Uwongo umeniponza

Kuvunja vitu ni kuppenda, wivu au hasira? Sioni uhusinao kati ya uharibifu wa mali na kupenda. watu wa hivyo ni wabaya sana kwani jua wazi maisha ya ndoa ugomvi wa hapa na pale ni part na parcel. Sasa atakuwa anakutia hasara kila siku. mkigombana anavunja vioo vya gari. Kesho anavunja TV. Mtaendelea kweli. I hate that. My colleague had a similar problem. Mkewe wivu mbaya. Yaani kila siku wanaanza kununua vitu upya ndani. Mara utasikia wife kachoma moto nguo. Mara wife kavunja vioo vya gari. Taabu kweli kweli.
Lakini dada NK wanawake wa hivo ni waaminifu sana kwenye ndoa vitu nitanunua tu lakini hata nikisafiri mwaka na amani, halafu si mpaka nifanye kosa kubwa ndio anavunja vitu ?
 
hiyo ni noma mtu wangu, umeona faida ya kutokuwa mkweli kwa mwenzio sasa kazi kwako, kama mdomo pazuri mpe maneno matamu tu na ahadi nyingi na atatulia tu, na kama ulikuwa unamfikisha mahali pake aaaaaaaah atoki.
 
Nina girlfriend wangu ambaye amekuwa ni mchumba wangu ila huenda kuanzia sasa uchumba umeisha baada ya kugundua kuwa nimemdanganya.
Nilipokuwa chuo nilizaa na wanawake wawili tofauti si unajua tena mambo ya ushamba.
Baada ya kupata kazi nikapata mchumba ambaye ndiye huyu sasa. Tuna mwaka mmoja na nusu na kwa kipindi hicho chote sikuwahi kumweleza kuwa nina watoto wawili. Yeye alikuwa anajua kuwa ninao wawili. Moto wake si mdogo, kavunja vyombo vyote kabatini, kavunja dressing table, kavunja coffee table yaani ni kasheshe, binti kapandisha majini ya kichaga. Najaribu kumtuliza hatulii, naombeni mnisaidieni kwani nampenda sana na ninamuhitaji maishani na sikupanga kumuumiza moyo
kumbe kuna majin ya kichaga loh!
 
Kagundua mwenyewe

yani mi nashangaa kwanini wanaume wengi hawabadiliki kwanini usiwe muwazi tangu mwanzo kama akiridhika ok bt if not aangalie ustaarab kwngine! We unafkir kulea wtt2 wa mama tofauti tofaut mchezo, hapo bado hajaanza kua na wakwake. Bora kama mama zao wanaj22mua bt kama ni golikipa je? Mh!
 
........uwongo mbaya na kweli ulikosea, hivi kuna ubaya gani hadi anaamua kuvunja vitu? Kwani kasikia upendo wako kwake umeisha!! Hebu mwambie kwamba unampenda sana tu japo una watoto nje..........omba msamaha kama ni mwelewa atakuelewa, kwanza watoto ni baraka inabidi akusamehe tu na maisha yaendelee.
 
uwoga wa kuwa mkweli utafanya watoto wako waje wateswe hapo baadae.....

mwambie huyo msichana wako advantage ya wewe kuzaa kabla ni kuwa hutamsumbua sana azae..au azae mtoto wa jinsia ipi?
atakuwa free zaidi hata kutokuzaa....
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

jamani kweli kwasasa kuna mtu asiyependa mtt wa kuzaa mwenyewe?
 
Pole sana gwakumyitu.
Tafuta watu anaowaamini wakuombee msamaha, akikataa anza upya kubembeleza we mwenyewe, si mbaya ukadondosha machozi mbele yake.
 
mi nadhan huyo dada anakupenda mno dat y aliumia sana alipogundua umemcheat. Kaa chini jipange hasira zake zikiisha atakuelewa tu. Bt its better wtt hao uwatunze mwenyewe na mkeo uwafundishe maadili mema mapema kabla hawajapollutiwa na mama zao, c unajua watoto wa kambo lawama!
 
Pole sana. Lkn kilichojificha ndani ya kuvunja vitu ni kasoro kubwa na kielelezo cha ROHO MBAYA. Yaani Tukose wote na hao watoto wasifaidi. Hakuna sababu ya kuuma maneno, huyo mtu hawezi kuwapokea hao watoto, na wakirudi kwa baba yao ni mateso mtindo mmoja. Kadri mnapozungumza kupatana, suala la kuvunja vyombo liwe sehemu ya mjadala, msiliweke kando eti ni HASIRA.
 
Nina girlfriend wangu ambaye amekuwa ni mchumba wangu ila huenda kuanzia sasa uchumba umeisha baada ya kugundua kuwa nimemdanganya.
Nilipokuwa chuo nilizaa na wanawake wawili tofauti si unajua tena mambo ya ushamba.
Baada ya kupata kazi nikapata mchumba ambaye ndiye huyu sasa. Tuna mwaka mmoja na nusu na kwa kipindi hicho chote sikuwahi kumweleza kuwa nina watoto wawili. Yeye alikuwa anajua kuwa ninao wawili. Moto wake si mdogo, kavunja vyombo vyote kabatini, kavunja dressing table, kavunja coffee table yaani ni kasheshe, binti kapandisha majini ya kichaga. Najaribu kumtuliza hatulii, naombeni mnisaidieni kwani nampenda sana na ninamuhitaji maishani na sikupanga kumuumiza moyo

Pole sana Mikela na mkasa ulokupata. Dada bado anahasira ungempa nafasi ya kupoa, akisha poa kili ukweli kwake kua ulikua unaogopa kumkwaza lakini hukuwa na nia mbaya.

Huyo dada amechanganikiwa cause nafikiri anakupenda sana, hapo mahala kafika na hakutegemea kua kuna wakati inaweza fika mkapata tatizo la kusababisha muachane. kilichomchanganya zaidi kichwani kwake sio kusikia kua una mtoto mwingine... bali kwamba wewe si mwaminifu kabisa na kwamba unaweza mficha kitu kikubwa kama hicho! maswali anayojiuliza ni kua atakuamini vipi tena? una siri gani nyingine hujamwambia? watoto ni hao wawili tu? ungemwambia wewe mwenyewe ingekua kesi nafuu kidogo - lakini issue kagundua mwenyewe. Na usipoangalia huyo dada unampoteza hata kama bado anakupenda; Trust ni muhimu sana katika mahusiano...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom