Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Mkuu hebu hii history andika kitabu,najua kweli sio mwandishi omba msaada kwa waandishi wakusaidie,nadhani watu kama nyinyi ni watu muhimu katika history ya nchi yetu,
Watoto wetu leo hata mashuleni sidhani kama wanafundishwa habari za vita ya kagera wala kujua tu majina ya mashujaa wetu,
Khofu yangu miaka 20 ijayo nchi itakuwa imepoteza history yake yote,

tatizo la watanzania ni wavivu kusoma. Kitabu kipo kinaitwa "War In Uganda: ISBN: 9789976100563". MImi ninacho tangu mwaka 1995.
 
Mkuu Echolima

mbali na majeshi ya miguu mlitumia pia majeshi ya majini katika vita hii??

Vipi kuhusu majeshi ya anga nayo yalitumika sana au hatukua wazuri sana upande wa anga??

Mkuu,

Soma maelezo yote ndipo uulize unapohitaji. Kakuambia kwamba Mboma aliongoza vikosi vya ndege sasa unazidi kuuliza kama vile hukuelewa.

Swali lako la pili kuhusu majeshi ya majini lina mantiki kidogo na ninalijibu kama ifuatavyo.

Hatukuwa na lengo la kumpindua Idi Amin, bali kumfukuza mvamizi Idi Amin. Yeye alivamia eneo la Kagera, yaani north of Kagera river was annexed into Uganda as a new Ugandan district.

Sasa ukiangalia geography ya nchi yetu, bandari pekee kama tungetumia navy units basi tungetakiwa kutua Bukoba tu ambako ni kilomita 50 kutoka maeneo yaliyovamiwa yaani kutoka Kyaka.

Hivyo, kazi ya kwanza iliyofanyika November 1978 ilikuw akumfukuza toka ardhini mwetu na hivyo ililazimu kutumia infantry ya akina Echolima.

Echolima kafafanua vizuri, maana mimi kwa mara ya kwanza ndipo nimejua kwamba kumbe kuna majeshi yaliingilia Rwanda na hivyo geographically wavamizi wakawa wamezingirwa. Nimeielewa hili baada ya kuisoma hii story ya Echolima nikiwa na ramani ya Tanzania mbele yangu.

Kama tungekuwa tunataka tu kumpindua Idi Amin bila uchokozi wowote, basi hapo navy attacks yaani majini ingewezekana. Ingekuwa ni kiasi cha kuchukua meli kutoka Mwanza na kusogea kimyakimya hadi Entebbe na kuilipua Ikulu ya Entebbe anakopenda kukaa Rais wa Uganda.

Lakini hata hivyo, kumuua Rais wakati majeshi yake yapo bado haitoshi. Na hata hivyo angeweza kukimbilia Kampala na huko meli hazifiki.

Na mwisho ndicho kilichofanyika. Idi Amin alipinduliwa April 10, 1979 na akakimbia Uganda. Lakin majeshi ya Tanzania hayakuishia Kampala tu. Vita ilihesabika imekwisha June 03, 1979 siku Silas Mayunga na vikosi vyake vilipojikuta vimekanyaga ardhi ya Sudan huku wasudan wameshikilia bunduki wakidhani na wao wanavamiwa baada ya idi Amin.

Mayunga akasalimiana na wasudan na kisha akainua fimbo yake kwa askari wake kushangilia kwamba wameyafukuza majeshi ya Idi Amin hadi nje ya Uganda.

Nadhani kwa kifupi nimejibu swali lako.

Cc: Jasusi, Pasco, Echolima,
 
A nice story. kwa kweli story kuhusu vita ya Kagera vin mvuto sana. yeyote aliyeshiriki anaweza kuandika simulizi yake na watu watapenda kuzisoma. thanks
 
Mkuu,

Kitabu hiki ninacho na ninakitunza kama mboni ya jicho langu. Niliwahi kumuonyesha mkubwa mmoja hapa nchini mwaka jana, kumbe hakuwahi kukiona na alishangaa sana kuniona nacho.

Na humo utagundua kwamba kumbe Nyerere alikuwa mmoja wa marais wachache kumuweka detention rais wa nje.

Nyerere alimuweka detention Rais Yusuf Lule wa Uganda kwenye ikulu ya D'Salaam kuanzia June NN, 1979 hadi July 06, 1979
kama inavyoelezwa kwenye ukurasa wa 204 hadi 206.

Nyerere alikuwa kiboko.
sijui kama itafaa kuweka records sawa, niliwahi kusikia kuwa rais wa wakati huo aliyepinduliwa na idd amin ni Milton obote na alikuwa kafichwa ikulu ndogo ya Lushoto.
 
sijui kama itafaa kuweka records sawa, niliwahi kusikia kuwa rais wa wakati huo aliyepinduliwa na idd amin ni Milton obote na alikuwa kafichwa ikulu ndogo ya Lushoto.

Mmh, ndivyo name mimi navyojua, huyo rais mwingine itakuwa no new story
 
Mmh, ndivyo name mimi navyojua, huyo rais mwingine itakuwa no new story
huyo yusuph lule alimpindua obote badae kama sikosei, yusuph lule alikuwa miongoni mwa majeshi ya ukombozi ya upande wa Uganda, wanaojua watatuwekea records sawa.
 
Wadau vitabu vya vita yetu na Idd Amin na Raid in Entebe vinapatikana wapi? Navitafuta kwa udi na uvumba.
 
sijui kama itafaa kuweka records sawa, niliwahi kusikia kuwa rais wa wakati huo aliyepinduliwa na idd amin ni Milton obote na alikuwa kafichwa ikulu ndogo ya Lushoto.

Hakufichwa Lushoto. Nyerere aliitamkia dunia kwamba hamtabui Idi Amin. Nyerere akampa Obote nyumba ya jiarni kabisa na yeye palepale Msasani yaani unatembea kwa miguu tu. Ni nyumba iliyokuwa ya Oscar Kambona.
 
Nimesoma kwa makini sana,kama unaweza shirikiana nami,naweza kukusaidia tukaweka stori yako katika kitabu na kitakuja kuwa kizuri sana,naomba tu ufafanuzi katika terms zifutazo,brigedia ,platoons,kombania,kikosi,na baadhi ya terms zingine za kijeshi yenye maana zinazofanana na hizo..
 
Echolima vipi muendelezo wa hii historia ya vita vya kagera? Na vipi umefanikiwa kutengeneza kitabu kama ulivyosema?
 
Back
Top Bottom