Vifo vya viongozi vyenye utata

Wadau mtakumbuka kwamba huyu mheshimiwa Dr. Omar Ali Juma alikuwa makamu wa rais wa JMT na ghafla mwezi Julai mwaka 2001 wakati wa maadhimisho ya Sabasaba baada ya kutembelea maonesho hayo akionekana mwenye afya nzuri kabisa, alfajiri ya tarehe 5 Julai ndo tulitangaziwa kwamba alikuwa amefariki dunia kwa shinikizo la damu. Hata hivyo, baadae yalisemwa mengi kuhusu kilichosababisha shinikizo hilo la damu. Wengine wanadai kwamba aliauawa. Sasa nakuja kwenu wadau, hivi kifo hiki kilisababishwa na nini hasa? Karibuni tufunguke kila mtu kile anachokijua kabla sheria yao haijaanza kutumika. Nawasilisha.

kwani kale kasheria ketu kapya kameshaanza kutumika effectively? au?
 
Tukafukue mwili tufanye uchunguzi upya.

Walishajihami maana sheria inasema hadi miaka 30 ipite ndiyo wanaweza kufukua kufanya uchunguzi.

Watoto wa Sokoine walitaka kufanya hilo wakaambiwa kuhusu sheria hiyo. Bongo Dar es Salaam!
 
Walishajihami maana sheria inasema hadi miaka 30 ipite ndiyo wanaweza kufukua kufanya uchunguzi.

Watoto wa Sokoine walitaka kufanya hilo wakaambiwa kuhusu sheria hiyo. Bongo Dar es Salaam!
Nimeikumbuka hii habari ilandikwa katika gazeti moja.



Nchi ngumu sana hii!
 
Serikali yeyote lazima iue.Serikali nzuri zinaua maadui wakubwa wa taifa.Serikali mbaya kama ya kwenu inaua wenye manufaa kwa taifa na kuwatuza maadui wakubwa wa taifa.Huu ndio ubaya wa serikali yenu na ndio maana hao wote mnaofikiri wameuawa na serikali ni kwamba walikuwa wabaya kwa maadui wa taifa.Ni hivyo,bora iondoeni hiyo serikali yenu octoba
 
Wee mleta mada umetumwa na nani wewe kukumbusha yaliyopita?au na wewe ulikuwa miongoni mwa Wahanga wa ''Mtandao'' uliokuwa chini ya Mamvi?

Wala sio hivyo mkuu, mimi wala sio kwenye siasa kabisaaaa. Mimi nachapa kazi serikalini tu.
 
Sokoine alikufa na ajali za barabarani 1984. wakati huo hata traffic jam haikuwepo. tuhuma ya kwamba aliuawa na wahujumu uchumi ilienea baada ya kifo chake, na yule dereva aliyesababisha ajali kuelezea mazingira.
Kuhusu Salome Mbatia iliyotokea Iringa inawezekana, ndiyo maana nilisema labda ilipangwa. pia kumbuka kuwa Zitto alikuwa wa kwanza kufika eneo la tukio kuokoa majeruhi.
Vicent Nyerere ameelezea kwa utashi wake. Usiamini tu kwakuwa jina lake ni Nyerere ukadhani anajua kila kitu kuhusu Nyerere.
Pia gonjwa kubwa siyo lazima iwe ngoma, hata Saratani ya damu pia ni gonjwa kubwa maana tiba yake ni ngumu!

Mkuu,

Saratani ya damu pia inasababisha mkanda wa jeshi as one of the symptoms? Kuna video moja on YouTube, Mzee Kingunge anaeleza jinsi alivyomkuta Mwl. Nyerere akiwa kitandani (Hopital - UK) akiwa na mkanda wa jeshi. Nafikiri kuna umuhimu JF member Maeskron atujuze hapa symptoms za saratani ya damu. Sikiliza kwa makini kuanzia dakika ya 14:00 hadi 14:25 kwenye hii video wakati Jaji Warioba akielezea hali ya Mwalimu Nyerere.

 
Last edited by a moderator:
Wadau mtakumbuka kwamba huyu mheshimiwa Dr. Omar Ali Juma alikuwa makamu wa rais wa JMT na ghafla mwzi Julai mwaka 2001 wakati wa maadhimisho ya Sabasaba baada ya kutembelea maonesho hayo akionekana mwenye afya nzuri kabisa, alfajiri ya tarehe 5 Julai ndo tulitangaziwa kwamba alikuwa amefariki dunia kwa shinikizo la damu. Hata hivyo, baadae yalisemwa mengi kuhusu kilichosababisha shinikizo hilo la damu. Wengine wanadai kwamba aliauawa. Sasa nakuja kwenu wadau, hivi kifo hiki kilisababishwa na nini hasa? Karibuni tufunguke kila mtu kile anachokijua kabla sheria yao haijaanza kutumika. Nawasilisha.[/QUOTE
Inasemekana baada ya maandamano na watu wengi kufa kule pemba kwa amri ya amir jeshi mkuu dr. Omar ilimuuma sana kuona wapemba wenzake wanauwawa kama wanyama pori jumuiya za kimataifa zilipouliza kunani dr. Omar aliekuwa shahidi pekee alipotea gafla
 
Kumekuwepo na maneno ambao hayajawahi kukanushwa wala kusibitishwa na viongozi wa serikali ya CCM juu ya vifo vya viongozi mbalimbali waliowahi kushika nyazifa za juu kwenye serikali ya CCM. lakini walikuja kufa kwenye mazingira ya kimagumashi/ kutatanisha hasa baada ya kuhitirafiana na CCM na wananchi kuituhumu serikali kuwa ilihusika kuwaua viongozi hao vipenzi vya watanzania walio wengi …
Sasa ni wakati mwaka kutueleza kinaga ubaga juu ya vifo hivi maana kuna wengine wako njiani ambao wamekuwa wakitajwa tajwa kuwekewa sumu na serikali ya CCM na wenyewe kukiri tofauti na walio tangulia mbele ya haki, ni wakati mafaka hasa baada ya Mtoto wa marehemu Mwalimu JK Nyerere kuweka baya kuwa raisi mstafu ndg Benjamini Wiliam Mkapa alimuua Nyerere .
Kama ifatavyo

  • Karume
  • Edward Moringe Sokoine
  • Kighoma Malima
  • Horace Kolimba
  • Imrani Kombe
  • JK Nyerere
  • Salome Mbatia
Orodha inaendelea

Bila kumsahau
Komba
Dr. Mgimwa
Balali
 
Serikali yeyote lazima iue.Serikali nzuri zinaua maadui wakubwa wa taifa.Serikali mbaya kama ya kwenu inaua wenye manufaa kwa taifa na kuwatuza maadui wakubwa wa taifa.Huu ndio ubaya wa serikali yenu na ndio maana hao wote mnaofikiri wameuawa na serikali ni kwamba walikuwa wabaya kwa maadui wa taifa.Ni hivyo,bora iondoeni hiyo serikali yenu octoba

Inasemekana kazi ya kuwafuta watu katika uso wa taifa hili na kusahaulika kabisa inatekelezwa na mbunge mmoja ambaye ofisi zake zinapatikana pale jengo la E TOWERS, pia inasemekana ni member wa TISS wakuda/wambea wamenitonya kuwa alihusika na uchomaji moto wa nyaraka na jengo la NASSAKO nao wanaita WATER FRONT! Akakimbia nchi akasubiri Mwalimu amekufa akarudi kuwekeza hapa Tz kwa hela zetu! Sasa hv ni mmiliki wa benki moja hv iko jijini!
 
Bila kumsahau
Komba
Dr. Mgimwa
Balali

K katangulia msituni baada ya kutusaliti kwenye Katiba Mpya, Huyo B inasemekana bado yupo hai hajafa! Ushahidi wa kuwa hajafa ni mazingira ya kifo chake huku akienda kuzikwa nje wakati ndugu zake wapo hapa Tz Zaidi ya yote hatujawahi kuletewa hata kapicha tu kwenye gazeti au kavideo ka mazishi yake! Msiba Balali inasemekana ulihudhuriwa kwa kadi maalumu lakini Serikali hawakupewa kadi za mwaliko ingawa walipaswa kuwepo!
 
Back
Top Bottom