Vifo vya Comoro na Darfur: Hivi JWTZ wanafundishwa kuogelea??

@ Jokakuu
nakubaliana na wewe kuwa we need Jeshi lenye utaalam mkubwa wa kiteknolojia, na hilo tunaweza kulifanikisha kwa kupitia kuwa na vyombo imara vya utafiti pekee! Kuanzia Nyumbu Kibaha,TATC, MAZAO na MZINGA CORPORATION pamoja na Suma JKT
Kilichotokea ni kuwa kuna kipindi walijisahau na tukawa tunapiga mark time kwa muda mrefu, kwa mfano Suma JKT Walikalia kutengeneza masofa na viti kule Keko tu bila kuajiri wataalam wapya kwenye maswala ya Engneering wala nini, ila kuanzia amekuja huyu CDF mpya amejaribu kubadilisha liwe la kisasa zaidi
......SUMA JKT wamewezeshwa kuanzisha Suma sec Guards,wameshiriki kwenye miradi mingine mikubwa tu mfano Ujenzi wa Nyumba za Polis kilwa road(maflet mapya), chuo kipya cha polis mwanza,makazi mapya ya jamaa wa Uwt pale kNyama, Mrradi wa Kisasa Dom,Mradi wa Mbweni yote wameshiriki kwa asilimia 100, Hiiinaonyesha kabisa kuwa wanaweza ila ilikua ni mipango mibovu tu.

.......ila hela ilivyo shetani kama Ndahani alivyosema wametengeneza Meremeta nyingine kina Col Mmwakang'ata na wenzake, Army Engineering Corps ni sehemu ya newly formed Land forces cammand kwahiyo ni sehemu muhimu wa new modernisation plan

Ndahani si kweli kuwa wanaokwenda ni cream, nilishawahi kukaa na Major mmoja pale mlalakua akawa ananiambia yeye hawezi kwenda hta siku moja kulinda amani kwakua wanapigwa cha juu na hilo linajulikana so maofisa wengi hawaendi ila huwa wanachukua wale vijana waliotoka mafunzoni tu ambao wanatamani kwenda nje na nini ndo wanaenda kwa ujira mdogo SIKUMWAMINI, Ila baada ya tetesi za mabilioni ya south Africa kidogo nikapata mwanga na pia angalia hao vijana waliokufa woteni NCOs, mkubwa saana ni sajent na kuna mtoto mmoja ni Private kaingia mwaka jana tu hana hata 25years of age

@ Nzi si kweli waliokwenda sio Red berrets, TANZBAT6 wameenda askari Zaidi ya 800 na hamna nchi yenye uwezo wa kupeleka vitani maKomando 800, hata china haiwezi letalone kulinda amani upeleke 800 comandos

Pamoja wakuu
 
Wakuu natamani mngejua ni jinsi gani jeshi letu linaheshima katika international Peace keeping missions kama zile za Lebanon na Darful copy me they are well trained,professionals and Most respected ni nchi chache sana za Africa zinafikia viwango vya JWTZ
 
You may have a point lakini ni kuwa hujui unachokisema. Hivi unafikiri ku-train a soldier kuogelea ni kumwambia nenda kajitupe baharini? NO thank you. Package ya kuruta ni fully packed kiasi kwamba utahitaji kuongeza muda wa mafunzo kwa ajili tu ya basic swimming skills. Baada ya kuruta askari wote hutawanywa vikosini. Hivi unaelewa dispersion ya vikosi vyetu? Au unadhani vyote viko Dar Es Salaam? Kama kuogelea ndio unakokuona ni uaskari zaidi kwa nini basi usipiganie askari wa Navy ndio wapelekwe Darfur? Kesho utasikia kuna askari wamefariki kwa ajali ya chopper, utaanzisha mada nyingine kutaka kujua ni kwa nini askari hawafundishwi parachute. Wakipinduka utahoji ni kwa nini hawajifunzi kuruka kwenye magari! Hivi unajua kwamba ili nchi iruhusiwe kupeleka askari kwenye mission za UN ni lazima itimize vigezo fulani ikiwamo aina na kiwango cha mafunzo? Je, kuogelea ni sehemu ya hitaji la askari ili akatumike Darfur? Ingawa mambo yote yanaathiriwa na siasa, si kila kitu ni siasa.

Nyenyere,

..u also have a point, tatizo una majibu ya kijeuri-jeuri.

..mwanzo uliniambia nikaangalie ramani, sasa unakuja na habari ya "hujui unachokisema."

..tuko hapa kuelimishana, kama unaona kuna mahali nimekosea ur very welcome kunielimisha.

..kesho na keshokutwa kukitokea ajali nyingine na kusiwepo taarifa za kutosha na kuaminika basi lazima sisi kama wananchi tudai maelezo. WHY NOT??

..with all due respects, tunapenda kujua kwanini tumepoteza vijana wetu Comoro na Darfur kwa ajali za kuzama ktk maji? Je, ni kutokana na kukosa MAFUNZO YA KUTOSHA ktk uogeleaji?

..Hakuna mahali nimesema kuogelea ndiyo "uaskari zaidi." Lakini isije ikawa mnafundisha askari wetu kupasua matofali kwa vichwa, rejea maonyesho pale national stadium, huku mkisahau kuwapa mafunzo ya kujiokoa ktk maji.
 
Mpaka hapo Nimeamua kwamba huna lolote ulijualo kuhusu majeshi. Wewe ni vuvuzela tu kama baadhi ya wanasiasa. Ila just to warn you, Kikosi sha Tz huku Darfur ndicho kinachoheshimika kwa kuwa highly trained na very professional katika majukumu yao. Every UN staff wishes they had Tanzanians around them. Nabii hakubaliki... Nawaacha na uvuvuzela wenu na huo utumwa wa kudharau kwenu. Careless talks!

Inawezekana weekend imeshika kasi...mkuu Nyenyere, mimi nimeamua kuwa mwanafunzi mtii maisha yangu yote. Ntajifunza tena kwa bidii ili nifahamu lolote lile nalo taka kulifahamu.Sijawahi kuwa mjuaji na hiyo sifa naachia wenyewe kwa raha zenu.Kwa maana hiyo basi nauliza ili nielewe kitu nisichokielewa kwa nia nzuri tu.
Majadiliano haya si ya kulidhalilisha jeshi kama unavyotaka kusema. Soma uelewe vizuri. halafu kwanini mnapenda kuwa na watu wanaowapigia makofi tu na kuwasifia na kuwabeza wanaotaka kuangalia mambo broadly? Inamsaidia nani?
Napata shaka kama wewe ndio unataka kuwadhalilisha wanajeshi wetu maana hutaki kitu chochote kiongelewe zaidi ya sifa za kijinga zisizoleta tija yoyote. Weekend njema mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu gobore
Suma Sec guards ni nini? Swala la kupigwa cha juu jeshini ni Kweli wakubwa wanawaonea sana askari wadogo kwenye swala la Malipo sio hayo ya nje tu hata mengine ya ndani ambayo ni haki zao na ukizingatia nidhamu ya jeshi ni vigumu kwa hawa wadogo kulalamika na kusikilizwa,hawana pa kusemea tukiamua tunaweza kulitumia hili jukwaa kuwasemea kumbuka kuwa hawa ndo watendaji/wapiganaji wakuu wakikatishwa tamaa na Akina Shimb......o na tamaa zao za utajiri ipo siku kama taifa tutakuja kuaibika
 
Inapotokea gari lolote lenye watu ndani limesombwa na maji ghafla, hata wanaojua kuogelea kama wako ndani wanaweza wasiweze kujiokoa kwa kutegemea ujuzi wao huo wa kuogelea kwa sababu huenda wasiweze kupenya kutoka nje au wakatoka wamejeruhiwa wasiweze kuogelea.

Vivyo hivyo kwa gari la kivita ambapo pengine dreva au crew mwingine anabidi aingie na kujiweka katika nafasi yake kwa kufuata utaratibu fulani kutokana na mpangilio wa vifaa na zana ndani ya gari - pengine si rahisi kurukia kwenye kiti na kuruka kutoka kwenye kiti. Hii ndio sababu tumeelezwa wapo walioweza kujiokoa na wengine wakanasa ndani ya gari au wakatoka wakiwa wameumia kiasi cha kushindwa kuogelea.

Hivyo kwa vifo vya Dafur, kujua au kutokujua kuogelea kunaweza kusiwe ni ishu.
Silent Burner,

..at least wewe umekuja na maelezo mazuri kuhusu nini kinaweza kuwa kimetokea.

..mimi sina nia ya kubeza askari wetu. tena naamini thread kama hii inaweza kuwa-validate askari wetu kwamba huenda madhara yangeweza kuwa makubwa zaidi.

..inawezekana kabisa hao waliofariki walijeruhiwa vibaya ndiyo maana wakashindwa kujiokoa.

..but we need someone with information like that kutueleza wananchi nini kilichotokea.

..hakuna mtu anafurahia vijana wetu kupoteza maisha.
 
Last edited by a moderator:
I thought this is a thread to provoke thoughts from great thinkers and not specifically targeting the darful incident alone.
You thought it was a topic to provoke thought about Darfur and what else, Afghanistan?
 
Wakuu natamani mngejua ni jinsi gani jeshi letu linaheshima katika international Peace keeping missions kama zile za Lebanon na Darful copy me they are well trained,professionals and Most respected ni nchi chache sana za Africa zinafikia viwango vya JWTZ
Sabayi,

..lakini habari kama hizo siyo za kuzikalia nyinyi wenyewe.

..hivi wananchi wa kawaida wanajua kwamba askari wao, vijana wao, wanaheshimika huko nje??

..huo ndiyo ulitakiwa uwe utetezi kwamba askari wetu wamepatiwa mafunzo ya kutosha.

..masuala ya kuita watu "mavuvuzela", "watumwa," na majina mengine mabaya mabaya kama anavyofanya Nyenyere siyo mazuri kwa kweli.

..sasa isije ikawa Nyenyere ni mwanajeshi halafu anatujibu vibaya sisi wazazi/wajomba/kaka zake. sasa ktk mazingira hayo mnategemea nabii atakubalika nyumbani?

..wa-Tanzania tujifunze public relations haswa miongoni mwetu sisi wenyewe.
 
Last edited by a moderator:
I discourage all answers which intimidate one another let's educate/inform each other

Sabayi, kuna mada ambazo baadhi yetu wanaona mwiko kuzijadili. wanataka wao tu tena kwenye corridors zao ndio wawe wanaziongea. Badala ya kujadili hoja, naona kuna nia za makusudi za kupindisha mtiririko wa mjadala uwe kama ni kuwakebehi wanajeshi wetu. Kitu ambacho si kweli.
 
Mkuu gobore
Suma Sec guards ni nini? Swala la kupigwa cha juu jeshini ni Kweli wakubwa wanawaonea sana askari wadogo kwenye swala la Malipo sio hayo ya nje tu hata mengine ya ndani ambayo ni haki zao na ukizingatia nidhamu ya jeshi ni vigumu kwa hawa wadogo kulalamika na kusikilizwa,hawana pa kusemea tukiamua tunaweza kulitumia hili jukwaa kuwasemea kumbuka kuwa hawa ndo watendaji/wapiganaji wakuu wakikatishwa tamaa na Akina Shimb......o na tamaa zao za utajiri ipo siku kama taifa tutakuja kuaibika


SUMA JKT Security Guards, ni private company ya ulinzi inamilikiwa na jeshi, ni mpya na walinzi wake wanatrai JKT, Kwa sasa wanalinda baadhi ya strategic places za serikali tu ila in coming days hata watu binafsi mnaweza kuwakodi haswa Mabenki ndo target ya hii biashara kwasababu kimfumo Benki hazitakiwi kulindwa na Polis bali "Private Guards" Hawa wanashirikiana kwa karibu na Auxilliary Police. Wapo kivukoni, bandari na Udom nasikia inalindwa na hawa watu
 
Hawajui kuogelea! Sasa huko ziwa nyasa si watakwisha wote
Hata Marekani na Uingereza si kila askari ni bingwa wa kuogelea ingawa kama hapa kwetu wapo wa kitengo hicho yaani Navy Forces. Isitoshe vifo vya maji vinategemea mazingira yaliyomkuta mhanga kwani yapo mazingira kadhaa ambayo hata kama anajua kuogelea kiasi gani; kifo kinaweza kisiepukike.
 
Ndahani, Sabayi, gobore,

..hivi wahusika jeshini hawakuulizwa maswali haya tunayouliza hapa??

..kwasababu naona majibu mengine yanayotolewa ni kama vile baadhi yetu tumevunja mwiko fulani.
 
Last edited by a moderator:
Jokakuu
hahahahaaaaa You made my day bro,I'm not a soldier I'm just a salesman,Sales and Marketing is my profession even though I'm a son of a retired soldier. Mkuu kama umefuatilia posts zangu nimekuwa very open on the need to accommodate basic swimming trainings katima mafunzo ya jeshi na kama wanajeshi wetu kweli hawajui kuogelea then we should look into it and these two incidents Darful & Comoro should act as a wake up call.Ninachokataa mimi ni lindergrade jeshi letu kwa vifo hivyi vya Darful na niliifuatilia kwa karibu sana hiyo habari who knows what happened to these two soldiers wakati gari linasombwa na maji? Tuna uhakika gani kama walikuwa hawajui kuogelea? Silent Burner ameelezea vizuri hapo juu pengine shida yangu ni kuwa nilishindwa kutoa maelezo mazuri kama yake but that never meant I'm a soldier bro.
 
Inawezekana weekend imeshika kasi...mkuu Nyenyere, mimi nimeamua kuwa mwanafunzi mtii maisha yangu yote. Ntajifunza tena kwa bidii ili nifahamu lolote lile nalo taka kulifahamu.Sijawahi kuwa mjuaji na hiyo sifa naachia wenyewe kwa raha zenu.Kwa maana hiyo basi nauliza ili nielewe kitu nisichokielewa kwa nia nzuri tu.
Majadiliano haya si ya kulidhalilisha jeshi kama unavyotaka kusema. Soma uelewe vizuri. halafu kwanini mnapenda kuwa na watu wanaowapigia makofi tu na kuwasifia na kuwabeza wanaotaka kuangalia mambo broadly? Inamsaidia nani?
Napata shaka kama wewe ndio unataka kuwadhalilisha wanajeshi wetu maana hutaki kitu chochote kiongelewe zaidi ya sifa za kijinga zisizoleta tija yoyote. Weekend njema mkuu.

Wewe ungekuwa na uzalendo wa kiwango hicho ungedharau uvunjaji matofali wewe? Unaudhi kweli kweli. Lete constructive criticism. Ama unadhani military ni digital? You are very wrong my friend. There is no replacement for physical ability. Haya ya matofali hata huko USA mpaka leo YAPO whether you like it or not!! You better learn something.

0023ae73cfef0e3f4ba702.JPG


142581016.jpg


JWTZ ni highly celebrated katika mission zake. Wakati wajuaji hapa JF wanahoji uwezo wao wa kimafunzo na vifaa, huku UN wanashawishi liongeze vikosi vingine zaidi kwa sababu ubora wake ni exceptional, believe me! Na kuhusu vifaa, tuzungumzie hapa nyumbani, lakini mission za UN sio uswazi. Kama hauna vifaa vyenye viwango vinavyotakiwa huruhusiwi ku-deploy. Na kuna regular inspection kuhakikisha vifaa vyote viko up to std.
 
Ndahani na Jokakuu
Nina uhakika hamna mahali humu ambapo nimemjibu mtu vibaya JF ni jukwaa ninaloliheshimu sana kwakujua binafsi ni jinsi gani nimeelimika na kuwa informed toka humu ndani na siamini katika kufunika mijadala kwa kisingizio cha usalama wa taifa au kuwa ni haki ya watu fulani tu (hasa huko kwenye corridors zao) kuzijadili.
Msimamo wangu kwenye hii thread ni kuwa tusiwahukumu vijana wetu waliokufa kuwa hawajui kuogelea na tusihukumu trainings za jeshi letu kwa kuwa tu wanajeshi wetu wote hawajui kuogelea sijui ni asilimia ngapi ya mazingira yetu ya kazi za jeshi zinawakutanisha wanajeshi wote na maji nasisitiza kuwa matukio ya Darful na Comoro iwe wake up call kwa trainings za jeshi letu kuangalia umuhimu wa kuaccomodate hichi kitu kwenye trainings zao ila kumbukeni kuna nchi nyingi sana tunazozitrain africa kwenye masuala ya kijeshi na huu ni uthibitisho kuwa trainings zetu ni nzuri tunachokosa sasa hivi kwenye jeshi letu ni vifaa vya kisasa hasa kwenye air command kama mliona statistics za vifaa vya anga vya majeshi ya Africa kwenye The East Africa la last two weeks if I'm not mistake Tanzania hatuna air command nzuri na vita vya siku hizi ni vya anga zaidi infantly inapitwa na wakati na sina uhakika na level ya uzalendo hasa wa viongozi wetu wa jeshi inaonyesha wapo busy kujilimbikizia mali kwa kuwaibia askari wadogo kuliko kulimodernisi jeshi letu
 
Nzi si kweli waliokwenda sio Red berrets, TANZBAT6 wameenda askari Zaidi ya 800 na hamna nchi yenye uwezo wa kupeleka vitani maKomando 800, hata china haiwezi letalone kulinda amani upeleke 800 comandos Pamoja wakuu
Oh! Kumbe makomando wetu uvaa red beret?! Ndahani, umeona jibu lingine?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nyenyere
Hivi ukipeleka vikosi kwenye peace keeping missions vifaa unatoa wewe au unapewa na UN? Kama unatoa wewe are you paid by UN? I'm just asking to know
 
Back
Top Bottom