Vurugu Mwanza: Wamachinga Vs. Jiji - Damu yamwagika

Mkurugenzi wa mwanza bwana KABWE ni tatizo sana,mkuu wa mkoa hana shida ila huyu mkurugenzi ndiye tatizo,WABUNGE WA CHADEMA walishashauriana na mkuu wa mkoa walishakubaliana ila tatizo huyu bwana KABWE.
 
Nimeshangaa kusikia naibu waziri wa mambo ya ndani aliposema hakuna aliyekufa katika vurugu kati ya polisi na wamachinga, mwanza. Nimeogopa wakati kuna walio mwanza wanadai wapo walio kufa katika vurugu hizo.
Si huyu ndiye aliyewaita raia waliouawa Nyamongo kuwa ni majambazi? Sishangai kabisa.
 
Mie siyo mtabiri ila ninachokiona ni kuendelea kuwepo kwa ugomvi mbaya na mapigano baina ya dola na wananchi. Huwezi ziba masikio juu ya kero / mateso ya wananchi waliongojea utatuzi wa kero zao bila majibu na ukabaki kuwa salama, polisi watauwa na wananchi watauwawa na siku moja wananchi watawazidi nguvu polisi na kujilipizia kisasi. Mbegu tunayopanda ni mbaya sana.

Hii tabia ya watu wachache kutaka kuhodhi kila kitu na kuiacha jamii katika lindi la umaskini itakuja gharimu taifa hili siku moja. Fahamuni kwamba wananchi waliokata tamaa ni hatari zaidi kuliko faru aliyejeruhiwa nyikani! Watu wa aina hii wanaweza fanya lolote. Ee Mungu tuepushe na balaa hili la kujitafutia!
 
usipotezee ..... umechemka......sijataja wilaya ... nimetaja baadhi tu ya majimbo ya uchaguzi ya mkoa wa Mwanza ambayo huunda councils tatizo la ukilaza hili ... eti mkoa wa mwanza ni Ilemela na Nyamagana puke .... disparity of the mental order elimu ya ngumbaru hii
Jibu basi Geita ni Mkoa au Wilaya?..hoja yetu sio majimbo ya uchaguzi
 
Maisha yanazidi kuwa magumu sana tunapoelekea ni kubaya! Sasa hivi mtu kupigwa risasi na polisi imekuwa jambo la kawaida
 
Mkurugenzi wa mwanza bwana KABWE ni tatizo sana,mkuu wa mkoa hana shida ila huyu mkurugenzi ndiye tatizo,WABUNGE WA CHADEMA walishashauriana na mkuu wa mkoa walishakubaliana ila tatizo huyu bwana KABWE.

wote magamba hapo hakuna kupongezwa , kwa kufuata CODE of practise kati ya mkuu wa mkoa na mkurugenzi nani mkuu wa huo mkoa?
mkuu wa mkoa ni mwakilishi wa raisi kwa hivyo yeye ana sauti kuliko mkurugenzi
achukuwe hatua
 
Is Tanzania now under Police Control?Where is the president while people are killed openly by police as they wish?Or may be the president is still abroad with his routine business of travelling!!!!
 
Hawa ndio wenye nchi........walichofanya ni taarifa kwa CCM na serikali yake kwamba inawezekana....
 
Watu wa Mwanza tunaomba taarifa kamili, kweli kuna vifo vimetokea na kwamba vimesababishwa na polisi? maana Khagasheki kakanusha jana usiku
 
karl max alisema njia pekee ya kudai haki ni hii, mtu akibisha na hii basi huyo ni sugu na bado tutapigana mbaka tone la mwisho la damu yetu kwaa ajiri ya kuikomboa nchi yetu
 
Back
Top Bottom