Waandishi bora 25 wa Tanzania ni hawa wafuatao...

Hongera kwa uchunguzi wako, Nadhani si vibaya ukatufahamisha zaidi juu ya uchunguzi wako huu, ulitumia criteria gani na uliuendesha vipi? kama uliuendesha kwa njia ya mahojiano,je ni watu wangapi ulio wahoji, wanawake wangapi? , wanaume wangapi, wanavyuo wangapi, viongozi wa wadini wangapi etc. na unaweza hata kutuwekea in terms of percentage, nafikiri inaweza kutusaidia zaidi, sababu naona uchunguzi wako uko too general inakuwa ngumu kidogo kuufanyia kazi
 
Nimekuwa nafanya uchunguzi kwa mwaka wa 5 sasa juu ya waandishi wa kitanzania wenye ushawishi kwa wananchi, uchunguzi nimeufanya kwenye vyuo vikuu, mikoani, mijini, kwenye nyumba za ibada, vyama vya siasa na vijijini nikishirikiana na team ya watafiti wa maswala ya kisiasa wa chama cha Republican cha Marekani na wafuatao ni waandishi wanaokubalika sana miongoni mwa watanzania tena habari zao zinapendwa sana............
1.Jenerali Ulimwengu( gazeti la Rai zamani na kwa sasa Raia Mwema pia ni mchangiaji kwenye The East African la kenya)
2.Mwanakijiji(Mwanahalisi, Tanzania Daima na mitandaoni)
3.Lula Wa Ndali Mwana Nzela(Raia Mwema)
4.Saed Kubenea(Mwanahalisi)
5.Ansbert Ngurumo(Tanzania Daima)
6.Evarist Chahali(Raia Mwema na www.chahali.com)
7.Ojuku Abraham(Dira kwa sasa)
8.Msomaji Raia(Raia Mwema)
9.Johnson Mbwambo(Raia Mwema)
10.Kondo Tutindaga(Mwanahalisi na Kwanza jamii)
11,Fr Privatus Karugendo(Raia Mwema)
12.Nova Kambota(zamani Dira kwasasa mtandaoni www.novakambota.com)
13.Dismass Lyassa(Mwananchi na mkurugenzi Global Source Watch GSW ubungo)
14.Kinabo(Tanzania Daima)
15.Samson Mwigamba(Tanzania Daima)
16.Fredrick Katulanda(Mwananchi)
17.William Shao(Majira na mwandishi wa "Miaka 2000 ya ukristo historia iliyopotoshwa)
18.Godfrey Dilunga(Raia Mwema)
19.Maggid Mjengwa(Raia Mwema na mtandaoni MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo)
20.Ndimara Tegambwage(Mwanahalisi na mtandaoni uhuru hauna kikomo )
21.Nkwazi Nkwabi(Dira na mtandaoni )
22.Marehemu Adam Lusekelo(Daily News with the light touch na mtandaoni)
23.Freddy Macha(Mwananchi, The Citizen na mtandaoni Freddy Macha)
24.Issa Michuzi(mtandaoni www.issamichuzi.blogspot.com)
25.Bubelwa Bandio(mtangazaji voice of America na mtandaoni "The Way You See The Problem Is The Problem")

HAWA NDIYO WAANDISHI 25 WA KITANZANIA WENYE USHAWISHI MKUBWA SANA KWA WANANCHI NA MWISHO WA UTAFITI WETU TULISHAURI TAASISI MBALIMBALI ZIWATUMIE WATU HAWA KWENYE KUHIMIZA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO MFANO KILIMO KWANZA, ELIMU NA KATIBA MPYA......NI HAYO TU WADAU , IWAPO UNA MAONI USISITE KUNIANDIKIA KWENDA kiwalanikwagude@rocketmaail.com

Utafiti huu ni wa kishabiki na haukufuata vigezo vya kitaalam. Nadhani mwandishi ametumia
zaidi utashi wake katika kuyapanga majina bila kufafanua kama ni waandishi wa makala au wa
uchunguzi? Huwezi kuchanganya waandishi wa makala na wale wa uchunguzi, na wengine kazi
yao kuripoti tu fulani kasema hivi! Fanya utafiti wa kina kabla hujakurupuka kuandika.
 
kati ya tafiti tata....!
waandishi wenye mlengo fulani pekee...!
lakini inategemea wakati anafanya tafiti kulikuwa na kundi gani (kusanyiko lenye mlengo mmoja)
 
Nilijua tu. Orodha ndefu ya kama hii haiwezi kukosa mamluki. Heading inasema waandishi bora 25 Tanzania, lakini mwishoni unamalizia kwa kusema hawa ndio waandishi wenye ushawishi. Uandisho bora na uandishi wenye ushawishi sio lazima viende pamoja. Lakini pia, ukitaka kutenda haki, lazima utenganishe waandishe wa makala, wa taarifa na picha. Wote hawa wapo ktk fani ya habari, lakini majukumu yao ni tofauti kabisa. Unaweza hata ukatenga makundi ya waandishi wa makala za kila siku na kila wiki-hawa kazi zao tofauti na ni watu tofauti kabisa.

Sina shida sana kama hii ni orodha ya waandishi wenye ushawishi (sio lazima awe bora), la sivyo ningeanza kwa kuwatoa Issamichuzi-kwasababu siwezi kuwaweka Ulimwengu na Michuzi kwenye sentensi moja na pia Mjenga Maggid kwasababu ya ushabiki na kuhamisha akili zake kila wakati wa uchaguzi mkuu. Kuna wengi wa kuwatoa kwenye list hiyo..
 
Nimekuwa nafanya uchunguzi kwa mwaka wa 5 sasa juu ya waandishi wa kitanzania wenye ushawishi kwa wananchi, uchunguzi nimeufanya kwenye vyuo vikuu, mikoani, mijini, kwenye nyumba za ibada, vyama vya siasa na vijijini nikishirikiana na team ya watafiti wa maswala ya kisiasa wa chama cha Republican cha Marekani na wafuatao ni waandishi wanaokubalika sana miongoni mwa watanzania tena habari zao zinapendwa sana............
1.Jenerali Ulimwengu( gazeti la Rai zamani na kwa sasa Raia Mwema pia ni mchangiaji kwenye The East African la kenya)
2.Mwanakijiji(Mwanahalisi, Tanzania Daima na mitandaoni)
3.Lula Wa Ndali Mwana Nzela(Raia Mwema)
4.Saed Kubenea(Mwanahalisi)
5.Ansbert Ngurumo(Tanzania Daima)
6.Evarist Chahali(Raia Mwema na www.chahali.com)
7.Ojuku Abraham(Dira kwa sasa)
8.Msomaji Raia(Raia Mwema)
9.Johnson Mbwambo(Raia Mwema)
10.Kondo Tutindaga(Mwanahalisi na Kwanza jamii)
11,Fr Privatus Karugendo(Raia Mwema)
12.Nova Kambota(zamani Dira kwasasa mtandaoni www.novakambota.com)
13.Dismass Lyassa(Mwananchi na mkurugenzi Global Source Watch GSW ubungo)
14.Kinabo(Tanzania Daima)
15.Samson Mwigamba(Tanzania Daima)
16.Fredrick Katulanda(Mwananchi)
17.William Shao(Majira na mwandishi wa "Miaka 2000 ya ukristo historia iliyopotoshwa)
18.Godfrey Dilunga(Raia Mwema)
19.Maggid Mjengwa(Raia Mwema na mtandaoni MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo)
20.Ndimara Tegambwage(Mwanahalisi na mtandaoni uhuru hauna kikomo )
21.Nkwazi Nkwabi(Dira na mtandaoni )
22.Marehemu Adam Lusekelo(Daily News with the light touch na mtandaoni)
23.Freddy Macha(Mwananchi, The Citizen na mtandaoni Freddy Macha)
24.Issa Michuzi(mtandaoni www.issamichuzi.blogspot.com)
25.Bubelwa Bandio(mtangazaji voice of America na mtandaoni "The Way You See The Problem Is The Problem")

HAWA NDIYO WAANDISHI 25 WA KITANZANIA WENYE USHAWISHI MKUBWA SANA KWA WANANCHI NA MWISHO WA UTAFITI WETU TULISHAURI TAASISI MBALIMBALI ZIWATUMIE WATU HAWA KWENYE KUHIMIZA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO MFANO KILIMO KWANZA, ELIMU NA KATIBA MPYA......NI HAYO TU WADAU , IWAPO UNA MAONI USISITE KUNIANDIKIA KWENDA kiwalanikwagude@rocketmaail.com
Wenyeji huwa tunasema "Kwa...gude!!!" hahahahah, umenikumbusha mbali sana!!
 
Hii taarifa nzuri. Lakini mimi hapo naona Waandishi wa Habari wawili tu. Ni Saed Kubenea na Frederick Katulanda. Wengine wote, hakuna anayeandika habari, ila maoni yao, au kuchambua habari zilizokwishaandikwa na wenzao. Hawa ni waandishi wa safu (columnists). Ungewatendea haki kama ungewapambanisha peke yao; na waandishi wa habari (wanaoandika habari), yaani wanaoibua matukio ya kiuchunguzi, kama kubenea na katulanda wakae peke yao. Hao wote waliotajwa, pengine waliwahi kuwa waandishi wa habari lakini mimi sikumbuki kuona wakiibua STORY, yaani jambo jipya, kama kashfa, ufisadi, ubadhirifu, ukiukaji wa maadili, matukio, badala yake nimekuwa nikioni uchambuzi wao mzuri, wenye kuibua fikra za jamii na kuhamasisha mabadiliko, kutokana na habari ambazo zimeshatangazwa/kuandikwa na wenzao. Kumbuka Uchambuzi wa habari unaweza kufanywa na mtu yeyote...na mchambuzi haitaji kuwa mwandishi wa habari, na wengi hako hivyo.

Nawasilisha.
 
yuko wapi meena wa mwananchi????na umetumia vigezo gani kutoa orodha hii?????toa data kamili ili thread yako ieleweke au kwa mujibu wako?????????????
 
Nimekuwa nafanya uchunguzi kwa mwaka wa 5 sasa juu ya waandishi wa kitanzania wenye ushawishi kwa wananchi, uchunguzi nimeufanya kwenye vyuo vikuu, mikoani, mijini, kwenye nyumba za ibada, vyama vya siasa na vijijini nikishirikiana na team ya watafiti wa maswala ya kisiasa wa chama cha Republican cha Marekani na wafuatao ni waandishi wanaokubalika sana miongoni mwa watanzania tena habari zao zinapendwa sana............
1.Jenerali Ulimwengu( gazeti la Rai zamani na kwa sasa Raia Mwema pia ni mchangiaji kwenye The East African la kenya)
2.Mwanakijiji(Mwanahalisi, Tanzania Daima na mitandaoni)
3.Lula Wa Ndali Mwana Nzela(Raia Mwema)
4.Saed Kubenea(Mwanahalisi)
5.Ansbert Ngurumo(Tanzania Daima)
6.Evarist Chahali(Raia Mwema na www.chahali.com)
7.Ojuku Abraham(Dira kwa sasa)
8.Msomaji Raia(Raia Mwema)
9.Johnson Mbwambo(Raia Mwema)
10.Kondo Tutindaga(Mwanahalisi na Kwanza jamii)
11,Fr Privatus Karugendo(Raia Mwema)
12.Nova Kambota(zamani Dira kwasasa mtandaoni www.novakambota.com)
13.Dismass Lyassa(Mwananchi na mkurugenzi Global Source Watch GSW ubungo)
14.Kinabo(Tanzania Daima)
15.Samson Mwigamba(Tanzania Daima)
16.Fredrick Katulanda(Mwananchi)
17.William Shao(Majira na mwandishi wa "Miaka 2000 ya ukristo historia iliyopotoshwa)
18.Godfrey Dilunga(Raia Mwema)
19.Maggid Mjengwa(Raia Mwema na mtandaoni MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo)
20.Ndimara Tegambwage(Mwanahalisi na mtandaoni uhuru hauna kikomo )
21.Nkwazi Nkwabi(Dira na mtandaoni )
22.Marehemu Adam Lusekelo(Daily News with the light touch na mtandaoni)
23.Freddy Macha(Mwananchi, The Citizen na mtandaoni Freddy Macha)
24.Issa Michuzi(mtandaoni www.issamichuzi.blogspot.com)
25.Bubelwa Bandio(mtangazaji voice of America na mtandaoni "The Way You See The Problem Is The Problem")

HAWA NDIYO WAANDISHI 25 WA KITANZANIA WENYE USHAWISHI MKUBWA SANA KWA WANANCHI NA MWISHO WA UTAFITI WETU TULISHAURI TAASISI MBALIMBALI ZIWATUMIE WATU HAWA KWENYE KUHIMIZA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO MFANO KILIMO KWANZA, ELIMU NA KATIBA MPYA......NI HAYO TU WADAU , IWAPO UNA MAONI USISITE KUNIANDIKIA KWENDA kiwalanikwagude@rocketmaail.com

hapo kwenye red angekaa joseph mihangwa, huyu kichwa bwana huwezi mlinganisha na watu kama michuzi na majid mjengwa
 
Pengine si mwafaka sana kwa mie kama mtajwa kwenye orodha hiyo kuchangia chochote kwani inaweza kutafsiriwa kama "mwamba ngoma..."

Hata hivyo,kwa vile mie pia ni mwana-JF,naomba nitoe mawazo yangu binafsi kuhusu post husika.Mwandishi anasema amefanya utafiti wake na kutoa findings za utafiti huo.Kama mwanafunzi wa utafiti,nadhani njia sahihi ya kuukosoa utafiti ni kufanya utafiti mbadala.Mara nyingi tafiti zinapingwa si kwa vile hazina mantiki bali matokeo ya tafiti husika kutoendana na matarajio ya wanayapokea.Lakini ikumbukwe kuwa tafiti nyingi hutokana na tafiti zilizotangulia,aidha kwa nia ya kuziboresha theory zilizoibuliwa kwenye tafiti hizo,au pengine kuzipinga.

Sasa kwa mtazamo wangu,mwana-JF mwenzetu ametoa changamoto,nakama kuna wasioafikiana nae basi pengine it's high time nao wakafanya tafiti mbadala ambazo kwa bahati nzuri zina pa kuanzia i.e. findings za utafiti huu.

Kama nilivyobainisha mwanzoni,chochote nitakachoandika kinaweza kuhusishwa na uwepo wa jina langu katika orodha hiyo.Hata hivyo,pengine wakati tunakosoa ni muhimu kuangalia kwa mapana kuhusu suala la tafiti katika medani ya elimu (hususan ya juu).Moja ya "ugonjwa" unaowakabili wasomi wetu ni kuzipa kipaumbele tafiti zinazoelekezwa na wafadhili kwa vile zina fedha.Mzalendo kama huyo aliyetumia muda wake kutafiti suala ambalo yayumkinika kuamini kuwa halina faida kifedha anaweza kabisa kufungua sura mpaya ya kutafiti masuala mbalimbali yanayolihusu taifa letu badala ya kusubiri fadhila za wafadhili ambao mara nyingi wanaendesha tafiti kwa maslahi yao binafsi au ya taasisi/nchi zilizowatuma.
 
Hapo bila Joseph mihangwa wa Raia mwema na Rai, mtakuwa hamjamtendea haki mi namkubali sana. Anajua mambo mengi sana hasa kwenye siasa,uchumi na kijamii. Nimejua mambo mengi ya zanzibar kupitia kwake (hayo ni maoni yangu)

Mkuu hiyo ni kweli kabisa. Mihangwa anajua mambo mengi tena kwa kina. Akichambua habari za mapinduzi ya Zanzibar utafurahi, akija kwenye Muungano hapo ndio nyumbani kwake, akiongelea siasa za Africa utadhani anaongelea mambo ya nyumani kwake hapa Shinyanga. Kwa kifupi ni mchambuzi mahiri.
 
Kati ya wote uliowataja kuna hata mmoja kachapisha sahihisho kuhusu maandishi yake yoyote?

Indeed, kuna gazeti lenye strip ya masahihisho Tanzania? Na kama hakuna, ina maana magazeti yetu hayakosei?
 
Back
Top Bottom