VIDEO: Dr. Ulimboka; kwa kinywa chake mwenyewe! | Ambayo hukuyajua...

Kuna mtu yoyote amesikia tamko rasmi la Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusiana na unyama uliomkuta Dr Ulimboka? Tamko lolote, liwe la kupongeza, kulaani, kutaka uchunguzi (huru au wa polisi), lolote. Na kama CCM hawatoa tamko kwanini? Siku 10 hawajatoa tamko lolote?
 
Kuna mtu yoyote amesikia tamko rasmi la Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusiana na unyama uliomkuta Dr Ulimboka? Tamko lolote, liwe la kupongeza, kulaani, kutaka uchunguzi (huru au wa polisi), lolote. Na kama CCM hawatoa tamko kwanini? Siku 10 hawajatoa tamko lolote?
Kwahiyo Mkuu kama CCM hawajatoa tamko kwa siku hizo 10 ndio watakua wanahusika?
Kazi kwelikweli. Vipi kuhusu vyama vingine? nao watakua wanahusika?
 
Kwahiyo Mkuu kama CCM hawajatoa tamko kwa siku hizo 10 ndio watakua wanahusika?
Kazi kwelikweli. Vipi kuhusu vyama vingine? nao watakua wanahusika?


Ngarenaro, nilidhani swali limekaa vizuri na niliuliza kama kuna mtu aliyesikia tamko rasmi la CCM kuhusiana na huu unyama uliomkuta Dr Ulimboka. Kama unalo tafadhali tuwekee hapa. Habari za nani anahusika ni jambo jingine natafuta tamko la CCM.
 
Kwa hapa huu mchezo ulipo fikia ni swala la muda tu maana tayari uchi uko wazi, hata kama tume ikiundwa kama itakuwa kinyume na hisia zetu pamoja na haya tunayoshuhudia kwenye mikanda bado serikali ina maswali ya kujibu.

Asante Invisible, take big cares of yourself wasije waka ku Uli...

kweli aisee..manake serikali imeshaishiwa sera kwa wananchi sasa inatumia njia za mauaji kushinikiza kupendwa na raia. Tujilinde pia tuwalinde makamanda wetu like G.lema, mnyika, Tundulisu, zito,mdee na wengine wengi ambao wanaichimbua serikali ya magamba {wauaji}
 
Hatuna serikali,tuna genge la wahuni na wauaji.Tume huru iundwe mapema hatuhitaji hizi blaablaa na uswahili wa hawa majambazi ya ccm

nani aunde? Je serikali ndiyo iunde? Sasa kama wao ndio wataunda je huoni kuwa watajiundia watu wao ili wasipakwe matope?labda tume ya kimataifa ije ichunguze ndio nitakuwa na imani kidogo.
 
Ngarenaro, nilidhani swali limekaa vizuri na niliuliza kama kuna mtu aliyesikia tamko rasmi la CCM kuhusiana na huu unyama uliomkuta Dr Ulimboka. Kama unalo tafadhali tuwekee hapa. Habari za nani anahusika ni jambo jingine natafuta tamko la CCM.


Kwa mfano ikiwa ni kweli hawakutoa tamko, pasipo sababu yoyote, kwa mtazamo wako unadhani Implication yake itakua ni nini? na kwanini iwe CCM tu vipi vyama vingine?
 
Hawa vijana wa kazi serikalini ni kama voda fasta tu-half baked product. Wao walipewa kazi ya kummaliza Dr. Ulimboka bila kutumia chuma(risasi) wakafanya kazi nusunusu. Kumpiga chuma ingeihusisha serikali moja kwa moja. That was a very shabby work! Huhitaji kwenda mbali kuyaona hayo. Angalia namna akina kamanda Kova wanavyo-behave,angalia viongozi mbalimabili wanavyo-behave-its all shabby,shabby.

Serikali ilimpenda sana Dr.Ulimboka lakini umma wa Watanzania ulimpenda zaidi- now we know better
 
Waliofanya hii kazi hawakutumia mbinu Kali/ foolproof , kwa maelezo ya mlalamikaji, kuna ushahidi wa kutosha kuwa Ni polisi au usalama wa taifa. Mie nilikuwwa polisi for five years na mbinu waliyotumia nimeitumia sana kwa majambazi sugu pale unapotaka ataje wenzake au aonyeshe alikoficha silaha au Mali aliyoiba. Mie nilikuwwa natumia priers/koleo nakubana mapumbu mpaka utasema. Au tutakudunda Kama mpira wa kona . Na Maria nyingi hutokea pale mshitakiwa atakapoonyesha Dharau kwa Askari kujiona ka soma sana au ana hela nyingi

mkuu hiyo yakubana kwa kutumia koleo embu immagine kama wewe ndiye unayefanyiwa. Utajiskiaje? Na ulimboka wamemng'oa meno pamoja na kucha kwa kutumia koleo bila ya ganzi. Fikiria kama wewe ndiye unayefanyiwa hayo yote.
 
Kwa mfano ikiwa ni kweli hawakutoa tamko, pasipo sababu yoyote, kwa mtazamo wako unadhani Implication yake itakua ni nini? na kwanini iwe CCM tu vipi vyama vingine?

Ngarenaro, tuweke mambo ya kiiitakadi pembeni, naamini wewe ni mtu mzima, kama ndivyo utakubaliana na mimi kuwa tukio lilimkuta Dr Ulimboka si la kawaida kabisa kwa jamii iliyostaarabika na inayofuta misingi ya utawala wa kidemokrasia. Nasema hivi kwa sababu kwa jamii yoyote misuguano na hata migogoro ni sehemu ya maisha lakini kama kweli wanaishi dhana ya utawala wa demokrasia basi watafuta misingi inayokubalika na inayolinda haki za kila upande ili kupata muafaka.

Dr Ulimboka ametekwa, ameteswa usiku mzima na kutupwa mbali na makazi ya watu - msituni. Lakini leo hii mimi na wewe tunapojadili hapa ini siku ya 10 bado hatujasikia kauli za watu ambao kwa namna moja au nyingine wanatakiwa/walitakiwa watoe mchango katika kutafuta muafaka baina ya serikali na madaktari.

CCM ndicho chama chenye serikali, kina nafasi ya pekee kabisa katika kuishauri serikali juu ya mambo mengi. Tukio la Dr. Ulimboka si tu limeathiri maisha ya raia mmoja (Dr Ulimboka) lakini pia limezua hali ya hofu ndani ya jamii ya watanzania na mbaya zaidi ni tukio ambalo linaweza kabisa kuondoa imani ya watanzania kwa vyombo vya dola. Ndio maana najiuliza kauli ya CCM ni ipi, wanachukuliaje hili tukio? wanaelewa kweli madhara yake?

Serikali iliyopo madarakani inatekeleza ilani/sera za chama cha mapinduzi. Je ndani ya ilani ya CCM suala la ulinzi na usalama lipo? Haki za raia zipo? Na zinatekelezwa? Familia ya Dr Ulimboka na Dokta mwenyewe wana haki gani kwa kutumia ilani ya CCM?
 
JK atakufa vibaya kama ni yeye kawatuma kumfanyia Uli hivi,mungu aliye hai atamuadhibu tu

Jamaa hana wasi kabisa! kwenye gazeti la mwananchi la leo tarehe 7 mwezi wa 7 front page wamemtoa anacheza bao na mke wake!
 
Ila Dr. Ulimboka ni kichwa kweli kwa sababu akili yake ilibaikia ikiwa fit sana pamoja kipigo chote kile. Maneno yake yanaonyesha wazi kuwa mtu aliyemdhuru ni wakala wa serikali aliyokuwa akishindana nayo katika kusaini makubaliano; keywords hapa ni "kusaini makubaliano."
 
Nafikiri sote tu Watu wazima, MSG inajieleza na kila kitu kinajieleza

Sote tu wanadam na iPo siku na wao watakutana na haya

Mungu akujalie upate kupona na uwe na afya njema dr. Ulimboka
 
Nyani Ngabu we sail in the same boat, maana humu JF watu wamekalia porojo tu without action, nadhani huu sasa ni muda muafaka wa kuwapa contract wale wapiga nondo wa Mbeya.

Tena na hii mipolisi yetu inavyopenda pombe za dezo yaani ukitaka kuiteketeza kwa sumu unaweza ukasafisha Barracks nzima.
 
Last edited by a moderator:
Kwa vyombo vya dola vinavyofanya kazi zake sawasawa, maelezo aliyotoa Dr. Ulimboka yanatosha sana kuwakamatisha perpetrators na kuwaleta mbele ya sheria, ila sidhani kuwa hilo litatokea Tanzania.
 
Halafu mimi siwaelewei wale wote 'wanaoiomba serikali' iunde tume huru.

Yaani kweli mnataka kuniambia hii serikali ya CCM (ambayo mimi ninaamini kwa asilimia 110 kuwa imehusika) mna imani nayo kiasi cha kuiomba iunde tume huru itakayochunguza nani anahusika kumteka na kumtesa Dkt. Ulimboka?
 
Kuna mtu yoyote amesikia tamko rasmi la Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusiana na unyama uliomkuta Dr Ulimboka? Tamko lolote, liwe la kupongeza, kulaani, kutaka uchunguzi (huru au wa polisi), lolote. Na kama CCM hawatoa tamko kwanini? Siku 10 hawajatoa tamko lolote?
Aibu zaidi hata wapiga kelele akina Sitta na Mwakyembe wamekaa kimya!! Hata wastaafu wapo kimya!! Ingekua hii kashfa inahusisha upinzani kila siku ungekua wimbo katika vyombo vya habari!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom