Viongozi wa CCM waanza Kugeukana juu ya malipo ya Dowans

Mimi naomba kuuliza maswali mawili madogo sana;


  1. Kama serikali ina pesa ya kulipa DOWANS chapchap, mbona hii pesa haijatumika kuturekebishia matatizo yetu ya umeme siku zote hizi?
  2. Je, haikuwa sahihi kuwapeleka RICHMOND/DOWANS mahakamani au kuwawajibisha waliohusika pindi tu ilipogundulika juu ya utapeli huu?

Mimi nadhani huu ni wakati wa kuchukua hatua kwa wakati, ikionekana yeyote amevurunda hatua zichukuliwe mara moja. Haya yote ya watawala yanakuja kwa kuwa loop-holes ni nyingi mno na kila wanapozitumia hakuna anayeonyesha kusisimka na upuuzi wao wowote.

Sasa hivi tunaona kila mtu akisisimka na kuonyesha juhudi zake, wenye nia njema wanafanya bidii isilipwe na wenye nia mbaya wanafanya bidii ilipwe. Huu ni wakati wetu (wenye nia njema) kuamka na kuwawajibisha wale wote waliowahi kuhujumu nchi hii kwa namna yeyote ile, si RICHMOND / DOWANS tu ndio zitufanye tuwe na hamasa ya kwenda mahakamani. Yeyote aliyewahi kufanya hujuma yeyote apelekwe tu popote pale sheria itapochukua mkondo wake, wanaharakati waonyeshe juhudi zao juu ya yote yaliyowahi kutokea kwenye nchi hii ambayo yanaonyesha hujuma za wazi kabisa.
 
Back
Top Bottom