Jk acha unafiki kama kweli malipo hayo yankuuma sana kwa nini usiwajibike na kujiuzulu kwa kuliletea taifa hasara kubwa ambayo wewe uliipika baada ya kuingilia Bodi ya tanesco kwenye uteuzi wa Dr. Rashid ambaye hakuwa na sifa wala umri wa chini ya miaka 60 na wala hata kazi yenyewe hakuiomba......................
MBUNGE wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuandaa maelezo ya kuwasilisha bungeni yatakayoonyesha wapi amepata Sh94 bilioni za kuilipa kampuni ya Dowans.
Cheyo alisema hayo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili kwenye mkutano wa kujadili uwajibikaji wa pamoja katika matumizi ya fedha za wahisani, uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema fedha hiyo haiwezi kulipwa kwa kuwa haiko kwenye bajeti ya Serikali iliyotengwa na Bunge mwaka jana na ili ilipwe lazima bunge liidhinishe.
"Sh94 bilioni zinatoka wapi? Nimechukizwa sana na hili. Wanasema walipe ina maana kama watalipa na sisi ndiyo tulipitisha bajeti inaonyesha kuwa bajeti hupitishwa kwenye makaratasi tu,"alisema Cheyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Nape Mnauye alisema kwamba haamini yale aliyoskia juu ya kuwalipa Dowans ni uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM anayoifahamu.
"Siamini kama yale niliyosikia juu ya kuwalipa Dowans ni uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM ninayoifahamu. Katika mazingira ambayo hukumu ile haijasajiliwa nchini, utata juu ya wamiliki na uhalali wa mikataba ya Richmond na baadaye Dowans,"alisema
Nape alisema kwamba chama chake , CCM hakiwezi kufanya maamuzi kama hayo wakati kuna asasi za kiraia zimefungua kesi kortini kupinga hatua ya Serikali kuwalipa Dowans. "Nina mashaka kama taarifa iliyotolewa na CCM ni ile iliyoamuliwa na Kamati Kuu," alisema Nape
Wabunge wa CCM waigomea Dowans Tuesday, 25 January 2011 08:08
WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameigomea Serikali wakitaka isilipe kabisa fidia ya Sh94 bilioni dhidi ya Kampuni ya Dowans, iliyorithi mkataba wa kifisadi wa Richmond au deni hilo lipunguzwe.
Tayari sakata hilo limekwishaitikisa Serikali ya CCM huku kukiwa na shinikizo kubwa la wanaharakati wa mashirika 11 ambao wamefungua kesi Mahakama Kuu kukata rufaa, kupinga malipo hayo.
"Serikali imekubali kamati ya wabunge wa CCM kuhusu Dowans kuona kama inaweza ama kupunguza au kuliondoa kabisa deni hili ili kupunguzia mzigo Watanzania," alifafanua Waziri Mkuu Pinda wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Waziri Mkuu aliongeza kwamba, Dowans ina historia ndefu ambayo ni kuanzia Richmond na kuongeza kwamba, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inaweza kuzamia katika hilo kuona kama kuna mianya ya rushwa na kuongeza, "Ingawa hadi sasa sijapata taarifa zozote za namna hiyo."
Pinda aliongeza katika kulifanyia kazi vema sakata hilo, "'ndiyo maana kamati imeshauri Serikali isikilize ushauri wa kisheria na jaji atoe ushauri wake."
Kuhusu kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema kwamba fedha hizo lazima zilipwe na hakuna jinsi, Pinda alisema tatizo lililokuwepo awali ni kwamba kila mtu alipoulizwa na chombo cha habari aliweza kutoa kauli kwani kama asingesema vyombo vingeandika Serikali yagoma kuzungumzia Dowans.
Pinda akizungumzia mvutano wa hoja kati ya mawziri, alisema ndiyo maana imefanyika semina hiyo kwa lengo la kuondoa tofauti na kuwezesha mawaziri kuweza kuzungumza mambo bila kutofautiana.
Duru zaidi zilifafanua kwamba, hata Rais Kikwete alipozumgumzia suala hilo alitamka wazi kwamba linalomuumiza sana, huku akiweka bayana amekuwa akijadiliana na Waziri Mkuu kuona kama linaweza kuepukwa.
Taarifa hizo zilimnukuu Naibu Waziri Malima akiwaambia wabunge kwamba, fedha hizo ni nyingi, lakini wizara haikuwa na la kufanya kutokana na ushauri waliopewa na AG Werema kwamba hakuna jinsi wanavyoweza kukwepa kulipa.
Kauli hiyo ya Malima inatotafautiana na ile ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ambaye aliutangazia umma kwamba Serikali inajipanga kuilipa Dowans kiasi hicho cha fedha, hatua ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na wananchi wengi.
Uchunguzi uliopendekezwa na wabunge ni ule unaohusu uhusiano baina ya kampuni ya awali ya Richmond na Dowans, pamoja na jinsi kampuni hizo mbili zilivyoingia mkataba wa kuzalisha umeme.
Awali, ilielezwa baada ya hoja za kisheria za Dk Mwakyembe alisimama mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrodi Mkono, aliyejitolea akisema ataisaidia Serikali kuhakikisha ama deni hilo linapunguzwa au halilipwi.
kama source ya taarifa ina uhakika bora EDWARD LOWASSA kuliko mizengo pinda.
Pinda hajui alifanyalo sasa anatapata baada ya kuona moto umewaka, yeye alikuja na kampuni yake ya kisheria bungeni 2008 na kuisifu kweli kweli, tanesco ikaingia mkenge..... Rex Anttoneys ikarudi tena na kushauri Dowans ilipwe.... Pinda kimya,sasa yanamtokea puani, anataka kujisafisha.... Leo hii ndiyo anaona umuhimu wa wanaharakati? Kweli za mwezi arobaini....Si wameuona moto unawakaribia? wapuuzi kweli, yaani wanafanya watanzania wote ni mabwege, wajinga kabisa