VIDEO: Dr. Ulimboka; kwa kinywa chake mwenyewe! | Ambayo hukuyajua...

Huyu bwana akipona kabisa na akarudia uzima kama aliokuwa nao mwanzoni basi kingwendu atakuwa next president. Wapigaji walikuwa wanajua vizuri wapi pa kupiga kwa lengo la kuua ama kumpa kilema cha maisha.
Mwacheni Mungu aitwe Mungu,kama alimpigania mikononi mwa mashetani watano,iweje ashindwe kumpigania sasa akiwa anapatiwa matibabu?
 
Mbona Video inaelezea 1/4 tu ya mkasa mzma? Nadhan kama ingekuwa kamili ingejibu maswali yetu ila kwa sasa bado kuna kitendawili!

Moja ya swali ni kwamba wakati anatekwa huyo jamaa wa ikulu alikuwa wapi?n.k
 
mkuu invisible, natumia samsung gt-7722i ila sijaambulia hiyo video, je, simu yangu haina uwezo au! vile vile natumia uc browser 8.3 ku download,
 
Mbona Video inaelezea 1/4 tu ya mkasa mzma? Nadhan kama ingekuwa kamili ingejibu maswali yetu ila kwa sasa bado kuna kitendawili!
Moja ya swali ni kwamba wakati anatekwa huyo jamaa wa ikulu alikuwa wapi?n.k

invisible ataweka video nzima (21 minutes) hapa muda si mrefu nadhani nitajibu swali lako
 
Tumeweka access kwa devices zote, na tumeruhusu watu kuweza ku-embed kwenye tovuti zao ili kusambaza ujumbe. Hakuna watermark!

Unatumia PC?

Nimesikiliza vyema, hata hivyo naona kama bado inaendelea. Tafadhali tuwekeeni kipande kinachofuata, kama itakuwa vyema kwa sasa.

Nilichogundua ni kweli kwamba serikali na vyombo vyake wanahusika. Hadi sasa hakuna mshukiwa aliyekamatwa juu ya jambo hili. Kwa nini polisi, hasa Kova anayependa kuonekana 'mchapa kazi' hajatangaza kukamatwa kwa mshukiwa yeyote? Ina maana hawakufuatilia mtandao wa simu kujua 'nani' aliwasiliana na Dr. Ulimboka kabla hajatekwa? Kwa layman kama mimi huu ni ushahidi tosha wa kimazingira kuwa Polisi na serikali wana jambo wanaloficha.
 
mkuu mi nadownload hapa ina 11.377mb...ndio hii ya 21min?
 
pamoja na kupigwa kwake je? bado anahimiza mgomo? au damu yake ndo inathamani sana kuliko ya watanzania wengine? mm naona adui mkubwa wa dr. ulimboka ni ndg na jamaa waliopoteza maisha kutokana na mgomo huu wa madaktari
 
Kaka mbona ina elekea kunoga ndio umeikatisha?
naona kunavitu vingine bado unavyo, tuwekee vitu hivi kaka.

My TAKE:

Hii kitu ni simple sana kwani huyo jamaa yiupo na Deo inasemekana anamjua, sasa kwanini atuambiwi kuwa ni suspect number moja, alafu huyu Deo yupo wapi? nashaka naye kwani atumsikii kabisa.
 
There are currently 648 users browsing this thread. (159 members and 489 guests)
 
mlokwisha kuiona hiyo cli.Tuandikieni aloyasema ,sio wote tunatumia Pc au simu zenye uwezo.
 
tumbiri loe umeteleza mkuu...ya nini kukopi majina yote hayo mkuu wangu..!!!
 
Wameua sana hao, ni kawaida yao, Igunga wameua, Arumeru wameua, Ulimboka wametaka kumuua. Nchi sio yao peke yao.
 
Aisee inasikitisha sana! huo ulikuwa ni usiku wa mateso makali kwa Dr Ulimboka, ninaamini damu yako na mateso yako Dr si bule Mungu atajilipizia kisasi kwa hao waliofanya unyama huo bila hata na chembe ya huruma!
 

Serikali, madaktari wazidi kuvutana
• Sasa yawashtaki ili wachukuliwe hatua Na Irene Mark

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima


SERIKALI imewashtaki katika Baraza la Madaktari Tanzania, madaktari wanafunzi wa vitendo walioshiriki kwenye mgomo wa madaktari uliofanyika nchini kwa tuhuma za kuhatarisha maisha ya wagonjwa na kukiuka maadili ya taaluma yao.

Kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, madaktari wanafunzi hao zaidi ya 200 waliandikiwa barua zenye kumbukumbu namba MP. 72763 wakishtakiwa kwa baraza hilo ili liwachukulie hatua za kinidhamu ikiwemo kuwafutia usajili wao endapo watabainika kutenda kosa kilaatuma.

Kwa nyakati tofauti madaktari wanafunzi hao waliotimuliwa hospitalini hapo na uongozi wa MNH walipokea barua hizo za Julai 2, 2012 na kutakiwa kwanza kutoa taarifa kwa baraza la madaktari baada ya kupata barua zao.

Hata hivyo, jana ilikuwa ni siku ya mwisho kwa madaktari wanafunzi hao kuripoti wizarani baada ya kuwepo kwa agizo la kufanya hivyo lililotolewa na MNH mwanzoni mwa wiki.

Kwa mujibu wa kila barua waliyopewa madaktari hao ambayo pia imesainiwa na P.A.Chando kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, madaktari hao walikuwa katika mgomo kati ya Juni 23 hadi Juni 29 mwaka huu.
Imeelezwa kuwa walipelekwa kufanya kazi MNH kwa ajili ya kuboresha taaluma yao katika mafunzo ya vitendo lakini wizara imepokea malalamiko kwamba walikuwa hawafanyi kazi katika kipindi hicho na badala yake walikuwa wakishiriki mgomo.

Barua hiyo imefafanua kuwa kitendo hicho cha kushiriki mgomo si tu kilihatarisha maisha na usalama wa wagonjwa, bali pia kimekwenda kinyume na taratibu za taaluma hiyo ya utabibu.

Hatua ya kuwashtaki kwenye baraza hilo, imetokana na baraza hilo kuhusika katika usajili wa madaktari wanafunzi hata hivyo wizara imelitaka kufanya uchunguzi wa kina wa madai hayo na kuchukua hatua za nidhamu.

Wakati hayo yakiendelea, huduma katika hospitali hiyo ya Taifa na Kitengo cha Mifupa cha hospitali hiyo (MOI) zimeendelea kudorora kwa wagonjwa wengi kukosa huduma baada ya madaktari kuendelea kugoma.

Mgomo unaoendelea sasa unaelezwa kwamba ni mshtuko uliowapata madaktari baada ya kupokea taarifa za hali mbaya ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, anayepatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.

Dk. Ulimboka alitekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye msitu wa Pande ulioko nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam hivi karibuni, jambo lililoibua maswali mengi hadi serikali kutuhumiwa kuhusika.

Licha ya uongozi wa MHN kuendelea kuwahadaa watanzania kwamba huduma katika hospitali hiyo zimerejea, hali hiyo imeonekana tofauti.

Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminieli Eligaeshi, alikataa kuzungumza na waandishi wa habari waliohoji sababu za kuendelea kuwepo kwa mgomo, badala yake alisema atatuma taarifa kwa vyombo vya habari kupitia barua pepe.

Gazeti hili lilitembelea baadhi ya wodi za hospitali hiyo na kukuta idadi ndogo ya wagonjwa waliodai kwamba wanahudumiwa na wauguzi huku askari wakilinda mlango wa mapokezi ya dharura ambao haukuwa na wagonjwa.

Kuhusu afya ya Dk. Ulimboka, mmoja wa madaktari hao aliyetaka jina lake lisichapishwe gazetini alisema juhudi za madaktari zinaendelea huko Afrika Kusini ili kunusuru maisha ya mwenyekiti huyo.

 
Mkuu inawezekana something went wrong kwenye plan nzima ndo maana machoni petu inaoenekana kama ni "amateur means"

Shida ni kwasababu, kwanza walimtorture na kutaka kupata maelezo kutoka kwake kuwa "nani yuko nyuma ya mgomo wao"

Inawezekana kulitokea something, maybe some dissaggrement miongoni mwao wakati wakifanya unyama huo.

Damu aliyopoteza na majeraha aliyonayo, ni wazi walitegemea afe.

Mkuu jmushi1, mimi naamini kwamba hawa walijua dhamira yao ya kumuua Dr Ulimboka walikuwa wameikamilisha hasa ukitilia maanani kwamba huyo Afisa wa Upelelezi Ahmed Msangi Dr Ulimboka anamfahamu hivyo wasingekuwa tayari kufanya makosa ya kumuacha hai ili baadaye aweze kuyasimulia yote yaliyojiri katika sakata hili.
 
97 Reactions
Reply
Back
Top Bottom