Epuka majuto utu uzima ukifika

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
5,707
11,962
Maisha ni safari ya miaka michache ya duniani ila ambayo huwa na vitu vingi sana na hivyo kuonekana mingi. Na katika miaka hii ambayo wanadamu tunaweza kuwa na uhakika wa kutumia miaka 120 kwa makadirio ya juu, ni miaka michache sana ambayo ndio huwa msingi wa furaha yaani umri kuanzia utoto hadi utu uzima karibia na kuingia uzee yaani kuanzia miaka 1 hadi 50 ndio umri ambao huwa na purukushani nyingi sana za ujenzi wa future zetu.

Katika umri huu wa miaka 50 ya kwanza ni kuanzia miaka 18 ndipo huwa tunakuwa na uhuru wa kufanya mambo yetu kwa uhuru na maamuzi binafsi bila kuamuliwa na mtu yoyote. Ukipiga kuanzia miaka 18 hadi 50 ni sawa na miaka 32 tu ya uhuru ambayo ndio tunaweza sema ni miaka active ya ujana na kufanya fujo za dunia.
Lakini baada ya miaka 50 kuendelea tayari kuna kuwa na mazingira tata ambayo inabidi kuwa makini sana maana utu uzima unakuwa umeanza so uhuru unaanza tena kupungua unaishi tena kwa heshima na kujilimit ili kulinda heshima yako na ya wengine especially mkeo, watoto wako na familia yako.

Hivi ndivyo vitu vijana wengi wa miaka hii watakuja kujutia baadae kuanzia kumri wa miaka kuanzia 45 kwenda umri wa juu kama matokeo ya kutokuwa na matumizi sahihi ya miaka 32 ya uhuru wa kuyatumia maisha vizuri. Nitalist hapa baadhi ya vitu kulingana na jinsia.

Naomba nianze na jinsia ya kike:

1. Kuanzia umri wa miaka 45,ndio umri ambao mwanamke anakuwa ametulia katika familia yake na kuanza kuenjoy maisha ya ndoa na kudeal na mambo serious.
Huu umri ukikukuta bado unasema wanaume wote ni mbwa huku hautengi hata dakika moja ya siku kujidadisi kwann wanaume wote wawe wabaya kwako tu ile hali hata hao uliosema wabaya wameshaanza maisha na wanawake wengine then sahau kuhusu kuwa na familia yako. Labda kama utavunja ndoa ya mtu of which hautakuwa na amani.

2. By the age 45 kama hukuwahi kufanya ile serious dating ya kukutana na mwanaume wa ndoto zako,na kwenda out na kuwa romantic na kuexperience true love.
Kujua mtu kwa personality yake na sio kwa akili za kudanga kuwaza utolewe out ukanywe na kula bure kisha utoe mzigo au umtoroke then sahau kwasababu katika umri huu hauwezi tena kutana na mwanaume katika innocent character.
Utakutana na wanaume waliovurugwa na maisha, ambao hawakutazami tena kama rafiki bali adui wa kuishi nae kwa tahadhari na hawawezi kukuamini hata iweje.

3. By age 45 kama haukuwahi kuwa mama wa mtoto, basi umri huu si wa kuhangaika maana ukiacha uzazi tu kuwa wa mashaka pia ni umri ambao unatakiwa kuwa na experience kubwa ya malezi na kuwafahamu watoto kwa kuwalea na kuelewa ishara zao zote.
Sasa umri huu ukiwa na rekodi ya kutoa mimba tu na hukuwahi kulea mtoto au ulikuwa unapata watoto unasukumia mama yako alee then sahau kuwa mama.

4. By 45 kama hukuwahi kukaa chini na mwanaume ukashiriki utafutaji mali yaani ile ya mume na mke sahau kabisa swala la kurithi mali za mwanaume yoyote kwasababu katika huo umri mwanaume utakayekutana nae mwenye mali nyuma yake kama si mkewe waliyepambana nae, basi ni watoto wake au ndugu zake na wazazi.
Ukigusa jiandae kuishi kwa mashaka, wasi wasi na kukosa amani ikiwamo kupoteza mali zenyewe na kubakiwa na aibu kubwa.

5. By age 45 kama haukujifunza maadili ya kike then utapata shida sana kuwa mwanamke kwa mwanaume yoyote utaekutana naye kwasababu tabia ikishakuwa sugu ni ngumu kuicha. So kama ni mdangaji utaendelea na akili za kidangaji.

6. Kama haukuwahi kumudu kuishi na mtu moja yaani mwanaume wa maisha yako aidha kwa kukosea kudate au ulikuwa busy na masomo au kazi, ukifika 45 sahau tena kuweza kushika mwanaume wa kueleweka kwasababu mwanamke hublend vema na mwanaume ambaye ni mkubwa kwake kuanzia miaka 5 kuendelea.
Mwanamke akifanana umri au akiwa mkubwa kumzidi mwanaume huwa ni changamoto. Umri huo wanaume wa size yako watakuwa na umri wa kuanzia miaka 50+. Sasa utakuta wapi mwanaume wa kuanza nae mahaba katika huo umri asiye na makando makando.

7. Ukifika miaka 45 hukuwa ukizingatia maswala ya kumaintain afya ya mwili na muonekano wako kwa kwenda gym kujiweka fit basi sahau kuwa na mwili ule wa ufiti sababu majority ya wanawake umri huo wanakuwa wameshapasuka mwili michirizi mwili mzima, vitambi vya uzazi, na nyama nyuma ya mikono vinakuwa vimeshika kasi. So ni ngumu kuweza kukaza mwili utakuwa na kazi ya ziada kuwa na ule muonekano wa ufiti ambao utaweza kuwa free kuvaa nguo za mitego au za mvuto wa kimahaba.

8. Oh nilisahau hii, inaingia kwenye baadhi ya point hapo juu ila inauzito wa pekee ndio maana nairudia. Kama hadi unafikia miaka 45 ndoa bado, hebu kawe sista tu maana umri huo kwa mwanamke kufunga ndoa huwa inachukuliwa kama comedy na mzaha so watu watahudhuria tu ili wale na kunywa na kuondoka wakuseme huko njiani.

Muda mzuri wa ndoa kwa mwanamke ni kuanzia miaka 18 na asizidi 30. 30 hadi 35 hapo ni lala salama au ndoa za dharula. So achana na kusumbua watu na michango sijui sherehe kafanye issue zingine. Tafuta mwamba wa kuvumiliana nae tu katika safari ya kuanzia miaka 45 kwenda juu.

9. Ukifika miaka 45 kama ulikuwa unategemea uzuri kuishi na wanaume then ni muda ambao hautaweza tena kuvutia wanaume sababu mabinti ambao ni umri wa mtoto wako wa kwanza au wapili watakuwa wameshakamata soko la mahusiano kama Plate namba E wewe utakuwa ni Plate namba A. So be aware na majivuno. Usije ukajutia wale unaowaringia watakuwa wameshakata tamaa na kuendelea na watoto wako.

Kwa wanaume:

1. Ukifika 50 ndio umri mwanaume unajua umeoa mke au adui yako. So ule msemo wa kosea kujenga utabomoa ila usijekosea kuoa. Huu ndio umri utajua umeoa kitu gani. So kuwa makini sana mahusiano unayoyaingia sasa.

2. Ukifika miaka 50 na umetumia muda mwingi kuhangaika na ajira za watu ndio muda wa kujitafakari na kuanza kujijenga kwa shughuli ambayo itakuwa ndio life time occupation yako.
Umri huu ndio second chance yako. Mwanamke second chance yake ni akiwa na miaka 25 kuelekea 30.

3. Ukifikia miaka 50 kama haukwenda club, haukuwa ukila bata viwanja, kuvaa kibishoo. Huu ndio umri wa kuachana na hayo mambo. Labda kukula mabinti na pia umri huu ni umri ambao huwezi kula mabinti kwa speed ile ya kukomoa.

So pay attetion, mambo ya kula ujana fanya sana at the early age ya kati ya 15 hadi hapo 25 then uwe unaanza kuwa serious na maisha ili ujenge msingi bata zinakuwa za kiutu uzima tu.

4. Ukifikia miaka 50 ndio umri wa kuanza kuona matunda ya kutunza afya yako maana umri huo mwili uimara wake hutegemea uliishi vipi miaka ya chini yake.

Ukiwa kuna uzembe wa kutozingatia maswala ya afya ya mwili ulifanya huo ndio umri wa kupata kisukari, pressure, kiharusi, figo, na matatizo mengineyo.

5. Ukifika miaka 50,kama haukuwahi kukula mademu na kuenjoy pepo wa ngono lazima aje kukugongea hodi. Utahitaji kuwa imara sana kushindana nae katika umri huo maana mkeo anakuwa si kigoli tena na hana mvuto wa kingono, ila vitoto vya mtaani sasa ndio vinawaka. Na wewe ushakuwa mtu mzima kufukuzia inakuwa mtihani inabidi uwe mpole.

6. Kabla ya miaka 50,hakikisha umeshasafiri sana enzi za ubwana mdogo wako. Unaweza kuwa katika umri wa miaka 15 kwasasa au 18 anza kuweka buku buku hizo usave ili baadae ukianza hata kufanya vikazi vya kitaa uweze jazia hata na pesa kidogo ya uwe hata na milioni utafute na mshikaji wako m'moja nae asave amounts halafu mnakubaliana at maybe age 24 mtatembea mikoa kadhaa na kuijua tanzania vizuri fursa zake pamoja na kukutana na watu wajamii hizo.

Mnapanda basi mnakwenda mikoani kushangaa kidogo kwa mfano unapanga muende mwanza mnakaa wiki au wiki mbili au hata mwezi mkifika mnafanya na vikazi kidogo ili kujazia kipato then mnakwenda kagera, then mnarudi tabora, then singida, then dodoma halafu mnarejea Dar.

Exposure ya kusafiri ni muhimu sana. Ukifika umri mkubwa utajutia sana kutokutembea na kuijua tanzania. Usijizuie tu Tanzania unaweza kwenda hata nje ya tanzania unaweza safiri mataifa ya nje kama utamudu. Maana utu uzima hautakupa ruhusa hiyo. Majukumu na familia vitakubana.

7. Kunywa beer mtoe out crush wako. Mtongoze mdada mzuri ambaye amekaa usawa wako usiogope kuulizia bei ya samaki sababu ya ukubwa wake. Ukiwa mtu mzima kutongoza itakuwa mtihani maana utamtongoza nani tena.
Sasa usijifiche sana ukiwa kijana tongoza wadada na kuwatreat vizuri wanapokukubalia si lazima ulale nao ila unaweza watoa out for a drink mfano beer mbili au tatu na nyama choma mkakiss or maybe 2 or 3 rounds of sex but don't promise them a relationship kama huwezi kujicommit nao.
Ukiendekeza drama za kudeal na mwanamke m'moja ambaye hamuendani baadae utakuja kuwa na husuda sana na kisirani na utashindwa mpenda utakayekuwa nae maana akili yako itajawa visasi.

8. Fungua biashara na jifunze vitu vingi sana kuhusu uchumi na biashara sababu ndio eneo lako kubwa la maisha, kuna msemo wanasema wanawake kwao nyumbani mwanaume mtaani na mjini. Kama unabisha subiri umri ufike utaona.
Sasa kama haujajielimisha usitegemee ukifikia umri wa utu uzima wa miaka 50 kichwa chako kitakuwa tayari kujifunza kitakuwa kinawaka moto. Jenga mazoea mapema ili baadae kichwa kinakuwa loaded na materials za ufahamu.

Haya ni machache tu ila yapo mengi sana ambayo umri ukishakwenda huwezi kuyafanya tena na hubakia kuwa majuto na huwezi badilisha.

Haya mawazo nimepata baada ya kukaa na mzee mstaafu wa CRDB ambaye kwa sasa ana miaka kama 78 akijilaumu sana kwamba kwann hakuwa akijifunza biashara alikuwa akitegemea ajira tu. Na akanisisitiza sana sisi vijana wa sasa tuna uhuru mkubwa wa kujifunza maana resources zipo za kutosha, vitabu, internet, Library yaani kujifunza ni wewe tu usitake mwenyewe.

Na mwingine ni shangazi yangu umri wa miaka 56 kwa sasa amezungumza mengi sana na mimi na kunipa sana majuto yake especially eneo la mahusiano. Pia mitandaoni testimony za watu wazima zipo nyingi sana especially ukienda Facebook na Twitter.
.
Niliona confession ya mzee m'moja ambaye alikuwa anafanya kazi kiwandani kipindi chote hadi anastaafu. Kulikuwa na binti wakati huo akiwa janki alimpenda sana. Akawa anaishia kumsalimia tu na kutosema chochote anasema yule binti alikuwa akimchangamkia vizuri sana.

Miaka kadhaa hakumuona tena maana binti na wazazi wake walihamia jimbo lingine na yeye alienda jimbo lingine. Miaka kadhaa akaja kitaa chao kusalimia wazazi akakutana na bibi jirani yao ambaye alikuwa nyumba ya jirani na alipokuwa akiishi yule binti aliyempenda sana. Yule bibi akampatia barua ambayo binti aliiacha, ilikuwa ni barua ya kumuaga na kumjulisha kuwa anaenda mji mwingine na wazazi wake. Na kama atakuwa interested kumtafuta akampa addressed.

Jamaa akaenda hadi huko kumtafuta ila akakuta binti alishaondoka kwao anaishi sehemu nyingine na mtu mwingine sababu miaka ilipita sana. Ila hawakuwa na mtoto. So jamaa alimjulisha tu kuwa amepata barua ile. Mwanamke akafurahi sana. Then wakawa wanawasiliana. Baadae wakaanza kutembeleana na kuanza mahusiano. Akasema angejua mapema angemwambia wangeanza kudate tokea teenagers sasa wamekutana utu uzimani. So wamemiss vitu vingi sana vya ujanani.
 
Ujumbe umefika mzuri wapendeza,ila ongezea na kadiri unavyozidi kua mtu mzima tuombe kua na hekima ili tuwe mabalozi wazuri kwa watoto wetu nakuwarithisha moments nzuri sisi kama wazazi wao,tusiwachokoze watoto wetu wakakata tamaa.
 
Kimsingi, decision na choices nyingi utakazozifanya ukiwa kijana wa miaka 18 mpaka 40 utaanza kuona faida zake au hasara zake pale utakapovuka miaka 45 kwenda mbele.

Kingine ukifika umri wa miaka 50 nguvu ya kutafuta hela inaanza kupungua, na kwa wengine, matatizo ya afya yanakuwa tayari yameshapiga hodi. Presha, kisukari, magonjwa ya moyo, maini, figo, gaut na mengineyo. Pia nguvu za kiume nazo zinakuwa za kuviziavizia, kwaiyo kama hukuutumia ujana wako vizuri kuwekeza kwenye assets ziwe zinakuingizia hela ukiwa uko nyumbani wakati wa umri mkubwa basi inakuwa imekula kwako. Pia kama hukuwekeza vizuri kwenye afya na well being yako, basi wakati wa utu uzima, matatizo ya afya yanaweza yakawa yako na wewe kila kukicha.

1. Invest kwenye real estate, shares, bonds etc ili uzeeni ule pension vizuri, na uweze ku afford bima nzuri za afya na matibabu ya gharama pale inapobidi. Hii ina apply kwa wote, wanawake na wanaume.

2. Ishi maisha mazuri, kula vizuri na kunywa vizuri, na kwa kiwango kizuri unapokuwa kijana, pia pigana miti vizuri, na kwa viwango vizuri ili unapokuwa kwenye utu uzima, usiwe na majuto ya aina yoyote ile.

3. Ishi na kila mtu vizuri, maana hujui kesho yako itakukuta wapi na katika mazingira gani, na nani atakuwepo kukusaidia pale utakapopata changamoto zozote zile. Kuishi vizuri na watu ni hazina kubwa sana.

4. Jitahidi kuwa karibu sana na Mungu nyakati zote za maisha yako, kwa kufanya ibada, kutoa sadaka, kutoa misaada kwa mayatima na wagonjwa.

5. Tembelea makaburi mara kwa mara, inasaidia kujikumbusha kuwa maisha ya hapa duniani yana mwisho wake. Iko siku nafsi yako itaonja umauti na utarudi mavumbini.
 
Maisha ni safari ya miaka michache ya duniani ila ambayo huwa na vitu vingi sana na hivyo kuonekana mingi. Na katika miaka hii ambayo wanadamu tunaweza kuwa na uhakika wa kutumia miaka 120 kwa makadirio ya juu, ni miaka michache sana ambayo ndio huwa msingi wa furaha yaani umri kuanzia utoto hadi utu uzima karibia na kuingia uzee yaani kuanzia
Hata kama ni wewe ungechagua kukijiajiri wakati kuna mshahara wa 30,000 bank wakati serikalini wanalipana sh. 3000?🤣🤣🤣
 
Ujumbe umefika mzuri wapendeza,ila ongezea na kadiri unavyozidi kua mtu mzima tuombe kua na hekima ili tuwe mabalozi wazuri kwa watoto wetu nakuwarithisha moments nzuri sisi kama wazazi wao,tusiwachokoze watoto wetu wakakata tamaa.
Kabisa. Ingawa hekima huja na umri automatic. Maana tafasiri ya neno hekima ni kushuhudia mambo kwa usahihi wa fikra.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom