Viongozi wa CCM waanza Kugeukana juu ya malipo ya Dowans

Kide

Member
Jan 23, 2011
74
15
Mh mkuu wa wilaya ya masasi Nape Mnauye adai haamini kama CC aijuayo ndio iliyotangaza malipo ya DOWANS hayaepukiki!habari kwny gazeti la mwananchi
 
Na yeye kishaingia kwenye mkumbo? kweli system haikwepeki, alikuwa msafi huyu jamaa...
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Masasi,
Nape Mnauye alisema kwamba
haamini yale aliyoskia juu ya
kuwalipa Dowans ni uamuzi wa
Kamati Kuu ya CCM
anayoifahamu.
"Siamini kama yale niliyosikia juu
ya kuwalipa Dowans ni uamuzi
wa Kamati Kuu ya CCM
ninayoifahamu. Katika mazingira
ambayo hukumu ile haijasajiliwa
nchini, utata juu ya wamiliki na
uhalali wa mikataba ya
Richmond na baadaye
Dowans,"alisema
Nape alisema kwamba chama
chake , CCM hakiwezi kufanya
maamuzi kama hayo wakati kuna
asasi za kiraia zimefungua kesi
kortini kupinga hatua ya Serikali
kuwalipa Dowans. "Nina
mashaka kama taarifa iliyotolewa
na CCM ni ile iliyoamuliwa na
Kamati Kuu," alisema Nape
Naye Mhadhiri Msaidizi wa Shule
ya Sheria katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, Onesmo Kyauke,
ameitaka Serikali ilipe kwanza
deni la mfanyabiashara mwenye
asili ya Asia Devram Valambhia
na Watanzania wote wanaoidai.
Kyauke ambaye pia ni wakili wa
kujitegemea anaungana na
wasomi, wanasiasa na watu wa
kada mbalimbali ambao
wanalaani hatua hiyo ya Serikali
kutaka kuilipa Dowans.
Akizungumza na waandishi wa
habari jana Kyauke alisema
haoni sababu ya Serikali kuwa na
uharaka wa kuilipa Dowans
wakati kuna Watanzania wengi
wanaidai kwa kipindi kirefu na
hawajalipwa.
Mwanasheria huyo alihoji kwa
nini Serikali ikazanie kuilipa
Dowans wakati kuna hukumu za
nyuma za Watanzania ambazo
hadi sasa bado hazijalipwa.
Valambhia anaidai Serikali kiasi
hicho cha pesa yakiwa ni malipo
ya magari kadhaa kutoka nchini
Chechslovakia aliyoiuzia Wizara
ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
miaka ya 1980.
 
Na yeye kishaingia kwenye mkumbo? kweli system haikwepeki, alikuwa msafi huyu jamaa...

Na wewe mbona umeshindwa kumuelewa? Yeye anashangazwa na uamuzi wa CC na kwa hakika anashangaa kama CC anayoijua yeye inaweza ikaamua hivyo ilivyoamua. Sasa kwa kauli hiyo usafi wake umeondokaje?
 
huyu mtu hafai kuwa ccm kwa kwel maana ni msafi ndo mana wakamnyima uenyikiti wa UVCCm n last yr wakampiga majungu kugombea ubunge na kisha wakamfariji na ukuu wa wilaya!!
 
Watamvua na huo ukuu wa wilaya..............................maana hawana maana hata kidogo.
 
haha!hawana uwezo huo...kwa madudu ayajuayo kwny ufisadi wa jengo la UVCCM na EL ,that wil b the last thng 4them to do!
 
Wabunge wa CCM waigomea Dowans Tuesday, 25 January 2011 08:08

*WAIBANA SERIKALI ISILIPE SH 94 BILIONI AU DENI LIPUNGUZWE
Na Waandishi Wetu
WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameigomea Serikali wakitaka isilipe kabisa fidia ya Sh94 bilioni dhidi ya Kampuni ya Dowans, iliyorithi mkataba wa kifisadi wa Richmond au deni hilo lipunguzwe.

Tayari sakata hilo limekwishaitikisa Serikali ya CCM huku kukiwa na shinikizo kubwa la wanaharakati wa mashirika 11 ambao wamefungua kesi Mahakama Kuu kukata rufaa, kupinga malipo hayo.

Hata hivyo, joto hilo la Dowans lililipanda zaidi jana katika siku ya mwisho ya kikao cha wabunge wote wa CCM ambao walikutana kwa siku mbili tangu juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa duru za ndani za kikao hicho nyeti cha chama ambacho kimefanyika siku chache kabla ya mkutano wa Bunge la 10, asilimia kubwa ya wabunge walitoa msimamo dhahiri wakitaka deni hilo lisilipwe huku wengine wakitaka lipunguzwe.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ni mkuu wa shughuli za Serikali bungeni anayetarajiwa kukumbana na sakata hilo katika Bunge linaloanza Februari 8, alithibitisha mapendekezo hayo mawili na kuongeza, "Serikali imekubaliana na ushauri wa kamati."

"Serikali imekubali kamati ya wabunge wa CCM kuhusu Dowans kuona kama inaweza ama kupunguza au kuliondoa kabisa deni hili ili kupunguzia mzigo Watanzania," alifafanua Waziri Mkuu Pinda wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alifafanua kwamba, uamuzi huo umekuja baada ya kamati hiyo kuishauri Serikali kuhusu deni hilo.

Waziri Mkuu aliongeza kwamba, Dowans ina historia ndefu ambayo ni kuanzia Richmond na kuongeza kwamba, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inaweza kuzamia katika hilo kuona kama kuna mianya ya rushwa na kuongeza, "Ingawa hadi sasa sijapata taarifa zozote za namna hiyo."

Pinda maarufu kama mtoto wa mkulima, aliweka bayana kwamba wakati wa mjadala kuhusu kuilipa au kutoilipa Dowans au kupunguza deni, walijitokeza wabunge wa CCM ambao kitaaluma ni wanasheria walikubali kujitolea kuisadia Serikali katika hilo.

kuhusu Dowans kurudishwa bungeni, Waziri Mkuu alisema hayo ni maoni ya watu ambao wana uhuru wa kufanya hivyo huku akisisitiza, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni ingawa katika hilo kulirudisha bungeni itakuwa ni kujadili sheria juu ya sheria na kwamba litaangaliwa kwa makini.

Pinda aliongeza katika kulifanyia kazi vema sakata hilo, "'ndiyo maana kamati imeshauri Serikali isikilize ushauri wa kisheria na jaji atoe ushauri wake."

Kuhusu kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema kwamba fedha hizo lazima zilipwe na hakuna jinsi, Pinda alisema tatizo lililokuwepo awali ni kwamba kila mtu alipoulizwa na chombo cha habari aliweza kutoa kauli kwani kama asingesema vyombo vingeandika Serikali yagoma kuzungumzia Dowans.

Pinda akizungumzia mvutano wa hoja kati ya mawziri, alisema ndiyo maana imefanyika semina hiyo kwa lengo la kuondoa tofauti na kuwezesha mawaziri kuweza kuzungumza mambo bila kutofautiana.

Lakini, duru za ndani zaidi kutoka kikao hicho zilisema wabunge wengi wa CCM wakiongozwa na Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, ambao kitaaluma ni wanasheria ndiyo walibadili upepo wa kisiasa ndani ya kikao hicho.

Mawaziri hao kwa mujibu wa duru hizo, waliwezesha wabunge wa CCM kutoa azimio hilo wakati wa mada ya hali ya umeme nchini iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ambaye alipendekeza kwa wabunge kutoa mawazo jinsi Serikali inavyoweza kuepuka kubeba mzigo huo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa mjadala mzima wa masuala ya nishati ya umeme yalijikita katika suala la Dowans na kwamba wabunge wote wapatao 10 waliochangia mada hiyo walipendekeza Serikali kutolipa fedha hizo.

Miongoni mwa wabunge waliochangia mada hiyo mbele ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Pinda aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho ni Waziri Sitta, , Dk Mwakyembe na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka.

Duru zaidi zilifafanua kwamba, hata Rais Kikwete alipozumgumzia suala hilo alitamka wazi kwamba linalomuumiza sana, huku akiweka bayana amekuwa akijadiliana na Waziri Mkuu kuona kama linaweza kuepukwa.

Taarifa hizo zilimnukuu Naibu Waziri Malima akiwaambia wabunge kwamba, fedha hizo ni nyingi, lakini wizara haikuwa na la kufanya kutokana na ushauri waliopewa na AG Werema kwamba hakuna jinsi wanavyoweza kukwepa kulipa.

Kauli hiyo ya Malima inatotafautiana na ile ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ambaye aliutangazia umma kwamba Serikali inajipanga kuilipa Dowans kiasi hicho cha fedha, hatua ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na wananchi wengi.

Ngeleja hakuhudhuria semina hiyo ya wabunge wa CCM na haikufahamika mara moja sababu za kutokuhudhuria kwake.

Mara baada ya Rais Kikwete kufunga rasmi semina hiyo ya wabunge wa CCM, baadhi yao walionekana wakimpa mkono Malima, huku baadhi yao wakimpongeza kwa kile walichosema kuwa ni ujasiri wa kusema kweli.

Katika maazimio yao, wabunge wa CCM walisema suala hilo lirejeshwe serikalini na kufanyiwa uchunguzi upya na kwamba lifanyike kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizo hazilipwi.

Uchunguzi uliopendekezwa na wabunge ni ule unaohusu uhusiano baina ya kampuni ya awali ya Richmond na Dowans, pamoja na jinsi kampuni hizo mbili zilivyoingia mkataba wa kuzalisha umeme.

Kadhalika, wabunge hao wa CCM wanataka kupatikana kwa mwenendo wa kesi hiyo kwani wengi wao katika kuchangia kwao walionekana kutilia mashaka.

Taarifa kutoka ndani ya semina hiyo ya siku tatu zinadai kuwa Rais Kikwete alisema anakubaliana na mawazo ya wabunge kwamba fedha hizo ni nyingi sana, huku akitamka bayana kwamba hilo ni, “suala linalomuumiza sana .”

Awali, ilielezwa baada ya hoja za kisheria za Dk Mwakyembe alisimama mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrodi Mkono, aliyejitolea akisema ataisaidia Serikali kuhakikisha ama deni hilo linapunguzwa au halilipwi.

Tangu kutangazwa kwa uamuzi wa ICC wa Noovemba mwaka jana, sakata hilo la Dowans limeibua mjadala mzito katika CCM na Baraza la Mawaziri.

Habari hii imeandaliwa na Neville Meena, Ramadhan Semtawa na Fidelis Butahe
 
Hii haraka ya malipo lazima kuna msukumo nyuma yake. Haya yote yatajulikana muda sio mrefu
 
Taarifa kutoka ndani ya semina hiyo ya siku tatu zinadai kuwa Rais Kikwete alisema anakubaliana na mawazo ya wabunge kwamba fedha hizo ni nyingi sana, huku akitamka bayana kwamba hilo ni, "suala linalomuumiza sana ."

Jk acha unafiki kama kweli malipo hayo yankuuma sana kwa nini usiwajibike na kujiuzulu kwa kuliletea taifa hasara kubwa ambayo wewe uliipika baada ya kuingilia Bodi ya tanesco kwenye uteuzi wa Dr. Rashid ambaye hakuwa na sifa wala umri wa chini ya miaka 60 na wala hata kazi yenyewe hakuiomba......................
 
Lakini, duru za ndani zaidi kutoka kikao hicho zilisema wabunge wengi wa CCM wakiongozwa na Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, ambao kitaaluma ni wanasheria ndiyo walibadili upepo wa kisiasa ndani ya kikao hicho.
Miongoni mwa wabunge waliochangia mada hiyo mbele ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Pinda aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho ni Waziri Sitta, , Dk Mwakyembe na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka.
Hawa ni viongozi ambao wenye utashi na ujasiri mkubwa sana.......................They are leaders to watch in future..........................very promising and highly potential to lead this nation out of this abyss................
 
QUOTE;"Duru zaidi zilifafanua kwamba, hata Rais Kikwete alipozumgumzia suala hilo alitamka wazi kwamba linalomuumiza sana, huku akiweka bayana amekuwa akijadiliana na Waziri Mkuu kuona kama linaweza kuepukwa"

...Kama Rais wa Nchi mwenye Madaraka Makubwa anasema hivi mie Nimechoka Kuchangia
 
Na wewe mbona umeshindwa kumuelewa? Yeye anashangazwa na uamuzi wa CC na kwa hakika anashangaa kama CC anayoijua yeye inaweza ikaamua hivyo ilivyoamua. Sasa kwa kauli hiyo usafi wake umeondokaje?

Nnauye amekwepa hoja, otherwise atuambie tamko halisi la CC ni lipi!
 
Tuesday, 25 January 2011 08:08 0diggsdigg

*WAIBANA SERIKALI ISILIPE SH 94 BILIONI AU DENI LIPUNGUZWE
Na Waandishi Wetu
WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameigomea Serikali wakitaka isilipe kabisa fidia ya Sh94 bilioni dhidi ya Kampuni ya Dowans, iliyorithi mkataba wa kifisadi wa Richmond au deni hilo lipunguzwe.

Tayari sakata hilo limekwishaitikisa Serikali ya CCM huku kukiwa na shinikizo kubwa la wanaharakati wa mashirika 11 ambao wamefungua kesi Mahakama Kuu kukata rufaa, kupinga malipo hayo.

Hata hivyo, joto hilo la Dowans lililipanda zaidi jana katika siku ya mwisho ya kikao cha wabunge wote wa CCM ambao walikutana kwa siku mbili tangu juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa duru za ndani za kikao hicho nyeti cha chama ambacho kimefanyika siku chache kabla ya mkutano wa Bunge la 10, asilimia kubwa ya wabunge walitoa msimamo dhahiri wakitaka deni hilo lisilipwe huku wengine wakitaka lipunguzwe.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ni mkuu wa shughuli za Serikali bungeni anayetarajiwa kukumbana na sakata hilo katika Bunge linaloanza Februari 8, alithibitisha mapendekezo hayo mawili na kuongeza, "Serikali imekubaliana na ushauri wa kamati."

"Serikali imekubali kamati ya wabunge wa CCM kuhusu Dowans kuona kama inaweza ama kupunguza au kuliondoa kabisa deni hili ili kupunguzia mzigo Watanzania," alifafanua Waziri Mkuu Pinda wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alifafanua kwamba, uamuzi huo umekuja baada ya kamati hiyo kuishauri Serikali kuhusu deni hilo.

Waziri Mkuu aliongeza kwamba, Dowans ina historia ndefu ambayo ni kuanzia Richmond na kuongeza kwamba, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inaweza kuzamia katika hilo kuona kama kuna mianya ya rushwa na kuongeza, "Ingawa hadi sasa sijapata taarifa zozote za namna hiyo."

Pinda maarufu kama mtoto wa mkulima, aliweka bayana kwamba wakati wa mjadala kuhusu kuilipa au kutoilipa Dowans au kupunguza deni, walijitokeza wabunge wa CCM ambao kitaaluma ni wanasheria walikubali kujitolea kuisadia Serikali katika hilo.

kuhusu Dowans kurudishwa bungeni, Waziri Mkuu alisema hayo ni maoni ya watu ambao wana uhuru wa kufanya hivyo huku akisisitiza, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni ingawa katika hilo kulirudisha bungeni itakuwa ni kujadili sheria juu ya sheria na kwamba litaangaliwa kwa makini.

Pinda aliongeza katika kulifanyia kazi vema sakata hilo, "'ndiyo maana kamati imeshauri Serikali isikilize ushauri wa kisheria na jaji atoe ushauri wake."

Kuhusu kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema kwamba fedha hizo lazima zilipwe na hakuna jinsi, Pinda alisema tatizo lililokuwepo awali ni kwamba kila mtu alipoulizwa na chombo cha habari aliweza kutoa kauli kwani kama asingesema vyombo vingeandika Serikali yagoma kuzungumzia Dowans.

Pinda akizungumzia mvutano wa hoja kati ya mawziri, alisema ndiyo maana imefanyika semina hiyo kwa lengo la kuondoa tofauti na kuwezesha mawaziri kuweza kuzungumza mambo bila kutofautiana.

Lakini, duru za ndani zaidi kutoka kikao hicho zilisema wabunge wengi wa CCM wakiongozwa na Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, ambao kitaaluma ni wanasheria ndiyo walibadili upepo wa kisiasa ndani ya kikao hicho.

Mawaziri hao kwa mujibu wa duru hizo, waliwezesha wabunge wa CCM kutoa azimio hilo wakati wa mada ya hali ya umeme nchini iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ambaye alipendekeza kwa wabunge kutoa mawazo jinsi Serikali inavyoweza kuepuka kubeba mzigo huo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa mjadala mzima wa masuala ya nishati ya umeme yalijikita katika suala la Dowans na kwamba wabunge wote wapatao 10 waliochangia mada hiyo walipendekeza Serikali kutolipa fedha hizo.

Miongoni mwa wabunge waliochangia mada hiyo mbele ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Pinda aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho ni Waziri Sitta, , Dk Mwakyembe na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka.

Duru zaidi zilifafanua kwamba, hata Rais Kikwete alipozumgumzia suala hilo alitamka wazi kwamba linalomuumiza sana, huku akiweka bayana amekuwa akijadiliana na Waziri Mkuu kuona kama linaweza kuepukwa.

Taarifa hizo zilimnukuu Naibu Waziri Malima akiwaambia wabunge kwamba, fedha hizo ni nyingi, lakini wizara haikuwa na la kufanya kutokana na ushauri waliopewa na AG Werema kwamba hakuna jinsi wanavyoweza kukwepa kulipa.

Kauli hiyo ya Malima inatotafautiana na ile ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ambaye aliutangazia umma kwamba Serikali inajipanga kuilipa Dowans kiasi hicho cha fedha, hatua ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na wananchi wengi.

Ngeleja hakuhudhuria semina hiyo ya wabunge wa CCM na haikufahamika mara moja sababu za kutokuhudhuria kwake.

Mara baada ya Rais Kikwete kufunga rasmi semina hiyo ya wabunge wa CCM, baadhi yao walionekana wakimpa mkono Malima, huku baadhi yao wakimpongeza kwa kile walichosema kuwa ni ujasiri wa kusema kweli.

Katika maazimio yao, wabunge wa CCM walisema suala hilo lirejeshwe serikalini na kufanyiwa uchunguzi upya na kwamba lifanyike kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizo hazilipwi.

Uchunguzi uliopendekezwa na wabunge ni ule unaohusu uhusiano baina ya kampuni ya awali ya Richmond na Dowans, pamoja na jinsi kampuni hizo mbili zilivyoingia mkataba wa kuzalisha umeme.

Kadhalika, wabunge hao wa CCM wanataka kupatikana kwa mwenendo wa kesi hiyo kwani wengi wao katika kuchangia kwao walionekana kutilia mashaka.

Taarifa kutoka ndani ya semina hiyo ya siku tatu zinadai kuwa Rais Kikwete alisema anakubaliana na mawazo ya wabunge kwamba fedha hizo ni nyingi sana, huku akitamka bayana kwamba hilo ni, “suala linalomuumiza sana .”

Awali, ilielezwa baada ya hoja za kisheria za Dk Mwakyembe alisimama mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrodi Mkono, aliyejitolea akisema ataisaidia Serikali kuhakikisha ama deni hilo linapunguzwa au halilipwi.

Tangu kutangazwa kwa uamuzi wa ICC wa Noovemba mwaka jana, sakata hilo la Dowans limeibua mjadala mzito katika CCM na Baraza la Mawaziri.

Habari hii imeandaliwa na Neville Meena, Ramadhan Semtawa na Fidelis Butahe
 
Hivi jamani deni la dowans ni 94 Bil au 180 na kitu? Nakumbuka kama awali hesabu ilikuwa kubwa au sikusoma vizuri?
 
JK anachekesha...Kama suala hilo linamuumiza kwanini asitoa amri hela hiyo isilipwe?...
AMECHOKA MWILI NA ROHO HUYU KIBABU!
 
Katika kuonyesha kuwa malipo ya dowans ni ya mafisadi wachache,mtoto wa mkulima ametofautiana na AG werema aliposema kijanja(indirectly) kuwa serikali ikishirikiana na wanaharakati italiangalia upya swala la dowans
my take:ccm wanaelekea kubaya maana kila siku wanakuja na kauli tofauti,kumbe hawa jamaa wakiwa pressed to the corner wanaweza wakaachia madaraka
 
Back
Top Bottom