Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Echolima

JF-Expert Member
Oct 28, 2007
3,826
2,057
Jana wakati naangalia TBC Kwenye sherehe za Mashujaa zilizoongozwa na Rais nilipatwa na masikitiko makubwa sana hasa nilipouona ule Mnara wa MASHUJAA wa vita vya Kagera niliwakumbuka sana wapiganaji wenzangu waliopoteza maisha yao wakiwa mstari wa mbele wa mapambano ya kuuondoa Utawala wa Nduli Idd-Amin wa Uganda.

Niliwakumbuka askari 25 waliokufa wakiwa kwenye platoon yangu niliwakumbka mmoja baada ya mwingine na nilisema MASHUJAA TULIORUDI TUMERUDI KISHUJAA NA MASHUJAA WALIOKUFA WAMEKUFA KISHUJAA LENGO NA NIA YETU ILIKUWA NI MOJA TU KUILINDA HADHI YETU YAANI NCHI YETU.

Tarehe 28-10-1978 nilikuwa kambini LUGARO kikosi cha MMJ nilikuwa nimejipumzisha ghafla likapigwa Baragumu na tulipoenda kusikiliza tuliambiwa kuwa kuwa Idd-Amin kavamia huko Kagera tukaamliwa kuchukua vitu vyetu na kuvipeleka kwa STORE-KEEP vikiwa na majina mimi nilichukua bage langu na kuliandika jina langu na kulikabidhi kwa STORE-KEEPER.Na hapo hapo tulianza kuchukua vifaa vya kivita kama vile Combat mpya Bunduki SMG ya kwangu ilikuwa NHN 66482612.

Jioni hiyo ya 28-10-1978 Tulichukuliwa na magari ya Jeshi kwenda station ya Railway huko Dar-es-salaam na tuliondoka usiku huo huo kuelekea station ya ISAKA-Kahama.

Tulifika Station ya Railway ya Isaka 01-01-11-1978 Mchana tulikuta mabasi mengi sana ya kiraia yametusubiri kwenda Vitani mimi na wenzangu tulipanda Basi moja lilikuwa limeandikwa LUPONDIJE lilikuwa na namba MZA 234 Tuliondoka hapo isaka saa 9 mchana kuelekea Kahama mjini bahati mbaya sana Basi letu lilipofika tu pale stand ya Kahama Msafara wa magari yote ndo ulipoanza kuondoka na sisi ilibidi tupitilize tu bila kupata chakula hapo na kwa kufupisha habari nilifika kwenye uwanja wa Mapambano 03-11-1978 Mchana

Nilipofika wakati nateremka Kwenye Basi mimi niliitwa na Major mmoja kuwa nichukue askari wanne niende kwenye Landrover ya Jeshi ilikuwa imefunikwa na turubai na nilifanya hivyo nilipofungua nilikutana na Maiti za askari wetu watatu waliolipuliwa na Bomu la kutupwa ilibidi tuzishushe Maiti hizo na mimi ilikuwa mara yangu ya kwanza kubeba Maiti katika Maisha yangu Kwangu mimi niliona kama ni Uchuro kwangu kufika tu Mstari wa mbele na kukutana na Maiti kwangu mimi ilinipa taabu sana.

VITA VILIPOANZA
Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier Walden.

Msimamo wa vita ulikuwa umepangwa vizuri sana na ulikuwa na MAKAMANDA wafuatao-

1. Brigadier Marwa waliingia Uganda kwa kupitia mpaka na Rwanda na Zaire.
2. Brigadier Kiwelu alielekea Mbarara,
3. Brigadier Marwa alielekea Masaka
4. Brigadier Walden aliingia Uganda pia kwa kupitia Rwanda na kuelekea Kasese
5. Brigadier Mayunga yeye alibaki upande wa Tanzania ambapo brigade yake iligawanya katika makundi mawili, kundi moja liingia maeneo ya Mtukula kutokea Rwanda, , wakati kundi jingine lilibaki pale pale mto Kagera lakini likiwa na mizinga mizito (BM-40) kiasi cha kuweza kurushia makombora hayo moja kwa moja hadi askari wa Amini waliokuwa pale Mutukula. Ilichukua muda wa karibu wiki tatu kwa plani ya vita kukamilika na majeshi yetu kujipanga vile.

KIPIGO TOKA MAJESHI YA AMIN

Baada ya majeshi ya Amin kuchukua eneo la Mutukula, walipandisha bendera ya Uganda na kubomoa lile daraja la mto Kagera. Brigadier Yusuf Himid ambaye alikuwa Brigade Commander wa Kanda ya Magharibi wakati huo alituma Battalion moja kujaribu kuvuka mto ule kwa kutumia mitumbwi wakati wa usiku kusudi wakapambane na wavamizi wale. Hata hivyo wakati platoon za kwanza kwanza zinaanza kutekeleza amri hiyo, wakaonekana na majeshi ya Amin ambayo yalikuwa yamejikita kilimani; Askari wetu wale walimiminiwa mizinga ambayo ilisababisha hasara kubwa kwa askari.

Bahati mbaya sana tulipigwa sana na majeshi ya amin na kupelekea Majeshi yetu kurudi nyuma kujijenga upya na kupelekea lile daraja kuvunjwa conteravertially Bahati nzuri mimi na wenzangu tulikuwa tumewahi kuvuka kwenye hilo Daraja na Tulipojijenga upya kazi ilianza na ilikuwa ngumu sana maana ilikuwa ni masika Mvua zilikuwa zinanyesha sana sana kwa sababu mimi na wenzangu tulikuwa askari wa Miguu Infrantry haikutupa taabu tuliendelea kusonga mbele kitendo hicho cha kurudishwa nyuma kilisababisha Brigedier Yusuph Hamid kuondolewa mstari wa mbele hivyo Brigade ya magharibi ikawekwa mikononi mwa Colonel (wakati huo) Kotta ambaye legacy yake kama kamanda shupavu pamoja na vijana aliopigana nao bega kwa bega na wote wakiwemo makamanda ,maafisa na askari waliokomboa Afrika, kama mnavyojua role ya jeshi letu kivita angola,msumbiji,namibia,comoro ets...kwa waliopo na waliotangulia mbele za haki.

Baada ya kile kipigo bregedia Yusuph Hamid aliondolewa from front line kama ilivyokawaida ya war plans...maana kamanda aliyepigwa hulazimika kupumzishwa kwanza ili atafakari wapi wapi alikosea.

Pale Ngome, kamanda aliyepanga vita ile yote alikuwa ni Colonel Lupogo Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier Walden.

Kipindi hicho mimi nilikuwa na ki-radio kidogo cha mfukoni niliweza kusikiliza Radio Ujerumani na Radio nyingi tu kila zilipokuwa zinatangaza kutadhimini uwezo wetu wa kivita na uwezo wa Majeshi ya Amini ilionekana wazi kuwa Maeshi ya Amini yalikuwa Bora na zana Bora kuliko zetu kwa upande wa vifaru sisi tulikuwa na T 34 vya kizamani sana na Uganda vifaru walikuwa navyo T 55 Kwa wakati huo walikuwa navyo Bora sana kuliko sisi. Pia Amini alisikika kwenye vyombo vya habari akishangilia kuwa jeshi lake limeweka rekodi kwa kuteka Mtukula kwa muda wa dakika 25 tu.

VITA VYAANZA RASMI FRONTLINE

Baada ya mejeshi yetu kujipanga ndipo filimbi ilipopigwa na Brigadier Kiwelu akarusha risasi ya kwanza dhidi ya Barracks moja ya Amin iliyokuwa pale Mbarara. Brigadier Marwa naye akawarushia risasi (ya kuwambia kuwa kazi imeanza) wale askari wa Amini walikuwa pale Mutukula.

Brigadier Mayunga naye akadonoa kidogo kutokea Magharibi, harafu akatumia ujumbe mwingine wa BM-40 kutokea Kagera. Askari hao wa Amin waliokuwa pale Mutukula (Simba Battalion) walipoona wanapata kipigo kutoka pande zote wakaomba msaada kutoka Mbarara, hata hivyo wakaambiwa kuwa ile Battalion ya Mbarara nayo ilikuwa imeelemewa na kipigo cha Kiwelu, ndipo wakaomba msaada utokee Entebbe. Ile Battalion iliyoletwa kutokea Entebbe ikakutana na kizingiti pale Masaka ambapo Brigadier Marwa alikuwa kajichimbia.

Wakati Amin bado anafikiria afanyeje kuhusu vipigo hivi vya Masaka, Mbarara na Mtukula, akapewa taarifa nyingine kuwa kulikuwa na kipigo kingine kimeanza kutokea Kasese kuelekea Kampala; hiki kilikuwa ni kipigo cha Brigadier Walden. Basi kuanzia hapo ndipo vita ile ilipoanza kupendeza kweli kweli kwa majeshi yetu,. Walianza kuwabomoa majeshi ya Amini yaliyokuwa miji hiyo huku yakiayaacha yale ya Mtukula pale pale na bendera yao ili wajifie wenyewe kwa kukosa supplies kwa vile walikuwa hawapati chakula wala msaada wowote kutoka ndani ya Uganda tena.

Baada ya kugundua kuwa kuwa alikuwa amezungukwa sana kwa vile majeshi yake mazito yalikuwa ndiyo yameshathibitiwa, Amini akaitangazia dunia kuwa amevamiwa na majeshi ya Tanzania (na kweli safari hii alikuwa amevamiwa kikwelikweli). Hata hivyo Nyerere naye akajibu kuwa jamaa huyu alituvamia akachukua sehemu ya Kagera, na kuitangazaia dunia. Ili kuionyesha dunia kuwa anasema kweli, Nyerere na Sokoine walikaribisha ujumbe wa OAU pale Kagera na kuwaomnyesha kuwa lie eneo la Mutukula bado lilikuwa linakaliwa na majeshi ya Amin na bendera yake bado inapepea. Kufanya hivyo kulifanya jumuia ya kimataifa isimwamini Amin katika kipindi ambacho alikuwa akipewa kipigo safi sana.

HISTORIA FUPI YA MAKAMANDA

Mwaka 1978 jeshi letu likuwa na Major General wawili tu, Major General Twalipo (aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati huo) na Major General Sarakiya ambaye alikuwa balozi wetu huko Nigeria. Baadaya ya Major General kulikuwa na Mabrigadier sita au saba tu: Brigadier Marwa, Brigadier Musuguri, Brigadier Mayunga, Brigadier Walden, Brigadier Kiwelu, Brigadier Yusuf Himid nadhani na Brigadier Mkisi. Chini ya Mabrigadier kulikuwa na makanali kadhaa ikiwa ni pamoja na akina Moses Nnauye, Abdallah Natepe na wengineo.

Jeshi letu lilikuwa limegawanyika katika Brigade kama nne hivi: Kusini, Magharibi, Mashariki, na Zanzibar. Baada ya vita ile, ndipo Twalipo alipopandiswa cheo na kuwa Luteni General wakati Mabrigadier wale walipandishwa kuwa ma-major general;Muundo wa jeshi letu ukabadilishwa kidogo kuwa na division tatu. Miaka wiliwili baadaye Luteni General Twalipo alipandishwa cheo tena na kuwa General ambapo chief of staff wa Jeshi akawa na cheo cha Luteni General. Baadaye sana cheo cha Brigadier kikabadilishwa na kuwa Brigadier General.

Kuhusu majina kama 'Black mamba" hayo yalikuwa maalumu au tunaweza kuita "usernames" ili kuficha utambulisho wao halisi hasa kwenye mawasiliano ya kijeshi vitani. Kila kamanda alikuwa na username yake.of course mengine yalitokana na jinsi kamanda alivyokabiliana na changamoto za kivita. Mfano Maj.Gen. Mwita Marwa (Kambale)aliitwa hivyo kwa sababu yeye binafsi na brigade yake walipigana wakiwa ndani ya maji kwa muda wa wiki mbili maji yanayofika kiunoni.Na bado walijitoa kimasomaso kukabiliana na adui. Brigade hiyo ilipata shida sana ya kuharibikiwa vifaa kama vile vya mawasiliano n.k.

KIPIGO CHA LUKAYA

Hapo mimi mwenyewe nilishiriki na nilijua kabisa kuwa sasa ushindii ni wetu baada ya kufanyia AMBUSH ambayo askari wengi wa Libya walipoteza maisha yao na wengine wengi kutekwa ilikuwa AMBUSH tamu sana yenye mshiko ambayo baada ya saa moja magari mengi sana yalionekana yakiwaka moto na Vilio vilikuwa vimetawala eneo hilo walisikika wakisema ALLAH-AKBAR enzi hizo mimi sikujua wana maana gani

Kilichonihakikishia ushindi ni Amin kuleta askari ambao wana uwezo kupigana Jangwani leo kawaleta kupigana kwenye misitu minene kama ya Uganda nilijua fika kuwa wata-Prove failer tu.Mateka waliletwa mpaka Dar-es-salaam Cha kilichowashangaza wengi ni kuwa walirudishwa makwao Bure kabisa Mwalimu alikataa Msaada wa mafuta kwa mwaka mzima ambayo Libya iliahidi kulipa kukomboa askari wao waliotekwa katika vita hiyo.Hapo Mwalimu alisema sisi hatufanyi Biashara ya kuuza watu. lakini kuna historia nzuri kuhusu kutekwa kwa mji wa kampala, ambapo Brig. Kiwelu (wakati huo) aliongoza mapambano kutokea lukaya, kuanzia usiku wa manane mfululizo kwa karibu masaa nane, BM 24 zikiunguruma na Kampala ikawa mikononi mwa jeshi la ukombozi.

Jambo jingine, Generali Mboma wakati huo alikuwa Pilot na ndiye aliyeongoza kipigo kilichoziacha ndege yingi za amini kwenye uwanja wa Entebe taabani. Kama mnakumbuka ndege yetu iliyotunguliwa na majeshi yetu wenyewe kwa bahati mbaya,Rubani wa kijeshi aliyetunguliwa kwa makosa na JWTZ alikuwa ni Capt. Alexander Kaleya Mshana.

Basi hawa akina mbona waliondoka Ngerere bila kutoa taarifa kwa makamanda wa vikosi vya nchi kavu (Hili lilifanyika makusudi) na wakaruka hadi Uganda. This wa the most precise target JWTZ did hadi Amin akalalamika kwamba JWTZ ina mamluki wa kukodiwa. Kwa sababu ndege za amini zilikuwa zinajianda kuja kushambulia TZ, lakini ghafla, wakajikuta Ndege zatu zinaruka chini sana usawa wa ziwa hivyo kusababisha taharuki kubwa sana, na kwa kuwa ziliruka chini sana na kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani mwendo unaozidi sauti zilisababisha hofu kubwa na majengo mengi ya vioo vilivunjika-vunjika na wetu wengi walitibiwa kwa Presha,wakati huo Benki kuu ya Uganda nayo ikapigwa.

Battelfield tactics zilipangwa na Col. Lupogo.

Makamnada walioongoza vita walikuwa ni Brig. Marwa, Brig. Mayunga, Brig. Kiwelu, na Brigadier Walden. Hawa ndio waliongia msituni na wapiganaji. Makamanda hawa alipata vyeo vyao hivyo kutokana na umahiri wao wa katika uongozi wa kijeshi, na wote walihudhuria mafunzo ya uongozi wa kijeshi ndani na nje ya nchi mara kadhaa. Baada ya Uhuru hatukuwa na wasomi wengi katika majeshi yetu. In fact ni hawa hawa makamanda walioweka mkakati wa kuhimiza elimu jeshini na kuanzisha Elimu ya sekondari compulsory kwa wanajeshi wote na kuhimiza ajira za kijeshi kwa wasomi.

BRIG GEN MOSES NNAUYE

Huyu alishiriki kama muhamasishaji ni muhimu sana akiwa ni vikosi vya bendi na burudani [ie mwenge jazz,na kwaya ya luteni komba...]hawa walikuwa na wajibu wa kuhakikisha askari wanaburudishwa na kuliwazwa baada ya kazi ngumu na kuwatia hamasa...na propaganda za ushindi...

Ma-CDF wetu kwa kadri niwezavyo.

WAKUU WA MAJESHI CDF

1.1964-1974: Sarakikya
2.1974-1980: Twalipo
3.1980-1988: Musuguri
4.1988-1994: Kiaro
5.1994-2001: Mboma
6.2001-2007: Waitara
7.2007-2016 Mwamunyange
8.2016-Venance Mabeyo-

CHANGAMOTO ZA VITANI

Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mble wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya KarumaKwa maajabu, Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario. Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu. ikimzunguzia Marehemu Gen. Imran Kombe. Katika makamanda waliopiganisha vita kitaalamu na kwa ufundi wa hali ya juu mmoja wao alikuwa ni Gen Kombe

2. Gen Msuguri alikuwa siyo msomi sana lakini mabrigedia wake walikuwa wanaelimu ya kutosha na ndiyo maana waliweza kupanga mashambulizi ya kiufundi, ungeweza kuona jinsi hivi vikosi vilikuwa vinasonga mbele basi ungeona haikuwa kazi ya kubahatisha. Kutokusoma kwa Gen Msuguri siyo hoja kwani alikuwa na uwezo wa kujua mapungufu yake na ndio maana alizungukwa na makamanda wazuri, na hiyo ni sifa kubwa kwa kiongozi.

3. Askari wa Lupogo walipata matatizo kwasababu walikuwa wanapigana na kikosi cha Amini kilichokuwa mlimani.Hivyo wao walikosa OP Obsevartion Post wakajikuta wanashambuliwa kirahisi.

Kuna uwezekano kabisa kwamba Lupogo alipandishwa cheo kwa kuzingatia rekodi yake ktk vita nzima na siyo wiki tatu za mapambano ambayo alifanya vibaya. labda tatizo lilitokana na intelligence na military planning.

Lt.Col. Ben Msuya. Huyu ndiyo aliongoza utekaji wa jiji la kampala, na baadaye ku-act kama mayor wa kampala, mkuu wa itifaki, na mwisho kuandaa shughuli ya kuapishwa Yussuf Lule.

Lt.Col. Hassani Boma na Lt.Col. Mazora wametajwa kwa umahiri wao ktk medani ya vita.

Maj. Gen.Silas Mayunga "mti mkavu" ndiyo aliingia kijiji cha koboko ambako alizaliwa Iddi Amini.

Luteni Col Ben Msuya alistaafu jeshi akiwa MEJA JENERALI..na jukumu lake la mwisho alikuwa mkuu wa kamandi ya tabora...yenye jukumu la kuangalia hadi Kigoma, Rukwa ..Masaka na Mbarara zilikuwa smoothered na mizinga kabla ya kutekwa. Hapo hatukupoteza askari wengi.

Amini na askari wake waliingia uoga tangu wapigwe na kutolewa Kagera. walianza kudai kuna Wacuba, Wachina, ati wanasaidia Tanzania.

Baada ya Mbarara kutekwa Mayunga alipandishwa cheo kuwa Major General na kupewa Brigade mbili kuziongoza. Chini yake walikuwepo Brig.Hemedi Kitete[rip] na Brig.Roland Makunda.

Namkumbuka Brig.Gen.Ramadhani Haji Faki kama mmoja wa makamanda toka Zenj waliotunukiwa nishani na Mwalimu Nyerere uwanja wa taifa.

Mchango wa Mwita Marwa ktk vita vya Kagera ulikuwa mkubwa.

Every nation and every country has been blessed by great individuals. They have left footprints. Their lives and actions tells us the purpose of life and living. Maj. Gen Mwita Chacha Marwa a.k.a Kambale was never a scholar neither a good politicians but he is worth a role model to many of us. we can learn from him and make our lives beuatiful and worth living. God has decided to call him at the time when Tanzania may have wanted him more, we are in a critical time of struggle, struggle that can not be compared to theirs at that time. But it a struggle that pose danger to survival of this nation

Ndugu zangu, vita huwa havipiganiwi ardhini, angani au kwenye maji peke yake, vita hupiganwa pia kwenye Media, na kuongeza chumvi hufanya watu wasife moyo na kuwapa motisha, "Ingekuwa ajabu sana kama vyombo vya habari vya nchi yetu vingesema jana tulipigwa sana lakini leo afadhali tunajaribu kuwapiga." Think about it.

Mimi Binafsi siwezi kumsahau Baba Nape kweli alikuwa Mwanasiasa safi aliweza kuwahamasisha watu mpaka wengine tulisahau kama kuna kufa vitani alikuwa na uwezo mzuri sana wa kujieleza na kumwelezea Adui alivyo dhaifu mpaka ninyi askari mnamkubali na mnaamini kuwa kweli Adui huyu si chochote tutamfumua tu, vilevile John komba alikuwa ana uwezo wa kutuburudisha kiasi cha kujisikia kuwa tuko nyumbani na aliyekuwa tunamzimia sana ni wale vijana wa Johns corner ile Bendi ya JKT na tuliporudi kweli walituimbia wimbo ambao wengi uliwatoa machozi ambao unasema hivi-MASHUJAA TULIORUDI TUMERUDI KISHUJAA NA MASHUJAA WALIOKUFA WAMEKUFA KISHUJAA&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];.Mwenge Jazz nao hawakuwa nyuma kutumbuiza wapiganaji tunawashukuru sana.

Nitaendelea...
 
Asante kwa history nzuri na ya kusisimua kuhusu mashujaa wa Vita vya Kagera isipokuwa tu amesahaulika mtu mmoja nyeti sana Nchini naye ni Mh Rais Kikwete na ningependa kufahamu namna alivyoshiriki katika hivyo vita na alikuwa katika Battalion ipi.Asante.
 
I wish more could read this. Its very touching and of course you guys deserve better

You were willing to lose everything so as we could be free. You were okey to be loners so as we shud rejoice today! You gave your lives so as strangers like us who had no ideas if there was ever a war to survive and live! May God bless you guys with the courage you showed us and still show to us! For ever and ever.. RIP to all fallen soldiers of JWTZ
 
Echolima,

Thank u for ur service to our country.

Nakushauri uandike kitabu kinachohusu vita vya Kagera.

Suala kwamba wewe siyo mwandishi lisikukatishe tamaa.

Tafuta msaada wa waandishi, na wana historia.

John Walden, Mwita Marwa, Silas Mayunga, Imran Kombe, Yussuf Himid, Moses Nnauye,wote wametangulia ktk haki.
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa history nzuri na ya kusisimua kuhusu mashujaa wa Vita vya Kagera isipokuwa tu amesahaulika mtu mmoja nyeti sana Nchini naye ni Mh Rais Kikwete na ningependa kufahamu namna alivyoshiriki katika hivyo vita na alikuwa katika Battalion ipi.Asante.
Mmm! Huyu ajawai kwenda front line. Yeye alikuwa akishika chaki kufundisha madhumuni ya azimio la Arusha.
 
Kipindi hicho Mkuu wa kaya alikuwa chuoni na alikwa mwalimu wa siasa jeshini pamoja na wakuu wengine.

Asante kwa history nzuri na ya kusisimua kuhusu mashujaa wa Vita vya Kagera isipokuwa tu amesahaulika mtu mmoja nyeti sana Nchini naye ni Mh Rais Kikwete na ningependa kufahamu namna alivyoshiriki katika hivyo vita na alikuwa katika Battalion ipi.Asante.
 
Kwenye sehemu ya pili nitajikita zaidi kwenye medani za kivita vituko na mikasa kwenye uwanja wa vita vya KAGERA.

Thank u for ur service to our country.

Nakushauri uandike kitabu kinachohusu vita vya Kagera.

Suala kwamba wewe siyo mwandishi lisikukatishe tamaa.

Tafuta msaada wa waandishi, na wana historia.

John Walden, Mwita Marwa, Silas Mayunga, Imran Kombe, Yussuf Himid, Moses Nnauye,wote wametangulia ktk haki.
 
Last edited by a moderator:
Kwenye sehemu ya pili nitajikita zaidi kwenye medani za kivita vituko na mikasa kwenye uwanja wa vita vya KAGERA.
Thank u for ur service to our country.

Nakushauri uandike kitabu kinachohusu vita vya Kagera.

Suala kwamba wewe siyo mwandishi lisikukatishe tamaa.

Tafuta msaada wa waandishi, na wana historia.

John Walden, Mwita Marwa, Silas Mayunga, Imran Kombe, Yussuf Himid, Moses Nnauye,wote wametangulia ktk haki.
 
Last edited by a moderator:
hiyo ya kupigana ukiwa ndani ya maji kwa week mbili,ni balaa.kuna mwanajeshi mstaafu aliyepigana vita hivi aliniambia alitembea kwa miguu umbali wa takribani kilimeter 500 ama zaidi akiwa vitani kuelekea kampala,naomba experience yako pia juu ya hili
 
Msandawe Halisi Kwani kulikuwa na dhambi gani kipindi hicho kushika chaki na kufundisha Azimio la Arusha?
 
hiyo ya kupigana ukiwa ndani ya maji kwa week mbili,ni balaa.kuna mwanajeshi mstaafu aliyepigana vita hivi aliniambia alitembea kwa miguu umbali wa takribani kilimeter 500 ama zaidi akiwa vitani kuelekea kampala,naomba experience yako pia juu ya hili
Hiyo balaa sana
 
Back
Top Bottom