Huyo JK " WENU " alitoa sababu gani?......nadhani washauri wake mtakuwa mlimuambia kuwa tayari anapewa za uso huku JF
Heshima kwako Phillemon Mikeal,
Mkuu JF iko juu sana washauri wake watakuwa wamemwambia jana TBC1 walikuwa wakimwonyesha JK akiifungua MT Meru Hotel ndani ya hotuba yake aliusifia mji wa Arusha kwamba ni mji wa kimataifa kwasababu mikutano mingi ya kimataifa inafanyika hapa pia alisisitiza serekali yake itaendelea kutoa support ili mikutano mingi mkubwa ifanyike jijini Arusha.
Niligundua tayari sisimizi wake wamemtonya juhudi zikafanyika TBC1 ikatumika kutujibu habari ndiyo hiyo.
Heshima kwako Phillemon Mikeal,
Mkuu JF iko juu sana washauri wake watakuwa wamemwambia jana TBC1 walikuwa wakimwonyesha JK akiifungua MT Meru Hotel ndani ya hotuba yake aliusifia mji wa Arusha kwamba ni mji wa kimataifa kwasababu mikutano mingi ya kimataifa inafanyika hapa pia alisisitiza serekali yake itaendelea kutoa support ili mikutano mingi mkubwa ifanyike jijini Arusha.
Niligundua tayari sisimizi wake wamemtonya juhudi zikafanyika TBC1 ikatumika kutujibu habari ndiyo hiyo.
Hili la mkutano kufanyika Dar badala ya Arusha ni vigumu kulihusisha na ajenda binafsi ya Jakaya. Mikutano ya Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki huwa inafanyika katika nchi mbalimbali na kwa mara ya mwisho nakumbuka mkutano kama huu ulifanyika Bujumbura. Summit moja kwa mwaka ambayo ni ya kawaida (Ordinary) ni lazima ifanyike Arusha yalipo Makao Makuu ya Jumuia. Hii ya sasa si ya kawaida (Extra ordinary) na hivyo inaweza kufanyika sehemu yoyote kama nchi inayoomba kuhost itachukua sehemu kubwa ya gharama. Hii inaongeza visibility ya Jumuia kwa watu wa Afrika Mashariki. Kuna mmoja ametolea mfano wa East Africa Legislative Assembly ambao kila mkutano huwa wanazunguka katika miji tofauti ya Jumuia. Siupendi sana huu mfano kwani binafsi nadhani kitendo cha EALA hakinufaishi jumuia bali ni kutaka kuvuja fedha za Jumuia bila sababu. Kikao hiki cha sasa kimefanyika Dar es Salaam kwa sababu kulikuwa na Mkutano mwingine wa Uwekezaji wa Afrika ambao wakuu wa nchi walikuwa wanahudhuria na hivyo ikaonekana ni vyema ikaungana. Ndiyo maana napata kigugumizi kuhusisha suala hili na ubaguzi wa wazi wa JK. Hata hivyo, anything is possible.
Tumechoka na mambo ya uvumi na ya kufikirika yasiyo hata na msingi. Kwanza kama kupingana na JK ndiyo uadui basi Mwandosya, Mwakyembe, Mary Nagu, Magufuli, Kagasheki na wengine wengi wasingekuwa mawaziri au Njoolay asingekuwa RC, maana hao wote walipinga ugombea wake. Haya ni mambo yasiyo na msingi na hata hili la kuhamisha mkutano kutoka arusha kuja dar es salaam ni porojo zisizostahili hata kutupotezea muda. Kama ingekuwa hivyo basi hata vikao vya Council of Ministers ambavyo vimekuwa vikifanyika mpaka mwisho wa wiki iliyopita vingekuwa vimehamishwa. Suala la mkutano ufanyikie wapi ni suala la convenience na ingewezekana kufanyikia hata Tabora. Hivi Arusha kuna nini cha ajabu alichofanyiwa JK ,mpaka awalipizie visasi maana kama ni wabunge wa upinzani basi Mkoa wa Mwanza una wapinzani wengi kuliko Arusha. Hoja nyingine ni potofu mpaka inakera.
ivi cdm mbna mko kama was*** kwani mkutano kufanyikia dar badala ya arusha kuna tatzo gani?sio lazima arusha,,na mtataapika nyongo mwaka huu,leteni hoja za msingi kama kweli nyie ni wanasiasa mlio timamu,acheni majungu ya kinafiki fanyeni kazi .
Philemon Mikael,
..hivi Raisi alipowaambia wananchi wa Mwanga-Kilimanjaro wasifikirie kuhamia mkoa wa Pwani akidai hakuna ardhi ni kutokana na magomvi yake na Nicodemus Banduka?
..Raisi alitoa kauli hiyo wakati anatembelea jimbo la Mwanga ambako ndiko alikozaliwa Nicodemus Banduka.