Kunani "beria" ya Kihomoka mkoani Kigoma?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Mojawapo ni jina lake sahihi: Kihomoka, Kiyomoka, Kyomoka, Kiomoka, n.k. Wenyeji wa Kakonko waliomo humu watarekebisha.

Ni kizuizi cha kukagulia magari. Kipo Kakonko mkoani Kigoma, ikiwa ni kizuizi cha kwanza mara tu baada ya kuvuka daraja la mto Muyovozi (sijui kama ndivyo inavyoandikwa) ukitokea upande wa Biharamulo.

Eneo hilo lina askari Polisi, Uhamiaji, maafisa wa TRA, Maliasili n.k.

Ni eneo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na wenyeji kuwa linawanyanyasa vijana wenyeji wa huko kama kwamba si Watanzania. Kuna tetesi pia kuwa hata madereva wa magari makubwa, hasa wa kutoka nchi jirani, nao wamekuwa wakikutana na kashikashi ya aina yake kiasi cha kuwafanya kupachukulia hapo kama "beria" ya kipekee kwa usumbufu unaolenga kufanikisha rushwa.

Nimeshaenda Kakonko mara kadhaa kwa miezi ya hivi karibuni. Wakati mwingine, nikiwa katika mizunguko yangu huko, nililazimika kutumia usafiri wa bodaboda. Nilishangaa nilipokuwa na safari ya kupita hapo "beria" bodaboda akaribiapo, huchepuka kuingia porini na akishaipita ndipo hurejea barabarani. Wanafanya hivyo kwa madai kuwa wakipita hapo hawawezi kutoka salama. Lazima watafutiwe kosa kwenye pikipiki au la namna nyingine, ilimradi tu watolewe cho chote.

Kuna tuhuma za hivi karibuni kuwa kijana mmoja aliuliwa na maafisa Uhamiaji wa hicho kituo, wallipomtuhumu kuwa siyo Mtanzania. Mwili wa huyo kijana ulikuja kupatikana ukiwa umezikwa porini siku chache baada ya kupotea. Wanaodaiwa kumwua na kumzika kwa siri ni maafisa Uhamiaji wa hiyo "beria". Nafikiri walikamatwa, ila sijui kesi yao ilipofikia

Inasemekana hicho kituo kimeshalalmikiwa sana na raia pamoja na viongozi wao wa Serikali ya Mtaa lakini hakuna lililobadilika. Wanahisi kuwa huenda kuna baadhi ya viongozi wanaonufaika na "mateso" wanayoyapata.

Wengi wao wameshapoteza matumaini ya hiyo kero kushugjulikiwa. Namna pekee wanayoona kwa sasa ni kusubiria kipindi cha uchaguzi ili nao waweze kulipiza.

Japo ni mara chache nimeshafika Kakonko, lakini malalamiko ya hao watu yana mashiko. Haiwezekani, kwa mfano, bodaboda anayeishi jirani na beria aendeshe pikipiki yake kwa uhuru maeneo ya Kakonko mjini kuliko na Polisi wengi lakini akose uhuru wa kupita kwenye "beria" iliyo jirani na makazi yake. Haileti picha sahihi.

Lazima kuna tatizo hapo. Na kama ndivyo, ni kweli Serikali imeshindwa kulipatia ufumbuzi?

Inasemekana hata Rais wa JMT alishaandikiwa barua kwa ajili ya suala hilo.

Kwa nini iwe Kyomoka "pekee"? Kunani hapo?
 
Back
Top Bottom