Salim ni Rais wa tanzania ambaye haikuwa riziki

Hamid Rubawa

Member
May 23, 2018
72
202
SALIM NI RAIS WA TANZANIA AMBAYE HAIKUWA RIZIKI

DOKTA Salim Ahmed Salim, alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kilikuwa kipindi cha uhaba mkubwa wa bidhaa. Nguo, viatu, sabuni, dawa za meno, vilikuwa adimu.

Alikalia kiti baada ya kifo cha Edward Moringe Sikoine, aliyeendesha vita ya uhujumu uchumi. Mazingira ya kufanya biashara yalikuwa magumu. Wafanyabiashara walichepukia magendo. Wengi wakafungwa jela.

“Salim alipokuwa Waziri Mkuu, alifanya ziara nchi nzima, akahoji matatizo ya wananchi. Kila alipokwenda aliambiwa shida ya sabuni, dawa za meno, nguo, viatu na kadhalika. Naye alijibu vyote vingekuja. Baadaye nguo zilianza kupatikana kwa wingi, dawa za meno na sabuni,” alinisimulia mama yangu, Mwenyezi Mungu amrehemu.

Hiyo ndio simulizi ya kila nyumba Tanzania, mwaka 1984, Salim alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Yapo maeneo nchini, watu walivaa magunia. Majani ya papai yakatumika kama mbadala wa sabuni. Katambuga (viatu vitokanavyo na matairi ya magari), vilivaliwa na wenye uwezo.

Salim, kijana pendwa wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, vilevile rafiki kipenzi cha Wachina. Baada ya kujionea adha za wananchi, Salim aliketi na Mwalimu, ambaye ndiye alikuwa Rais. Wakakubaliana, Salim akafunga safari hadi China.

Mahaba ya Wachina kwa Salim yanaanzia mwaka 1969, alipokuwa Balozi wa Tanzania China, kisha yakaimarishwa na siasa za Umoja wa Mataifa, alipokuwa mjumbe wa kudumu UN. Vilevile, Wachina na Mwalimu walikuwa chanda na pete. Ni sababu China kupokea ombi la Salim na wakajibu kwa vitendo mara moja.

“Vitu vitajaa madukani, mtashindwa wenyewe kununua,” mama yangu alinisimulia, akinukuu ahadi ya Salim. Shehena za kanga, nguo za mitumba, viatu, sabuni, dawa za meno, vilimiminika Tanzania kutoka China. Salim alitatua kero kubwa ndani ya muda mfupi.

Hata sasa, unapoona biashara ya mitumba inashamiri, tambua asili yake ni Salim. Unaposhuhudia uhusiano wa kibiashara baina ya Tanzania na China umekuwa mkubwa, mwanzo wake ni Salim. Msingi aliouweka alipokuwa Waziri Mkuu kwa mwaka mmoja tu.

Ni jaribio la kujenga picha halisi kuhusu Salim, kipindi hiki ambacho imezinduliwa makumbusho maalum ya kidigitali kuhusu maisha ya Salim, hususan ya kikazi, kwenye tovuti ya www.salimahmedsalim.com.

MAKUMBUSHO YAMECHELEWA

Kwa kila shule Tanzania miaka ya 1980 na 1990, jina la Salim lilifundishwa na kutajwa kwa fahari kubwa. Wanafunzi walisoma na kujivunia kuchangia uraia na mwanadiplomasia mwenye sifa nyingi za kipekee.

Salim, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) kwa miaka 12, jina lake lilifundishwa kila shule Afrika. Jarida la Africa Events, toleo la Septemba 1989, lilipambwa na sura ya Salim, kichwa cha habari kikiwa “Salim Ahmed Salim; Africa’s Superson” – “Salim Ahmed Salim; Mtoto Bora wa Afrika.”

Mei 23, 2014, Rais wa Pili wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, alipokuwa akimwelezea Salim kama mgeni rasmi wa Kongamano la Tano la Thabo Mbeki la Siku ya Uhadhiri, alisema, watu wote wangetamani kuwa kama Salim, kwa aliyoyafanya katika utumishi wake.

Mbeki alisema, maneno “tunajivunia kuwa Waafrika”, yamesababishwa na watu aina ya Salim. Alifafanua kwamba hakuna atakayeisema Afrika vibaya, kama hoja yake ataijenga kupitia mambo ambayo Salim ameyafanya kwa Afrika.

Alieleza kuwa alipokuwa Rais wa Afrika Kusini, asingepokea balozi nchini kwake mwenye umri wa miaka 22, maana ingekuwa sawa na kumkubali mtoto awakilishe nchi yake.

Mbeki alisema, mtazamo wake unakosolewa na Salim, kwani aliteuliwa kuwa balozi akiwa na umri wa miaka 22 na alifanya kazi kubwa, nzuri na yenye kutukuka.

Salim alipokuwa na umri wa miaka 22, aliaminiwa na Mwalimu Nyerere pamoja na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume, akateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri.

Kabla ya hapo, Salim alipokuwa na umri wa miaka 19, alikuwa Naibu Mwakilishi wa Zanzibar, Havana, Cuba. Ofisi hiyo madhumuni yake yalikuwa kujenga ushawishi wa kimataifa, kuisaidia Zanzibar kupata uhuru.

Salim, mwandishi wa habari na mhariri wa gazeti la kila siku Zanzibar, akiwa na umri wa miaka 20. Salim, Katibu Mkuu wa Umoja wa Waandishi wa Habari Zanzibar, alipokuwa na umri wa miaka 21.

Salim, kijana mwenye akili nyingi, aliyekatisha masomo baada ya kumaliza kidato cha nne, akiwa na umri wa miaka 16, akajiunga na harakati za kisiasa za kusaka uhuru Zanzibar.

Salim, mwanachama na kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP), mwenye umri mdogo zaidi. Alishiriki kuasisi Umma Party akiwa na umri wa miaka 17.

Salim, mwaka 1965, alipoteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini India, alianza kusoma akiwa kazini. Alipata shahada ya awali, kisha uzamili, baadaye uzamivu (PhD). Ndio maana ni Dk Salim Ahmed Salim.

Salim, Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 1976. Rais wa Mkutano wa Mkuu wa Umoja wa Mataifa (Unga) mwaka 1979. Vilevile aliongoza kamati nyingi za UN kipindi alipokuwa Mjumbe wa Kudumu wa Tanzania mwenye Umoja wa Mataifa.

Mwaka 1981, alikaribia kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Salim aliingia kwenye kinyang'anyiro dhidi ya aliyekuwa Katibu Mkuu kwa vipindi viwili, Kurt Waldheim wa Austria. Hata hivyo, aliyekuwa Rais wa Marekani, Ronald Reagan, alimpinga Salim kwa Veto.

Salim, aliongoza duru ya kwanza ya uchaguzi kwa kura 11 dhidi ya 10 za Waldheim. Reagan aliinua Veto kwa hoja kuwa Salim alikuwa na msimamo mkali dhidi ya sera za Marekani, alitetea uhuru wa Palestina na alipinga serikali ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Umoja wa Nchi za Soviet (USSR), hawakuinua Veto, ila walimpinga Salim kwa kuwa alikuwa mtu wa China zaidi. Hiyo ni sababu ya Salim kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha ukatibu mkuu UN. Javier de Cuellar wa Peru, alishinda kiulaini baada ya Salim kugomewa na Marekani.

Mwaka 1996, Marekani chini ya Rais Bill Clinton, walitoa pendekezo la kumuunga mkono Salim awe Katibu Mkuu UN, baada ya kutoridhishwa na uongozi wa muhula mmoja wa Mmisri Boutros Boutros-Ghali. Hata hivyo, Ufaransa iliweka dhamira ya kumuinulia Veto Salim. Kofi Anna wa Ghana, alishinda.

Huo ni muhtasari kuwa makumbusho ya Salim yamechelewa. Kuna kundi kubwa la vijana na hata watu wazima, limechelewa kupata mahali pa kupata elimu na taarifa sahihi kuhusu Salim. Angalau sasa, ipo chaneli ya kumsoma na kumwelewa kiundani, gwiji Salim.

Salim, mwanamajumui kindakindaki wa Afrika, ameshiriki na kuongoza harakati nyingi za ukombozi wa nchi za Afrika kutoka kwenye makucha ya wakoloni. Ndio maana Salim ni jina ambalo limefundishwa kwenye shule za kila nchi Afrika.

MAKUMBUSHO HAYAKIDHI

Salim ni Rais wa Tanzania ambaye Watanzania hawakupata bahati ya kumwona kwenye karatasi za kupigia kura ili wamchague. Ni kwa bahati hiyo mbaya, Salim ni Rais ambaye hakufanikiwa kula kiapo wala kukalia kiti cha urais.

Mwalimu Nyerere alimpenda Salim na alikusudia kumwachia kiti, alipokuwa anang’atuka mwaka 1985. Hayo yamefafanuliwa na Rais wa Tatu, Benjamin Mkapa, katika kitabu chake “My Life, My Purpose” – “Maisha Yangu, Kusudi Langu.”

Rais wa Pili, Ali Hassan Mwinyi, katika kitabu chake “Mzee Rukhsa; Safari ya Maisha Yangu”, naye amesimulia kuwa dhamira ya Mwalimu Nyerere, ilikuwa kumrithisha kiti cha urais Salim.

Mwinyi ameingia ndani zaidi kwa kueleza (kwa masikitiko) kuwa wazee wa Zanzibar walimtuhumu vibaya Salim, bila ushahidi kuwa ndiye aliyemuua Rais Karume mwaka 1972, vilevile huwa hasemi maneno “Mapinduzi Daima”.

Ukimsoma Mwinyi, anapinga waziwazi Salim kuhusika na kifo cha Karume. Ameandika kwamba ingekuwa kweli, Mwalimu Nyerere angejua na asingempendekeza kuwa mrithi wa kiti cha urais.

Mwinyi ameandika kwenye kitabu, kama ilivyosimuliwa na Spika wa Bunge mstaafu, Pius Msekwa, kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM (Nec), walimpitisha Mwinyi kwa hoja ya uandamizi. Mwinyi alikuwa Makamu wa Rais na Makamu Mwenyekiti wa chama, Salim alikuwa Waziri Mkuu.

Msisitizo wa Mwinyi ni kuwa Mwalimu aliamua kuruhusu demokrasia ichukue mkondo, kwani angeamua kushinikiza chaguo lake, hakuna ambaye angemzuia. Hivyo, Salim hajawa Rais wa Tanzania kwa sababu ya utii wa kidemokrasia aliokuwa nao Mwalimu.

Sifa za Salim ni nyingi. Ukipitia makumbusho yake ya kidigitali, huwezi kupata majibu wala hisia zake kuhusu alivyokaribia kuwa Rais wa Tanzania mwaka 1985, ila akapigwa vita na Wazanzibari wenzake.

Hakuna maelezo wala hisia za Salim kuhusu tuhuma dhidi yake za muda mrefu, kwamba ndiye alimuua Karume. Na kwa nini alitajwa yeye? Karume aliuawa kwa kupigwa risasi kipindi Salim akiwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Umoja wa Mataifa. Ofisini kwake ni New York, Marekani.

Iweje, tukio la Karume kupigwa risasi, litokee Kisiwandui, Zanzibar, ahusishwe yeye? Karume alimwamini Salim katika umri mdogo kabisa. Ukiacha siasa za kugombea uhuru wa Zanzibar, je, Salim alipata kupishana popote na mzee wake huyo?

Viulizo hivyo vinaleta hoja kuwa kauli ya Salim kuhusu Karume na kifo chake, ingeweza kukidhi mahitaji ya muda mrefu. Wauaji walifahamika na walikamatwa. Iweje Kwa miaka 51, tuhuma ziwe kwa Salim?

Tuje tena urais wa Tanzania mwaka 1995. Mkapa amesimulia kwenye My Life, My Purpose, kuwa Mwalimu Nyerere alimtaka Salim awe Rais baada ya Mwinyi lakini akawa anasita.

Rais wa Nne, Jakaya Kikwete, alipata kusimulia alipokuwa Chuo Kikuu cha New York, Africa House, kuwa mwaka 1995, aliitwa na Mwalimu Nyerere, akamtaka waunde timu ya pamoja ya kumshawishi Salim agombee urais.

Kitendo cha Salim kutokutokeza kugombea urais mwaka 1995, kinathibitisha kuwa Mwalimu Nyerere na Kikwete walifeli kumshawishi. Inaelezwa kwamba Salim alihofia ya mwaka 1985, akaona angeweza kuacha kazi OAU, kisha urais nao akaukosa.

Kwa nini hakutokeza mwaka 1995, pamoja na Mwalimu Nyerere kumtuma Kikwete akamshawishi? Hili ni eneo ambalo vema lisimuliwe kinagaubaga na Salim mwenyewe, halafu maelezo yake yasikosekane kwenye makumbusho yake.

Kisha, kuna Uchaguzi Mkuu 2005, uliotawaliwa na vitimbi vingi. Propaganda za kila aina ziliibuliwa kumwelekea Salim. Ya kuitwa Hizbu, vilevile kuambiwa ndiye alimuua Karume.

Jina lake halikupita CCM, kilichomuuma sio kukosa urais, bali jinsi heshima yake ilivyochafuliwa. Alipata kusema: “Nimegundua kugombea urais Tanzania ni aina nyingine ya kujivunjia heshima.”

Salim ni mtoto bora wa Tanzania na Afrika. Ni Rais wa Tanzania aliyeaminiwa na Mwalimu Nyerere, vilevile Watanzania wengi waliamini ingefika siku, Salim angekula kiapo kuongoza dola yao. Hata hivyo, haikuwezekana. Kwa mtazamo wa kiimani, tunasema haikuwa riziki.

Makumbusho maalum kuhusu maisha ya Salim ni jambo jema mno, ila nyaraka zilizopo hazijakidhi maswali muhimu. Bado kitabu cha Salim chenye majibu ya maswali yote hasa urais na kifo cha Karume, kinahitajika.

Vyotevyote unavyoweza kutafsiri, Salim ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye haikuwa riziki. Hakuna mfanowe katika nyanya ya diplomasia Tanzania. Salim ni historia ya Afrika. Salim ni moja ya zawadi za thamani isiyopimika kwa Tanzania.

Mwaka 2020 nikiwa Pemba, nilikutana na mwalimu mstaafu, Khamis Mhidini Vuai. Ni rafiki wa zamani wa Salim. Walisoma wote Shule ya Msingi Uweleni, Pemba. Khamis na Salim, ni wanafunzi pekee wa Uweleni, waliofaulu kwenda kidato cha kwanza Shule ya Sekondari ya King George, Unguja.

“Wazazi wangu hawakuwa na uwezo, nilishindwa kuripoti shule kwa ajili ya masomo ya sekondari. Salim baba yake alikuwa na uwezo, lakini aligoma kwenda shule. Alimshinikiza baba yake anilipie na mimi ili tukaripoti shule pamoja. Ilibidi Mzee Ahmed (baba yake Salim), anilipie,” alisema Khamis.

Salim ni rafiki mwema sana. Ndivyo alisema Khamis. Maneno yake yanasadifu ushuhuda wa wengi kuwa Salim ni muungwana, mwenye utu, mkarimu lakini daima misimamo yake ni thabiti.

Ndimi Luqman MALOTO
FB_IMG_1696071004680.jpg
 
Viongozi Kama Salim hamna Tena. Siku hizi anateuliwa kuwa mbunge (siku hizi hawachaguliwi) tayari anajiita Dokta. Salim Ni Dk halali kabisa na Ni nadra kusikia akipenda aitwe Dokta au MHESHIMIWA halafu haringi.
Kuna Bumunda fulani lilipata ubunge wa michongo. Siku moja tumekutana break point Kino akategemea nimuite MHESHIMIWA, Mimi nikasema hili Bumunda siwezi kuliita MHESHIMIWA japo Ni naibu wazr. Kaagiza Hennessy mie castle lite kila mtu akajilipia.
 
Ndimi Luqman MALOTOView attachment 2774086
Tupeni na kisa Cha Major Zongo kule Addis,ilikuwaje?
 
Back
Top Bottom