VETA wagundua gari linatotumia mionzi ya jua

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645

MAMLAKA ya Mafunzo na Ufundi Stadi Tanzania (VETA) imesema kuwa wameunda gari linalotumia mfumo wa sola.
Mtafiti wa Soko la Ajira wa VETA, Abdallah Mhagama, alisema gari hilo walilolibuni halina moshi wala kelele lakini likiwa mahali ambapo hakuna jua kwa saa tano haliwezi kufanya kazi.
Alisema utafiti wa gari hilo ulichukua mwaka mmoja ambapo lina uwezo wa kubeba watu wanane. “Gari hilo la sola lina spidi 100 kwa saa. Veta tuna uwezo wa kubadilisha gari lolote kulipeleka kwenye sola,” alisema na kuongeza kuwa magari yanayotumia sola hayana gharama.

Kwa mujibu wa mtafiti huyo, alisema gari hilo limegharimu shilingi mil. saba. Alisema ubunifu huo utasaidia kupunguza gharama za mafuta.

Tecknologia hiyo ni nzuri lakini SIDO hawawezi kuichukua na kuanza kuitumia kwa walaji, VETA watabaki nayo hiyo gari kisha wawe wanaileta mara kwa mara kwenye maonyesho tu.

Kwa ushauri, VETA watangaze kuwa watu wenye Bajaji wapeleke kwao wakawabadilishie mfumo ili bajaji ziweze kutumia sola!
 
hiyo solar panel ya kuweza kuendesha gari utakuwa ina ukubwa gani?,hizi solar tulizo nazo majumbani zinashindwa kuendesha compressor ya friji leo iendeshe gari?,nina wasiwasi sana na hili!
Hata mimi ninawasiwasi na hii kitu,nikipata muda nitaenda 7 7 kuchek hii kitu imekaaje.
 
1. usiegeshe kivulini au ndani ya jengo
2. usiendeshe kama hali ya hewa ni mbaya au mawingu na usiku
3. teh teh ...Jokes! mimi si msemaji wa VETA
 
veta nawapongeza kwa ubunifu.
Nawaomba wasibweteke, ila waongeze bidii watengeneze gari yenye mifumo miwili, wa nguvu za jua na wa mafuta, ili gari ikikaa gizani kwa zaidi ya masaa matano, iweze kutumia mfumo wa nafuta na kufanya kazi kama kawaida.
 
"wamegundua" nafikiri unawapa credit kuliko wanavyostahili. Gari zinazotumia mionzi ya jua zimeshakuwapo, kusema kuwa sio "ugunduzi" mpya. Nachelea kuwapa pongezi hadi nitakapopata specs zake zaidi.

Je wanazungumzia conversion from diesel to solar au wamelitengeneza from scratch?

Pia nikiwa kama mtumiaji mkubwa wa umeme-jua, nataka kufahamu zaidi kuhusu paneli walizotumia. Mwanzo mzuri, ila kwa 7mil. bado nina doubts.
 
Kichwa cha habari kinachanganya, si kweli kama VETA wamegundua solar car, hii teknolojia ipo na gari za kutumia nguvu ya jua zipo, japokuwa bado hazijaingizwa kwenye soko, ila boat zinazo tumia nguvu ya jua zipo na unaweza kuzinunua.

Wanachotakiwa VETA, ni kuunganisha hiyo teknolojia hiweze kutumika pamoja na magari yenye kutumia petrol au diesel, kwa namna ya kuweza kuifadhi nguvu ya kuendesha mpaka pale mtu anapoishiwa mafuta, ndipo nguvu ya jua inatumia kwa dharula.
 
mwanzo mzuri japo teknolojia hii ya solar kujaribu kwenye magari hata wenzetu wanajaribu.
 
MAMLAKA ya Mafunzo na Ufundi Stadi Tanzania (VETA) imesema kuwa wameunda gari linalotumia mfumo wa sola.
Mtafiti wa Soko la Ajira wa VETA, Abdallah Mhagama, alisema gari hilo walilolibuni halina moshi wala kelele lakini likiwa mahali ambapo hakuna jua kwa saa tano haliwezi kufanya kazi.
Alisema utafiti wa gari hilo ulichukua mwaka mmoja ambapo lina uwezo wa kubeba watu wanane. “Gari hilo la sola lina spidi 100 kwa saa. Veta tuna uwezo wa kubadilisha gari lolote kulipeleka kwenye sola,” alisema na kuongeza kuwa magari yanayotumia sola hayana gharama.

Kwa mujibu wa mtafiti huyo, alisema gari hilo limegharimu shilingi mil. saba. Alisema ubunifu huo utasaidia kupunguza gharama za mafuta.

Huyu ndio wewe nini!?

Sorce Tanzania Daima
 
Hawajagundua, lugha sahihi ingekuwa wametengeneza. Magari ya solar yapo ila inabidi iwe na uwezo wa kutumia petrol incase battery ikiwa low.
 
Vizuri, tunategemea serikali itaunga mkono jambo muhimu kama hili kuliko kukaa wanagombana kisa elfu sabini za posho bungeni!
 
na sio kwamba wametengeneza tu ni "wameiga kutengeneza" huyo abdallah wao anajitafutia umaarufu tu,mbona huku mitaaani watu wanagundua vi2 vya maana lakini hawarushwi hewani.....wabongo wamezidi kughushi idea za wenzao na kuzuga kwamba ni zao,,,,sio ishu wala nn
 
Ugunduzi wao uwa ni wa kwenda kuwafuraisha viongozi wetu malimbukeni ktk maonyesho ya 77, baada ya hapo nothing, hawana lolote
 
na sio kwamba wametengeneza tu ni "wameiga kutengeneza" huyo abdallah wao anajitafutia umaarufu tu,mbona huku mitaaani watu wanagundua vi2 vya maana lakini hawarushwi hewani.....wabongo wamezidi kughushi idea za wenzao na kuzuga kwamba ni zao,,,,sio ishu wala nn
.........wameiga na wamefanikiwa kutengeneza........weye hata hujajaribu. usidharau sana
 
"wamegundua" nafikiri unawapa credit kuliko wanavyostahili. Gari zinazotumia mionzi ya jua zimeshakuwapo, kusema kuwa sio "ugunduzi" mpya. Nachelea kuwapa pongezi hadi nitakapopata specs zake zaidi.

Je wanazungumzia conversion from diesel to solar au wamelitengeneza from scratch?

Pia nikiwa kama mtumiaji mkubwa wa umeme-jua, nataka kufahamu zaidi kuhusu paneli walizotumia. Mwanzo mzuri, ila kwa 7mil. bado nina doubts.

mkuu unajua unachosema lakini? nimeishi miaka si chini ya 30, nimefuta ujinga mpaka university ila sijawahi kusikia kitu hicho..... weye ndio umegundua sasa....
 
na sio kwamba wametengeneza tu ni "wameiga kutengeneza" huyo abdallah wao anajitafutia umaarufu tu,mbona huku mitaaani watu wanagundua vi2 vya maana lakini hawarushwi hewani.....wabongo wamezidi kughushi idea za wenzao na kuzuga kwamba ni zao,,,,sio ishu wala nn

Wachina walianza kuiga na sasa wanagundua vile vile, ni wazo.
 
Back
Top Bottom