Mwenge, Dar: Mapambano ya Polisi na Wamachinga. Mabomu ya machozi yatembezwa

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,755
Polisi wanapiga mabomu ya machozi muda huu hapa Mwenge. Wanapambana na Wamachinga ambao wanajihami kwa mawe.

Chanzo cha vurugu ni kwamba wamachinga wanagoma kuondoka maeneo waliyoamuriwa kutoka na kwenda kwenye eneo walilopangiwa katika barabara ya kwenda Cocacola.

Nguvu kubwa inatumika. Hekima itumike.

=======

Pia soma mdau huyu aliyekumbushia kuhusu sakata la Wamachinga Mwanza:
Sakata la Wamachinga na mgambo Mwanza lilishia wapi? Walipewa maeneo au walirudi barabarani?
 
Itumike hekima Kwa mtu aliyeshika jiwe kama silaha?

Yale Yale ya Bi Simba kutetea jambazi lenye silaha na kusema hakutakiwa kuuawa alitakiwa kukamatwa na wakati amekufa akiwa anapambana na askari.

Tusiwe wepesi wa kutetea uhalifu, askari huwa wanaotoa amri kabla ya kutekeleza. Kwa Nini machinga wasikubali ili kuepusha Shari maana askari wapo kwenye utekelezaji wa majukumu?
 
Hili swala la Machinga limekuwa shida sana ,yule mtu wenu ndio alilea huu uozo.

Sasa Serikali ilipe fidia maeneo wanavyotaka Ili biashara zifanyike

Pia nimewahi shairi kwamba tunapojemga Barabara Tujenge Kwa kuzingatia maeneo rafiki ambayo yatawezesha Machinga kufanya biashara kando kando ya Barabara
 
Nilipita eneo hilo mchana nilikuwa polisi na mgambo wamezingira eneo hilo

Usiku huu imenilazimu kutoka nfukk kwa sababu polisi walianza kurusha mabomu ya machozikuwatawanya wamachinga wakiokuwa wanajikusanya
 
Hili swala la Machinga limekuwa shida sana ,yule mtu wenu ndio alilea huu uozo.

Sasa Serikali ilipe fidia maeneo wanavyotaka Ili biashara zifanyike

Pia nimewahi shairi kwamba tunapojemga Barabara Tujenge Kwa kuzingatia maeneo rafiki ambayo yatawezesha Machinga kufanya biashara kando kando ya Barabara
Sisiem ni wale wale Misukule to the core hata mbaguane hakuna msafi.
 
Back
Top Bottom