Vijana wawe makini sana kwenye kuchagua wapenzi wa maisha yao

Pleasepast

JF-Expert Member
May 30, 2023
325
454
Habarini za asubuhi wapendwa

Kama kichwa cha habari kinavyoonekana leo napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha vijana awe wa kike au wakiume kwamba wawe makini sana kwenye kuchagua wapenzi wa maisha yao ili kuepusha majuto kwa badaye

Na cha muhimu zaidi hakikisha unatunza izo shaha....w...a zako usije kujikuta unazimwaga kwa kichaa ambae yeye unamuona ana akili timamu lakini kimbembe kitaanza siku mkisha pata mtoto yani hapo ndio utajutia uwe wa kiume au wakike inatokea kwa wote

Tafadhali hii ni serious issue Naomba ichukulieni kwa uzito mkubwa sana fuatilia nyuzi nyingi humu utaskia ni malalamiko mzazi mwenzangu mzazi mwenzangu hivyo ni heri kua makini kabla hujaamua kumwaga izo mambo kwa mtu yeyote au kumwagiwa hakikisha uko tayari na majuto ya badae naongea kutoka kwenye experience niliyonayo mimi.

Kuna mwanamke unazaa nae unaishi nae ghafla bin vuu anabadilika na anaenda kuishi maisha yake ilihali wewe bado unampenda na unampenda mtoto wako lakini ndio ivyo tena mke kachagua maisha ya kudanga
Au

Mwanamke unazalishwa na mwanaume mara ghafla bin vuu anakuacha anaenda kuoa mwanamke mwingine.

Na kinacho uma zaidi unakuta anaye achwa anakua alikua amesha settle kujenga maisha na mwenza wake.

Mwenye kusikia na asikie.
 
Maisha ya ndoa yana changamoto sana, kujua yupi atakuwa mtu sahihi katika ndoa ni vigumu mno, walio wengi hubadilika wakiwa ndani ya ndoa tena baada ya kuishi muda mrefu kama Mume na Mke.

Kuna wakati Mume au Mke anaweza kubadilika tabia lakini Mwenza wake asijue kwa kuwa mabadiliko mengine ya tabia hufanyika kwa siri mno.

Hivyo kupata Mume au Mke sahihi ni neema tu ya Mungu lakini kwa utashi wetu ni ngumu sana.
 
M

Mungu atusaidie sana kiukweli inaumiza sana
 
Changamoto ni kubwa sana ambayo inaweza kusababisha matatizo makubwa sana maishani
 
wizara hii ni ngumu sana wengi wametumbuliwa hapo ni kuomba MUNGU asaidie kukupa zwadi ya mpenzi hakuna lingine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom