Uzito wa Zitto, Wepesi wa Hoja kwa Suala zito

Asante kwa mchango wako,

ndugu mchambuzi....swala la kwanza; hoja yako kuhusu umri inaelekeza kuwa kijana hastahili kuwa rais na hivyo hakuna mifano mahala popote ambapo rais amekuwa kijana na akafanya mambo mazuri.

Sijaelekeza hivyo lakini pamoja na hayo, pia sio wakati wote mtu mzima hufanya mambo mazuri akiwa na nafasi ya uongozi ngazi ya Rais; Wapo kina George Bush, na wengine wengi kama mifano, dunia nzima; Suala la msingi hapa ni tujiulize kwanini Demokrasia yenye mafanikio kuliko yote (USA) na demokrasia kubwa kuliko zote duniani (India), na nchi nyingine nyingi, kikatiba kigezo cha umri miaka 35; Vile vile ujiulize - kwanini CCM imefanikiwa kukushawishi wewe kwamba umri wa miaka 40 ndio sahihi, huku CCM hiyo hiyo enzi za TANU (1965-1977), kigezo kikatiba kilikuwa miaka 30;

pili; kwako wewe umri wa ujana unaishia miaka 35 kama vile wewe ni mwanachama wa UVCCM;

Mimi sio mwanachama wa UVCCM, lakini muhimu zaidi ni majibu yangu kwa nukuu yako hapo chini:

NI VYEMA nikukumbushe kuwa range of youth age varies a lot.-Youth is the time of life between childhood and maturity. Definitions of the specific age range that constitutes youth vary. An individual's actual maturity may not correspond to their chronological age, as immature individuals could exist at all ages.( wikipedia).

mfano kulingana na united nations umri wa ujana unaishia miaka 24. cheki hapa. The policy adopts the definition of youth as declared by the United Nations, which defines a youth as a person aged between 15 to 24 years. www.tanzania.go.tz/ilfs%5CChapter%2012.doc.
angalia pia tafiti za karibuni za nchi mf Uingereza ambazo mara nyingi si sahihi kujilinganisha nao. utafiti huu ulifanyika mwaka huu huu.A survey of 2,200 people questioned as part of researchby the Department for Work and Pensions, showed that on average, Britons thinkold age starts at 59, while youth ends at 41.
kwahiyo suala la ujana unaishia umri gani ni suala lipo dynamic na linaendana na mitizamo tofauti.

Kwanza, suala la ujana kuishia miaka 35 sio kauli yangu au mtazamo wangu binafsi bali ni kigezo rasmi kwa mujibu wa umoja wa mataifa (UNESCO), ambapo unatambua ujana kuwa umri kuanzia miaka 15 hadi 35; Kwahiyo naomba uelewe kwamba hoja yangu juu ya hili na mimi sijaitoa barabarani; Vinginevyo suala la variance katika kigezo husika, mimi sijabisha, suala muhimu ni kujengea hoja, na nimejitahidi katika hilo, kwahiyo kinachoendelea baina yangu na wewe katika hili ni mgongano tu wa mawazo, jambo ambalo ni la kawaida;

Vinginevyo kutumia research ya UK kujengea hoja contradicts na hoja yako hapo chini kuhusu umuhimu wa mimi kuelimika kwamba mifano ya marekani haiendani na mazingira ya nchi kama Tanzania; Kwa maana hii, basi na wewe haustahili kunipa mifano ya UK kwa Tanzania, kwani kwa mujibu wa hoja yako, kufanya hivyo sio sahihi...

Hapa pia nikueleze tu kwamba - tafiti za nchi kama UK ambazo zinachukua random sample ambapo age structure katika population yao na ya kwetu ni tofauti kabisa; kwa mfano, kwa UK, idadi ya wananchi walio chini ya miaka 15 ni 17%, wakati kwa Tanzania ni 50%; Wananchi wengi wa UK wamevuka miaka 35; nchini Tanzania, kwa mujibu wa benki ya dunia, watanzania chini ya miaka 25 sasa wanafikia 60% (2010), na idadi hii inatarajiwa kufikia 75% ifikapo mwaka 2015;

Kwahiyo ukihoji wananchi elfu mbili randomly Tanzania na UK kwa swali hilo hilo, majibu hayatakuwa sawa; Sidhani kama nina haja ya kufafanua zaidi kwanini ingawa nipo tayari kufanya hivyo iwapo haukubaliani nami katika hilo;

Ukitoa mfano wa marekani hautakuwa sahiihi sababu ya culture ,environment,maandalizi gani wanapewa watoto wa kule kuingia ujana na utu uzima; je yanawawezesha kuingia mapema zaidi?

Hii ndio hoja yako uliyojikanyaga ndani ya bandiko moja kama nilivyofafanua hapo juu;

hata na hivyo marekani yenyewe pamoja na umri mkubwa wa taifa lao ni mwaka 1970 tu ndio iliporuhusiwa wenye miaka 18 kupiga kura.
The Twenty-sixth Amendment (AmendmentXXVI) of the United States Constitution standardized the voting ageto 18. It was adopted in response to student activism against the VietnamWar and to partially overrule the Supreme Court's decision in Oregonv. Mitchell. It was adopted on July 1, 1971
If we were old enough to die in theViet Nam war, we thought we were also old enough to vote.

Sioni mantiki yako ni nini katika hili...
 
ndugu mchambuzi....swala la kwanza; hoja yako kuhusu umri inaelekeza kuwa kijana hastahili kuwa rais na hivyo hakuna mifano mahala popote ambapo rais amekuwa kijana na akafanya mambo mazuri.

pili; kwako wewe umri wa ujana unaishia miaka 35 kama vile wewe ni mwanachama wa UVCCM;

NI VYEMA nikukumbushe kuwa range of youth age varies a lot.-Youth is the time of life between childhood and maturity. Definitions of the specific age range that constitutes youth vary. An individual's actual maturity may not correspond to their chronological age, as immature individuals could exist at all ages.( wikipedia).

mfano kulingana na united nations umri wa ujana unaishia miaka 24. cheki hapa. The policy adopts the definition of youth as declared by the United Nations, which defines a youth as a person aged between 15 to 24 years. www.tanzania.go.tz/ilfs%5CChapter%2012.doc.
angalia pia tafiti za karibuni za nchi mf Uingereza ambazo mara nyingi si sahihi kujilinganisha nao. utafiti huu ulifanyika mwaka huu huu.A survey of 2,200 people questioned as part of researchby the Department for Work and Pensions, showed that on average, Britons thinkold age starts at 59, while youth ends at 41.
kwahiyo suala la ujana unaishia umri gani ni suala lipo dynamic na linaendana na mitizamo tofauti.

ukitoa mfano wa marekani hautakuwa sahiihi sababu ya culture ,environment,maandalizi gani wanapewa watoto wa kule kuingia ujana na utu uzima; je yanawawezesha kuingia mapema zaidi?

hata na hivyo marekani yenyewe pamoja na umri mkubwa wa taifa lao ni mwaka 1970 tu ndio iliporuhusiwa wenye miaka 18 kupiga kura.
The Twenty-sixth Amendment (AmendmentXXVI) of the United States Constitution standardized the voting ageto 18. It was adopted in response to student activism against the VietnamWar and to partially overrule the Supreme Court's decision in Oregonv. Mitchell. It was adopted on July 1, 1971
If we were old enough to die in theViet Nam war, we thought we were also old enough to vote.

Nakubaliana na uchambuzi wako wenye kutuelewesha na kutufunza wengi kuhusu umri wa ujana kwamba may vary kutegemeana na mazingira, utamaduni, malezi na mengine mengi tu huchangia.

Mtoto aliyezaliwa marekani mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka miwili huwezi kumlinganisha na mtoto aliyezaliwa afrika mwenye umri sawa kwa watoto waliowengi labda familie zenye kujiweza. Maana yake living standard pia inamwathiri mtoto kukua au kutokua vizuri kmwili na kiakili.

Hatujawa na mazoea ya kumlinda sana mtoto wa mwaka mmoja na nusu Afrika kwamba anaweza kuhatarisha usalama wake, lakini mtoto aliyezaliwa kama Marekana miezi kuanzia 18 utashangaa anajua

  • kufungua na kuzima TV, turn on and off light
  • Anajua power supply socket ya umeme
  • Mnapoondoka mwepesi kukumbuka kuzima TV na lights kitu ambacho wakubwa huwa wasahulifu.
  • Atapanga vitu mbalimbali kama ngazi kukifikia kilichojuu ambako hafiki kwa uwezo wake wa kawaida
  • Anajua kupambanua gari ipi inatumiwa na baba yake na ipi inatumiwa na mama yake
  • Anajua child seat restr. anapoingia kwenye gani anakimbilia kiti chake mashuhuri
  • Akiona napy imejaa mkojo atavua suruali au kaputula yake na kuivuaa kisha kukuonyesha ili umvishe nyingine.
  • Anajua kupambanua vipindi vipi vya umri wake TV
  • Mtoto akishafikisha miezi kuanzia mitano hadi 7 utaona anakataa kunyonya ziwa la mama maana ubongo umeshaanza tofautisha utamu wa maziwa ya kawaida yenye vikolezo na yale ya mama yenye vikolezo natural, wakati watoto wengi afrika hunyonya ziwa la mama na kuachishwa huwa kazi hadi ziwa la mama kunyumbuka.
  • Nk.

Kwa mifano hiyo michache utaona watoto wengi waliozaliwa mazingira ya Afrika ni vigumu kufanya mambo hayo kwa vile mazingira yao, lishe duni, chanjo na vyakula ambavyo vimeakisiwa kwa hakika kwa usalama na ujenzi na ukuzi wa mtoto na madini muhimu anayohitaji mwilini mtoto vinahakikishwa matoto anapata, na kama mtoto hana uwezo serikali inatoa voucher kwa watoto na ukichukua kisichostahili computer itakatalia hadi ulete kile kilichoaaninishwa na lishe ya mtoto.

Mfano huu nimeuleta ili mleta mada ajaribu kutofautisha ukuaji wa vijana kama ulivyoanisha ni tofauti kulinganisha na mazingira ya mtu anayoishi, kukulia na mambo mengine mengi tu. Kwamba kufikisha miaka 35 basi kijana amekomaa na kuwa na uwezo wa kuongoza nchi ni jambo ambalo tunaweza kujifunza na nchi nyingi hata hapa vijana wadogo walipokabidhiwa nchi na yanayotukuta. Zenj mtakumbuka Komandoo alifanya majamboz yake.

Vigumu kuchukua kukua kwa kijana ni kule kushinikiza jambo fulani ili lifuatwe anavyotaka, bali vijana wanatakiwa kuwa na uelewa wenye weledi wa mambo kadhaa yenye kutokana na kukamilika katika jamii kielimu, kimaadili, kimapokeo, kiutamaduni na ukomavu katika ushirikishi. Kuna hali ambayo vijana wengi wa kiafrika kuna kuwa na hali ya kujiamini mno na kufikiria wa kizazi kabla ya uhuru si wakuwategemea katika masula ya maisha na maendeleo, utaona hapo ndipo kinapokosekana kile kitu cha msingi katika ushirikiano bila kutegemea rika bali kuweka ufa kati ya wazee na vijana.

Vijana wanatakiwa kuonyesha uwezo wao katika mambo kadhaa mengi ili waaminiwe na jamii kwamba wanaweza kukabidhiwa jukumu zito la kuongoza badala ya kushinikiza umri fulani tunataka kuanza kuongoza nchi. Taifa si la vijana tu, ni la watoto, vijana, watu wazima na wazee wote kwa pamoja wanaunda taifa na anyeongoza taifa awe na uwezo wa kuwaunganisha wote hao badala ya kuweka madaraja na kubeza kizazi fulani huu ni upungufu wa kifikra katika kuunganisha jamii moja na badala yake kuitenganisha kwa misingi ya kiumri wakati wengine tunaona familia yote mababu, mababa, vijana na watoto tu kitu kimoja.

Mbunge Deo Filikunjombe kuna vyombo vya habari vilianikwa mara tu baada ya kuwa mbunge aliunda jopo la wabunge waliomtangulia kushirikishwa katika mipango ya ushauri wa maendelea jimboni mwake kwa vile wanajua wapi walianza na wapi waliishia ili aendeleze. Pia aliunda jopo la wazee wa ushauri wa kumshauri katika utendaji kazi jimboni mwake. Huo ni mfano mzuri ambao vijana wanatakiwa kufanya na hivyo kutoweka ufa wa wazee, watu wazima na vijana. Lakini hii ya kwamba kizazi cha kabla ya uhuru hatukihitaji sasa hivi, mmh! ufa huu unaweza kusababisha kijana mwenye kuutengeneza kutoaminika kwani wengi wetu tumekulia mazingira ya kiafrika tunajali wazee wetu na kila siku tunajitahidi kuwa karibu nao tushirikishwe hekima na busara zao.

Hata Mataifa ya ulaya na marekani utaona sikukuu za thanksgiving na X-mass ni nafasi ya family union, hapo utaona vijana baada ya kutawanyika huku na kule lakini siku hizi wanarudi kwa wazazi wao kupata ile tamu ya familia na kusimuliwa historia ya kizazi cha wazazi wao na kushirikishwa mambo muhimu wanayohitaji katika maisha yao.
 
nimelipenda hilo la filikunjombe,i mean kushirikisha wabunge waliotangulia na kuunda jopo.
 
Tumerudi pale plae, hoja za kumpinga Zitto kugombea Urais kutokana na umri wake kuwa chini ya miaka 40 ifikapo 2015, ni hoja nyepesi sana; Wepesi wake unatokana na ukweli kwamba ifikapo mwaka 2015, katiba ya sasa yenye kigezo hicho ambacho binafsi naamini kwamba kilikuwa ni cha kisiasa kuliko kimantiki, Katiba hiyo haitakuwepo tena; Ni wajibu wetu watanzania kuhakikisha kwamba masuala yote yanayoingizwa kwenye katiba mpya yanakuwa ni ya kimantiki kwa mujibu wa matakwa ya wengi, na sio ya kisiasa;

Haiingii akilini kufahamu kwamba Katiba Tanzania 1965 - 1977, kigezo cha mtanzania kugombea urais kiumri ilikuwa ni miaka 30; Na wakati huo, karibia nusu ya watanzania walikuwa wamevuka umri wa miaka 30; Kwa maana nyingine, wapiga kura wengi kwa wakati ule walikuwa na umri zaidi ya miaka 30; Tofauti na wakati ule, ifikapo mwaka 2015, watanzania wenye umri chini ya miaka 30 watakuwa 70% kama sio zaidi; Vile vile wapiga kura wengi zaidi watakuwa hawajafika miaka 40;

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, umri wa kijana unaishia miaka 35; Kuna utofauti gani (kwa hoja za kimantiki, sio viroja vya kisiasa) - kati ya umri wa miaka 36, 37, 38, 39 na 40 na Urais? Nchi zote duniani zenye ku practice demokrasia ya uliberali - kuanzia demokrasia kubwa kuliko zote duniani - INDIA na demokrasia yenye mafanikio makubwa kuliko zote duniani - USA, katiba zao zimeweka kigezo hiki kuwa miaka 35, kwani by the time Rais anaanza kazi yake, anakuwa ameshavuka ujana na kuingia utu uzima;

Ni vizuri tukafanya maamuzi kimantiki juu ya suala hili, bila y akujali zitto yupo au hayupo; Hivi kweli, kigezo cha umri wa miaka 40 ni kigezo cha kisiasa zaidi au kimantiki zaidi? Kama ni cha kimantiki, ni mantiki ipi? Inafurahisha kuona wabunge wengi wameanza kuona suala hili ni kama kiini macho na kwamba uamuzi wake ulikuwa ni wa kisiasa zaidi, lakini nilitegemea Zitto angejengea hoja nzito suala hili badala ya kuja na hoja nyepesi nyepesi kwa suala zito kama hili, hasa pale alipojenga hoja kwamba kigezo cha umri kilichopo sasa kikatiba ni suala la USHAMBA; Katika bandiko langu namba moja kwenye uzi huu, nilihoji, na ninahoji tena wale wanaomuunga mkono zitto swali lifuatalo:

  • Zitto Anasimamia Wapi Kuhusu Katiba Mpya, hasa nini kiwemo na nini kisiwemo, pamoja na mkakati wake wa kusimamia na kuyalinda hayo?

Natumaini kwenye suala la umri kugombea Urais na Katiba mpya, kuna hoja nzito zaidi kuliko hoja ya USHAMBA, na zitto na wafuasi wake wataacha USHAMBA na badala yake kuja na mikakati effective zaidi ili kusaidia watanzania waelewe na pia watofautishe mantiki na siasa katika masuala muhimu kama haya;
 
Mchambuzi,
Nadhani wewe ni msomi mzuri na mzuri ktk kujenga hoja. Swala hapa sio Umri wa ujana ambao muda wote umeutumia kujenga hoja yako isipokuwa swala ni nafasi ya RAIS iwe na vigezo gani. Sasa unapotumia Umri wakati wewe mwenyewe umeandika kwamba Ujana huishia miaka 24 sielewi kwa nini hukutaka Umri unaoruhusu mtu kugombea Urais ushuke hadi miaka 25 badala ya 35!..sasa pengine wewe tueleze sababu ya kuwa 35 badala ya miaka 25 ambayo inatambuliwa kuwa utu uzima na Unesco.

Mantiki unayoitaka sisi tuijenge ktk swala hili ni pamoja na swala la HEKIMA na BUSARA hivi haviuzwi dukani wala University. Yawezekana kabisa kijana wa miaka 35 Marekani akawa na hekima na busara kuliko wetu sisi kutokana na mazingira yao lakini hatuwezi kuiga sababu zilizoifanya India ama Marekani kuweka umri huo japokuwa hawajawahi kumchagua rais yeyote mwenye Umri huo acha mbali kugombea tu hajawahi kutokea! hivyo sheria ipo tu ktk katiba kama sheria mama iliundwa kwa minajiri yao.. Haikutungwa sheria hiyo kwa sababu walikuwepo vijana wanaotaka kugombea isipokuwa sheria ilitungwa pasipo kuwepo vijana wanaotaka kugombea Urais hivyo picha nzima ilitazamwa kitaifa na sio kukidhi matakwa ya Zitto au January.

Leo sisi tunataka kubadilisha Umri kwa sababu vijana wamepatikana?.. Hii sii itaonyesha wazi tunaibadilisha katiba kwa sababu ya watu badala ya watu hao kufuata misingi ilokuwepo?. Na pengine nikuulize jambo jingine. Huyo kijana aliye na Umri wa miaka 35 akichukua Urais ina maana atastaafu na miaka 45 (mihula miwili)umri ambao taifa hili linamhitaji zaidi na pengine hekima na busara ndio kwanza inaanza ku kick in!!? Halafu itatugharimu kiasi gani cha mafao yake ikiwa leo hao walotangulia tu kina Mwinyi, Mkapa, Mawaziri wakuu na viongozi tunahemea mashine kuwalipa mabillioni ya fedha. Fikiria maslahi ya Taifa mbele ya haki ya kila mtu maana tunapozungumzia haki ni kuwawezesha watu wote wenye asili hiyo kupata haki sawa na wengineo. Hivyo kuweka hoja ya umri wa miaka 35 haijengi wala kujibu hoja ya miaka 25 wala 40.
 
napata shida sana na namna tunavyojadili mambo mazito kwa mstakbali wa nchi yetu.mkandara umesema vema sana na kwa kweli mjadala huu tusiuchukulie kwa mzaha na sioni sababu za kuiga kila jambo.
 
Mkandara,
ni wapi nimesema ujana unaishia miaka 24?

Usikimbilie hoja ya usomi, hizo ni siasa, jenga hoja zenye mantiki kwani hivyo ndivyo hatimaye tutakubaliana kutokukubaliana; Suala hili hali hitaji mtu kuwa msomi bali ni suala la kimantiki tu; Vinginevyo kama ni suala la usomi, nadhani unajua kwamba moja ya kazi ya msomi ni kuhoji mambo ambayo jamii inaaminishwa kwamba ni norm or obvious or the unquestionable;

Inanishangaza kwanini hamjiulizi au kujadili kigezo cha miaka 40 kilifikiwa vipi, na kwanini kilirushwa kwa miaka kumi zaidi
i.e. kutokea umri wa miaka 30 katiba ya 1965-1977, na kuwa miaka 40 Katiba ya 1977 ambayo tunayo hadi sasa, kigezo ambacho wewe na wengine kadhaa mnaona kwamba kigezo cha busara sana; mkiulizwa hoja za kimaintiki? mnakimbillia hoja za siasa; Naomba nirudie tena swali langu kwenu: Je mantiki ya umri wa miaka 40 ni nini? na nini tofauti ya mtu ambae ana miaka 35, 36, 37, 38, 39, na 40?

Naomba nikusaidie kidigo uelewe kwanini umri wa iaka 35 ulichaguliwa kwani aidha kwa makusudi au kutojua, mnakwepa kujadili suala hili kwa undani; ni hivi - demokrasia nyingi za kiliberali (ambazo wewe najua fika ni mmoja wa mashabiki wake wakubwa), zimeweka umri huu kwa sababu moja tu - wanahisi kwamba, mtu chini ya umri huo hawezi kuwa na uzoefu wa kutosha wa kuongoza taifa; hii ndio sababu ya msingi kwa Marekani na kwingine kote, hata ukifanya utafiti;

Tukirudi nyumbani Tanzania, Katiba hiyo hiyo ambayo mnapenda ibakie kama ilivyo kwenye kigezo cha umri wa mgombea rais, pia inasema kwamba mtanzania kugombea ubunge minimum ni umri wa miaka 21, na kwa mantiki zenu - vigezo vilivyowekwa na watawala juu ya umri na nafasi mbalimbali za uongozi kikatiba, inaonekana kwamba kwa ujumla wake hamuoni haja ya ku=question hilo; Kama tupo pamoja, Katiba hiyo hiyo mnayoipenda na kutokubali kuihoji kwenye suala la uongozi na umri, inasema kwamba moja ya sifa kuu za mtu kuchaguliwa kuwa rais ni lazime awe na sifa za kuwa mbunge, sasa kwanini miaka 35 isiwe sawa kwa urais? Miaka 35 ni miaka 14 zaidi ya kigezo cha ubunge....; hivi hamuoni tatizo hapa? Kama mna hoja, njooni na hoja holistic, sio hoja za kumega hiki na kuacha kile kwani hoja za kisiasa hazina concluion or final analysis, na mbaya zaidi, zipo subjective...; tulieni kidogo mchambue mambo haya, na ikiwezekana hata kisomi kama unavyoshauri, kwani kwa nji ahiyo mnaweza kuja na some objectivity zaidi ya blah blah za siasa kwamba mtu mwenye miaka 40 mtu ana busara zaidi kuliko mtu wa between 35 and 40 - on whose terms? What so magic about 40?

Wakati unajiandaa na counter argument juu ya hili, naomba nikueleze mantiki nyingine kwanini ni muhimu tukashusha umri huo Kikatiba Tanzania - ni suala la demographic changes ambapo jinsi miaka inavyozidi kwenda mbele, age pyramid inazidi kupanuka chini na kuwa nyembamba juu huku watu wa juu wakiwa ni wale wenye umri mkubwa, na umri mdogo ikiwa ni wale wa chini all the way to the base; sasa watu wa juu wakiwa ni only 15-20% of the population - as rulers, how can they rule the 80% ambao ndio the majority? and 40 vis a vis 35 makes a statistical significance, na nadhani kisomi unajua hili;

Hoja zenu zingeeleweka kwa ufasaha zaidi kama zingeachana na siasa, na naomba kwa muda wenu mje na hoja to counter arguments zangu za hapo juu; ninazo nyingine nyingi lakini nianze na hizo kwanza, lakini pia suala muhimu hapo chini:

Muhimu:
Mkandara, ni muhimu wewe na wengine mkatofautisha mijadala hii miwili: Kwanza ni mjadala kuhusu kigezo cha umri wa miaka 35 kwa mujibu wa katiba na pili ni mjadala kuhusu utayari wa Tanzania kuwa na Rais mwenye umri wa miaka 35; Haya ni masuala mawili tofauti kabisa; Katiba kusema umri wa kugombea Urais ni miaka 35 haina maana kwamba kuanzia 2015, Rais ni lazima awe na miaka 35 kwa mujibu wa sheria, sijui kwanini wewe na wengine wengi mnapotea katika msitu huu kiuchambuzi; Hata Zitto na watu wanaomuunga mkono juu ya hili wana hoja dhaifu sana juu ya umuhimu wa suala hili, ndio maana wanachanganya watanzania; Suala la umri kikatiba kugombea Urais linajengewa hoja za blah blah na za kisiasa ndio maana linaishia kuwa ni suala la Zitto, badala ya kuwa ni suala la watanzania; Kwa bahati mbaya sana, 99% ya wachangiaji wa nyuzi zote humu JF juu ya Urais na umri wanachanganya masuala haya mawili (rejea sehemu nime highlight blue na kijani above);

The bottom line is - let the constitution do its work, hasa kwa kufuatana na democracy and demography, then let the people speak at the polls, na iwapo mgombea wa miaka 35 ataonekana hafai compared to mgombea wa miaka 36, 37, 38, 39, 40, 50, 60, etc, hayo ni maamuzi ya wapiga kura, na sio kazi yako kuwasemea wananchi kwamba mgombea mwenye umri chini ya miaka 40 hana busara; hayo yataamuliwa na the electorate; Ukiweza lielewa hili, na pia kutofautisha baina ya mambo mawili ya awali pale juu, nadhani mjadala wangu na wewe juu ya umuhimu wa umri wa urais kikatiba utafikia kikomo, angalau kwa sisi to agree to disagree, kwani sasa utakuwa umeelewa umuhimu na pia crucial link between democracy na demography, kwanini Katiba should take account of this, na pia kuelewa umuhimu na maana ya median age in a population, demographic characteristics in a population, and the importance of incorporating these kwenye demokrasia, hasa kupitia Katiba ya nchi;
 
naikumbuka sana hii thread, sidhani kama bado itakuwa na afya kwa zitto.
Mkuu Zumbe, asante sana kutukumbusha hii kitu!. Hapa ndipo ilipo moja ya thamani kubwa sana za jf, ni uwezo wa kufanya rejea, ukikumbuka ulisema nini. Mimi najikumbusha nilichochangia uzi huu

Pasco.

Mkuu Mchambuzi, to start with, naomba kwanza ku declare my interest!. Namsupport ZZK kuonyesha nia na sio kutangaza rasmi nia hiyo!.
Tofauti ya kuonyesha nia mapema na kutangaza rasmi nia mapema ni hizi zifuatazo!.
Kuonyesha nia: Kubehave ki "presidential hopeful" ili kujenga nia "will" utakayoitumia kama "power" ili kukipata unachokitaka. (Where there is a will, there is a way!"). Faida ya kuonyesha nia mapema ni kukipa chama na sisi wananchi fursa ya kukupima ili muda muafaka ukifika, Chama ndicho kikushauri kijana chukua fomu gombea, unaonekana unatufaa.
Kutangaza rasmi nia: Ni kitendo cha kujitangaza rasmi nia kuwa mtu utagombea urais wa Tanzania mwaka 2015. Kwa utaratibu wa sasa, mtu huwezi kutangaza utagombea urais, ten a ukatangaza wazi mchana kweupe kwenye kadamnasi ya watu!, kwa sababu, wagombea ni wa vyama!. ZZK hakupaswa kutangaza wazi ki vile, this was a mistake, mimi ZZK ni rafiki yangu, na pia nimeshamwambia maoni yangu kwenye hili. Kwa jinsi alivyotangaza is as if alishafikia uamuzi hivyo kutishia kuwa Chadema isipomsimamisha yeye, patachimbika!. Hili nimelieza wazi katika mada yangu ya Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!.

Baada ya kutoa utangulizi huo, sasa nije kwenye hoja zako.
  • Kitendo cha ZZK kutangaza rasmi nia yake mapema, hakuna kanuni yoyote iliyokiukwa, hivyo ZZK hajavunja kanuni yoyote!.
  • Wanao muunga mkono ZZK na wanaompinga ZZK wako wa aina kumi (10), wako wenye busara, wako waoga, wako wadini, wako wa wakabila, wako wa kanda, wako wanafiki, wako waumini, wako wafuasi, wako washabiki, wako wakweli. nitawafafanua katika mada yangu itakayojitegemea.
  • Kwa vile ZZK bado sio mgombea rasmi wa urais kupitia Chadema, na wala mchakato bado haujaanza, hana sababu yoyote ya kutoa misimamo yake kuhusu mada zote hizo ulizo riorodhesha kwa sababu kinachotangulia ni sera za "Chadema kinapigania nini kwenye hayo" sera/ilani ikishatolewa, ndipo mchakato wa ni nani ataweza kuipeperusha vizuri bendera ya Chadema kwenye hayo, na ndipo watawashindanisha kwa vigezo vya sifa, uwezo, kukubalika na kuchagulika, kisha atateuliwa mtu wa kusimamia hayo na ni akisha teuiwa ndipo itafuatia hiyo misimamo na kwenda zaidi kwa kueleza atatekeleza vipi!.
  • Hili la huko mbeleni tujitahidi kupima wagombea wote kutoka vyama vyote kwa ushindani wa siasa wenye tija kwa wananchi ni suala la maana sana, ila kila siku huwa ninauliza, kwani tulipompa JK, tulimpima kwa lipi zaidi ya sura, cheko na bashasha zake?. Watanzania tunachagua sura tuu au majina, ndio maana nilipojibaishisha mimi nasimama na EL, watu humu wanatetemeka!.
  • 2015 lazima tutafanya midahalo ili kuwapambanua wagombea kwa siasa za issues badala ya hizi siasa zetu za sasa za watu!.

Pasco.
 
Mkuu Zumbe, asante sana kutukumbusha hii kitu!. Hapa ndipo ilipo moja ya thamani kubwa sana za jf, ni uwezo wa kufanya rejea, ukikumbuka ulisema nini. Mimi najikumbusha nilichochangia uzi huu

Pasco.

mkuu Pasco kinachonikumbusha ni haya maneno yako,
Wanao muunga mkono ZZK na wanaompinga ZZK wako wa aina kumi (10), wako wenye busara, wako waoga, wako wadini, wako wa wakabila, wako wa kanda, wako wanafiki, wako waumini, wako wafuasi, wako washabiki, wako wakweli. nitawafafanua katika mada yangu itakayojitegemea.
kwamba zitto ameamua kukubaliana na wote wanaomuunga mkono bila kuangalia wana muunga mkono kwasababu zipi? za ukanda? ukabila? udini? au wanafiki (CCM)? ...... hayo makundi niliyoyataja ndo sababu za kufeli kwake, kama angeyakemea tangu mwanzo huenda angefika mbali, ila kwasababu na yeye ni muumini wa makundi hayo, basi ngoja tusubiri, utanielewa......
 
Last edited by a moderator:
Hawezi kugombea umri utakuwa haujatimia yeye kugombea uraisi, kwa hiyo ni upuuzi kulizungumzia.
 
Walivyokutibua mara ya kwanza ulirudi kigoma ukafanya mikutano kigoma na kasulu, ukavuta pumzi sasa anza nao, najua slaa kigoma anaiona kongo lazima abebe ffu wa kutosha, sasa rudi kigoma anza kuchukua tambo.
 
Jmn wana jf, siasa za tanzania zimetengeneza mfumo wa miungu watu ivi inakuwaje unamtuhumu mtu kwa jambo unatoa hukumu lakini ukiulizwa utoe uthibisho huna halafu unamfukuza namna hii kweli tutajenga taasisi imara?
 
Unamzungumzia nani?kama ni zitto inaeleka hujausoma ule waraka wa mapinduzi.Walipotimuliwa wale madiwani kule arusha hamkulia hivi!!!!
 
Back
Top Bottom