Visasi vya JK kwa watu wa Arusha? Ahamishia mkutano wa wakuu wa EAC Dar

Foleni ya leo tar 19 Aprili 2011 ni kiboko kweli kweli, shuguli za kawaida hapa mjini zitaanza Saa nne asubuhi. Yote kwa sababu ya ujinga wa mtu mmoja.
 
hivi mkutano ulipofanyika hiyo jana ..........ulikuwa jimbo gani na mbunge wake ni wa jimbo gani?

Edson unataka kusema Ubungo..sio ..na wageni walilala jimbo gani??? na walitua jimbo gani....

tunaongelea mambo serious ..yametokea kwenye circle ...na wenzetu kwenye EAC Wanatushaangaa sana....si walazimishi kuamini haya..but ndio ukweli halisi........Tazama hata kampala Museveni hapendwi lakini hajahamishia mikutano Jinja au RWAKITURA
 
aiseee nimeisoma hiyo hotuba kweli kuna watu vilaza duniani!

no wonder he is not my president...
 
Sasa asipofanya hivyo watu wa Arusha watajuaje kuwa yeye ndiye Rais na chama chake ndicho kilichoko madarakani?

Katika kile ulifanyalo ni lazima ujieandae na madhara yake,

Arusha ilipokubali kugeuzwa kuwa kitovu cha mapambano ya kisiasa ni lazima wawe tayari kufaidi matamu na machungu yake. Kama kiongozi wa nchi Rais ana wajibu wa kuhakikisha hawaexpose wakuu wa nchi zingine na rabsha za kisiasa ambazo ni vigumu kuzitabiri kutokana na hali ya kisiasa Arusha lakini pia ukichukulia historia isiyo nzuri ya jiji hilo kiusalama huko nyuma.

Lakini pia ni wazi gharama zingekuwa kubwa zaidi kufanya kikao cha wakuu wa nchi Arusha halafu kuwakimbiza katika jiji kitovu cha biashara Dar ili kushiriki kikamilifu katika mkutano wa uwekezaji ambao umetayarishwa na kituo cha uwekezaji chini ya Mwana - Arusha Ole Naiko kwa kushirikiana na Commonwealth

All in all, katika kila ukulima, unavuna ulichopanda. Na ni wajibu wa mpiganaji wa kweli kuembrace ukweli huo badala ya ku-agonise...
 
Foleni ya leo tar 19 Aprili 2011 ni kiboko kweli kweli, shuguli za kawaida hapa mjini zitaanza Saa nne asubuhi. Yote kwa sababu ya ujinga wa mtu mmoja.
Ndio maana tuliamua kuhamisha ofisi zetu kutoka mjini sababu ya upuuzi kama huu
 
Mwanakijiji na wewe unaingia kwenye mtego huu??? Kwamba ni kisasi?? This is too low. Inamaana Arusha ndio sehem pekee nchi hii panapostahili mikutano yote? Na mikutano haijawahi kufanyikia DSM? Hizi ni hoja za kitoto

Nadhani ni busara ukamsoma tena mtoa hoja kabla hujampalamia. Baada ya kusoma combine na akili zako ndipo utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujuwa kilichoandikwa. Rejea alichokisema dodoma huyo rais wenu na sababu za msingi hasa za kuamishia kikao Dar badala ya Arusha. It feels very bad indeed time and again kujuwa kwamba we have a very very wrong person at Magogoni.
 
Katika kile ulifanyalo ni lazima ujieandae na madhara yake,

Arusha ilipokubali kugeuzwa kuwa kitovu cha mapambano ya kisiasa ni lazima wawe tayari kufaidi matamu na machungu yake. Kama kiongozi wa nchi Rais ana wajibu wa kuhakikisha hawaexpose wakuu wa nchi zingine na rabsha za kisiasa ambazo ni vigumu kuzitabiri kutokana na hali ya kisiasa Arusha lakini pia ukichukulia historia isiyo nzuri ya jiji hilo kiusalama huko nyuma.

Lakini pia ni wazi gharama zingekuwa kubwa zaidi kufanya kikao cha wakuu wa nchi Arusha halafu kuwakimbiza katika jiji kitovu cha biashara Dar ili kushiriki kikamilifu katika mkutano wa uwekezaji ambao umetayarishwa na kituo cha uwekezaji chini ya Mwana - Arusha Ole Naiko kwa kushirikiana na Commonwealth

All in all, katika kila ukulima, unavuna ulichopanda. Na ni wajibu wa mpiganaji wa kweli kuembrace ukweli huo badala ya ku-agonise...
Hili umeliona leo??? Vivyo hivyo kimsingi hapo naona kuna suala jingine tu mtu huwezi kuniambia eti Rais anachukua precaution measures za kuhamisha mkutano (Kama ni kweli) kutoka Arusha kuja Dar eti kwasababu ya kutowaexpose wakuu wa nchi nyingine na rabsha kwani hao wakuu sisi tuna ajenda gani nao hadi tuwadhuru vile vile ghasia za uchaguzi za Arusha ikumbukwe wao wenyewe ndio chanzo mpaka yametokea hayo yaliyotokea.

Pia nikisoma hotuba ya JK iliyowekwa hapa na mmoja wa member nadiriki kusema inawezekana kuna ukweli fulani kutokana na jinsi tunavyomjua JK kwa visasi na jazba
 
Hayo nayo yana mwisho, acha atapetape, ukweli utajulikana 2
Ile kauli ya hasira na kisasi aliyoitoa Rais Kikwete tarehe 5 feb 2011 pale Nyerere Square wakati wa kusheherekea kuzaliwa CCM ambapo kwa hasira alisema...."...natamani kuhamisha shughuli za kimataifa Arusha ..." imeanza kudhibitika kuwa ni kweli..

Katika hali iliyoshangaza hata watu wa protocal wa jumuia ya Afrika mashariki....serikali ya Tanzania bila kutoa sababu ,waliwaeleza kuwa mkutano ulioanza leo ambao ulikuwa ufanyike Arusha ,makao makuu ya jumuia ya Afrika mashariki ,unafanyika DAR..Taarifa za kijasusi zinaeleza kuwa watu wa protocal wa nchi wanachama hawakupenda mkutano ufanyike dar ....hasa kutokana na usumbufu unaotokana na msongamano wa dar ambako ni kitovu cha biashara......hasa ikizingatiwa kuwa wakiwa Arusha huwawia rais kwa maafisa usalama wa nchi wanachama kuratibu vyema uwepo wa marais wao.....taarifa tulizonasa zinasema ,kama hali ikiendelea hivi wanatarajia kurudisha hoja ya kuhamishia makao makuu ya afrika mashariki nchi nyingine..kwani inaonekana Tanzania hawataki nafasi hiyo na wanaelekea kuitelekeza Arusha yalipo makao makuu ya jumuia...
Wachambuzi wa mambo wanachukulia hatua ya Kikwete kuchukia Arusha ghafla na kuwa tayari kuweka rehani Arusha kama mji wa kimataifa kama ni tabia mbaya na ya kisasi kufanywa na mkuu wa nchi........watu kutoka Kenya wanajiuliza kama angekuwa rais kwao angefanyaje kwa watu wa Nairobi ...ambao hawakumpa Kibaki kura ..lakini mara zote Kenya ilikuwa mstari wa mbele kutetea ofisi za kanda za UMOJA WA MATAIFA zilizopo GILGIL ,NAIROBI zisihamishwe kama adhabu ya vurugu za baada ya uchaguzi,,,,,na wameendeelea kupiga ndogondogo kuwa makao makuu ya jumuia yahamishiwe Nairobi.....

Ushauri wangu kwa wananchi kwa ujumla wetu na hususan wakazi wa Arusha ni kuhakikisha mnapaza sauti kuhakikisha chuki na visasi vya kisiasa visigharimu nchi kwa kupoteza nafasi ya Arusha kam Geneva ,of Africa..kwa kuwa haya maneno ya kusudio la kuwabagua aliyaongea Rais hadharani na tunaona anaaza kutekeleza kwa kuinyima Arusha fursa zake..za kimataifa ...kuna umuhimu wa wazee wa Arusha na wa Tanzania kwa ujumla kumfuata Rais na kumueleza wazi kuwa chuki za kisiasa na visasi havitakiwi kutufikisha huko......ili kutoa fursa kwenye nchi kuna migawanyo ndio maana kwa mfano ukienda afrika kusini kuna makao makuu ya serikali,bunge,biashara ,etc...miji ya pretoria,johanesburg,capetown etc kila mmoja una role yake .....hapa kwetu pamoja na kuwa kwenye katiba haipo ...tunajuwa kuwa ...dar es salaam ni mji wa kibiashara,dodoma -serikali,na Arusha -makao makuu ya jumuia na mashirika ya kimataifa...ni muhimu kupinga mbinu yeyote ya ku undermine eneo kwa ajili ya visasi....kwani ni muhimu tuweke Taifa mbele!!!

Mungu ibariki Tanzania!!!!
 
HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KATIKA SHEREHE ZA
KUTIMIZA MIAKA 34 YA KUZALIWA KWA CCM
UWANJA WA JAMHURI, DODOMA
TAREHE 05 FEBRUARI, 2011

CCM Oyee!
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!

Ndugu William Kusila; Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma;
Ndugu Lt. Mst. Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM;
Waheshimiwa Wabunge;
NduguViongozi mbalimbali mlioko hapa;
Ndugu Wana-CCM na
Ndugu Wananchi;

Utangulizi:
Naomba nianze kwa kuwashukuru wenyeji wetu, viongozi, wana-CCM na wananchi wa Dodoma kwa mapokezi mazuri na kwa maandalizi mazuri ya sherehe hii. Sherehe zimefana sana. Sisi sote ni mashahidi. Vile vile matembezi ya mshikamano yalikuwa mazuri ingawaje umbali ulikuwa mfupi kidogo. Safari ijayo tufikirie kuongeza umbali.

Utawala wa Sheria
Ndugu Wana-CCM na Ndugu Wananchi;
Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwaka 2010, nilidokeza taarifa ambazo vyombo vya usalama vinazo kuhusu mipango ya makusudi ya uvunjifu wa amani kwa kutumia njia ya migomo na maandamano. Niliwatanabaisha ndugu zangu kutambua njama hizo na kuepuka kushiriki katika maandamano au migomo ya aina hiyo. Wanaoandaa wana agenda yao ya kisiasa iliyojificha nyuma ya jambo linalotangulizwa kama sababu. Wanataka kujitengenezea mazingira ya ushindi mwaka 2015 kwa vurugu. Nilitahadharisha kuwa watu wajiepushe kugeuzwa mbuzi wa kafara kwa kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani fulani.
Niliyoyasema yametokea Arusha na dalili zipo za mipango ya namna ile kuandaliwa kutokea sehemu nyingine hapa nchini. Napenda kurudia tena kuwasihi Watanzania wenzangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hao. Wanawasakizia kwenye hatari ambayo mnaweza kuiepuka. Naomba muwakumbushe tena kuwa wanayo fursa Bungeni na kwenye majukwaa mbalimbali kutoa hoja zao badala ya kuwagombanisha nyinyi na vyombo vya dola. Niwaombe wanasiasa wenzangu kutumia fursa tele walizonazo badala ya njia ya uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha na mali za watu pamoja na kuharibu sifa ya nchi yetu.

Ndugu Viongozi, Wana-CCM Wenzangu na Wananchi Wenzangu;
Ukweli huu ndiyo uliotupatia ushindi mnono katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010 pamoja na vitimbi na mbinu chafu tulizofanyiwa na wapinzani wetu. Wakati mwingine haya yanayoendelea sasa ya vurugu zinazofanywa na wapinzani wetu ni hasira ya hasara waliyoipata, hasa wakikumbuka kiasi walichowekeza, pamoja na ubaya na hujuma mbalimbali walizotutendea bila ya mafanikio. Wanasahau Mola ndiye mtoaji. Akiandika kupata unapata.

Kwa nini tujisikie wanyonge baada ya kupata ushindi mnono kiasi hicho? Nadhani tunatishwa na kelele na propaganda za Chama fulani na Bwana fulani ambazo zinajenga hisia kama vile wako wengi sana na wamepata ushindi mkubwa sana hata kuliko CCM. Hilo si kweli, ingawaje safari hii wamepata viti vingi kuliko uchaguzi uliopita. Ukweli ni kwamba Chama hicho kimepata asilimia tisa tu ya viti vyote vya Majimbo.

Ndugu Wana-CCM na Ndugu Wananchi;
Miongoni mwa mambo mengine ambayo tutayafanya mwaka huu ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya nchi yetu kwa nia ya kuihuisha na hatimaye kuzaa Katiba mpya inayolingana na taifa lenye umri wa miaka hamsini na itakayotupeleka miaka 50 ijayo. Kiserikali matayarisho yanaendelea ya kupeleka Bungeni Mswada wa Sheria wa kuanzisha mchakato huo ikijumuisha kuundwa kwa Tume ya kuongoza mchakato huo.
Hata kama kusingekuwepo mapendekezo ya CUF, CHADEMA na wengineo ilikuwa ni dhamira yetu kufanya hivyo

Utawala wa Sheria
Ndugu Wana-CCM na Ndugu Wananchi;
Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwaka 2010, nilidokeza taarifa ambazo vyombo vya usalama vinazo kuhusu mipango ya makusudi ya uvunjifu wa amani kwa kutumia njia ya migomo na maandamano. Niliwatanabaisha ndugu zangu kutambua njama hizo na kuepuka kushiriki katika maandamano au migomo ya aina hiyo. Wanaoandaa wana agenda yao ya kisiasa iliyojificha nyuma ya jambo linalotangulizwa kama sababu. Wanataka kujitengenezea mazingira ya ushindi mwaka 2015 kwa vurugu. Nilitahadharisha kuwa watu wajiepushe kugeuzwa mbuzi wa kafara kwa kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani fulani.
Niliyoyasema yametokea Arusha[wakati mwingine natamani kuhamisha shughuli na maofisi ya kimataifa pale] na dalili zipo za mipango ya namna ile kuandaliwa kutokea sehemu nyingine hapa nchini. Napenda kurudia tena kuwasihi Watanzania wenzangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hao. Wanawasakizia kwenye hatari ambayo mnaweza kuiepuka. Naomba muwakumbushe tena kuwa wanayo fursa Bungeni na kwenye majukwaa mbalimbali kutoa hoja zao badala ya kuwagombanisha nyinyi na vyombo vya dola. Niwaombe wanasiasa wenzangu kutumia fursa tele walizonazo badala ya njia ya uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha na mali za watu pamoja na kuharibu sifa ya nchi yetu

Asanteni kwa kunisikiliza!

Kidumu Chama cha Mapinduzi!
Hizi zinaonekana ni jazba na hasira za kushindwa kwa CCM kwenye jimbo la Arusha
 
Mwanakijiji na wewe unaingia kwenye mtego huu??? Kwamba ni kisasi?? This is too low. Inamaana Arusha ndio sehem pekee nchi hii panapostahili mikutano yote? Na mikutano haijawahi kufanyikia DSM? Hizi ni hoja za kitoto

mwanakijiji hajaingia kwenye mtego kama unavyodhani, mwanakijiji amekupa rhetoric question inayolalia kuponda uamuzi wa kikwete. Kwa uamuzi usio wa busara wa namna hii wa JK, ukizingatia kuwa mamlaka ya jiji la nairobi imefikishwa mpaka namanga, ikiwa tabia hii itaendelea, tusishangae nchi wanachama wengine wa EAC wakipropose EAC Hq kutolewa Arusha.
 
Katika kile ulifanyalo ni lazima ujieandae na madhara yake,

Arusha ilipokubali kugeuzwa kuwa kitovu cha mapambano ya kisiasa ni lazima wawe tayari kufaidi matamu na machungu yake. Kama kiongozi wa nchi Rais ana wajibu wa kuhakikisha hawaexpose wakuu wa nchi zingine na rabsha za kisiasa ambazo ni vigumu kuzitabiri kutokana na hali ya kisiasa Arusha lakini pia ukichukulia historia isiyo nzuri ya jiji hilo kiusalama huko nyuma.

Lakini pia ni wazi gharama zingekuwa kubwa zaidi kufanya kikao cha wakuu wa nchi Arusha halafu kuwakimbiza katika jiji kitovu cha biashara Dar ili kushiriki kikamilifu katika mkutano wa uwekezaji ambao umetayarishwa na kituo cha uwekezaji chini ya Mwana - Arusha Ole Naiko kwa kushirikiana na Commonwealth

All in all, katika kila ukulima, unavuna ulichopanda. Na ni wajibu wa mpiganaji wa kweli kuembrace ukweli huo badala ya ku-agonise...

Sawasawa kabisa mwanaccm,

Hapo umepigia mstari kwamba mwenyekiti wako anaendesha nchi kwa visasi na jazba.

Ndiyo sababu ya kutaka kuhamishia uwanja wa ndege na bandari bagamoyo kwasababu ya visasi, ubinafsi na jazba.

Nadhani muda si mrefu mikutano yote ya kimataifa itahamishiwa bagamoyo, kwakuwa huko hakuna "vurugu" wala "upinzani" kwa ccm na rais jk.
 
Sawasawa kabisa mwanaccm,

Hapo umepigia mstari kwamba mwenyekiti wako anaendesha nchi kwa visasi na jazba. Ndiyo sababu ya kutaka kuhamishia uwanja wa ndege na bandari bagamoyo kwasababu ya visasi, ubinafsi na jazba. Nadhani muda si mrefu mikutano yote ya kimataifa itahamishiwa bagamoyo, kwakuwa huko hakuna "vurugu" wala "upinzani" kwa ccm na rais jk.

With petty and shallow mindness like this its obvious the UKOMBOZI we are forced to trust is never the one that we dream of....
 
With petty and shallow mindness like this its obvious the UKOMBOZI we are forced to trust is never the one that we dream of....[/QUOTE]

We endelea kuota tu, kwani ni kawaida yenu kuota ndoto tena za mchana.

Mwenyekiti wako anaendesha nchi kwa visasi na wewe unashadidia kwa kuwakejeli watu wa arusha, sasa kuambiwa ukweli unaanza kutapatapa.

Nadhani kati ya watu wenye shallow minded wewe ni kiongozi wao, labda hadi hapo utakapojiruhusu kujitoa kwenye box lenu la ufisadi.
 
Habari zilizopo za kiterijensia zinasema kwamba Chadema walikua wameandaa maandamano Arusha na yange ishia nje ya ukumbi kunako fanyiwa mkutano!
 
Foleni ya leo tar 19 Aprili 2011 ni kiboko kweli kweli, shuguli za kawaida hapa mjini zitaanza Saa nne asubuhi. Yote kwa sababu ya ujinga wa mtu mmoja.

Mkuu imenichukua masaa 2 kutoka Mwenge kufika Millenium tower hapo kijitonyama. Hii traffic jam ni balaa hakuna tofauti na India. Nimemchukia sana ****** nilipokumbuka akisema kuongezeka kwa foleni na magari Dar ni sababu ya maendeleo yaliyoletwa na chama chake!!
 
Binafsi sishangai kwa Kikwete kutumia visasi kwani hata waziri Magufuli anatumia sana visasi kuwaumiza watu wengine. Mfano kwa hili ni alivyo kwepesha barabara ya lami badala ipitie makao makuu ya wilaya Biharamulo yeye aliipitisha chato ili hali wakati huo chato haikuwa wilaya.

Tuseme CCM kawaida wana mkakati wa kutumia visasi kwa watu/vyama vinavyo wapinga. Lakini mwisho wake ni kukosa fursa zote kwa sababu ya ujinga wa visasi.

Kikwete acha visasi........ huoni aibu kuwatesa watanzania wenzako??? Mbona Mkapa pamoja na wizi wote aliowaibia watanzania bado analalia kitanda kimoja ndani ya chumba kimoja na siyo viwili???
 
Mkutano huu umeandaliwa na kudhaminiwa na nani? Mnamtwisha JK wetu lawama zisizo zake. Mlimwona Mzee wetu Mengi na vyombo vyake jinsi walivyoupamba ukumbi ule? Kwa nini Bunge la EAC linafanyika kokote Afrika Mashariki?
 
Back
Top Bottom