Vurugu Mwanza: Wamachinga Vs. Jiji - Damu yamwagika

MWANZA LEO
attachment.php
 
RAI YANGU:

Mh.Wenje ahirisha bunge la leo wapigakura wako huku wanakufa wakitetea mkate wao. Mh.Kikwete muondoe huyu mkurugenzi W.Kabwe.[/QUOTE]

kwa hiyo akiahirisha afanye nini? ajifungie hotelini hapo dodoma ili asipigwe mabomu?
na akiahirisha kikao cha leo itasaidia nini? waliopigwa na kujeruhiwa watapoa maumivu yao? ama waliokwishauwawa watafufuka?
AMA UNATAKA AHAIRISHE KIKAO CHA BUNGE LA LEO ILI AJE MWANZA....??? Na akija mwanza ataafanya nini? ama naye aje apigwe mabomu kama
wapiga kura WAKE...??

Nini mantiki yako ya kumtaka aahirishe kikao cha BUNGE.....?

FIMBO YA MBALI.......!!!!
 
Kama imelazimu, silaha za moto zitatumika. Hilo ni jambo la kawaida.Muhimu ni kulinda amani ya walio wengi dhidi ya wakorofi wachache.Tuwaunge mkono vyombo vya usalama kwa usalama wetu, si kulaumu kwa haja potofu.
hapo police unaowatetea ni kama manyang,au tu. Kwani wameambiwa kla ktu kuua 2?
 
Nchi isiyokuwa na Nidhamu inayowachwa Wahuni wafanye fujo watakavyo huku wanasiasa wavaa Magwanda wakihamasisha fujo kuwa ni moja ya sera zao matokeo yake ndio haya ya leo asubuhi Mjini Mwanza, hivi sasa tumeshawafikiosha vijana wetu kuvamia raia wenzetu wenye ngozi nyeupe na kuwahujumu kwa rangi zao?

Kama ilivyotokea wakati wahuni Wakenja walivyokuwa wakifanya? hivi kuwapiga wahindi, waarabu ndio Ukombozi huo wachama cha Magwanda kutukomboa? haya moto wa ubaguzi mushauwasha huo kuuzima ni kazi kubwa siasa sio ucheza siasa ni hekima na busara, haya tusubiri na Mzee Sabodo nae kupigwa si ana rangi Nyeupeeeeee
 
habari zaidi zinasema idadi ya walipigwa risasi na kufa hapo hapo ni watu wa5. Nashindwa kuwapa pcha kwani nipo na sehemu mbaya.

Hivi hawa polisi hawana rubber bulets? Kwa nini wanapenda sana kutumia live ammunations? Na hii order ya shoot and kill nani anaitoa?i dont think we can solve internal problems by mtutu wa bunduki.nahisi polisi wetu wanaitaji kupigwa msasa,wamezidi kuwa triger happy sana?poleni sana ndugu zangu wa mwanza.
 
poleni sana wabangaizaji, ila ipo siku mtapata tu ukombozi, mungu yupo nanyi.
 
Nimesikiliza SupaMix EA Radio, chanzo kinasemekano mgongano wa maamuzi kat ya madiwan wa CCM na CHADEMA kuhusu mahali pa wamachinga kufanya Biashara, hivyo wamachinga wamekuwa njia panda kujua wapi waende.
Vyovyote vile polisi hawana haki ya kuua rai...
 
Hii kitu inahusiana na maelezo ya Dk Slaa ile juzi? nakumbuka member mmoja DAUGHTER alimwambia Dk Slaa kwamba jiji la mwanza chafu,vioski kila kona, taka nyingi, maachinga kibao, nae akafanya follow-up na akaongea na watendaji na akatupa update!! Vp hii ya leo ina mahusiano yoyote na Ile ya Dakta?? safisha JIJI??
Lengo lako ni kusikia ina uhusiano basi ngoja nikuambie NDIO INAUHUSIANO umefurahi sasa eeeh watu wengine bana akili fupi ka mkia wa mbuzi.
 
Na bado magamba watakuja watadai chadema ndo wamechochea.
Haya mauaji ya raia hadi lini? jk, saidi mbaya, nahodha achieni ngazi.
 
Ni kweli ..inabidi JiJi la Mwanza litafute sehemu muafaka kwa wamachiga kufanya biashara zao.Hivi karibuni mitaa ya makoroboi haipitika maana wametandaza bidhaa njiani na kila kona.

Busara na masikilizano vitumike kwenye utatuzi wa suala hili ili kuepusha vurugu zaidi
 
HAta hili lipo mahakamani, hivo msijali. Hivi ndivo tutakavyosikia kutoka kwa msaidizi wa kikwete Mhesh Makinda! Tanzania tulipofikia ni mahali pa kuanza kuwa na uhasama mkali na hawa wanaojiita walinzi wa Taifa! Poleni sana watu wa mwanza! Ngojen tusikie uamuzi wa kikwete juu ya hili nalo! FREEDOM Z COMING SOON!
 
Hivi ni lini wa-Tanzania tutaanza kufuata sheria? Ni mpaka tufukuzwe na polisi hadi kupigwa risasi? Inatakiwa elimu ya kutosha kuwafundisha wamachinga kuwa hawawezi kufanya biashara mahali popote katika miji.
 
wana mwanza poleni kwa maswaiba ... hii nchi tunakoenda ni wapi hata kama wananchi hawana haki na kitu kuna njia mbadala za kiubinbadam zafaa zifuatwe kuliko kuwahi kumaliza kitu kwa suluhisho tata
 
Back
Top Bottom