Dkt. Salim Ahmed Salim ni Rais wa Tanzania ambaye haikuwa riziki

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
324
909
DOKTA Salim Ahmed Salim, alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kilikuwa kipindi cha uhaba mkubwa wa bidhaa. Nguo, viatu, sabuni, dawa za meno, vilikuwa adimu.

Alikalia kiti baada ya kifo cha Edward Moringe Sikoine, aliyeendesha vita ya uhujumu uchumi. Mazingira ya kufanya biashara yalikuwa magumu. Wafanyabiashara walichepukia magendo. Wengi wakafungwa jela.

“Salim alipokuwa Waziri Mkuu, alifanya ziara nchi nzima, akahoji matatizo ya wananchi. Kila alipokwenda aliambiwa shida ya sabuni, dawa za meno, nguo, viatu na kadhalika. Naye alijibu vyote vingekuja. Baadaye nguo zilianza kupatikana kwa wingi, dawa za meno na sabuni,” alinisimulia mama yangu, Mwenyezi Mungu amrehemu.

Hiyo ndio simulizi ya kila nyumba Tanzania, mwaka 1984, Salim alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Yapo maeneo nchini, watu walivaa magunia. Majani ya papai yakatumika kama mbadala wa sabuni. Katambuga (viatu vitokanavyo na matairi ya magari), vilivaliwa na wenye uwezo.

Salim, kijana pendwa wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, vilevile rafiki kipenzi cha Wachina. Baada ya kujionea adha za wananchi, Salim aliketi na Mwalimu, ambaye ndiye alikuwa Rais. Wakakubaliana, Salim akafunga safari hadi China.

Mahaba ya Wachina kwa Salim yanaanzia mwaka 1969, alipokuwa Balozi wa Tanzania China, kisha yakaimarishwa na siasa za Umoja wa Mataifa, alipokuwa mjumbe wa kudumu UN. Vilevile, Wachina na Mwalimu walikuwa chanda na pete. Ni sababu China kupokea ombi la Salim na wakajibu kwa vitendo mara moja.

“Vitu vitajaa madukani, mtashindwa wenyewe kununua,” mama yangu alinisimulia, akinukuu ahadi ya Salim. Shehena za kanga, nguo za mitumba, viatu, sabuni, dawa za meno, vilimiminika Tanzania kutoka China. Salim alitatua kero kubwa ndani ya muda mfupi.

Hata sasa, unapoona biashara ya mitumba inashamiri, tambua asili yake ni Salim. Unaposhuhudia uhusiano wa kibiashara baina ya Tanzania na China umekuwa mkubwa, mwanzo wake ni Salim. Msingi aliouweka alipokuwa Waziri Mkuu kwa mwaka mmoja tu.

Ni jaribio la kujenga picha halisi kuhusu Salim, kipindi hiki ambacho imezinduliwa makumbusho maalum ya kidigitali kuhusu maisha ya Salim, hususan ya kikazi, kwenye tovuti ya www.salimahmedsalim.com.

MAKUMBUSHO YAMECHELEWA

Kwa kila shule Tanzania miaka ya 1980 na 1990, jina la Salim lilifundishwa na kutajwa kwa fahari kubwa. Wanafunzi walisoma na kujivunia kuchangia uraia na mwanadiplomasia mwenye sifa nyingi za kipekee.

Salim, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) kwa miaka 12, jina lake lilifundishwa kila shule Afrika. Jarida la Africa Events, toleo la Septemba 1989, lilipambwa na sura ya Salim, kichwa cha habari kikiwa “Salim Ahmed Salim; Africa’s Superson” – “Salim Ahmed Salim; Mtoto Bora wa Afrika.”

Mei 23, 2014, Rais wa Pili wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, alipokuwa akimwelezea Salim kama mgeni rasmi wa Kongamano la Tano la Thabo Mbeki la Siku ya Uhadhiri, alisema, watu wote wangetamani kuwa kama Salim, kwa aliyoyafanya katika utumishi wake.

Mbeki alisema, maneno “tunajivunia kuwa Waafrika”, yamesababishwa na watu aina ya Salim. Alifafanua kwamba hakuna atakayeisema Afrika vibaya, kama hoja yake ataijenga kupitia mambo ambayo Salim ameyafanya kwa Afrika.

Alieleza kuwa alipokuwa Rais wa Afrika Kusini, asingepokea balozi nchini kwake mwenye umri wa miaka 22, maana ingekuwa sawa na kumkubali mtoto awakilishe nchi yake.

Mbeki alisema, mtazamo wake unakosolewa na Salim, kwani aliteuliwa kuwa balozi akiwa na umri wa miaka 22 na alifanya kazi kubwa, nzuri na yenye kutukuka.

Salim alipokuwa na umri wa miaka 22, aliaminiwa na Mwalimu Nyerere pamoja na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume, akateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri.

Kabla ya hapo, Salim alipokuwa na umri wa miaka 19, alikuwa Naibu Mwakilishi wa Zanzibar, Havana, Cuba. Ofisi hiyo madhumuni yake yalikuwa kujenga ushawishi wa kimataifa, kuisaidia Zanzibar kupata uhuru.

Salim, mwandishi wa habari na mhariri wa gazeti la kila siku Zanzibar, akiwa na umri wa miaka 20. Salim, Katibu Mkuu wa Umoja wa Waandishi wa Habari Zanzibar, alipokuwa na umri wa miaka 21.

Salim, kijana mwenye akili nyingi, aliyekatisha masomo baada ya kumaliza kidato cha nne, akiwa na umri wa miaka 16, akajiunga na harakati za kisiasa za kusaka uhuru Zanzibar.

Salim, mwanachama na kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP), mwenye umri mdogo zaidi. Alishiriki kuasisi Umma Party akiwa na umri wa miaka 17.

Salim, mwaka 1965, alipoteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini India, alianza kusoma akiwa kazini. Alipata shahada ya awali, kisha uzamili, baadaye uzamivu (PhD). Ndio maana ni Dk Salim Ahmed Salim.

Salim, Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 1976. Rais wa Mkutano wa Mkuu wa Umoja wa Mataifa (Unga) mwaka 1979. Vilevile aliongoza kamati nyingi za UN kipindi alipokuwa Mjumbe wa Kudumu wa Tanzania mwenye Umoja wa Mataifa.

Mwaka 1981, alikaribia kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Salim aliingia kwenye kinyang'anyiro dhidi ya aliyekuwa Katibu Mkuu kwa vipindi viwili, Kurt Waldheim wa Austria. Hata hivyo, aliyekuwa Rais wa Marekani, Ronald Reagan, alimpinga Salim kwa Veto.

Salim, aliongoza duru ya kwanza ya uchaguzi kwa kura 11 dhidi ya 10 za Waldheim. Reagan aliinua Veto kwa hoja kuwa Salim alikuwa na msimamo mkali dhidi ya sera za Marekani, alitetea uhuru wa Palestina na alipinga serikali ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Umoja wa Nchi za Soviet (USSR), hawakuinua Veto, ila walimpinga Salim kwa kuwa alikuwa mtu wa China zaidi. Hiyo ni sababu ya Salim kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha ukatibu mkuu UN. Javier de Cuellar wa Peru, alishinda kiulaini baada ya Salim kugomewa na Marekani.

Mwaka 1996, Marekani chini ya Rais Bill Clinton, walitoa pendekezo la kumuunga mkono Salim awe Katibu Mkuu UN, baada ya kutoridhishwa na uongozi wa muhula mmoja wa Mmisri Boutros Boutros-Ghali. Hata hivyo, Ufaransa iliweka dhamira ya kumuinulia Veto Salim. Kofi Anna wa Ghana, alishinda.

Huo ni muhtasari kuwa makumbusho ya Salim yamechelewa. Kuna kundi kubwa la vijana na hata watu wazima, limechelewa kupata mahali pa kupata elimu na taarifa sahihi kuhusu Salim. Angalau sasa, ipo chaneli ya kumsoma na kumwelewa kiundani, gwiji Salim.

Salim, mwanamajumui kindakindaki wa Afrika, ameshiriki na kuongoza harakati nyingi za ukombozi wa nchi za Afrika kutoka kwenye makucha ya wakoloni. Ndio maana Salim ni jina ambalo limefundishwa kwenye shule za kila nchi Afrika.

MAKUMBUSHO HAYAKIDHI

Salim ni Rais wa Tanzania ambaye Watanzania hawakupata bahati ya kumwona kwenye karatasi za kupigia kura ili wamchague. Ni kwa bahati hiyo mbaya, Salim ni Rais ambaye hakufanikiwa kula kiapo wala kukalia kiti cha urais.

Mwalimu Nyerere alimpenda Salim na alikusudia kumwachia kiti, alipokuwa anang’atuka mwaka 1985. Hayo yamefafanuliwa na Rais wa Tatu, Benjamin Mkapa, katika kitabu chake “My Life, My Purpose” – “Maisha Yangu, Kusudi Langu.”

Rais wa Pili, Ali Hassan Mwinyi, katika kitabu chake “Mzee Rukhsa; Safari ya Maisha Yangu”, naye amesimulia kuwa dhamira ya Mwalimu Nyerere, ilikuwa kumrithisha kiti cha urais Salim.

Mwinyi ameingia ndani zaidi kwa kueleza (kwa masikitiko) kuwa wazee wa Zanzibar walimtuhumu vibaya Salim, bila ushahidi kuwa ndiye aliyemuua Rais Karume mwaka 1972, vilevile huwa hasemi maneno “Mapinduzi Daima”.

Ukimsoma Mwinyi, anapinga waziwazi Salim kuhusika na kifo cha Karume. Ameandika kwamba ingekuwa kweli, Mwalimu Nyerere angejua na asingempendekeza kuwa mrithi wa kiti cha urais.

Mwinyi ameandika kwenye kitabu, kama ilivyosimuliwa na Spika wa Bunge mstaafu, Pius Msekwa, kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM (Nec), walimpitisha Mwinyi kwa hoja ya uandamizi. Mwinyi alikuwa Makamu wa Rais na Makamu Mwenyekiti wa chama, Salim alikuwa Waziri Mkuu.

Msisitizo wa Mwinyi ni kuwa Mwalimu aliamua kuruhusu demokrasia ichukue mkondo, kwani angeamua kushinikiza chaguo lake, hakuna ambaye angemzuia. Hivyo, Salim hajawa Rais wa Tanzania kwa sababu ya utii wa kidemokrasia aliokuwa nao Mwalimu.

Sifa za Salim ni nyingi. Ukipitia makumbusho yake ya kidigitali, huwezi kupata majibu wala hisia zake kuhusu alivyokaribia kuwa Rais wa Tanzania mwaka 1985, ila akapigwa vita na Wazanzibari wenzake.

Hakuna maelezo wala hisia za Salim kuhusu tuhuma dhidi yake za muda mrefu, kwamba ndiye alimuua Karume. Na kwa nini alitajwa yeye? Karume aliuawa kwa kupigwa risasi kipindi Salim akiwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Umoja wa Mataifa. Ofisini kwake ni New York, Marekani.

Iweje, tukio la Karume kupigwa risasi, litokee Kisiwandui, Zanzibar, ahusishwe yeye? Karume alimwamini Salim katika umri mdogo kabisa. Ukiacha siasa za kugombea uhuru wa Zanzibar, je, Salim alipata kupishana popote na mzee wake huyo?

Viulizo hivyo vinaleta hoja kuwa kauli ya Salim kuhusu Karume na kifo chake, ingeweza kukidhi mahitaji ya muda mrefu. Wauaji walifahamika na walikamatwa. Iweje Kwa miaka 51, tuhuma ziwe kwa Salim?

Tuje tena urais wa Tanzania mwaka 1995. Mkapa amesimulia kwenye My Life, My Purpose, kuwa Mwalimu Nyerere alimtaka Salim awe Rais baada ya Mwinyi lakini akawa anasita.

Rais wa Nne, Jakaya Kikwete, alipata kusimulia alipokuwa Chuo Kikuu cha New York, Africa House, kuwa mwaka 1995, aliitwa na Mwalimu Nyerere, akamtaka waunde timu ya pamoja ya kumshawishi Salim agombee urais.

Kitendo cha Salim kutokutokeza kugombea urais mwaka 1995, kinathibitisha kuwa Mwalimu Nyerere na Kikwete walifeli kumshawishi. Inaelezwa kwamba Salim alihofia ya mwaka 1985, akaona angeweza kuacha kazi OAU, kisha urais nao akaukosa.

Kwa nini hakutokeza mwaka 1995, pamoja na Mwalimu Nyerere kumtuma Kikwete akamshawishi? Hili ni eneo ambalo vema lisimuliwe kinagaubaga na Salim mwenyewe, halafu maelezo yake yasikosekane kwenye makumbusho yake.

Kisha, kuna Uchaguzi Mkuu 2005, uliotawaliwa na vitimbi vingi. Propaganda za kila aina ziliibuliwa kumwelekea Salim. Ya kuitwa Hizbu, vilevile kuambiwa ndiye alimuua Karume.

Jina lake halikupita CCM, kilichomuuma sio kukosa urais, bali jinsi heshima yake ilivyochafuliwa. Alipata kusema: “Nimegundua kugombea urais Tanzania ni aina nyingine ya kujivunjia heshima.”

Salim ni mtoto bora wa Tanzania na Afrika. Ni Rais wa Tanzania aliyeaminiwa na Mwalimu Nyerere, vilevile Watanzania wengi waliamini ingefika siku, Salim angekula kiapo kuongoza dola yao. Hata hivyo, haikuwezekana. Kwa mtazamo wa kiimani, tunasema haikuwa riziki.

Makumbusho maalum kuhusu maisha ya Salim ni jambo jema mno, ila nyaraka zilizopo hazijakidhi maswali muhimu. Bado kitabu cha Salim chenye majibu ya maswali yote hasa urais na kifo cha Karume, kinahitajika.

Vyotevyote unavyoweza kutafsiri, Salim ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye haikuwa riziki. Hakuna mfanowe katika nyanya ya diplomasia Tanzania. Salim ni historia ya Afrika. Salim ni moja ya zawadi za thamani isiyopimika kwa Tanzania.

Mwaka 2020 nikiwa Pemba, nilikutana na mwalimu mstaafu, Khamis Mhidini Vuai. Ni rafiki wa zamani wa Salim. Walisoma wote Shule ya Msingi Uweleni, Pemba. Khamis na Salim, ni wanafunzi pekee wa Uweleni, waliofaulu kwenda kidato cha kwanza Shule ya Sekondari ya King George, Unguja.

“Wazazi wangu hawakuwa na uwezo, nilishindwa kuripoti shule kwa ajili ya masomo ya sekondari. Salim baba yake alikuwa na uwezo, lakini aligoma kwenda shule. Alimshinikiza baba yake anilipie na mimi ili tukaripoti shule pamoja. Ilibidi Mzee Ahmed (baba yake Salim), anilipie,” alisema Khamis.

Salim ni rafiki mwema sana. Ndivyo alisema Khamis. Maneno yake yanasadifu ushuhuda wa wengi kuwa Salim ni muungwana, mwenye utu, mkarimu lakini daima misimamo yake ni thabiti.
 
Attachments

  • download (4).jpeg
    download (4).jpeg
    9.8 KB · Views: 5

Shida ni majungu na fitina.
Kuna watu wamesomea kufitini wenzao hadi kuwaharibia.

Hakuna ambaye alikuwa hajua uwezo mkubwa alio kuwa nao dkt Salim lakini kuna kikundi cha watu ambao ni weledi wa kupiga majungu na fitina Kisha kupoteza kabisa ndoto zake.

Kinacho itesa Tanzania hadi leo hii ni majungu na fitina na hivyo kupelekea watu wenye uwezo mkubwa kupoteza nafasi.

Ushauri kwa viongozi wote kwenye idara mbalimbali za Serikali mnapaswa muwe na uwezo wa kuchuja majungu na ukweli ili tusiwapoteze watu makini na wenye uwezo mkubwa.
 
Nashauri uchunguzi ufanyike kuhusu hii mechi kwani staki kuamini kuwa iliocheza ndio Yanga hii ya sasa. Timu kubwa kufungwa na timu ndogo, sio jambo la ajabu kwani mpira ni mchezo wa makosa na hivyo mkubwa ukifanya kosa, basi unaweza adhibiwa na ukapoteza mchezo.
 
Makumbusho yamechelewa Ili kuongeza siku zake za kuishi huyu mwanadiplomasia nguli!!

Kikawaida hapa Bongo ukiona uzinduzi wa kitabu au kumbu kumbu za kiongozi fulani ujue siku zake zinahesabika!

Mkapa,Mengi ni mifano mizuri kabisa!!!
 
Shida ni majungu na fitina.
Kuna watu wamesomea kufitini wenzao hadi kuwaharibia.

Hakuna ambaye alikuwa hajua uwezo mkubwa alio kuwa nao dkt Salim lakini kuna kikundi cha watu ambao ni weledi wa kupiga majungu na fitina Kisha kupoteza kabisa ndoto zake.

Kinacho itesa Tanzania hadi leo hii ni majungu na fitina na hivyo kupelekea watu wenye uwezo mkubwa kupoteza nafasi.

Ushauri kwa viongozi wote kwenye idara mbalimbali za Serikali mnapaswa muwe na uwezo wa kuchuja majungu na ukweli ili tusiwapoteze watu makini na wenye uwezo mkubwa.
Huyu Kuna Mambo kadhaa yaliyomuangusha tangu 1985 Nyerere akiwa hai
1.Alikuwa Mpemba mwenye Asili ya kiarabu hivyo alikuwa tishio kwa waunguja ambao ndiyo walikuwa wanamapinduzi halisi.

2.Alihusishwa na Chama Cha hizbu na siyo asp hivyo kilirudisha kumbukumbu nyuma kuhusu kifo Cha karume 1972 hivyo waasisi na Viongozi wa Mapinduzi hawakutaka apate nafasi hiyo abadani

3.Wanamtandao 2005 waliendeleza kile kilichoanza 1985 na inasemekana bado nguvu na shinikizo bado lilikuwepo kutoka Unguja kwa wale wanamapinduzi

4.wivu na roho mbaya dhidi yake kutokana na kuwa cv kubwq tangu akiwa na umri mdogo wa miaka 18 Nyerere alimteua kuwa balozi hivyo Kuna Watu hawakupenda.

5.Marekani nayo inahusishwa kucheza faulo baada ya kuisaidia china kupata nafasi ya kudumu alipokuwa mjumbe wa umoja wa mataifa.

6.Uislamu na Chama chake Cha awali Cha hezbu nayo ilikuwa kikwazo.
 
Makumbusho yamechelewa Ili kuongeza siku zake za kuishi huyu mwanadiplomasia nguli!!

Kikawaida hapa Bongo ukiona uzinduzi wa kitabu au kumbu kumbu za kiongozi fulani ujue siku zake zinahesabika!

Mkapa,Mengi ni mifano mizuri kabisa!!!
Hapana Mkuu mbona Mwinyi bado anadunda tangu 2021 alipozindua chake?
 
Shida ni majungu na fitina.
Kuna watu wamesomea kufitini wenzao hadi kuwaharibia.

Hakuna ambaye alikuwa hajua uwezo mkubwa alio kuwa nao dkt Salim lakini kuna kikundi cha watu ambao ni weledi wa kupiga majungu na fitina Kisha kupoteza kabisa ndoto zake.

Kinacho itesa Tanzania hadi leo hii ni majungu na fitina na hivyo kupelekea watu wenye uwezo mkubwa kupoteza nafasi.

Ushauri kwa viongozi wote kwenye idara mbalimbali za Serikali mnapaswa muwe na uwezo wa kuchuja majungu na ukweli ili tusiwapoteze watu makini na wenye uwezo mkubwa.
Mkuu Dunia ya sasa inateswa na ubinafsi, hakuna anae mfikiria mwingine.
Kwenye idara wamewekwa watu wanao Linda maslahi ya wakubwa kwahiyo usiote hili ulilo sema kutokea
 
Nyerere alizungukwa na watu wanafiki, azimio la Arusha ilikuwa dira ya uchumi wa Tanzania na Kama lingetekelezwa Leo hii Tanzania ingekuwa inashindana na zile nchi za Asia zinazoitwa tiger of economic. Azimio la Arusha kulikuwa na sehemu kuu mbili maadili ya viongozi na umiliki wa njia kuu za uchumi. Viongozi wengi ama kwa kujifanya watiifu kwa Nyerere au kutolielewa azimio la Arusha waliziua watu kufanya hata zile biashara ambazo hazikuhusiana na azimio la Arusha Kama stationary, maduka makubwa zinazofanana na hizo. Sokoine na Dr. Salim ni viongozi wachache wenye uthubutu na kuruhusu watu binafsi waanze kumiliki biashara. Sokoine aliruhusu daladala baada ya UDA kuzidiwa uwezo na kuwa na tatizo kubwa la usafiri. Dr. Salim aliruhusu biashara ya mitumba kwa sababu viwanda vya nguo vilishindwa kuzalisha na kuzalisha nguo kukidhi nahitaji ya wananchi.
Kuhusu urais Nyerere alitaka Dr. Salim achukue nafasi take lakini siasa mbovu za ubaguzi Zanzibar za upemba na unguja pia baadhi waafidhina walioona wivu wa kuingizwa na kijana mdogo ndio waliozima ndoto zake za kuchaguliwa rais. Getrude Mongela na aliyekuja kuwa waziri wa mawasiliano akanunua kivuko kibovu na baadae akateuliwa balozi wa kudumu umoja wa Mataifa Mustapha Nyang'anyi waliongoza kampeni ya kumzuia Dr. Salim asipitishwe kuwa rais. Mongela alimkabili Nyerere na kumwuliza ataiambia Nini dunia Kama anamwacha makamu wake na kuchagua mtu mwingine awe rais, Ina maana alimweka makamu wake Kama boya.
Nyerere pamoja na kukubali maamuzi ya chama chake alimpigia Mwinyi kampeni ili achaguliwe, lakini Mwinyi alipovurunda Nyerere alisema hadharani hakuwa chaguo lake.
Mwaka 1995 Nyerere alitaka Tena aje kugombea urais lakini alisita sababu rais aliyepita alitoka Zanzibar pia alikuwa katikati ya ajira take ya.katibu mkuu was OAU.
Mwaka 2005 alipoamua kugombea siasa za Zanzibar, mtandao na hofu ya viongozi wengi wa CCM ambao walikuwa wamejiingiza kwenye ufisadi na Dr. Salim hakuwa miongoni mwao hivyo waliamua kumtosa Tena kwa kumwita Fisadi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom