Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Kuna taarifa kwamba vita ya Umeya Kigoma imechukua sura mpya baada ya Zitto kabwe kuitwa polisi na kuna habari kwamba amekwisha kuandaliwa mashitaka mazito ya kumtorosha mtuhumiwa kituo cha polisi, kosa ambalo kisheria dhamana yake ni ngumu na leo ni Ijumaa ya kuelekea Siku Kuu ya Krisimas hivyo anaweza kusota rumande hadi baada ya Sikukuu.
Wakati hayo yakiendelea, uongozi wa Halmashauri ya Kigoma wanafanya kama walivyofanya wa Arisha na sasa wanaandaa kikao kwa siri cha Baraza la Madiwani, ambacho kinaweza kufanyika Tarehe 27, siku ambayo upo uwezekano Zitto asiwe ametoka jela.
Taarifa zaidi zinasema kesi anayoweza kushitakiwa nayo Zitto inatokana na mmoja wa watu waliokuwa katika kampeni zake za mwaka huu kukamatwa na kuwekwa kituo kimoja kidogo cha polisi mkoani Kigoma akituhumiwa kwa mauaji, na baadaye kundi la wafuasi wa Chadema walikwenda na kuondoka naye. Tukio hilo lkilitafsiriwa kwamba lilichochewa na Zitto na sasa ndiye anatakiwa kushitakiwa. Lakini tujiulize hata kama kuna kesi, kwanini ifunguliwe leo Ijumaa ya Krismasi? Kwa kweli hawa CCM wanatupeleka pabaya.