi Wazawa Katika Sekta Hii

MISITU NA NYUKI
Upandaji Miti
Uanzishaji Wa Misitu Jamii
Kutengeneza Tanzania Ya Kijani.
Miti Itapandwa Katika Kila Eneo La Tanzania. Katika Kipindi Cha Miaka Mitano, Mti Billion Moja Itapandwa, Takribani Miti Millioni Mia Mbili Kwa Mwaka.
Kuhakikisha Kila Mtanzania Anakuwa Na Mti Wake Wakutunza Ili Kutengeneza Hali Ya Hewa Bora Zaidi. Hii Itatengeneza Ajira Kwa Watanzania Takribani Laki 5.
Hii Itasaidi Katika Mabadiliko Ya Hali Ya Hewa. Kwa Mwaka Dunia Inapoteza Takribani Miti 10 Billion Hii Inamaana Kiwango Cha Corbondioxide Inayonyonywa Kinazidi Kuwa Kidogo,Pia Ni Hatari Kwa Wananchi Wanaoishi Kwa Kutegemea Misitu.

Ufugaji Wa Nyuki Bado Ni Mdogo Sana.Kuhimiza Ufugaji Wa Nyuki Ili Kupata Mazao Mengi Ya Nyuki Kwa Ajili Ya Mauzo Ya Ndani Na Nje. Uhimizaji Na Utoaji Wa Elimu Ya Utengenezaji Wa Mizinga Nyuki Ya Kisasa Inayo Tumia Udongo Ili Kuendelea Kulinda Misitu. Lengo Ya Serikali Ya SAU Ni Kutengeneza Mizinga Laki Nne Na Ishirini, Mizinga Hii Itakuwa Na Uwezo Wa Kuzalisha 10-15kg Za Asali Kwa Mwaka. Ufugaji Wa Nyuki Unategemewa Kuzalisha Ajira Takribani Laki Tano Na Ishirini Na Asali Wastaniwa Tani 5066 Kwa Mwaka Ambao Watajipatia Kipato 50,660,000,000/= Kwa Mwaka Hivyo Kuongeza Kipato Cha Wananchi Sekta Hii Inaweza Kuleta Kipato Kikubwa Sana Katika Nchi Na Kuwa Msaada Wa Kukomboa Sekta Nyingine Kama Afya Na Elimu, Mikataba Iwe Ya Wazi Kwa Wananchi Wote Haswa Walio Karibu Na Eneo Husika.

NISHATI MBADALA
Tutawekeza Katika Nishati Mbadala Kama Solar Takataka,Biomass Na Biogas Na Upepo. Wananchi Wataruhusiwa Kutengeneza/Kuwekeza Na Kuuzia Jirani Zao.Pia Ofisi Za Serikali Zitakuwa Mfano Kwa Kuanza Kutumia Nishati Hizi Ili Kupunguza Gharama Za Uendeshaji Wa Serikali.

Bio Gas Itasaidia Sana Kupunguza Kukata Miti Kwa Ajili Ya Kupikia

VIWANDA NA BIASHARA
Kuanzisha Benki Ya Viwanda Kwa Kukiri Kuwa Kilimo Ndio Uti Wa Mgongo Wa Uchumi Wetu. Sau Itahakikisha Kuwa Viwanda Vingi Iwezekanavyo Vitajihusisha Na Usindikaji Na Uongezaji Wa Thamani Mazao Ya Kilimo Serikali Ya Sau Itachukua Hatua Za Maksudi Kulinda Na Kukuza Viwanda Vya Hapa Nchini Na Kuwahamasisha Watanzania Kupenda Na Kutumia Bidhaa Zinazotengenezwa Na Viwanda Vya Hapa Nchini.

Kwa Kushirikiana Na Sekta Binafsi Serikali Ya Sauti Ya Umma Ihimiza Uanzishwaji Wa Viwanda Vya Kutengeneza Mashine, Nyenzo Na Vipuli Vya Mashine Za Viwandani (Supporting Industries).
Kiwanda Cha Matrekta
Kiwanda Cha Kuunganisha Magari Ya Mizigo
Viwanda Vinavyotengeneza Bidhaa Zitokonazo Na Mali Ghafi Za Tanzania Vitapewa Kipaumbele Zaidi Mfano Nguo,Usindikaji, Kama Nyanya. Lakini Pia Viwanda Vya Viatu Mikanda Na Bidhaa Mbalimbali Za Ngozi,Ili Kuongeza Thamani Ya Mazao Ya Kilimo Yaani Kutouza Mali Ghafi.Lengo Ni Kuhakikisha Tunalishika Soko La East Africa Na Sadc Kwa Kuwauzia Bidhaa Zitokazo Na Kutengenezwa Nchini Tanzania.

Exemtion Katika Umeme Ilikupunguza Garama Za Uzalishaji Na Kusaidi Kushindana Katika Soko La Jumuiya Mbalimbali Na Dunia Kwa Ujumla. Kufungua Milango Zaidi Ya Uwekezaji Wa Viwanda Kutoka China,Uturuki Na Marekani Hasa Viwanda Vinavyotumia Malighafi Kutoka Nchini Serikali Ya Sau Tutawekeza Zaidi Katika Vikundi Vya Wanawake Wajasiriamali Wa Chini Na Wakati Katika Upatikanaji Wa Mitaji Na Masoko, Na Hawa Ndio Watapewa Kipaumbele Katika Tenda Za Manunuzi Ya Serikali.

Kile Kinachotumiwa Serikalini Kama Kinatengenezwa Nchini Serikali Haitonunua Nje Ya Nchi. Hii Itasaidia Kupunguza Matumizi Ya Fedha Za Kigeni Na Kuongeza Ajira Viwandani.

SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Utamaduni Ndio Uhai Wa Taifa, Unalitambulisha Taifa Na Kuliweka Katika Ramani Ya Ulimwengu.Katika Hili Serikali Ya Sau Inakusudia Kuyatambua Zaidi Maeneo Mbalimbali Ya Kiutamaduni Tena Kwa Gharama Za Ndani Ya Nchi Kusomesha Walimu Zaidi Wa Michezo Na Waamuzi,Lakini Pia Wasimamizi Makini Wa Wanamichezo.
Kuwekeza Katika Kukuza Vipaji Kwa Watoto Zaidi Ili Kujenga Wanamichezo Bora Wa Baadae. Kuweka Viwanja Vya Michezo Kila Kata,Pamoja Na Kuwa Na Shule Maalum Kwa Wanamichezo Na Wasanii Kuhamasisha Michezo Ambayo Haipewi Kipaumbele Kama Uendeshaji Wa Baiskeli Kulinda Na Kuenzi Mila Na Desturi Zinazofaa Na Kutokomeza Mila Na Desturi Zisizofaa.

MIUNDO MBINU
Miundo Mbinu Katika Nchi Yeyote Ile Hulinganishwa Na Mishipa Katika Mfumo Wa Damu Mwilini.Pasipo Miundo Mbinu Ya Kusafirisha Mahitaji Muhimu Na Ya Lazima Katika Mwili Ambayo Ni Imara Na Ya Kudumu Na Kutegemewa, Baadhi Ya Sehemu Za Mwili Zinaweza Kupooza Au Kufa Kabisa.Kila Kiungo Katika Mwili Kinapokea Au

Kupeleka Mahitaji Ya Viungo Vingine Kwa Njia Ya Miundo Mbinu Iliyopo Mwilini.Kama Viungo Vya Mwili,Nchi Yetu Ina Maeneo Mbalimbali Yenye Bidhaa, Neema Na Utajiri Wa Rasilimali Tele Zinazohitajika Sana Maeneo Mengine.

Kujenga Barabara Zinazopitika Kipindi Chote Hasa Vijijini /Mashambani Ili Kuwezesha Mbolea Kufika Kwa Wakati Na Kwa Gharama Nafuu.Lakini Pia Mazao Kuweza Kusafirisha Kwa Wakati Na Urahisi Kutoa Kipaumbele Kwa Wakandarasi Wazawa Katika Zabuni Mbalimbali Na Kuweka Ulazima Wa Ushirikishwaji Wa Wazawa Katika Zabuni Ambazo Amepewa Mkandarasi Ambaye Si Mzawa.

Kuboresha Reli Zilizopo Na Kuanzisha Njia Mpya Za Reli Ya Sgr Ikiwamo Zinazo Unganisha Nchi Jirani Kama Ilivyo Reli Ya Tazara Na Kuhamasisha Matumizi Ya Reli Hasa Katika Kusafirisha Mizigo. Kutumia Mali Ghafi Zilizopo Nchini Kwa Ajili Ya Kutengeneza Mataruma Ya Reli Serikali Ya SAU Tutajenga Na Kuanzisha Usafirishaji Wa Mafuta Kwa Njia Ya Mabomba Kutokea Bandarini Kuelekea Mikoa Mingine Na Mipakani Mwa Nchi Jirani Ili Kuendelea Kulinda Na Kutunza Barabara Zetu Lakini Pia Kupanua Zaidi Wigo Wa Kibiashara Na Nchi Jirani.

Matumizi Zaidi Ya Usafiri Wa Majini Kwa Mizigo Na Abiria Ususani Katika Mikoa Ya Pwani Na Dar Es Salam Kwa Kutumia Bahari Ya Hindi Lakini Pia Katika Maziwa Na Mito Mbalimbali Nchini Serikali Ya SAU Tutawekeza Zaidi Katika Usafiri Wa Umma Hasa Kwenye Miji Kwa Kuwa Na Train Na Njia Zaidi Za Mabus Ya Mwendo Kasi Ya Kisasa Na Madaraja Tofauti Lengo Ni Kuhakikisha Wananchi Wengi Zaidi Wanatumia Usafiri Wa Umma Ikiwemo Watumishi Wa Serikali Serikali Ya SAU Nia Ni Kuwekeza Katika Usafiri Wa Train Kwa Kuwa Ni Salama,Nafuu,Yakuaminika Na Yafuraha Ukifananisha Na Njia Nyingine Za Usafiri .Tunataka Reli Iwe Namba Moja Katika Usafiri Wa Umma Nchini.

 
Back
Top Bottom