heri kufa ukiamini katika fikra zinazoishi kuliko kuishi katika fikra zilizokufa. siku zote mapinduzi katika taifa lolote huletwa na watu wa chini na si wale wa tabaka la juu. Tunduma wanaishi katika fifra sahihi nawaunga mkono. Hizi sio enzi za zidumu fikra za mwenyekiti. PEOPLE ARE TIRED.
leo hii tunduma, hapana usalama baada ya bendera ya chadema kushushwa kwa kukata mlingoti wake wa chuma huku ikidaiwa kwamba, wameukata hili kuondoa uchafu kwa mgeni ambaye ni makamu wa rais na akisha ondoka watauludisha. lakini wananchi wamegoma kwa hiyo hapa ffu nyomi kuhakikisha bilal anautubia na kufungua soko hilo jipya. wananchi wanasema lazima kieleweke bla hivyo hakuna kuutubia mtu pale
Kwani huyo bilal ameenda kufungua hilo soko kama mwakilishi wa CCM ama Serikali?
Hiyo ndiyo kazi pekee polisisiemu wanayoweza kuifanya kwa umakini.
Chonde chonde ndugu zangu mjihadhari hao mapolisisiemu hawachelewi kuwalenga risasi za vifua na kusingizia kwamba mlikuwa mnataka kuvamia msafara wa dr. bilal, gari lao ama kituo cha polisi.
Je viongozi wa kitaifa wa cdm wanakubaliana na hiyo kama hawakubaliani nayo wamechukua hatua gani? Dr. Slaa na Mbowe tunataka majibu ya hili suala haraka iwezekanavyo
Haya ni matunda ya elimu ya uraia chini ya CDM...najisikia raha sana.
bilal kaenda kichama au kiserikali?
Tuuombe Mungu wasiwauwe tuu jamani yaanii
Mpaka muda huu Makamu wa rais hajafika na FFU wanalanda landa kila kona
Biashara zote zimesimama na watu kuingia mafichoni huku wakisoma upepo.
Kuna uwezekano makamu wa rais akalazimisha kukata utepe wa soko huku akishangiliwa na maFFU wananchi wametawanyika na hawapendi soko lifunguliwe kwani halijaisha na wamechukizwa na kitendo cha kushushiwa bendera ya chama chao kipendwa na askari.
Tatizo la viongozi wa nchi ni kulewa madaraka kiasi kwamba wanashindwa kutofautisha shughuli ya serikali na shughuli ya chama. Ndiyo maana Tunduma wana wapopoa kwa mawe kwa sababu wanatumia raslimali za serikali kwa manufaa ya chama, kitu ambacho si sahihi hata kidogo. Waacheni wapigwe mawe tuu mpaka watakapojifunza.
Mkuu wa Kaya kashaliona hili ndo maana siku hizi anafungua bank dar na kambi za vijana huko kwao. mikoani kimeo
Hivi huyu Bilali hana shughuli nyingine zaidi ya "Uzinduzi?"
Halafu huko Tunduma kunani mbona wanapishana tu kila leo. Akitoka siju Nahodha, mara bilali mara sijui nani....!
Suala ni kutatua matatizo ya wananchi na siyo kuzurura nchi nzima kujitetea.
Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno.