Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Mkuu mito sijui kama ulipata bahati ya kuupitia huu uzi, nao unachekesha sana.
 
Mkuu mito sijui kama ulipata bahati ya kuupitia huu uzi, nao unachekesha sana.
Hahaaaaa huu sasa ndo nilichekaga hatari, ila sikumbuki kama niliandikaga kitu, unachekesha mbaya!! ngoja nicheki tena kama kuna updates mkuu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Da! Nimecheka mpaka basi.
Mimi mara ya kwanza kupanda ndege ilikuwa 2008 Precision Air. Dar to shy naenda Nzega Resolute Mine kufanya field. Kwanza nilipopata email ya tiketi yangu sikulala siku hiyo. Nilipofika airport ndio mara ya kwanza kuona ngazi za umeme. Sikuzitumia kwa sababu ya uoga. Nilikuwa nimebeba spray1 Dawa ya mswaki, Kulikuwa na nyembe na mkasi kwenye begi vyote niliviacha airport.
Nilipokuwa ndani ya ndege haikuwa shida but kuna moment nilipata mshtuko mkubwa kidogo nipige kelele kwa sababu ya ndege kuchange altitude. Niliona kama utumbo unataka kutoka.
Kituko kingine wakati narudi Dar kutoka shy. Kwa sababu tiketi nilikatiwa na kampuni na pesa ya taxi nilishakula. Sikuwa na pesa ya taxi toka shinyanga mjini kwenda airport na nilitaka kutunza pesa nilokuwa nayo kwa sababu nilikuwa narudi chuo na Boom halieleweki linatoka lini. Ilibidi niulize nauli ya baiskeli mpaka airport ni sh ngapi. Shinyanga daladala ni baiskeli tu mpaka leo.
Jamaa akaniambia ni 3000 tu badala ya 35000 ya taxi. Asubuhi akaniijia tukaanza safari. Balaa tukapita short kati kwenye mashamba ya mpunga. Si tukapotea? Tukatokezea kwenye fance ya nyuma ya uwanja maana hata jamaa wa baiskeli sikumwambia kana naenda kupanda ndege yeye alijua naenda kutembelea ndugu tu karibu na airport. So ikabidi tuzunguke fance mpaka getini.
Kama si ndege kubadili arrival time ningeachwa.
Nilipofika airport wafanyakazi wa pale walinicheka baalaa. Wakasema hawajawahi ona mtu anakuja airport kupanda ndege kwa usafiri wa baiskeli.
Tiketi ya hiyo safari nimeitunza mpaka leo kama kumbukumbu toka 2008.
But namshukuru Mungu kwa sasa atleast nimezoea mpaka hivi vindege vidogo.
Chekazogo ya 5000 hiyo.
 
Mimi mara ya kwanza kukwea 1989 dege la jeshi kutoka musoma nilikuwa bado mdogo nilipoambiwa tumefika tushuke nikashangaa, nilijua ndege bado ipo palepale sasa iweje tushuke!!!, kutahamaki tushafika Dar.
 
kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyng baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"
JAMANI JAMANI NIMECHEKA MPAKA NIMEPALIWA
 
watanzania tofauti na Wa-Naija ama Wa-Kenya tumelala sana, waoga kujaribu opportunities za nje (kufundisha kiswahili, Mpira/Football/Basketball, filamu) so hata hizo ndege kuzipanda ni nadra sana. Nadhani ubovu wa kutojua lugha za "KIMATAIFA" unazidi kututia unyonge zaidi. Lakini kwa sasa si hoja mbona Wachina/Wacongo hawajui kiingereza wanaruka nje ya nchi zao? wamejaa hapa nchini utadhani kwao. TUAMKE.
 
Mimi ilikuwa 2009 pale JNIA naelekea Ethiopia wakati niko kwenye escaletor ile nafika juu nikawa nimetulia tu kama gogo ilibakia almanusura nidondoke sikujua kuwa pale mwishoni una step ili kuiacha,anyway it was a lesson.
 
day 1 nili enjoy sanaaaa yani sanaaaa

baada ya hapo safari zilizofata ni hofu tupu as ..sipendi wakati inapoanza kuruka na wakati wa kutua. Pia hali ya hewa ikiwa mbaya safar inakuwa hovyo.

kioja changu kilikuwa kwenye pasport jamani.. nilipata ile ya muda as ilikuwa ya karatasi huyo mbio stationary kuifanyia lamination eti isiharibike. Walahi kama sio yule binti wa stationery sijui huko airport ingekuwaje ..looo!
ahahahahaha
 
watanzania tofauti na Wa-Naija ama Wa-Kenya tumelala sana, waoga kujaribu opportunities za nje (kufundisha kiswahili, Mpira/Football/Basketball, filamu) so hata hizo ndege kuzipanda ni nadra sana. Nadhani ubovu wa kutojua lugha za "KIMATAIFA" unazidi kututia unyonge zaidi. Lakini kwa sasa si hoja mbona Wachina/Wacongo hawajui kiingereza wanaruka nje ya nchi zao? wamejaa hapa nchini utadhani kwao. TUAMKE.
Hapa tunajitetea sana,kutokujua kwetu lugha (ENGLISH) kwa watanzania inatuondolea confidence sana,tuanajifanya kujitutumua tu lakini huo ndio ukweli,angalia watanzania wenzetu ambao wako vizuri kwenye kimombo jinsi wanavojiamini hawana tofauti na wale wengine wa nchi zinazotumia kiengeraza kama lugha ya mawasiliano,take it or leave it huo ndio ukweli.
 
ki ukwel ndenge ni syllabus nyingine kabisa, ukitaka kujuabkuwa inashida, siku rubani atangaze kuwa ndege imeshindwa kutoa matail, na hvyo anaishisha hvyo hvyo weeeee, watu huwa wanasema makosa yote walio wahi kuyatoa,

tusimuliane tu kama hadithi il huo usafiri hauzoeleki kabisa, hata walio uzoea wanajua risk yake, na ukiona kuwa unauzoea huo usafiri ujue na kufa kunakarbia
 
sasa leo nasikia tena eti mafuta ya ndege sijui yamechakachuliwa daah mbona wanazidi kutupa hofu wasafiriii wa angani jamanii!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom