Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Ulinitangulia mwaka, mi nilikuwa mwaka wa pili ila 'Ngwine' mpaka leo sijawahi kupanda ndege...ila mwaka huu ntajitoa kimasomaso japo nikwee Fast Jet
Hahaaaa. utakwea tu kaka. Maana sisi wengine mpaka leo tunaendelea kukwea mapipa ndani na nje kwa hisani ya makampuni tunayofanya kazi na si kwa kulipa nauli zetu toka mfukoni. Hahah
 
Duuh ulifikiri ndege ni mabasi ya mkoani. Mimi nakumbuka nilibebda manukato (perfume) kwenye begi basi kwenye ukaguz nikaambiwa hairuhusiw kusafiri na perfumes kwa kiwango hicho nikaambiwa niache hapo. Anyway ndo kujifunza huko.
Duu kumbe ww ndio nilikubebea perfum zako kwenye kandoo kangu kasamaki wakati tunatoka Mwanza kuja dar
 
Mkuu clasi nafikiri hii Video ungeliiweka kwenye thread yako ya kwanza maana nimeona jamaa wanakula JIBINI kavukavu kama mie siku ya kwanza. Wanadai ina radha ya kama Sabuni. Mie walau nilikuwa najua ikoje ila sema Kifaransa kikawa kinanipiga chenga. Hahahaa.... Wasudan ni Sheeda kwenda USA.

Shower, how does look like? Shower :)

 
Ni ukweli Mpanda wana uwanja mpya na mzuri japo sina uhakika kama kule kuna biashara/abiria wa kutosha
 
Hahahaaa nakumbuka wakati ndege inafanya taxiing nilijua ishaanza kupaa coz ilikuwa usiku, nikajua easy tu, ilipoanza kuinuka kwa mbele daaah! Halaf ckujua ikiwa angan kuna smtym inayumba hasa mkipita kwenye hali ya hewa mbaya, nikawa naona jinsi bawa moja linavyoinama huku jingine likiinuka, moyo ulikuwa ukidunda sana, mpaka tulipotua ndiyo nikashusha pumzi
 
sijui lini na mie Allah atanijaalia kutembea angani kama wadau hapo juu!Allah tujaalie na sie wengine kwani wewe ndie qaadir.natamani na mimi cku moja nije nihadithie kitu kwenye huu uzi.
Usiombee ni usafiri wa pressure, hasa ukute dereva/ pilot ana msongo wa mawazo na anahisi mke wake si mwaminifu, mkifika salama basi mshukuru Mungu, au utatamani ungepanda tu bus.
 
Usiombee ni usafiri wa pressure, hasa ukute dereva/ pilot ana msongo wa mawazo na anahisi mke wake si mwaminifu, mkifika salama basi mshukuru Mungu, au utatamani ungepanda tu bus.
mkuu ulikutana na pilot mweny stress nini au ulitawaliwa tu na uoga?mi naomba tu Mungu anijaalie nikwee pipa ili walau nitoe tongotongo tu uku machoni,kila siku nimekuwa wa kuhadithiwa tu...aaah jamani!mkuu ebu tuseme amin ili nami niipande kama wewe,ili at least nije niseme kitu hapa kama wewe.
 
ila wahaya kwa sifa mmeongoza sasa mnataka "midege mikubwa" itue bukoba moja kwa moja? kwa abiria wapi na Auric tu hamjazi? Bukoba kuna nini hasa cha kujaza japo ndege ya abiria 50?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom