Uzalendo ni chanzo cha Usalama wa Taifa?

Ongezea mambo mengine kama yafuatayo yanomfanya mtu kuwa mzalendo.

1. Kujitoa na kuwa tayari kufa kwa ajili ya taifa lako.
2. Kutunza siri za nchi na kuzilinda kwa gharama yoyote ile.
3. Kujiona na kujisikia weye ni sehemu ya taifa.
4. Kujivunia utaifa na kuwa tayari kupigia kifua utaifa huo.
5.Kujisifia utaifa wako na kuwa tayari kuutangaza utaifa huo popote pale.
6 Kuweka kumbukumbu na historia ya taifa hilo kwa ajili ya vizazi vijavyo.
7.Kulinda Mali na Rasilimali za nchi na mipaka yake yote.

Namba 1, 2 na 7 ni Usalama wa Taifa vikiwemo vyombo vyake vyote.

Namba 3-7 ni wananchi .
Mkuu nashukuru sana nimepata kitu kipya hapa.
Shukran sana
 
UZALENDO NA AMANI

Naunga mkono hoja kwa kadri ulivyoijadili ingawa nitaongeza mtizamo wangu kwa kadri ya uelewa.

Kwanza ni kutambua kwamba hili ni suala muhimu sana na la msingi sana kwenye jamii iliyostaarabika na kuendelea.

Tunapozaliwa mara nyingi vichwa vyetu huwa wazi(vacuum) bila maarifa yoyote, hii ni kwa mujibu wa wanasaikolojia ya makuzi). Baada ya hapo mtoto huanza kujazwa maarifa kulingana na wale au yale yaliyomzunguka naye huwa mwanafunzi mwaminifu na baadaye kuja kuwa mwalimu.

Hivyo, msingi wa kwanza wa yote ni maarifa tunayopata wakati tukiwa wadogo na yale tunayoyaona. Maarifa haya ndo huja kuza msingi wa utambuzi wetu wote. Kujua thamani jema na baya na kiasi chake.
Samaki mkunje angali mbichi.

Kwa sababu hiyo, chachu muhimu ya uzalendo inaanza kwenye familia au jamaa waishio pamoja ikijumuisha makuzi yao kwa kila mmoja(mwanajumuiya).

Kujitambua:
Kutambua ubinadamu wako na mahitaji yako(wewe ni nani na unahitaji nini na vitatoka wapi)ni suala muhimu pia. Kama tunavyofahamu ukamilifu wa ubinadamu hautokani maarifa au mali, bali mahusiano na wengine wanaomzunguka. Hivyo, kujifunza thamani ya mahusiano mema ni kitu cha msingi ndani ya jamii yako ya awali. Tambua thamani ya unachopata toka kwenye mazingira na watu wanaokuzunguka. Huwezi kutoa chochote kwa mwenzako au kuwa tayari kutoa chochote bila kujua umuhimu wake kwa kuanzia kwako mwenyewe.

Kumtambua wenzako:
Kuwatambua binadamu mwezako na mahitaji yao. Baada ya safari ya kujitambua, safari inayofuata ni namna gani utamtambua binadamu mwenzako bila mipaka yoyote mfano: mrefu, mfupi, mweupe, aliye au asiye na mali nk. Pia kutambua mahitaji yake ya msingi na kujua kuwa mahitaji mengine yanatoka kwenye himaya yako. Utakapotambua kuwa hitaji la binadamu mwenzako ndilo lako basi kinachofuata ni kujengewa imani/ moyo wa kuthamini binadamu mwenzio. Hapo, utampa thamani linganifu na wewe kulingana na nafasi uliyopata kwenye makuzi yako.
Binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja.

Kujiweka tayari unapohitajika.
Baada ya safari mbili hapo juu, safari inayofuata ni kuuweka tayari moyo wako na akili kujitoa kwa hali na mali wakati wa hitaji na pasipokuwa na hutaji. Kwani mzalendo hasubiri kuhimizwa. Hata pale adui atakapofanikiwa kujipenyeza sehemu yoyote basi atakutana na nguvu ya uzalendo na kujitoa ambayo itampa wakati mgumu kutimiza azma yake.

Tukumbuke hata wakoloni walipokuja na siraha zao za kisasa, sehemu walizokuta umoja na uzalendo basi walipata shida kubwa kutawala. Hivyo, kuwa na idadi kubwa ya watu wenye mioyo ya uzalendo ni nafasi kubwa ya maendeleo na amani kwa taifa. Kama wakiws wachache kulingana na jamii au kizazi mara myingi watashindwa au kuangamizwa.
Umoja ni nguvu

Safari hizo hapo juu zaweza kwenda kwa pamoja ndani ya makuzi mtu. Zimewekwa kwa mafungu ili kuweza kuzieleza vyema.

Kwa msingi huo kaya zetu, jamii zetu, taasisi zetu zitakuwa zimejengwa na misingi ya uzalendo madhubuti. Uzalendo utasukuma kutokuwa tayari kuona haki ya binadamu mmoja inapotea au haki ya jamii au taifa.

Kwa msingi huo mnyororo huu uliofungwa ndani ya jamii zetu(uzalendo) utakuwa ndio ngome imara itakayomshinda adui kuibomoa na kupenyeza yasiyofaa.
Amani ni tunda la haki na penye haki pana uzalendo.

Hivyo, kabla ya kuulilia uzalendo ni vyema kujiuliza na kutafakari kwa muktadha huu:

1: Je ndani ya familia zetu kuna uzalendo?

2: Je tunajifunza uzalendo ndani ya familia?

3: Je tunaweza kutoa mafunzo ya uzalendo kwa watu wasiojua wala kuelewa umuhimu wa uzalendo tangu walipozaliwa?

4: Je tunaweza kuwafundisha watu uzalendo na wakauvaa bila kuona matunda ya uzalendo au uzalendo ndani yetu?

5: Je ndani ya nchi yetu kuna uzalendo wa kweli?

6: Je viongozi wetu wanaongoza kwa uzalendo wa kweli?
Aisee kaka, nakushukuru sana.
Nyongeza yko ni kubwa sana kias kwamba naona ilifaa sana kusimam kama uzi. Lkn kwa maana uzalendo halis umeamua kushare knowledge hiyo katk huu uzi wetu.

Mungu akubariki sana. Kupitia comment hii kuna mengi nimeyapata na naendelea kuyatafakar kwa kina kwajil y kujijeng na kujitayarisha muda wote
 
Maisha yakiwa magumu, tunaanza kuona mara wewe Mkenya, au ni Mtusi sijui ni Mnyasa
Na ndio imekuwa wakati huu, kwa jinsi kundi ya kubwa la wajinga linavyoongezeka mpaka uafrika unafatiliwa hata kama ni mzaliwa wa vizazi na vizazi, Mjaluo wa Musoma au Muha wa Kigoma tunamuona mgeni wa nchi
Zamani walikuwepo wanoko wanawaita Waarabu wa Mwamashilingi na Wahindi wa Kahama ni magabacholi
Aiseee dah
 
Aloo safi kabisa inapaswa kuwa hivyo maana hivi vyama vya kisiasa kupitia ushawishi wao(influence yao) wameigawa nchi kikanda na pia wamevuruga umoja wa kitaifa, raia mapenzi yao katika taifa (uzalendo) yamepungua na kuelekezawa katika vyama. Hapa ndipo tunakutana na chawa kina L. M.

Matokeo yake badala ya kua kitu kimoja tunaishia kurumbana(kukashifiana).

Badala ya kua kitu kimoja kutatua faults tunategeana na kusubili upande mwingine ukosee ili ipatikane sababu(justification) ya kushusha ushawishi wa chama fulani, Sasa hili ni tatizo kwani sote tunajenga nyumba moja yanini kugombea fito.

Kuhusu kuazisha shilika hili suala hatuna budi itabidi tuanzishe tu maana kuna ombwe hapo katikati ukiachana na vyama na hawa wanaharakati ambao wapo mmoja mmoja unaona kuna kitu kina miss ambacho kitatuunganisha wote kama taifa tukafocus/tukawa na shabaha moja pasipo kujali tofauti zetu.

Tunaweza kuthubutu kwa kuanza na resources tulizonazo kwasasa then tutaimalika taratibu taratibu, mfano Tunaweza tukaanza na movement kupitia mitandao (social media).
Aisee kaka umeandika hoja nzito nzito sana.
Me nadhan kuna haja serikali ifanye jambo maana sis wanainchi mmoja mmoja tunaweza kukwama.
Unaonaje ikaanzishwa shirika lisilo la kiserikali ambalo halifungamani na itikadi yyt ya chama likajikita katk kueneza uzalendo wa kweli..hasa katik jamii moja kwa moja.
Kupitia mikutano ya hadhara, majarida, machapidho, vyomb vya hbr na mambo kama hayo??
 
Ongezea mambo mengine kama yafuatayo yanomfanya mtu kuwa mzalendo.

1. Kujitoa na kuwa tayari kufa kwa ajili ya taifa lako.
2. Kutunza siri za nchi na kuzilinda kwa gharama yoyote ile.
3. Kujiona na kujisikia weye ni sehemu ya taifa.
4. Kujivunia utaifa na kuwa tayari kupigia kifua utaifa huo.
5.Kujisifia utaifa wako na kuwa tayari kuutangaza utaifa huo popote pale.
6 Kuweka kumbukumbu na historia ya taifa hilo kwa ajili ya vizazi vijavyo.
7.Kulinda Mali na Rasilimali za nchi na mipaka yake yote.

Namba 1, 2 na 7 ni Usalama wa Taifa vikiwemo vyombo vyake vyote.

Namba 3-7 ni wananchi .
1.hiyo ni vyombo vya ulinzi na usalama,wanalipwa
2.Kijeshi zaidi
3. Labda uwe kitengoni
4. Hata Taifa stars imefeli mbaya mbovu hapo AFCON.
5. Royal tours did that si unaona mwarabu alikuja kutimua njeree kule?
6. Kuna Mzee wetu humu anafanya hiyo kazi vizuri sana.
7. Umesikia wapi hiyo suala mkuu?bandari imekushinda kulinda,huko porini napo pamekushinda,unajua kabisa kuwa mali yote iliyoko hapa ni ya serikali kwa hiyo huo uzalendo ni pamoja na kutoa ushirikiano pindi serikali itakapo hitaji kuchukua mali zake.
Cha kufanya anza kuwafundisha watoto wako kuhusu uzalendo,ili siku moja watakua mfano wa kuigwa.
 
Samaki mkunje angali mbichi.
Shukran Mkuu, ufafanuzi wako umetupanua upeo kwamba msingi mkubwa wa uzalendo unaanzia katika ngazi ya familia katika malezi... hapa nimeelewa kwanini familia inatambulika kama Taasisi.

Katika hili nakubaliana nalo kwani mifano ipo wazi

Mfano.
Mataifa kama Japan China wanafundisha uzalendo na maadili mema tokea wanazaliwa kuna mahali nilisoma kua huko Israel tabia(Akili) ya mtoto inaanziwa kutengenezwa kuanzia kwenye ujauzito... nazani wote tunajua tabia za mataifa hayo kwa ujumla.

Hata hapa Tanzania kuna tofauti katika malezi mfano jamii ya watu wa nyanda za juu Kusini huwezi ukalinganisha na mikoa ya pwani(Dar, Moro,) kitu cha ajabu ni kwamba kutokana na kukosekana kwa jitihada za makusudi za kuendeleza uzalendo na maadili miaka ya hivi Karibuni hali imekua mbaya zaidi kiasi kwamba hata zile jamii zilizokua imara zimeanza kuporomoka kimaadili.

Jitihada zisipo chukuliwa kwa wakati hata hiki kizazi cha panyaroad wakiwa wakubwa na kwa wakati huo hali itakua mbaya zaidi pengine wakashindikana kudhibitiwa wakaunda magenge ya kihalifu kama kule Brazil.
 
Hiyo itakuaa hatar kubwa sana aisss. Kuna kitu kinahitajika sasa kuliko kawaida ili kushape hiki kizazi
 
chanzo ni uwe uvccc kuwasifia wazee wa ccm na kutii amri zao
Hao chawa ndiyo chanzo Cha uzalendo kupotea. Maana chawa Hana address Leo yupo kichwani, kesho yupo kwenye nguo...Mtu yeyote mwenye tabia za kusifu pasipo haja hawezi kuwa mzalendo. Na ndiyo hao ambao ni chanzo Cha matatizo yote haya ya Sasa.

Nampenda sana Baba wa Taifa, ila Kwa sehemu alichangia hii tabia kumea na kukua katika taifa kwakupenda kusofiwa na kitotaka kukosolewa hata alipoonekana kukosea.

Pia kuweka Katiba ambayo yeye aliishi ya impunity mpaka kusababisha watu wote kuwa loyal Kwa wenye nafasi na siyo nchi. Kwa hili lazima kama Taifa tukubali kuvunja huu mfumo Ili tujenge taifa ambalo Kila mtu mwenye mchango apate nafasi ya kuutoa Kwa faida ya nchi na siyo persons
 
Aloo safi kabisa inapaswa kuwa hivyo maana hivi vyama vya kisiasa kupitia ushawishi wao(influence yao) wameigawa nchi kikanda na pia wamevuruga umoja wa kitaifa, raia mapenzi yao katika taifa (uzalendo) yamepungua na kuelekezawa katika vyama. Hapa ndipo tunakutana na chawa kina L. M.

Matokeo yake badala ya kua kitu kimoja tunaishia kurumbana(kukashifiana).

Badala ya kua kitu kimoja kutatua faults tunategeana na kusubili upande mwingine ukosee ili ipatikane sababu(justification) ya kushusha ushawishi wa chama fulani, Sasa hili ni tatizo kwani sote tunajenga nyumba moja yanini kugombea fito.

Kuhusu kuazisha shilika hili suala hatuna budi itabidi tuanzishe tu maana kuna ombwe hapo katikati ukiachana na vyama na hawa wanaharakati ambao wapo mmoja mmoja unaona kuna kitu kina miss ambacho kitatuunganisha wote kama taifa tukafocus/tukawa na shabaha moja pasipo kujali tofauti zetu.

Tunaweza kuthubutu kwa kuanza na resources tulizonazo kwasasa then tutaimalika taratibu taratibu, mfano Tunaweza tukaanza na movement kupitia mitandao (social media).
Hii ni kazi nzuri ya mabeberu wa Dunia hii ..Walijua haya ndiyo yatakuwa matokeo ndiyo sababu walilazimisha masharti ya IMF
 
Umeeleza kirefu sana
Usalama wowote wa nchi cha kwanza hakikisha wananchi wana chakula cha kula Tanzania usalama wa chakula ni mzuri na watu wana chakula hamna shida ya upatikanaji wa chakula .Watu asilimia kubwa wana uhakika wa chakula.Kama wapo wasio na uhakika ni wachache sana

Pili hakikisha asilimia kubwa ya wananchi wana ajira .Tanzania asilimia kubwa ya wananchi wana ajira.Asilimia 85 ya watanzania huishi vijijini wamejiajiri kwenye kilimo,ufugaji na uvuvi na mijini asilimia kubwa imeajiriwa serikalini au sekta binafsi viwandani,masokoni,biashara ndogo na kubwa za aina mbali .Wasio na ajira kabisa ni asilimia ndogo mno ya wakazi wa mijini

Tatu usalama wa nchi ni kuhakikisha asilimia kubwa wana makazi kwa kuweka sera rafiki za wao kupata makazi hili limewezekana kwa kuwa na sera nzuri za ardhi ambazo asilimia kubwa ya watanzania wana uwezo wa kumiliki mashamba,viwanja au nyumba

Hayo maeneo ukishayafikia una uhakika nchi kuwa salama

Hayo ndio mambo makubwa ya nchi kuwa salama na kuzalisha wazalendo
 
Alo walituweza walitukamatia pazuri nadhani tulikua na hali mbaya kiasi kwamba tulikua hatuna budi ni kukubali tu.

Lakini mambo mengine ni kutokuwajibika kwa mamlaka husika kuna viongozi hawatekelezi wajibu wao ipasavyo mfano mipango miji nashidwaga kuwaelewa.
Hii ni kazi nzuri ya mabeberu wa Dunia hii ..Walijua haya ndiyo yatakuwa matokeo ndiyo sababu walilazimisha masharti ya IMF
 
Umeeleza kirefu sana
Usalama wowote wa nchi cha kwanza hakikisha wananchi wana chakula cha kula Tanzania usalama wa chakula ni mzuri na watu wana chakula hamna shida ya upatikanaji wa chakula .Watu asilimia kubwa wana uhakika wa chakula.Kama wapo wasio na uhakika ni wachache sana

Pili hakikisha asilimia kubwa ya wananchi wana ajira .Tanzania asilimia kubwa ya wananchi wana ajira.Asilimia 85 ya watanzania huishi vijijini wamejiajiri kwenye kilimo,ufugaji na uvuvi na mijini asilimia kubwa imeajiriwa serikalini au sekta binafsi viwandani,masokoni,biashara ndogo na kubwa za aina mbali .Wasio na ajira kabisa ni asilimia ndogo mno ya wakazi wa mijini

Tatu usalama wa nchi ni kuhakikisha asilimia kubwa wana makazi kwa kuweka sera rafiki za wao kupata makazi hili limewezekana kwa kuwa na sera nzuri za ardhi ambazo asilimia kubwa ya watanzania wana uwezo wa kumiliki mashamba,viwanja au nyumba

Hayo maeneo ukishayafikia una uhakika nchi kuwa salama

Hayo ndio mambo makubwa ya nchi kuwa salama na kuzalusga wazalendo
Nimepata point mkuu shukran
 
Ongezea mambo mengine kama yafuatayo yanomfanya mtu kuwa mzalendo.

1. Kujitoa na kuwa tayari kufa kwa ajili ya taifa lako.
2. Kutunza siri za nchi na kuzilinda kwa gharama yoyote ile.
3. Kujiona na kujisikia weye ni sehemu ya taifa.
4. Kujivunia utaifa na kuwa tayari kupigia kifua utaifa huo.
5.Kujisifia utaifa wako na kuwa tayari kuutangaza utaifa huo popote pale.
6 Kuweka kumbukumbu na historia ya taifa hilo kwa ajili ya vizazi vijavyo.
7.Kulinda Mali na Rasilimali za nchi na mipaka yake yote.

Namba 1, 2 na 7 ni Usalama wa Taifa vikiwemo vyombo vyake vyote.

Namba 3-7 ni wananchi .
Sawa,
Well elaborated.
 
Viongozi kama Hayati JPM ni mfano tosha wa wazalendo wa Taifa hili.
1. Alikuwa tayari kujitoa sadaka kwa ajili ya nchi yake
2. Alipambana na upigaji serikalini kadri alivyoweza
3. Alipambana usiku na mchana ili nchi ipige hatua kimaendeleo n.k.

Ukiwa na kiongozi kama Hayati JPM, ni rahisi kuwa Mzalendo.

Lakini kwa hawa wengine, kila mmoja afanye tu kile kilicho sahihi machoni pake mwenyewe
 
Back
Top Bottom