Uzi maalumu wa Darasa la Mafundisho ya Ndoa

Darasa la Mafundisho ya ndoa linaendelea kama kawaida leo tukizungumzia suala la MAHARI na MISINGI yake kisheria
 
DARASA NO 3: UTOAJI WA MAHARI.

MAANA YA MAHARI
Mahari ni pesa au mali anayatoa mwanaume (Muoaji) kwa Mwanamke ( muolewaji) ili kutimiza Lengo la ndoa. Mahari ni kama hidaya au zawadi anayopewa mwanamke kwa amri ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa anayemuoa.

Kabla ya mkataba wa ndoa kupitishwa jambo muhimu ni ulipaji wa mahari.

UHURU WA KUTAMKA KIASI CHA MAHARI UKO KWA NANI?
Moja Kati ya mambo ambayo pia yanafanya ugumu katika kuiendea ndoa, basi ni suala la MAHARI kuingiliwa na watu ambao hawatambuliki kisheria japo baadhi ya jamii hufosi kutambulika ila kisheria hawatambuliki mfano, Wazazi.

Uhuru wa kutamka kiasi cha mahari uko kwa muolewaji. Mwanamke ndiye mwenye wajibu wa kutaja kiasi cha MAHARI atakachopenda kupokea.

KWANINI MWANAMKE (MUOLEWAJI) NDIYE ANAYEPASWA KUTAMKA NA KUPEWA MAHARI??
Ni kwasababu MAHARI ndiyo inayomhalalishia MUME tendo la ndoa (jimai) kwa MKEWE, hivyo Wazazi au ukoo hawapaswi kutaja wala kupokea MAHARI

Sasa utakuta Wazazi/walezi au Ndugu wa ukoo ndiyo wanayotaja MAHARi na kuyapokea na mbaya zaidi hutumia MAHARI hiyo, sasa si kama wanajitusi wenyewe...

KIASI GANI KINAJUZU KUTOLEWA MAHALI
Hapana kiwango maalum cha MAHARI kilichowekwa na Sheria.

MAHARI ni haki ya mwanamke mwenye kuolewa na ndiye pekee mwenye uhuru kamili wa kutaja kiasi cha mahari anachokitaka. Akipenda anaweza kudai mrundi wa dhahabu na fedha, au akitaka anaweza kupokea kiasi kidogo sana cha mali kama vile shilingi 100/- au chini zaidi kuliko hivyo au akitaka anaweza akasamehe asitake kitu chochote ila kauli nzuri tu.

Lakini tunashauriwa kuwa mtoaji mahari na mpokeaji mahari waangaliane hali. Kama hali ya mtoaji ni nzuri, ni vyema azidishe mahari kuliko kile kiasi kilichotajwa iwapo ana uwezo huo. Na mpokeaji wa mahari, endapo ataona hali ya mtoaji si nzuri kiuchumi, basi ampunguzie mahari na apokee kiasi kidogo zaidi ya kile alichokitaja mwanzoni. Huku kuangaliana hali kunazidisha mapenzi na huruma baina ya mume na mke.

N.B
Pamoja na kuwa mahari hayana kiwango maalum kilichowekwa, inashauriwa yasiwe ya juu sana kiasi cha kuifanya ndoa kuwa jambo gumu na kurahisisha uzinifu katika jamii.

JE, MAHARI INASHUSHA HADHI YA MWANAMKE??

Ilivyo, ni kwamba katika baadhi ya jamii, mahari imefanywa kama bei ya kumnunulia mke inayotozwa na wazazi au walezi wa mwanamke anayeolewa.

Ni katika mtizamo huu wa biashara unaowafanya wale wajiitao watetezi wa Haki na Hadhi ya Mwanamke, waishutumu mahari kuwa imetoa mchango mkubwa katika kumnyanyasa mwanamke katika jamii, kwa kisingizio cha mahari, mwanamke amekandamizwa na kunyanyaswa kwa kiasi kikubwa na wanaume.

Lakini, ni kweli kuwa mahari waliyotoa wanaume katika jamii hizi ndio hasa sababu ya kuwashusha wanawake hadhi zao na kuwakandamiza???? Je, mahari yakiondolewa kama watetezi wa haki za wanawake wanavyodai, wanawake watapata haki zao na hadhi yao ikarudi mahali pake????
 

Attachments

  • maxresdefault.jpg
    maxresdefault.jpg
    125.1 KB · Views: 2
POINT OF CORRECTION

i. Kuhifadhi jamii na zinaa
HAPANA.
Njoo makazini uone wale wanandoa wanaishi mbali na ndoa zao (mke Dom na mume dar) wanavyofanya hiyo zinaaaa, mpaka ma single tunabaki kushangaaa.

iii. Kujenga mapenzi, huruma na ushirikiano katika familia
HAPANA.
Ni mara ngapi umesikia na kushuhudia ufisadi na dhuluma kwenye ndoa?

iv. Kukuza uhusiano na udugu katika jamii
HAPANA
Hawa watu ni hatari kwa ustawi wako.
Waendekezeee tu ndipo utakaponielewa.

v. Kukilea kizazi katika maadili
HAPANA
Wanavyochepuka hivi wanandoa kwa wanandoa, unazungumzi maadili gani hayo?

vi. Kumuendeleza mwanaadamu kiuchumi
Kwani hujui ile mnapata utajiri tu na talaka hapohapo.
Wanawake wa sasa unawajua vizuri wewe kwenye swala la mali?

"" Athari (madhara) ya kutokuoa
Kuenea kwa magonjwa ya zinaa mfano, maambukizi ya UKIMWI. ""

Ukimwi ulivyoingia miaka ya 2000 hivi unajua kuwa Wanandoa ndio waliokufa balaaa ndugu?

I STAND TO BE CORRECTED ila kwasasa NDOA SIO ISHUU KABISAAAAA.

#YNWA

Kaka mkuu,
Haya unayoyasema ni kweli yamekuwa hivyo lakini ukweli ni kwamba hizi ndoa ziliwekwa kwa maana uliyomkoti mwandishi
 
DARASA NO 1; MAANA YA NDOA, UMUHIMU NA ATHARI ZAKE KIJAMII.

MAANA YA NDOA.
Ndoa ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliowekwa na jamii.

Kisheria: ni mkataba wa hiari wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kuzingatia sharti na taratibu zilizoweka na jamii husika

UMUHIMU WA NDOA KIJAMII.

i. Kuhifadhi jamii na zinaa

- Ndoa hukinga wanandoa na jamii kwa ujumla na zinaa kwa kuhifadhi tupu zao na kukidhi matamanio baina yao.

ii. Kuendeleza kizazi cha mwanaadamu kwa utaratibu mzuri

- Lengo la ndoa pia ni kuhifadhi, kutunza na kuendeleza kizazi cha mwanaadamu bila kuzaliana kiholela.Hapa pia usaidia ustawi wa jamii



iii. Kujenga mapenzi, huruma na ushirikiano katika familia

- Ndoa huleta utulivu katika moyo kati ya wanandoa na kupatikana huruma, mapenzi na ushirikiano baina yao

iv. Kukuza uhusiano na udugu katika jamii

- Uhusiano na udugu kati ya wanafamilia walioana huimarika na kuongezeka zaidi kuwa ukoo, kabila, taifa, n.k

v. Kukilea kizazi katika maadili

- Ndoa inakusudiwa kuwa kiungo cha kulea na kuelimisha kizazi katika tabia na maadili mema.

vi. Kumuendeleza mwanaadamu kiuchumi

- Ndoa huchochea wanandoa na wanajamii kwa ujumla kujijenga kiuchumi ili kukidhi mahitaji muhimu ya kimaisha na kibinaadamu.

ATHARI (MADHARA YA KUTOKUOA)

Kuenea kwa magonjwa ya zinaa mfano, maambukizi ya UKIMWI. nk, kizazi kisicho na maadili, kukosekana kwa malezi kwa mtoto, watoto wa mitaani, kuingezeka kwa ongezeko la watu tegemezi (dependents population) , kutokuwa na muunganiko , upendo, na mshikamano katika jamii, n.k
View attachment 2811449
Hii ndoa kwa msingi wa Uislamu.Safi sana.
 
Somo letu leo linaendelea kama kawaida tutazangumzia taratibu za ndoa, masharti ya kuoa na Kuolewa pamoja na kumtambua muozeshaji
 
DARASA NO 4: TARATIBU ZA KUFUNGISHA NDOA, MASHARTI YA KUOA NA KUOLEWA PAMOJA NA KUMTAMBUA MUOZESHAJI NA WAJIBU WAKE KISHERIA.

Kabla ya kuelezea suala la (kufungisha ndoa), ni muhimu kwanza kuleta (mawaidha ya ndoa) kwa ufupi iii kuwakumbusha wanaooana na Wale waliokwisha oana na wengine wachunge ahadi waliyoichukua mbele ya Mwenyezi Mungu, kuwa watakaa kwa wema katika maisha ya ndoa na ikibidi kuachana, wataachana kwa wema vile vile.


Ni vyema katika mawaidha haya kuwafahamisha hawa wenye kuoana na Wale waliokwisha oana kuwa maisha ya ndoa yatakuwa ya furaha na upendo endapo kila mmoja, mume na mke, atajua wajibu wake kwa mwenziwe na akawajibika kwake ipasavyo.

Ndoa iliyofanikishwa kulingana na ahadi ya ndoa ni msingi wa furaha, ushirikiano, utulivu na amani katika familia na jamii kwa ujumla.

KUFUNGA NDOA.
Ili ndoa ifungike ni lazima yatekelezwe yafuatayo:
(i)Mume atekeleze masharti ya kuoa.
(ii)Mke atekeleze masharti ya kuolewa.
(iii)Pawe na Walii au Idhini yake. (Wafungishaji ndoa)
(iv)Pawe na mashahidi wawili au zaidi.
(v)Pawe na idhini (ridhaa) ya mwenye kuolewa.

MASHARTI YA KUOA
(a)Mke anayemuoa awe mwenye dini either Muislamu mwema au mkristo mwema.
(b)Awe anaoa kwa hiari yake (halazimishwi).
(c)Asiwe maharimu wa mke anayemuoa.
(d)Awe baleghe na mwenye akili timamu.


MASHARTI YA KUOLEWA
(a)Mume anayemuoa awe mwenye dini either muislamu mwema au mkristo mwema.
(b)Asiwe katika ndoa ya mume mwingine.
(c)Asiwe katika eda ya mume mwingine.
(d)Awe mwema
(e)Asiwe maharimu kwa mume anayemuoa.
(f) Awe na akili timamu.
(h) awe anaolewa kwa ridhaa yake, sio kwa kulazimishwa.


NANI MWENYE MAMLAKA YA KUOZESHA??
Ndoa haikamiliki mpaka awepo ndugu wa binti anayeolewa ambaye ndiye muozeshaji kwa jina lingine tuna mwiita Walii

Kazi ya Walii ni kufungisha ndoa yeye mwenyewe. Lakini anaweza kuwakilishwa na mtu mwingine, mwanamume mjuzi, afungishe ndoa kwa niaba yake.
Katika sheria ya ndoa mawalii wanaoweza kuozesha ni hawa wafuatao kwa mujibu wa daraja zao:

1.Baba Mzazi wa mwanamke anayeolewa.
2.Babu mzaa baba yake.
3.Ndugu yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja.
4.Ndugu yake wa kiume wa baba mmoja.
5.Mtoto wa kiume wa ndugu yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja (Mpwa wake).
6.Mtoto wa kiume wa ndugu yake wa kiume wa baba mmoja.
7.Baba yake mdogo (Ami) aliyezaliwa na baba yake kwa baba mmoja na mama mmoja..
8.Baba yake mdogo (Ami) aliyezaliwa na baba yake kwa baba tu.
9.Mtoto wa kiume wa baba yake mdogo wa kwa baba yake mdogo na mama.
1O.Mtoto wa kiume wa baba yake mdogo kwa baba tu.
11.Serikali. (Ndoa ya kiserikali au Sheria ya mahakama)

Walii wa daraja ya chini katika orodha hii hawezi kuozesha mpaka iwe walii wa daraja ya juu yake hayupo. Kwa mfano, babu hawezi kuozesha kama baba mzazi yupo, ndugu yake hawezi kuozesha ikiwa babu yupo, na kadhalika. Ikiwa waliii wa daraja ya chini ataozesha na hali yakuwa walii wa daraja ya juu yupo, na hakuridhia, basi ndoa haitasihi. Mtu ambaye hayumo katika orodha ya mawalii wala si mtoto wa kiume wa hao waliotajwa hapo juu hawezi kuozesha. Endapo mawalii wote watakosekana, Kadhi au kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu atamuozesha binti huyo.



Walii ili aweze kuozesha ni lazima atimizwe masharti yafuatayo:


(a)Awe Mwenye dini mwanamume.
(b)Asiwe mtumwa (awe muungwana).
(c)Awe mwenye akili timamu.
(d)Awe anaozesha baada ya kupatikana idhini ya mwenye kuolewa.


(e)Awe muadilifu.
(iv)Pawe na Mashahidi wawili
Ndoa haisihi bila ya kushuhudiwa na mashahidi wawili wenye sifa zifuatazo:
(a)Wawe watu Wazima waliokwisha baleghe. Watoto hawawezi kuwa mashahidi.
(b)Wawe na akili timamu.
(c) Wawe Wenye dini wanaume.
(d)Wawe waadilifu.
(e)Wawe waungwana (sio watumwa).
(v)Ridhaa (Idhini) ya mwenye Kuolewa

ILi ndoa ikamilike ni lazima idhini ya mwanamke anayeolewa ipatikane.

IJABU NA KABULI
Ijabu: ni yale maneno anayosema walii kumwambia mume anayeoa kama hivi:"Nimekuoza Aisha binti Salim" wala asiseme: "Ninakuoza..."
Kabuli ni maneno ya mume ya kukubali kumuoa binti anayetaka kumuoa kwa kusema: "Nimekubali kumuoa Aisha bint Salim", wala asisema: "Ninakubali kumuoa..."
Kwa hiyo Ijabu ni kauli rasmi anayotoa walii au muwakilishi wake mbele ya mashahidi wawili ya kumuoza mke kwa mume na Kabuli ni kauli rasmi anayoitoa mume ya kumkubali mke katika ndoa.


mfano:
Walii: Shaaban bin Abdurahman.
Shaaban: Labbayka.
Walii: Umekubali kumuoa Aisha bint Salim?
Shaaban: Naam, Nimekubali kumuoa 'Aisha bint Salim.
Walii atamuuliza Shaaban kama hivyo mara mbili na mara ya tatu atamalizia kama ifuatavyo:
Walii: (Mara ya tatu): Ewe Shaaban bin Abdurahman, nakuoza kwa namna alivyoamrisha Mwenyezi Mungu, nayo ni kukaa naye kwa wema na kutokana naye kwa wema vile vile.
Ijabu: Nimekuoza Aisha binti Salim kwa ridhaa yake mwenyewe, (Kutajwa mahari si lazima).
Kabuli: Nimekubali kumuoa Aisha bint Salim
Muhimu: Kilicho lazima katika kufungisha ndoa ni kupatikana kwa Ijabu na Kabuli. Kwa mfano, Walii badala ya kumuuliza Shaaban mara mbili: "Umekubali kumuoa.. .", anaweza kumuoza Shaban moja kwa moja kwa kauli ya Ijabu: Shaaban bin Abdurahman Nimekuoza..

love-1.gif
 
TOPIC 3 Review,: KUTANGULIZA NA KUCHELEWESHA MAHARI

MDAU ANAULIZA...

JE ipi inafaa na inajuzu kutanguliza au kuchelewesha mahari (kuilipa baadae kama deni)?????

JIBU.
Kutanguliza ama kuchelewesha mahari ni ada ama desturi ya mahala na ni katika uwezo wa mtu. Vyote vinafaa endapo pakiwepo makubaliano baina ya muolewaji (anayepokea mahari) na Muoaji (anayetoa)

Lakini kinachofaa zaidi ni kutanguliza mahari kama mlivyokubaliana apo kabla

#Shukurani
questions-reponses-profits.jpg
 
SWALI LA MAJADILIANO: Topic 3; MAHARI

JE MAHARI INASHUSHA HADHI YA MWANAMKE KWENYE JAMII?? NA KWANINI??

#Karibu wadau kutoa maoni yenu.
questions-reponses-profits.jpg
 
Ukisema maswala ya mafundisho ya ndoa, kwa wenzangu na mimi tuliooa enzi hizo. Roman .
Namkumbuka mama na mzee john chilipweli pale msimbazi. Mungu awabariki hawa wazee. Nina zawadi yao kila mwaka
 
Hamna kuoa labda mzungu ila Kama mwafrika unaenda kuwa maskini
Kataa ndoa
Maajabu ya Ndoa ya mwafrika
1.anashinda kanisani kumchangia mchungaji ajengewe nyumba yy akitaka kujenga anaombewa
2. Anacheza mchezo kila siku kupitia hela ya matumizi watoto wanakosa chakula akipata hela ananunua vyombo na Nguo badala ya kufungua biashara
3.anamheshimu mchungaji kuliko maisha yake
4.anakata mauno kanisani huku nyumbani hata kucheza hawezi
Ndoa inahitaji mtu asiyekuwa na maana yoyote ili aweze kuishi na mwanamke
5.kataa ndoa kwa faida ya akili na mwili
Karibu sana katika Darasa la Mafundisho ya ndoa

Endelea kufuatilia uzi huu muhimu. Tutakwenda kujadili WAJIBU WA MUME NA MKE KATIKA MAISHA YA NDOA.

#Shukuran
 
Back
Top Bottom