Nakumbuka ilikuwa Mwaka 2008 mwezi Juni nilikuwa naenda kikazi Lusaka, Zambia basi sijui hili wala lile kwenye tiketi iliandikwa saa ya ndege kuondoka saa 12 asubuhi (ndege ndo inapaa) mimi nikajipa kama dakika 20 kutoka home Tabata mpaka Airport, nikidhani ni kama Mabasi ya Mkoani pale Ubungo stendi duuh ile kufika nikaambiwa muda umeisha daah! Nilichokaje. But taratibu nikajifunza muda wa kufika airport, vitu visivyoruhusiwa kubeba kwenye ndege.
**NEW DEVELOPMENT
Mwezi Juni 2015 nilipata safari ya kwenda CAMEROON (kwa hisani ya Watu wamarekani USAID) sasa tukiwa huko tukalipwa posho kwa hela ya huko Central African Franc sasa nikazibana nije kubadilishia Bongo nafika bongo Bureau De Change zote hawabadilishi hizi pesa yaani nmepagawa sijui nikazitupe Coco maana....
****MPYA ya 2016
Mwezi Januari nilienda NEW DELHI duuh pale airport hakuna sijui kutangaza wala nini ni KIMYA KIMYA tu ukisubiri matangazo utastukia ndege ishakuacha.
HAKIKA USHAMBA MZIGO!