Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
Mimi naungana na EMT katika hoja yake ya kutanganza mtu mapema, vinginevyo kinafichwa nini? Hata wakati wa Mkapa uchaguzi 1995, kwa hoja ya EMT, ilimchukua Nyerere kazi kubwa sana kwenda kumuuza mgombea yule, na pamoja na hayo, akaambulia 60% tu ya kura; Ndio maana hata katika uchaguzi wa 2015, CCM haitaweka mtu mpya, ni hawa hawa tunaowasikia, watachukua mmoja wao, kwani haina muda wa kuanza kuuza mtu mpya;
Na mfano wa EMT kuhusu Obama na maandalizi ya muda mrefu, mfano huu ukusaidie kuelewa zaidi pia kwamba hata ndani ya vyama wagombea wana mitazamo tofauti - Obama, Clinton, Biden, etc, wote hawa walikuwa na mtazamo tofauti ndani ya itikadi moja; Sasa kusema Chadema kwa sasa waende kujiuza kwa wananchi, ni sawa, lakini kwa msimamo gani? Ina maana unataka wale wote watakaotia nia kugombea kupitia Chadema wawe na msimamo mmoja wakati wa kuchujwa na chama chao? Hii itakuwa na maana gani katika demokrasia?
Vema utaratibu huo ukawepo kama sheria za uchaguzi zitarekebishwa, maana mambo kama hayo si katiba ya nchi, ni sheria za ziada za uchaguzi ambazo huwa zinabadilikabadilika kutokana na sababu mbalimbali. Wakati walipoweka muda mfupi kulikuwa na sababu za wakati huo ambazo ziliridhisha. Lakini kama leo sababu hizo hazina uzito tena kwa sababu ya utambulisho wa mgombea kwa wananchi uongezewe muda, ni vema serikali, mbunge au mtu binafsi kama sheria zinaruhusu apeleke ajenda hiyo bungeni ijadiliwe na kuibadilisha sheria ya uchaguzi.