Visasi vya JK kwa watu wa Arusha? Ahamishia mkutano wa wakuu wa EAC Dar

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,534
8,619
Ile kauli ya hasira na kisasi aliyoitoa Rais Kikwete tarehe 5 feb 2011 pale Nyerere Square wakati wa kusheherekea kuzaliwa CCM ambapo kwa hasira alisema...."...natamani kuhamisha shughuli za kimataifa Arusha ..." imeanza kudhibitika kuwa ni kweli..

Katika hali iliyoshangaza hata watu wa protocal wa jumuia ya Afrika mashariki....serikali ya Tanzania bila kutoa sababu ,waliwaeleza kuwa mkutano ulioanza leo ambao ulikuwa ufanyike Arusha ,makao makuu ya jumuia ya Afrika mashariki ,unafanyika DAR..Taarifa za kijasusi zinaeleza kuwa watu wa protocal wa nchi wanachama hawakupenda mkutano ufanyike dar ....hasa kutokana na usumbufu unaotokana na msongamano wa dar ambako ni kitovu cha biashara......hasa ikizingatiwa kuwa wakiwa Arusha huwawia rais kwa maafisa usalama wa nchi wanachama kuratibu vyema uwepo wa marais wao.....taarifa tulizonasa zinasema ,kama hali ikiendelea hivi wanatarajia kurudisha hoja ya kuhamishia makao makuu ya afrika mashariki nchi nyingine..kwani inaonekana Tanzania hawataki nafasi hiyo na wanaelekea kuitelekeza Arusha yalipo makao makuu ya jumuia...
Wachambuzi wa mambo wanachukulia hatua ya Kikwete kuchukia Arusha ghafla na kuwa tayari kuweka rehani Arusha kama mji wa kimataifa kama ni tabia mbaya na ya kisasi kufanywa na mkuu wa nchi........watu kutoka Kenya wanajiuliza kama angekuwa rais kwao angefanyaje kwa watu wa Nairobi ...ambao hawakumpa Kibaki kura ..lakini mara zote Kenya ilikuwa mstari wa mbele kutetea ofisi za kanda za UMOJA WA MATAIFA zilizopo GILGIL ,NAIROBI zisihamishwe kama adhabu ya vurugu za baada ya uchaguzi,,,,,na wameendeelea kupiga ndogondogo kuwa makao makuu ya jumuia yahamishiwe Nairobi.....

Ushauri wangu kwa wananchi kwa ujumla wetu na hususan wakazi wa Arusha ni kuhakikisha mnapaza sauti kuhakikisha chuki na visasi vya kisiasa visigharimu nchi kwa kupoteza nafasi ya Arusha kam Geneva ,of Africa..kwa kuwa haya maneno ya kusudio la kuwabagua aliyaongea Rais hadharani na tunaona anaaza kutekeleza kwa kuinyima Arusha fursa zake..za kimataifa ...kuna umuhimu wa wazee wa Arusha na wa Tanzania kwa ujumla kumfuata Rais na kumueleza wazi kuwa chuki za kisiasa na visasi havitakiwi kutufikisha huko......ili kutoa fursa kwenye nchi kuna migawanyo ndio maana kwa mfano ukienda afrika kusini kuna makao makuu ya serikali,bunge,biashara ,etc...miji ya pretoria,johanesburg,capetown etc kila mmoja una role yake .....hapa kwetu pamoja na kuwa kwenye katiba haipo ...tunajuwa kuwa ...dar es salaam ni mji wa kibiashara,dodoma -serikali,na Arusha -makao makuu ya jumuia na mashirika ya kimataifa...ni muhimu kupinga mbinu yeyote ya ku undermine eneo kwa ajili ya visasi....kwani ni muhimu tuweke Taifa mbele!!!

Mungu ibariki Tanzania!!!!
 
Sasa asipofanya hivyo watu wa Arusha watajuaje kuwa yeye ndiye Rais na chama chake ndicho kilichoko madarakani?
Mwanakijiji na wewe unaingia kwenye mtego huu??? Kwamba ni kisasi?? This is too low. Inamaana Arusha ndio sehem pekee nchi hii panapostahili mikutano yote? Na mikutano haijawahi kufanyikia DSM? Hizi ni hoja za kitoto
 
Duh! Ni uamuzi wa kipuuzi kweli kweli! Rais wa nchi unafanya maamuzi ya kuikomoa sehemu moja ndani ya nchi yako kwa vile tu Wananchi wa sehemu hiyo hawakipigii kura chama chako! Kweli hizi ni dalili za kutapatapa.
 
Mwanakijiji na wewe unaingia kwenye mtego huu??? Kwamba ni kisasi?? This is too low. Inamaana Arusha ndio sehem pekee nchi hii panapostahili mikutano yote? Na mikutano haijawahi kufanyikia DSM? Hizi ni hoja za kitoto

From your urgument kama sio sehemu pekee ya nchi why CCM vikao vyao wanafanyia Dodoma? Si ndiko yaliko makao makuu? Why wasiende kufanyia Chanika au Kitunda? Nayo si ni sehemu ya nchi?
 
Mwanakijiji na wewe unaingia kwenye mtego huu??? Kwamba ni kisasi?? This is too low. Inamaana Arusha ndio sehem pekee nchi hii panapostahili mikutano yote? Na mikutano haijawahi kufanyikia DSM? Hizi ni hoja za kitoto

Labda unaweza ukapendekeza sababu ya msingi yenye kushawishi akili ya kwanini mkutano wa Afrika ya Mashariki haukufanyika Arusha yaliko makao makuu ya Afrika ya Mashariki? Ni mara ngapi mkutano wa viongozi hao umefanyika Dar au Dodoma?
 
Hii sio kweli, lazima kuna sababu za msingi. Yeye kama yeye hawezi ghafla kubadilisha sehemu ya mkutano kwa kuwa kuna kamati ya maandalizi naye siyo mjumbe.Haiwezekani kabisa.
 
Hii sio kweli, lazima kuna sababu za msingi. Yeye kama yeye hawezi ghafra kubadilisha sehemu ya mkutano kwa kuwa kuna kamati ya maandalizi naye siyo mjumbe.Haiwezekani kabisa.

hujui uncahoongea hebu nenda kalale bana unajaza forum tu hapa na urguments zako za kitoto...
 
Ile kauli ya hasira na kisasi aliyoitoa Rais Kikwete tarehe 5 feb 2011 pale Nyerere Square wakati wa kusheherekea kuzaliwa CCM ambapo kwa hasira alisema...."...natamani kuhamisha shughuli za kimataifa Arusha ..." imeanza kudhibitika kuwa ni kweli..

Katika hali iliyoshangaza hata watu wa protocal wa jumuia ya Afrika mashariki....serikali ya Tanzania bila kutoa sababu ,waliwaeleza kuwa mkutano ulioanza leo ambao ulikuwa ufanyike Arusha ,makao makuu ya jumuia ya Afrika mashariki ,unafanyika DAR..Taarifa za kijasusi zinaeleza kuwa watu wa protocal wa nchi wanachama hawakupenda mkutano ufanyike dar ....hasa kutokana na usumbufu unaotokana na msongamano wa dar ambako ni kitovu cha biashara......hasa ikizingatiwa kuwa wakiwa Arusha huwawia rais kwa maafisa usalama wa nchi wanachama kuratibu vyema uwepo wa marais wao.....taarifa tulizonasa zinasema ,kama hali ikiendelea hivi wanatarajia kurudisha hoja ya kuhamishia makao makuu ya afrika mashariki nchi nyingine..kwani inaonekana Tanzania hawataki nafasi hiyo na wanaelekea kuitelekeza Arusha yalipo makao makuu ya jumuia...
Wachambuzi wa mambo wanachukulia hatua ya Kikwete kuchukia Arusha ghafla na kuwa tayari kuweka rehani Arusha kama mji wa kimataifa kama ni tabia mbaya na ya kisasi kufanywa na mkuu wa nchi........watu kutoka Kenya wanajiuliza kama angekuwa rais kwao angefanyaje kwa watu wa Nairobi ...ambao hawakumpa Kibaki kura ..lakini mara zote Kenya ilikuwa mstari wa mbele kutetea ofisi za kanda za UMOJA WA MATAIFA zilizopo GILGIL ,NAIROBI zisihamishwe kama adhabu ya vurugu za baada ya uchaguzi,,,,,na wameendeelea kupiga ndogondogo kuwa makao makuu ya jumuia yahamishiwe Nairobi.....

Ushauri wangu kwa wananchi kwa ujumla wetu na hususan wakazi wa Arusha ni kuhakikisha mnapaza sauti kuhakikisha chuki na visasi vya kisiasa visigharimu nchi kwa kupoteza nafasi ya Arusha kam Geneva ,of Africa..kwa kuwa haya maneno ya kusudio la kuwabagua aliyaongea Rais hadharani na tunaona anaaza kutekeleza kwa kuinyima Arusha fursa zake..za kimataifa ...kuna umuhimu wa wazee wa Arusha na wa Tanzania kwa ujumla kumfuata Rais na kumueleza wazi kuwa chuki za kisiasa na visasi havitakiwi kutufikisha huko......ili kutoa fursa kwenye nchi kuna migawanyo ndio maana kwa mfano ukienda afrika kusini kuna makao makuu ya serikali,bunge,biashara ,etc...miji ya pretoria,johanesburg,capetown etc kila mmoja una role yake .....hapa kwetu pamoja na kuwa kwenye katiba haipo ...tunajuwa kuwa ...dar es salaam ni mji wa kibiashara,dodoma -serikali,na Arusha -makao makuu ya jumuia na mashirika ya kimataifa...ni muhimu kupinga mbinu yeyote ya ku undermine eneo kwa ajili ya visasi....kwani ni muhimu tuweke Taifa mbele!!!

Mungu ibariki Tanzania!!!!
Mkuu Phillemon Mikael, asumption ni kitu kinachoruhusiwa hata kama asumption hiyo is based on a wrong premes. Ni kweli Arusha ndio makao makuu ya EAC na makao makuu ya kudumu ya EAC yanajengwa pale jirani na ICC, hivyo hakuna tena discusion makao makuu yawe wapi.

Kenya haifanyi tena lobbying kuhodhi makao makuu ya EAC bali wanapiga ndogo ndogo achives za ICTR zihamishiwe Nairobi na hapa lengo sio kuhifadhi achives hizo, bali the life time stream of money toka UN pamoja na kutrap all future research funds on Rwandan genocide.

Mikutano ya EAC, huamuliwa kwenye vikao ifanyike wapi, sio lazima ifanyike Arusha, kama lilivyo bunge la EALA, kikao kinafanyika nchi yoyote ya jumuiya hii na ni host nation itaamua mkutano ufanyike mji gani.

JK akiamua kuikomoa Arusha, atamteu Dr. Burian, RC wa Arusha kama alivyomteau mkuu wa mkoa wa Mbeya baada ya kubwagwa. Subirini tuone!.
 
Yataisha haya baada ya muda mfupi tu 2015 sio mbali pili ni kosa kubwa sana, kwanza ni usumbufu kwa wananchi wa Dar tatu Arusha ni mji unaojitangaza wenyewe na sio serikali, so watarudi wenyewe tu kwa sababu Arusha ina vivutio vingi sana na vitega uchumi vingi sana kwa taifa hili la tanzania, pia ina mchango mkubwa sana kwa uchumi wa taifa letu kuliko hata huko walikokimbizia huo mkutano. Kwa hiyo waacheni wajisumbue next president atarudisha tu na aibu itabaki kwao!
Sasa asipofanya hivyo watu wa Arusha watajuaje kuwa yeye ndiye Rais na chama chake ndicho kilichoko madarakani?
 
Seriously huu uamuzi wa kuufanya mkutano huu Dar es Salaam badala ya Arusha umekuwa na negative impact kwa jiji kwa ujumla kwani jana (j3) kulikuwa na foleni isiyokuwa na kifani mida ya jioni. I wonder if they took all these into account when they took the decision to move this meeting from Arusha to Dar....
 
Labda unaweza ukapendekeza sababu ya msingi yenye kushawishi akili ya kwanini mkutano wa Afrika ya Mashariki haukufanyika Arusha yaliko makao makuu ya Afrika ya Mashariki? Ni mara ngapi mkutano wa viongozi hao umefanyika Dar au Dodoma?

Kwa Dodoma hawawezi Mwanakijiji, kwa sababu Dodoma haina uhusiano wowote na EAC ila ina uhusiano na Chama Cha Mapinduzi. Kwanza nashangaa hata wanavyosema kua makao makuu ya chama na serikali yapo Dodoma wakati wao wanaishi Dar na kazi nyingi kiserikali wanafanyia Dar. Dodoma wanaenda tu kwa vikao na vikishaisha wanachomoka. Kweli serikali inaingia gharama kubwa sana zisizo na msingi, pia Dar kwa hali ya hewa ilivyo traffic, utitiri wa magari na population bado inabaki kuwa ni usumbufu kwa raia na viongozi. Pia ni aibu kwa taifa, bado mimi naamini kwamba kizuri chajiuza kibaya chajitembeza haya ni mapito tu, baadae wao wenyewe wata realize kwamba Arusha ndio sehemu nzuri kwa mikutano.
 
Hakuna sababu nyingine ni kisasi na ubishoo, nakubaliana na mwanakijiji, huyu bwana sijui ana akili gani kwanza angalieni kwenye TV washiriki walivyodhalilishwa kwenye vile viji siti vidogo, wamebanana kama nyanya hakuna quality anatutia aibu sana na si Arusha tu kwani hajui kwamba ni mikoa yote tulimkataa? Anajua alipata 27% atoke atuachie nchi yetu hatutaki kiongozi kama huyu asiyeona mbali. Halafu ulisikia maongezi yenyewe rejea za kujenga barabara zilizopo alisema kutoka Arusha, Dodoma na Iringa, eti wakenya waweze kupeleka mizigo yao afrika kusini jamani hajui kwa nini hawafanyi hivyo?
 
Nilishasema hili long time, mkuu anaendesha nchi kimajungu zaidi kuliko utashi, itadhihirika taratibu. muda ndiyo kipimo halisi
 
hivi mkutano ulipofanyika hiyo jana ..........ulikuwa jimbo gani na mbunge wake ni wa jimbo gani?
 
HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KATIKA SHEREHE ZA
KUTIMIZA MIAKA 34 YA KUZALIWA KWA CCM
UWANJA WA JAMHURI, DODOMA
TAREHE 05 FEBRUARI, 2011

CCM Oyee!
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!

Ndugu William Kusila; Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma;
Ndugu Lt. Mst. Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM;
Waheshimiwa Wabunge;
NduguViongozi mbalimbali mlioko hapa;
Ndugu Wana-CCM na
Ndugu Wananchi;

Utangulizi:
Naomba nianze kwa kuwashukuru wenyeji wetu, viongozi, wana-CCM na wananchi wa Dodoma kwa mapokezi mazuri na kwa maandalizi mazuri ya sherehe hii. Sherehe zimefana sana. Sisi sote ni mashahidi. Vile vile matembezi ya mshikamano yalikuwa mazuri ingawaje umbali ulikuwa mfupi kidogo. Safari ijayo tufikirie kuongeza umbali.
Utawala wa Sheria
Ndugu Wana-CCM na Ndugu Wananchi;
Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwaka 2010, nilidokeza taarifa ambazo vyombo vya usalama vinazo kuhusu mipango ya makusudi ya uvunjifu wa amani kwa kutumia njia ya migomo na maandamano. Niliwatanabaisha ndugu zangu kutambua njama hizo na kuepuka kushiriki katika maandamano au migomo ya aina hiyo. Wanaoandaa wana agenda yao ya kisiasa iliyojificha nyuma ya jambo linalotangulizwa kama sababu. Wanataka kujitengenezea mazingira ya ushindi mwaka 2015 kwa vurugu. Nilitahadharisha kuwa watu wajiepushe kugeuzwa mbuzi wa kafara kwa kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani fulani.
Niliyoyasema yametokea Arusha na dalili zipo za mipango ya namna ile kuandaliwa kutokea sehemu nyingine hapa nchini. Napenda kurudia tena kuwasihi Watanzania wenzangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hao. Wanawasakizia kwenye hatari ambayo mnaweza kuiepuka. Naomba muwakumbushe tena kuwa wanayo fursa Bungeni na kwenye majukwaa mbalimbali kutoa hoja zao badala ya kuwagombanisha nyinyi na vyombo vya dola. Niwaombe wanasiasa wenzangu kutumia fursa tele walizonazo badala ya njia ya uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha na mali za watu pamoja na kuharibu sifa ya nchi yetu.
Ndugu Viongozi, Wana-CCM Wenzangu na Wananchi Wenzangu;
Ukweli huu ndiyo uliotupatia ushindi mnono katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010 pamoja na vitimbi na mbinu chafu tulizofanyiwa na wapinzani wetu. Wakati mwingine haya yanayoendelea sasa ya vurugu zinazofanywa na wapinzani wetu ni hasira ya hasara waliyoipata, hasa wakikumbuka kiasi walichowekeza, pamoja na ubaya na hujuma mbalimbali walizotutendea bila ya mafanikio. Wanasahau Mola ndiye mtoaji. Akiandika kupata unapata.
Kwa nini tujisikie wanyonge baada ya kupata ushindi mnono kiasi hicho? Nadhani tunatishwa na kelele na propaganda za Chama fulani na Bwana fulani ambazo zinajenga hisia kama vile wako wengi sana na wamepata ushindi mkubwa sana hata kuliko CCM. Hilo si kweli, ingawaje safari hii wamepata viti vingi kuliko uchaguzi uliopita. Ukweli ni kwamba Chama hicho kimepata asilimia tisa tu ya viti vyote vya Majimbo.

Ndugu Wana-CCM na Ndugu Wananchi;
Miongoni mwa mambo mengine ambayo tutayafanya mwaka huu ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya nchi yetu kwa nia ya kuihuisha na hatimaye kuzaa Katiba mpya inayolingana na taifa lenye umri wa miaka hamsini na itakayotupeleka miaka 50 ijayo. Kiserikali matayarisho yanaendelea ya kupeleka Bungeni Mswada wa Sheria wa kuanzisha mchakato huo ikijumuisha kuundwa kwa Tume ya kuongoza mchakato huo.
Hata kama kusingekuwepo mapendekezo ya CUF, CHADEMA na wengineo ilikuwa ni dhamira yetu kufanya hivyo

Utawala wa Sheria
Ndugu Wana-CCM na Ndugu Wananchi;
Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwaka 2010, nilidokeza taarifa ambazo vyombo vya usalama vinazo kuhusu mipango ya makusudi ya uvunjifu wa amani kwa kutumia njia ya migomo na maandamano. Niliwatanabaisha ndugu zangu kutambua njama hizo na kuepuka kushiriki katika maandamano au migomo ya aina hiyo. Wanaoandaa wana agenda yao ya kisiasa iliyojificha nyuma ya jambo linalotangulizwa kama sababu. Wanataka kujitengenezea mazingira ya ushindi mwaka 2015 kwa vurugu. Nilitahadharisha kuwa watu wajiepushe kugeuzwa mbuzi wa kafara kwa kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani fulani.
Niliyoyasema yametokea Arusha[wakati mwingine natamani kuhamisha shughuli na maofisi ya kimataifa pale] na dalili zipo za mipango ya namna ile kuandaliwa kutokea sehemu nyingine hapa nchini. Napenda kurudia tena kuwasihi Watanzania wenzangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hao. Wanawasakizia kwenye hatari ambayo mnaweza kuiepuka. Naomba muwakumbushe tena kuwa wanayo fursa Bungeni na kwenye majukwaa mbalimbali kutoa hoja zao badala ya kuwagombanisha nyinyi na vyombo vya dola. Niwaombe wanasiasa wenzangu kutumia fursa tele walizonazo badala ya njia ya uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha na mali za watu pamoja na kuharibu sifa ya nchi yetu

Asanteni kwa kunisikiliza!
Kidumu Chama cha Mapinduzi!
 
....JUU NIMEWEKA HOTUBA ALIYOSOMA ....MANENO ALIYOTAMKA JUU YA ARUSHA ...ALITAMKA KWENYE MSISITIZO ...JUU YA KILICHOTOKEA ARUSHA ...IWAPO TUTAPATA VIDEO CLIP YA HOTUBA YA RAIS PALE DODOMA TAREHE 5/2/2011 HAYA YATAJIELEZA WAZI....MWENDELEZO WA CHUKI HIZI PIA UMEJIDHIHIRISHA KWENYE TAMKO LA UMOJA WA VIJANA BAGAMOYO AMBAPO MTOTO WA RAIS ALIKUWAPO....

UKWELI NI KUWA KWENYE MKUTANO WA SEKRETARIET YA AFRIKA MASHARIKI ILIYOKETI ARUSHA KUANDAA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI JANA....KULIKUWA NA UBISHI MKALI KUTOKA KWA NCHI WANACHAMA AMBAZO ZILIKWERWA NA UAMUZI WA TANZANIA KUPELEKA MKUTANO DAR BILA KUWASIKILIZA .....WAO WANAONA KUTOKANA NA MISONGAMANO YA DAR NA UZOEFU WA MIKUTANO ILIYOPITA .....INAWAWIA VIGUMU WASHIRIKI KUFIKA SEHEMU KWA WAKATI....HASA WALE AMBAO HAWAPO KWENYE MISAFARA YA VIONGOZI WAO MOJA KWA MOJA....NA KWA UJUMLA PAMOJA NA UKUBWA WA DAR .....MIKUTANO MINGI IMEKUWA USUMBUFU KWAO NA KWA WANANCHI ....HASA PIA KUTOKANA NA MIUNDOMBINU KUTOKUWA RAFIKI...

KAMA DAR INATAKA KUVUTIA MIKUTANO BILA KUWEKA USUMBUFU KWA WASHIRIKI NI BORA WAFIKIRIE KUWA NA VILLAGE AMBAYO ITAJUMUISHA PIA SEHEMU ZA MALAZI ...KAMA ILIVYO KAMPALA,[COMMONWEALTH VILLAGE],NA NAIROBI[GILGIL]..etc.......lakini kama tutaendelea kulazimisha mambo tutapoteza nafasi ya ARUSHA AMBAPO NI ...MAKAO MAKUU YA AFRIKA MASHARIKI,CHUO CHA UONGOZI AFRIKA ,CHUO KIKUU CHA TEKNELOJIA AFRIKA ,MANDELA,SHIRIKISHO LA POSTA AFRIKA,MAKAKAMA YA RWANDA[na hata tuki lobby vema mahakama ya HAGUE wanataka kuweka tawi pale],mahakama kuu ya afrika,mahakama ya afrika mashariki...etc....are we ready to lose everything just kwa ajili ya visasi?????????......narudia tena kama ingekuwa visasi basi Kibaki angeutenga mji wa nairobi....na kulikuWA na hati hati ya makao makuu ya umoja wa mataifa na habitat ihame nairobi....ingeweza kuletwa Arusha au kuhama kabisa ukanda huu....
 
Back
Top Bottom