Viongozi wafinyangwe kiusalama, uzalendo, na uadilifu kwa maendeleo endelevu ya Taifa

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
899
715
Vyombo vyetu vya Ulinzi,Usalama na Ujasusi vinafanya kazi kubwa sana toka tupate uhuru..Lakini pia bado tuna mianya mingi na mapungufu ambayo vinapaswa kumulika zaidi Kwa faida ya Taifa letu.

Kama ambavyo Sisi watu wadogo tumekuwa tukishauri juu ya maboresho,Uwekezaji,ufinyanzi kikatiba wa vyombo husika ili kuvifanya imara zaidi ktk kukabiliana na Threats (Internal &External).

Wanasiasa ktk taifa letu wana nguvu na mamlaka kubwa sana ktk kuamua mustakabari wa maendeleo -Kijamii,Kiuchumi,Kiutamaduni na kisayansi). Uwezo wa vyombo vya usalama unapaswa kuwa mpana zaidi ktk Kuhakikisha michakato ya kisiasa tokea grassroots level ina reflects maendeleo endelevu ya nchi Kwa miaka 50;100,150

Kwenye hili grooming,recruitment,Capacity building,Sensitizations na etc vyapaswa kufanya ktk mfumo kitita Kwa maslahi ya nchi na sio watu ama vikundi ama vyama vya siasa.

Kwa sasa Siasa Za nchi zinamirikiwa na wachache,Vikundi vya wachache,wenye nguvu ya fedha na ukwasi. Ukwasi wa kununua ama kuhonga waunga mkono (taasisi Za dini, Michezo, Sanaa, vikundi vya kiuchumi-Boda boda, Vijana, Nk).Mtu mmoja aweza amua nani awe na akawa Kwa kutegemea mamlaka yake Kwa wakati husika.

Wenye kiu ya madaraka makubwa ktk nchi japo hawana Sifa/uwezo,Dhima nyoofu,Uzalendo,Uadirifu stahiki,Maono,Hekima na busara lakini wanapambana sana kushika hatamu Kwa udi na uvumba. Jua liwake ama lizime..Wafe watu, Wapone..Kura halali ama haramu.

.Nadhani tunahitaji siasa safi. Kwa wakati sahihi na namna sahihi..Tunahitaji Siasa zenye uwezo wa kuitoa nchi kwenye Lindi la umaskini na udumavu wa kimaendeleo na sio mashindano ya kuiba,Ubadhirifu,Ufisadi..Mbali ya siasa safi tunahitaji wanasiasa wasafi/Wazalendo/Ufahamu/Elimu/Maarifa na wenye uwezo (Nia,matamanio, Ufahamu, Uthubutu, Utendaji, Elimu, Exposure)

Wahuni,Wezi,Mafisadi,Wezi,Wajasiliamali wa kisiasa,Warithi Uongozi..Na wote wanaodhani wana hati miriki ya uongozi wa taifa Wakae ama kuwekwa pembeni na mfumo wa kizalendo.

Ni Fahari kubwa na zawadi kubwa Kwa vizazi vya sasa na baadae Kwa vyombo vyetu kutekeleza wajibu stahiki wenye kutukuka Kwa kuhakikisha nchi inatoka kwenye dimbwi la umaskini, Ujinga, Ufukara na umaskini uliokithiri licha ya jitihada nyingi tokea uhuru.

Kwa nini tunakwama kuwa na Wakulima wa kisasa wanaoweza kuzarisha mazao mtambuka kuepukana na utegemezi wa kuagiza -Sukari, ngano,M afuta, etc?

Tunakwama wapi kujenga viwanda zaidi vya bidhaa muhimu tunazotumia kila kukicha. Nguo,viatu, Ndala, chupi, tooth pick, masufuria, magari, pikipiki, baiskeli, vipuri, Madawa, etc?

Tunakwama wapi kujenga smelters Za kuchakata madini yetu?

Tunakwama wapi kuwekeza ktk viwanda vingi zaidi vya kuchakata mazao ya kilimo,misitu?

Tunakwama wapi kuanzisha upya viwanda vya zana Za kilimo,Uvuvi na ufugaji wa kisasa..?

ULINZI NA USALAMA KWA MAENDELEO YA TAIFA
 
Nnchi yetu, iko imara na madhubuti sana katika nyanja za ulinzi na usalama wa mipaka, raia na mali zao 🐒

dosari na kasoro chachechache za kimaadili na kiutendaji ni jambo la kawaida na ni vigumu kuepukana na kila kitu kisichostahili kulingana na malezi tofauti tangu kuzaliwa kwetu 🐒

Hata hivyo, suala la kujikwamua katika lindi la umaskini, ni jukumu binafsi la kila Mtanzania kuongeza juhudi katika kufanya kazi. Serikali ina jukumu la kujenga mazingira wezeshi na kumpa fursa kila mwanainchi kuamua kwa uhuru cha kufanya, kama ni, kilimo, biashara, uvuvi, ufugaji, usafirishaji , ujenzi n.k. mazingira ni mazuri sana na salama sana, ni uamuzi wako tu 🐒

suala la kujenga na kufufua viwanda ili kuongeza ajira, huduma na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa matumizi mbalimbali, bado mazingira ni mazuri sana kwa mtu binafsi, mashirika ya kitaifa na kimataifa, Taasisi au kikundi cha wafanyibiashara, kuanzisha viwanda. Fursa ya uwekezaji huu iko wazi na kila mwenye uwezo anaruhusiwa kufungua kiwanda. Suala la uhakika wa usalama na mazingira wezeshi linabaki chini ya serikali madhubuti iliyopo 🐒

kuhusu kilimo, kwasabb ni sekta inayovutia ajira nyingi zaidi kwa sasa, ni dhahiri kama inchi, katika muda usio kua mrefu mapinduzi katika sekta hii yatachochea uzalishaji wa ajira nyingi zaidi na ujenzi wa viwanda vingi zaidi, kwasabb upatikanaji wa malighafi utakuni ni rahisi, wa uhakika na wa kutosha 🐒

Mungu Ibariki Tanzania 🐒
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom