Vifo vya Comoro na Darfur: Hivi JWTZ wanafundishwa kuogelea??

Duuuu hao wachina ni noma wanavunja vyupa kwa kichwa? wakati sisi huku uswazi vyupa ndo silaha zetu kikiwaka ukimpiga mtu moja tu ya kichwa ana R.I.P kweli binadamu ni zaidi ya umjuavyo
 
Mkuu Nyenyere
Hivi ukipeleka vikosi kwenye peace keeping missions vifaa unatoa wewe au unapewa na UN? Kama unatoa wewe are you paid by UN? I'm just asking to know

Mkuu unaomba kupeleka vikosi, UN wanakupatia orodha ya vifaa, UNANUNUA HIVYO VIFAA, then unalipwa kwa muda wote vitakovyokuwa kwenye mision. Just like IPTL (joking).
 
Ndahani na Jokakuu
Nina uhakika hamna mahali humu ambapo nimemjibu mtu vibaya JF ni jukwaa ninaloliheshimu sana kwakujua binafsi ni jinsi gani nimeelimika na kuwa informed toka humu ndani na siamini katika kufunika mijadala kwa kisingizio cha usalama wa taifa au kuwa ni haki ya watu fulani tu (hasa huko kwenye corridors zao) kuzijadili.
Msimamo wangu kwenye hii thread ni kuwa tusiwahukumu vijana wetu waliokufa kuwa hawajui kuogelea na tusihukumu trainings za jeshi letu kwa kuwa tu wanajeshi wetu wote hawajui kuogelea sijui ni asilimia ngapi ya mazingira yetu ya kazi za jeshi zinawakutanisha wanajeshi wote na maji nasisitiza kuwa matukio ya Darful na Comoro iwe wake up call kwa trainings za jeshi letu kuangalia umuhimu wa kuaccomodate hichi kitu kwenye trainings zao ila kumbukeni kuna nchi nyingi sana tunazozitrain africa kwenye masuala ya kijeshi na huu ni uthibitisho kuwa trainings zetu ni nzuri tunachokosa sasa hivi kwenye jeshi letu ni vifaa vya kisasa hasa kwenye air command kama mliona statistics za vifaa vya anga vya majeshi ya Africa kwenye The East Africa la last two weeks if I'm not mistake Tanzania hatuna air command nzuri na vita vya siku hizi ni vya anga zaidi infantly inapitwa na wakati na sina uhakika na level ya uzalendo hasa wa viongozi wetu wa jeshi inaonyesha wapo busy kujilimbikizia mali kwa kuwaibia askari wadogo kuliko kulimodernisi jeshi letu
Sabayi,

..I am 100% with u kwamba umekuwa mstaarabu wakati wote wa mjadala huu.

..aliyetaka kuchafua hali ya hewa ni Nyenyere, lakini sisi ni watu wazima hakiharibiki kitu hapa.

..hapana, hatuna nia ya kulidhalilisha jeshi letu, au vijana waliopoteza maisha. tunachotaka kujua ni kama TAIFA liliwapa everything they needed ku-accomplish their mission. hapa tunazungumzia mafunzo na vifaa.

..again, sisi sote tunajivunia jeshi letu. Lets be honest, what else Mtanzania wa sasa hivi anaweza kujivunia zaidi ya jeshi letu?

..maswali yangu yalikuwa na nia ya kuboresha siyo kubeza.
 
Last edited by a moderator:
Sabayi,

..I am 100% with u kwamba umekuwa mstaarabu wakati wote wa mjadala huu.

..aliyetaka kuchafua hali ya hewa ni Nyenyere, lakini sisi ni watu wazima hakiharibiki kitu hapa.

..hapana, hatuna nia ya kulidhalilisha jeshi letu, au vijana waliopoteza maisha. tunachotaka kujua ni kama TAIFA liliwapa everything they needed ku-accomplish their mission. hapa tunazungumzia mafunzo na vifaa.

..again, sisi sote tunajivunia jeshi letu. Lets be honest, what else Mtanzania wa sasa hivi anaweza kujivunia zaidi ya jeshi letu?

..maswali yangu yalikuwa na nia ya kuboresha siyo kubeza.

Mimi naudhika sana na lugha kama "wapasua matofali wetu." Sivumilii lugha mbovu kama hiyo. I cherish my military.
 
Nadhani wote tulikuwa na lengo zuri pengine tulitofautiana lugha tu
Mimi nimeudhika zaidi na kejeli za waliosema eti wajeda wetu wanavitambi hawawezi kitu au wakienda Nyasa wote wataenda kufa maji.
Kuna swala kubwa sana la wajeshi wadogo kupigwa panga hela zao na wakubwa inabidi tulipigie sana kelele na kama kuna wajeda wanaodhulimiwa wanaweza kumwaga data humu kwa kuanzisha hiyo thread nina hakika JF ina nguvu kubwa sana siku hizi inaweza kusaidia kupunguza tatizo japokuwa haiwezi kumaliza.
 
Mkuu Nyenyere
Hivi ukipeleka vikosi kwenye peace keeping missions vifaa unatoa wewe au unapewa na UN? Kama unatoa wewe are you paid by UN? I'm just asking to know

Kimsingi ni kuwa UN Haina jeshi so wanachofanya ni kukodisha majeshi ya nchi mbalimbali, kama mkuu alivyoeleza hapo wanalipa kutokana na muda wote utakao fanya nao "biashara" ila naomba nitofautiane na ndugu hapo sio wanakupa listi ya vifaa ila mnapewa Maelezo ya mission then mnakuja na vifaa vyenu mkumbuke kuwa hizi mission huwa ni muda mfupi tu mnatakiwa kudeploy so swala la kununua hapo halipo( Logistically and Operationaly impossible) haswa ukizingatia kuwa kila nchi ina aina ya vifaa ilivyovizoea. Vifaa vinavyokwenda kule ujue vinatoka kwenye stock yetu

Kumbuka tulishawahi kujitoa kwenye ulinzi wa amani kuanzia 1993 ama 94 hivi, sikumbuki vizuri na sababu kubwa ni UN kushindwa kutulipa mpaka walipotuomba tena miaka hii ya karibuni
 
Oh! Kumbe makomando wetu uvaa red beret?! Ndahani, umeona jibu lingine?

Hahaaaa
kwakua hapa discussion ni UN Peacekeepers kule wote ni "Blue helmets" hamna Red wala Yellow
Sabayi

Sijalisoma hilo gazeti umelizungumzia na najaribu kulitafuta silioni ila wateva the case nadhani wewe au huyo muandishi alikua hajui vizuri kuhusu maswala ya defence, Tanzania tuna One of the best Air defence commands lakini si Air force, hapo ni almost nil. Hivyo ni vitu viwili tofauti
 
Last edited by a moderator:
Wewe ungekuwa na uzalendo wa kiwango hicho ungedharau uvunjaji matofali wewe? Unaudhi kweli kweli. Lete constructive criticism. Ama unadhani military ni digital? You are very wrong my friend. There is no replacement for physical ability. Haya ya matofali hata huko USA mpaka leo YAPO whether you like it or not!! You better learn something.

0023ae73cfef0e3f4ba702.JPG


142581016.jpg


JWTZ ni highly celebrated katika mission zake. Wakati wajuaji hapa JF wanahoji uwezo wao wa kimafunzo na vifaa, huku UN wanashawishi liongeze vikosi vingine zaidi kwa sababu ubora wake ni exceptional, believe me! Na kuhusu vifaa, tuzungumzie hapa nyumbani, lakini mission za UN sio uswazi. Kama hauna vifaa vyenye viwango vinavyotakiwa huruhusiwi ku-deploy. Na kuna regular inspection kuhakikisha vifaa vyote viko up to std.

Oooh! Kumbe nilivyosema wanaopasua matofali kwa kichwa ndio nimewatukana vijana wa kazi na kukosa uzalendo? Nikuulize, kwani ndani ya jeshi kila askari anaweza kufanya yale waliyofanya wale jamaa siku ile? Kwahiyo badala ya kuwaita special force au comando nilitumia lugha ya picha ambayo wewe msomaji umeichukulia ni kejeri. Nijuavyo mimi, askari wa aina ile wanaandaliwa sana ili waweze kufanya kazi katika mazingira yoyote yale tena wakiwa wachache tu. Kwahiyo hawawezi wakawa kamili kama baadhi ya mazoezi muhimu yakawa sio sehemu ya taratibu zao.
Hata hivyo, ninachoweza kusema ni kuwa wote tunaongelea kitu kile kile isipokuwa wewe unataka nitumie lugha which pleases you most....that I can't do.
Mwisho, hao jamaa kwenye picha wako njema sana...teh teh teh
 
Mimi naudhika sana na lugha kama "wapasua matofali wetu." Sivumilii lugha mbovu kama hiyo. I cherish my military.

Teh teh teh! Kwanini unakasirikia watu wote sasa? Kama alivyosema JokaKuu, nia si kukashifu wala kudharau watu waliojitolea uhai wao kulinda maslahi ya Taifa letu. Hivi sasa ni jeshi peke yake limebaki kama institution isiyo na kashfa za kuudhi watanzania...kwanini tusilipende? Kwanini tusilithamini? Kama lugha ile ilikuwa tatizo dawa sio kukasirika na kutumia lugha za maji taka maana hazisaidii lolote as long as wengine tumetuliza akili na kujadili hoja.
 
SUMA JKT Security Guards, ni private company ya ulinzi inamilikiwa na jeshi, ni mpya na walinzi wake wanatrai JKT, Kwa sasa wanalinda baadhi ya strategic places za serikali tu ila in coming days hata watu binafsi mnaweza kuwakodi haswa Mabenki ndo target ya hii biashara kwasababu kimfumo Benki hazitakiwi kulindwa na Polis bali "Private Guards" Hawa wanashirikiana kwa karibu na Auxilliary Police. Wapo kivukoni, bandari na Udom nasikia inalindwa na hawa watu

Kimuundo, na hii kampuni ya ulinzi itakuwa sehemu ya jeshi kama ilivyo SUMA JKT?
 
kufundishwa kujiokoa majini i9nahitaji technolojia gani???technolojia isiwe kichaka cha kujificha tunaposhindwa kuogelea,kila mwanajeshi lazima awe fit bhana,ndio maana wakati mwingine tunawaona wakitembea mwendo mrefu kwa miguu,lakini pia kusurvive katika mazingira magumu ndio kipaumbele chao maana ndio kazi yao,nadhani kumekuwa na ulegevu flani siku hizi katika mafunzo,ndio maana jeshi lina[poteza mvuto
Ndahani
I agree that this thread should provoke great thoughts
Kwa muundo na mfumo wa mafunzo wa jeshi letu sasa hivi ni ngumu wanajeshi wote kujua kuogelea inabidi kubadilisha kabisa mfumo wa mafunzo na bado nakubaliana na wanaosema kuwa inawezekana kujua kuogelea na bado ukafa maji.
Muundo na mfumo wa mafunzo wa jeshi letu ni wa kizamani hauendani na dunia ya leo yenye majeshi ya kisasa yenye technolojia ya hali ya juu lakini hatuwezi kubeza juhudi,ukakamavu,uzalendo na kujitolea kwa hali ya juu kwa wanajeshi wetu wanaofanya kazi katika mazingira magumu na kwa technolojia duni.
 
kwa kaauelewa kangu kadogo kwa kusoma hapa na pale na kuhudhuria maonyesho mbali mbali ninaju ya kwamba jeshi letu limegawanyika katika makundi kadhaa yenye ujuzi tofauti tofauti ingawaje basically wote walianza kama askari wa miguu.
Kuna askari wa nchi kavu
Askari wa majini ama navy
Askari wa anga ama airwing.
Wanaoenda darful wengi ni askari wa nchikavu na Sio kwmba ni makomandoo tu. Ila wamechanganyika kulingana na mahitaji.
Mwisho wa yote namimi naunga mkono hoja ya kwamba kwakuwa nchiyetu imezungukwa na waterbodies nyingi, ni vyema kuingiza somo la kuogelea katika basic training ya jeshi letu ingawaje siku zote bajeti haitoshi. Mungu azilaze roho za makamanda wetu waliopoteza maisha wakipeperusha bendera ya nchi yetu huko Darful.
 
gobore
Tofauti ya air defense commands na air force ni nini? how comes you might have a strong air defense commands without having a strong air force? Nielimisha please
Gazeti lilikuwa la trh 25 August na nikinukuu wanavyochambua air defence yetu wanaanza kwa kusema "Tanzania which has no air force to speak of..." Nadhani unaweza kuona ni jinsi gani wanavyodharau air force yetu na wameweka idadi na aina ya ndege za kivita tulizonazo pamoja na nchi nyingine.Kwa Africa S.A,Egypt,Nigeria,Ethiopia na Kenya ndo wako sawa kwenye air force japokuwa Askari marubani wa Ethiopia ndio most respected kwa trainings walizo nazo
 
my neighbor has no fence, nor is anybody in this side of the tracks. You missed the lesson about suggesting cake for breakfast.

teh teh teh...that is why I need to go back to the school again to learn English classes for the adults. Empty drum, makes a lot of noises! I can't hear what you say!
 
Wakuu natamani mngejua ni jinsi gani jeshi letu linaheshima katika international Peace keeping missions kama zile za Lebanon na Darful copy me they are well trained,professionals and Most respected ni nchi chache sana za Africa zinafikia viwango vya JWTZ

hiyo heshima ni ya kivipi?!, mi nadhani mawazo yako niya kujipendelea zaidi kuliko ukweli.
 
..Comoro tulipoteza askari mmoja.

..tena hata mwili wake haukupatikana.

..sasa Darfur nako tumepoteza askari wengine.

..kwa mtizamo wangu matukio haya yamelitia doa jeshi letu.

..ingekuwa tumepoteza askari hao ktk MAPAMBANO vifo hivi vingeeleweka.

..tatizo ni kwamba Comoro, na Darfur, wanasema ni matukio ya ajali.

..jambo lingine linalokera ni kitendo chetu cha kushindwa kuurejesha mwili wa askari aliyefariki Comoro.

..kwa majeshi ya wenzetu wanamsemo wao, "Every soldier must come home."

..hivi askari wetu wote waliofariki nchi za nje, miili yao imerejeshwa nyumbani na kuzikwa kwa heshima
wanazostahili??

Kwani hawa wamekufa wakiwa picnic? Au mapambano ni mpaka wangekufa kwa kupigwa risasi? Hivi unajua kweli unachokiongea?
 
Kwani hawa wamekufa wakiwa picnic? Au mapambano ni mpaka wangekufa kwa kupigwa risasi? Hivi unajua kweli unachokiongea?
Nyenyere,

..kama unafahamu ukweli zaidi ya hicho nilichoandika u r more than welcome kuueleza.

..zaidi, hakuna mahali ambapo nimesema, wala kumaanisha kwa namna yoyote ile, kwamba askari wetu wamekufa wakiwa picnic.
 
Last edited by a moderator:
Mapambano yanaanza pale askari wanapoingia anga ya Sudan. Hivyo muda wote wanapokuwa Sudan wako katika mapambano.
 
Back
Top Bottom