Yanayojiri Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu, na Mkutano wa Hadhara Temeke Leo Jumatano 25/1/2023

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Ni Asubuhi tulivu siku ya Jumatano,

Katika Jiji hili kuu la Kibiashara la Dar es Salaam leo majira ya saa 7:35 mchana anatarajiwa kutua mwanamapinduzi wa kweli Tundu Antipas Lissu ambaye anarejea nchini mwake baada ya kulazimika kuwa uhamishoni kwa takriban miaka 6 kutokana na Jaribio la kutaka kumuua.

Tundu Lissu mpinzani mkuu wa aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania John Magufuli anarudi nchini baada ya mazungumzo ya Maridhiano ya kisiasa yanayoendelea kati ya CCM na Chadema yaliyoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitangaza mwanzoni mwa mwezi huu kuondolewa kwa zuio haramu la mikutano ya hadhara lililowekwa kinyume na Katiba na mtangulizi wake John Magufuli.

Mapokezi ya Mwanasiasa huyo mashuhuri yataongozwa na Jabali la Siasa za Tanzania na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Viongozi mbalimbali wa chama hicho na wafuasi wa Chadema waliojiandaa kufanya maandamano makubwa ya kumpokea.

Maandamano hayo ya Mapokezi yatakwenda moja kwa moja Mpaka Uwanja wa Bulyaga Temeke Mwisho ambapo umeandaliwa Mkutano mkubwa wa Hadhara utakaohutubiwa na Lissu kuanzia saa 8 mchana.

Kama kawaida yetu sisi wa Molemo Media tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri katika Mapokezi hayo tangu anabusu ardhi ya Tanzania na Kisha Mkutano mkubwa wa Hadhara katika viwanja vya Temeke Mwisho.

Akizungumza na waandishi wa Habari hapo Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mapokezi ya Lissu Home Coming Mchungaji Peter Msigwa aliyekuwa ameambatana na Katibu wa Kamati Catherine Ruge alisema maandalizi yote yamekamilika na Watanzania watarajie mapokezi makubwa kuwahi kutokea hapa nchini.

Msigwa alisema chama kimeandaa mapokezi hayo kutokana na mazingira yaliyomlazimisha Lissu kukimbia nchi yake na Sasa anarudi nyumbani baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuanza kurejesha nchi katika ustaarabu wa kisiasa unaotakiwa.

Kamati hiyo pia inaundwa na Baraka Mwago ambaye ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani.

Karibuni Sana!

Tundu Lissu Awasili

Ilipotimu majira ya saa 7 mchana Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu amewasili na kupokelewa na Viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu John Mnyika, Viongozi wa Kamati ya Mapokezi, Wajumbe wa Kamati Kuu na Viongozi wa Mabaraza.

Msafara kuelekea Temeke waanza

Tundu Lissu amelakiwa na maelfu ya watu waliojipanga nje ya Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, wengine wakiwa kando kando ya Barabara huku Kiongozi huyo akiwa amepanda gari ya wazi.

Vikundi kadhaa vya waimbaji wa nyimbo na ngoma vimeshiriki Mapokezi hayo yanayoonekana makubwa na ya aina yake

Katika msafara huu wa Mapokezi Kuna maelfu ya vijana waendesha bodaboda wakiwa wamefunga bendera za Chadema huku wakipiga honi mfululizo kuashiria Furaha ya ujio wa Kiongozi huyo.

Jambo jingine kubwa linalovutia kwenye Mapokezi haya ni idadi kubwa ya watu hususan kinamama waliojipanga kandakando mwa barabara huku wakipunga mikono na kupiga vigelegele.

Wananchi wazungumza

Wananchi kadhaa waliopata nafasi ya kuzungumza wakati wa maandamano hayo wamewapongeza Viongozi wakuu wa kisiasa nchini Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kwa kuifikisha nchi katika maridhiano ya kisiasa.

Wananchi hao ambao wengi waliohojiwa ni watu waliovalia mavazi ya Chadema wamesema Rais Samia amepata heshima kubwa kwa wapenda Demokrasia wote nchini kwa kuachana na zama za utawala wa giza uliopita na kuruhusu mikutano ya hadhara na shughuli zote halali za kisiasa kwa Vyama vya upinzani.

Lissu Awasili Ullwanjani Temeke saa 10.00 Jioni

Msafara wa maandamano makubwa ya Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu umewasili hapa viwanja vya Bulyaga Temeke Mwisho.

Watu ni wengi kweli kweli na wengine wanashindwa kuingia ndani ya eneo la Uwanja.

Kamanda wa Kanda Maalum Jumanne Muliro yuko ndani ya Uwanja huu kusimamia na kuongoza zoezi la Usalama

Polisi wamefanya kazi kubwa Sana ya kusimamia Usalama kuanzia Uwanja wa Ndege Mpaka hapa Uwanjani Bulyaga

Mwenyekiti Mbowe awasili Uwanjani saa 10.15 Jioni

Mwenyekiti wa Chadema anawasili hapa viwanja vya Bulyaga na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na kukumbatiana kwa Furaha kubwa huku Umati mkubwa hapa Uwanjani ukilipuka kwa Shangwe

Mnyika asalimia wananchi

Katibu Mkuu John Mnyika akimkaribisha Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na kutoa salamu za chama amepaza sauti kuhusu kilio Cha wananchi Cha kupanda Bei za bidhaa Karibu zote nchini na kuitaka Serikali kuchukua hatua za haraka na za muda mfupi kurekebisha Jambo hilo.

Tundu Lissu Ahutubia

Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu akihutubia maelfu ya wananchi ameshukuru kwa Mapokezi makubwa aliyoandaliwa na kuonyesha Furaha kubwa ya kurejea tena nchini.

Lissu katika hotuba yake Jambo kubwa alilozungumzia ni Umuhimu wa Katiba Mpya

Lissu amewataka wananchi kuungana kwa kila hali na kwa kila nafasi kupigania Katiba Mpya ya Wananchi

Lissu amesema matatizo mengi hapa nchini ya kiutawala na kimfumo yametokana na ubovu wa Katiba iliyopo ambayo imepitwa na wakati.

Lissu amekosoa Katiba hii ya Sasa kumtwisha majukumu mengi Rais anayekuwepo madarakani kiasi Cha kumfanya kuwa hata dikteta akipenda.

Mbowe Ahutubia

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe katika kuhitimisha Mkutano huo amesisitiza Umuhimu wa wananchi kushikamana ili kupata Katiba Mpya inayofaa.

Mwenyekiti Mbowe pia amewaambia wananchi chama chake kinaendelea na mazungumzo ya kutafuta maridhiano ya kisiasa na kusema ni rai yake muafaka wa Katiba Mpya upatikane kwa njia ya mazungumzo kwa maslahi ya Taifa.

Mwenyekiti Mbowe alimalizia hotuba yake kwa kugawa sera mpya za chama hicho zilizofanyiwa utafiti na wataalam na kutaka sera hizo zitangazwe na kuenezwa kote nchini

Baadhi ya Viongozi waliopewa sera hizo kwa Niaba ya wengine ni Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu, Katibu Mkuu John Mnyika, Manaibu Katibu wakuu Salum Mwalimu na Benson Kigaila, wengine ni viongozi wa Mabaraza, Makatibu wa Kanda, Baraza la Wadhamini na Askofu Emaus Mwamakula kwa niaba ya Viongozi wa dini.

Mwisho

Mwenyekiti Mbowe aliufunga Mkutano huo saa 12:00 Jioni.

Molemo Media tunawashukuru wote kwa kutufuatilia tangu alfajiri Mpaka Sasa tunapomaliza kuripoti tukio hili.

Asanteni Sana na Mungu Awabariki nyote!
IMG-20230125-WA0130.jpg

IMG-20230125-WA0132.jpg

IMG-20230125-WA0113.jpg

IMG-20230125-WA0115.jpg
 
Asante sana Molemo Media kwa kuwa tayari kutuhabarisha

Asante sana Mwenyekiti Mbowe FA kwa hekima na ustahimilivu wako wa kupigania UHURU wa kweli wa mtanzania

Karibu sana wakili msomi na mwanaharakati wa kweli, muafrika wa kweli, ndugu yetu Tundu AL

NJOO TUPAMBANE mpaka Tanzania na watanzania wapate uhuru wa kweli
 
Yani hapo masisiem yanatamani wawaambie Chadema kua Moja ya maridhiano yetu. Mwamba Ant Pasi Lissu arudi kimya kimya ili kuogopa kumulikwa na vyombo vya habari kimataifa. Ila Ndio hivyo dhambi humfuata mwenye dhambi Maana hapa kitendo cha Mwamba kutua ni kama kufufua upya tukio lake la kupigwa mijegeje mchana wa Jua Kali mbuzi anakula majani, Amin nakwambia story ni kama inaanza upya na watu nje na ndani watahoji hatima ya uchunguzi wa tukio lake mpaka Leo,cha kushangaza sasa najua atasingiziwa Jiwe peke yake wakati aliyekufa ni Jiwe, serikali haijafa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom