Uzi maalumu wa Darasa la Mafundisho ya Ndoa

Darasa letu litaendelea kesho tukijaaliwa tutazangumzia wajibu wa MKE KWA MUMEWE.

#shukurani
 
DARASA NO 8: WAJIBU WA MKE KWA MUMEWE.

Wanawake nao wanawajibika kisheria kwa waume zao kama ifuatavyo.


(i)KUMTII MUMEWE KATIKA MAMBO YOTE MEMA ATAKAYO MUELEKEZA
Mke kumtii mumewe katika mambo ya kheri, si kwa ajili ya kumfurahisha mumewe tu bali ni katika kumtii Mwenyezi Mungu pia

Mwanamke bora ni yule anayempa (mumewe)furaha wakati anapomuangalia, anayemtii wakati anapomuelekeza afanye jambo) na ambaye hampingi kuhusu yeye mwenyewe na mali yake kwa kuchelea, kutomfurahisha (kumuudhi).

(ii)KUMFURAHISHA MUMEWW NA KUMLIWAZA.
Mke hana budi kuifanya nyumba yake mahali pa furaha na utulivu wa mawazo kwa mumewe. Inatakiwa mwanamume anapotingwa na mambo magumu katika harakati za kutafuta maisha na kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu.

Mume anatakiwa apate maliwazo kutoka kwa mkewe arejeapo nyumbani.

(iii) KUHIFADHI NYUMBA NA MALI ZA MUMEWE
Mwanamke ni malkia wa nyumbani mwenye jukumu Ia kuhakikisha kuwa usalama na unadhifu unakuwepo nyumbani.

Mwanamke hana haki ya kumkaribisha yeyote nyumbani kwake pasi na idhini ya mumewe. Kwa maana nyingine, mwanamke haruhusiwi katika sheria ya Ndoa, kumkaribisha mtu yeyote ambaye mumewe hataki akaribishwe nyumbani kwake, awe wa kike au wa kiume.

Mwanamke pia, ni wajibu wake kutunza mali ya mumewe na asitoe kumpa yeyote pasina ruhusa yake.

Ni jukumu Ia mke kuhakikisha kuwa hapana ubadhirifu wa chakula, nguo n.k. na kila kitu katika nyumba kinatunzwa

(iv)KUWA NA SUBIRA JUU YA MUMEWE
Mume na mke wote wanawajibika kuvumiliana na kusubiriana. Hakuna mwanaadamu aliyekamilika. Kama walivyo na udhaifu wanawake, vile vile wanaume wana udhaifu wao.

Takriban kila mtu hakosi udhaifu ambao si wenye kumpendezesha mwenziwe. Kama wanaume walivyosisitizwa kuwavumilia wake zao kwa udhaifu kama huu, na wanawake pia hawana budi kuwavumilia waume zao endapo watakuwa na udhaifu usiopendeza.

Kufanyiana subira ni jambo linalopendeza mno mbele ya Mwenyezi Mungu na lina malipo makubwa.


(v)KUTOSHEKA NA KILE ANACHOPEWA NA MUMEWE
Mwanamke hana budi kujizuilia na kumtaka mumewe ampatie matumizi ambayo hana uwezo nayo.

Kwa upande wa mume, kama tulivyoona hana budi kwa kadiri ya uwezo wake kukidhi mahitaji muhimu ya mkewe na familia yake kwa ujumla. Pia ni vyema, kama mume ana uwezo mkubwa, ampe mkewe ziada ya mahitaji muhimu na amzawadie mara kwa mara.

Mwenye wasaa agharimu kwa kadri ya wasaa wake; na yule ambaye amepungukiwa riziki yake, atoe katika idle alichopewa na Mwenyezi Mungu;

Endapo mke atamdai mumewe hiki na kile na hali anaona kuwa uwezo wake ni mdogo, kwa vyovyote vile atamfanya mumewe aishi kwa wasi wasi. Atamuona mkewe kuwa hamtakii jema na hiyo itakuwa ni sababu tosha ya kuondoa mapenzi na huruma katika unyumba na kuvuruga amani katika familia.


(vi) KUWAHUSIA NA KUMKUMBUSHA KUMCHA M/MUNGU
Ni nani anayependa mpenzi wake ahiliki motoni? Kama mke anavyompenda na kumhurumia mumewe kwa kumfanyia mambo kadhaa yanayompendeza na kumfurahisha katika maisha haya mafupi ya dunia,

basi anapaswa atoe kipaumbele katika kumuusia na kumkumbusha mumewe kumcha M/Mungu ili kwa rehma za M/Mungu waendelee kuwa pamoja katika starehe za kudumu milele huko peponi.


Darasa la Mafundisho ya ndoa.........
IMG_20231116_164913.jpg
 
Kesho pia darasa letu litaendelea kama kawaida endelea kufuatilia Ndugu msomaji Katika kupata maarifa juu ya Maisha ya ndoa

#Shukrani
 
Darasa leo linaendelea kama kawaida leo tutazungumzia namna ya kumfanya mumeo ashiriki tendo la ndoa ipasavyo
 
DARASA NO 9: NAMNA YA KUMFANYA MUMEO ASHIRIKI IPASAVYO TENDO LA NDOA..

Hii leo tutazangumzia mambo matano ambayo mwanamke akiyafanya atamvutia mumewe kushiriki barabara katika tendo la ndoa.

01. IMARISHA USAFI KWENYE ENEO LA BAFU.

Usafi ni kitu muhimu ambacho tumeamrshwa sisi wanaadamu kukifanya kwa malengo mengi ikiwemo kulinda siha zetu.

Mwanaume ili ashiriki ipasavyo katika tendo la ndoa inahitajika kumjenga kisaikolojia kukabiliana na tendo lenyewe, pale ambapo atakwenda bafuni na kukuta mazingira yasio masafi yanaweza yakamuathiri hadi akakosa morali wa kushiriki upasavyo katika tendo la ndoa. Mwanamke imarisha eneo hilo.

02. JENGA TABIA YA KUOGA NAE PAMOJA.

jambo hili la kuoga na mumeo humuanzisha hamu ya kiakili ya kufanya tendo la ndoa kiufasaha zaidi.

03. JENGA MAZOEA YA KULA NAE PAMOJA.

Waswahili tunasema "raha ya chakula umpate wa kula nae" mwanaume si wa kula peke yake ,msubiri kama kaenda kazini mle wote au hata kama ukianza usishibe kabisa ili uje ushibe na mumeo, kula pamoja kabla ya kufanya tendo la ndoa huimarsha ari na nguvu kwa mwanaume katika tendo la ndoa.

04. ZIDISHA USAFI WA KIWILIWILI CHAKO.

Kiashiria cha mwanzo cha kuhitaji tendo la ndoa mwanaume ni nwonekano imara na usafi wa nwanamke, jitahidi nwanamke kujiweka sawa kabla mumeo hajaingia ndani.

Jitahidi uwe unakuwa imara kwenye kucha na nywele za aina zote katika kiwiliwili chako kwani zikikaa zaidi ya siku nyingi huleta harufu itakkayomzuia mumeo kutotamani tendo la ndoa.

05. IMARISHA USAFI NA UPAMBAJI WA KITANDA.

Usije ukashangaa mwanaume kaingia ndani kisha ni yeye na TV au simu ,huenda allihitaji kuwahi kitandani lakini kutokuwa safi umekuwa sababu ya kutovutiwa.

Mwanamke ujue kuwa kitanda ni sehemu ya shukhuli tu na malazi si kabati la nguo ,fua shuka ziwe safi na uturi mzuri, mapambo ya kila aina na style za tofauti za uwekaji wa mito ,ni njia madhubuti ya kufanya mume kuwa na hamu ya tendo la ndoa.

Usilalalamike mumeo kutoshiriki vyema kwenye tendo la ndoa huenda wewe ndiye chanzo chenyewe, zidisha uwekezaji kwenye dondoo hizi tendo la ndoa litakuwa kipaumbele cha kwanza kwa mumeo voooh !!

Darasa la Mafundisho ya ndoa........
nguvu.jpg
 
DARASA NO 10: MAMBO 5 YATAMFANYA MUMEO AANGUKIE KATIKA PENZI LAKO.

Upendo ni miongoni mwa mahitajio ya msingi kwa mwanamke na mwanaume. Ili mwanaume aangukie katika penzi lako atataka kuhisi mambo 05 kutoka kwako, vinginevyo hali itakuwa tofauti kabisa. Haya ni mambo ambayo unapaswa kuyafanya ili mumeo aangukie ndani ya hubba lako moja kwa moja:

01. JE, WEWE NI SEHEMU SALAMA DUNIANI?

Mikono yako, macho yako, fumbatio lako ni kimbilio kwake. Iwapo mwanaume hahisi kuwa ni mwenye amani mbele yako, hatojaribu kujenga maisha yake pamoja nawe, na kwake hutakuwa kimbilio. Lakini iwapo atahisi amani kuwa na wewe na akahisi kuwa wewe ni eneo salama analoweza kukimbilia kwenye sayari ya dunia hii, ni muhali kukuacha.

02. JE, YEYE KWAKO NI SHUJAA?

Anataka ahisi kwamba wewe unamuona kama shujaa. Hili litatokea iwapo utakubali kuwa chini yake popote mtakapokuwa. Wanaume wanataka wahisi kwamba mwanamke anawaamini, na hili kwao ndilo wanalolitafsiri kama “upendo”. Hii ina maana kwamba unatakiwa uwe msikivu mbele yake na kumuunga mkono. Muamini kwamba anataka kukuhudumia na kukupeleka kule unakotaka.
Ndani mwake kuna “shujaa”, muoneshe heshima. Mwanaume huangukia katika upendo wa mwanamke anayemfanya ahisi kwamba yeye ni shujaa wake.

03. NI MTU ANAYESTAHIKI KUSIFIWA

Mpongeze kwa kazi nzuri, na usisumbuke kwa kazi mbaya. Usimponde... Hii ndio njia inayowavuta wanaume. Wanapenda uwaoneshe mbele ya watu kwamba ni watu bora.

04. UHUSIANO BORA WA KITANDANI

Mwanamke hakikisha unakuwa mtaalamu kitandani katika kumpa mumeo mahuba, kuwa ‘romantic’ kwa kauli, matendo na hisia. Ondoa aibu, jenga ubunifu kwa mumeo na ufunguke kwake.

05. ANATAKA KUSIKIA UKWELI NA UHALISIA WAKO:

Mshirikishe mambo yanayokupa wasiwasi, maumivu yako, raghba na ndoto zako kwa kiwango cha juu kabisa…. Muoneshe utu wako.

Anatafuta sehemu salama ambayo anahisi kwamba anaweza kuweka hisia zake. Iwapo huwezi kuelezea hisia zako, hutaweza kumsaidia kwenye hisia zake. Ili uhusiano wowote ufanikiwe yakupasa kwanza kuzielewa hisia zako. Mwanaume huangukia katika hubba la mwanamke ambaye anapokuwa naye huhisi kuwa anafurahia maisha.

Darasa la Mafundisho ya ndoa.......
beautiful-couple.jpg
 
Ni kweli usemayo ila kinachofanya ndoa kuwa hivi ni tamaa ya ngono na pesa....kwa mwanamke na kwa mwanaume
You are trying to change ma altitude and convincing me about something. I'm familiar wit your game.

Marriage is shit.

Wewe una tamaa ya ngono ?
 
DARASA NO 11; SINDANO TANO ZA KUMCHOMA MWENZA WAKO ILI ATULIE KATIKA NDOA.

Moja ya sekta ambazo hazihitaji kuziingilia kwa mazoea ni sekta ya ndoa, unapoingia kwenye ndoa kila siku unatakiwa uwe na kitu kipya ambacho kitamfanya mwenza wako atulie ndani ya ndoa barabara.

Leo nimekuandalia sindano tano ambazo mwanandoa anatakiwa awe nazo milele amchome mwenza wake ili amfanye mwenza huyo ampende milele bila kumchoka, sindano hizi ni kama ifuatavyo ;

01. UBUNIFU.

Ubunifu ni sindano pekee katika ndoa ambayo hufanya ndoa kuwa imara yenye msimamo na muonekano mzuri kwa wanandoa ,kila mwanandoa anatakiwa awe mbunifu kwa mwenza wake, ubunifu si katika tendo la ndoa tu bali hata lugha, mavazi ,upendo wa aina yake kwa mwenza na familia yake kwa ujumla.

02. VITENDO.

Upendo wa sasa umejaa matatizo mengi sana hususan kwa wanandoa wasiowajibika ipasavyo katika ndoa zao, imefikia hatua hata kuwa nadra mwanandoa kumwambia mwenza wake "Nakupenda" inakuwa ngumu sana ,vitendo ndio sindano pekee ambayo itaimarisha ndoa yenu ,hapa namaanisha upendo kwa vitendo ,kila siku mwanandoa anatakiwa aonyeshe vitendo zaidi kuwa ni jinsi gani anampenda mwenzake.

03. AHADI.

Ahadi ni vitu au maneno ambayo tunaambiana siku zote mfano nitakupa zawadi, nitafanya kadhaa, ahadi ni sindano pekee inayoongeza upendo katika ndoa, kumbuka unapoahidi kitu kwa mwenza wako na ukakitekeleza itamjenga mwenza wako kuona unamjali,kinyume na kuahidi bila kutekeleza ni onesho kuwa uliyenae humpendi na humjali.

04. KUMSHANGAZA.

Mwanandoa unatakuwa uandae matukio ambayo yatamshangaza mwenzako ,na hapa sio mshangao wa kumweleza habari za msiba la! hapa ni kumuonesha kitu ambacho hajawahi kukitarajia wewe kumfanyia ,mfano safari yoyote ambayo hamjawahi kwenda unamchukua na kupeleka, huku kunaongeza ladha ya mapenzi katika ndoa.

05. KUBEMBELEZA.
Kubembeleza ni suala muhimu ambalo mwanandoa anatakiwa kujipamba nayo na sindano muhimu, mfano unapomuona mwenza wako kuna jambo limemfika unaamiliana nae katika mfumo wa kumbembeleza.

Hizi ndio sindano nilokuja nazo leo ambazo kila mwanandoa anapaswa kujipamba nazo ili kumfanya mwenza wake ampende zaidi.

Darasa la Mafundisho ya Ndoa......
ba0166c7a50d96eb270097f3f911e08a_L.jpg
 
You are trying to change ma altitude and convincing me about something. I'm familiar wit your game.

Marriage is shit.

Wewe una tamaa ya ngono ?
nikiwa na MTU nimpendaye tena karibu napenda kusex Mara 5 kwa wiki.labda awe mbali ndiyo nakuwa sina namna.
 
nikiwa na MTU nimpendaye tena karibu napenda kusex Mara 5 kwa wiki.labda awe mbali ndiyo nakuwa sina namna.
Msihamasishane uzinzi, kama mpo tayari kufunga ndoa. Basi ni kheri mkafanya hivo kuliko kuwa kwenye uchumba wa muda mrefu
 
nikiwa na MTU nimpendaye tena karibu napenda kusex Mara 5 kwa wiki.labda awe mbali ndiyo nakuwa sina namna.
Wewe ukiwa na mwanajeshi si ndio mali yake unawapa wa nje kabisa maana wao kozi za miezi kadhaa kawaida mission za miaka kawaida wapo mbali na home muda mwingi.

Upo vizuri kwenye kitengo muhimu kwa nini kwenye ndoa haupo ?

Mimi binafsi sio mtu wa ndoa kabisa kwa jinsi navyo endesha maisha yangu. Maisha yangu yana nihitaji mimi zaidi kuliko mtu mwengine kushirikiana I'm so special
 
Back
Top Bottom