Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,598
Niseme tu kwamba mimi sina ufahamu iwapo katika demokrasia ya kiliberali ambayo ndio tunaifuata, suala la timing katika suala tunalojadili, linakuwa treated vipi, hasa ikizingatiwa kwamba hakuna a universal approach katika suala hili, hata katika mfumo unwritten...; ndio maana narudi kwenye Kanuni;
Kama ukiamua kunisoma vizuri, mada yangu hailengi kumjadili MTU kwa Kumfananisha na MTU, bali MTU na Masuala, kwanza ya ndani KIKANUNI na KIKATIBA na vile vile kwa nje, Msimamo wake dhidi ya MASUALA ambayo yanazunguka maisha ya wananchi wa leo;
Vinginevyo Siasa za timing katika ugombea Urais, zilizaliwa CCM, na inanishangaza kwanini Chadema wanaiga utamaduni huu na sina uhakika kama una manufaa; Ningeomba unielimishe zaidi juu ya hili;
Kwa vile wewe ni mwana CCM (naamini sijakosea) ungetumia muda wako kidogo kujielimisha kwa nini CCM iliasisi mfumo huo wa timing na kuzuia watu kugombea endapo kuwa Rais anayetaka kumalizia muhula wa pili.
Pia kwa vile tuko katika siasa zinazotawaliwa na CCM kwa kiasi kikubwa, ungejaribu pia kujielimisha kwa nini CCM inaongoza kwa mbinu chafu ikiwemo fitna, rushwa na hata kuondoa uhai wa watu ili mradi ibaki madarakani.
Sasa, mtu yeyote makini, atajuaje kama si mbinu za CCM kujaribu kupunguza idadi ya watu wa kushughulikia kabla ya 2015?
Nadhani ni vigumu kujadili hoja yako bila kuielewa Tanzania yetu na TANU hadi CCM!!