Uwongo umeniponza

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,645
155,012
Nina girlfriend wangu ambaye amekuwa ni mchumba wangu ila huenda kuanzia sasa uchumba umeisha baada ya kugundua kuwa nimemdanganya.
Nilipokuwa chuo nilizaa na wanawake wawili tofauti si unajua tena mambo ya ushamba.
Baada ya kupata kazi nikapata mchumba ambaye ndiye huyu sasa. Tuna mwaka mmoja na nusu na kwa kipindi hicho chote sikuwahi kumweleza kuwa nina watoto wawili. Yeye alikuwa anajua kuwa ninao wawili. Moto wake si mdogo, kavunja vyombo vyote kabatini, kavunja dressing table, kavunja coffee table yaani ni kasheshe, binti kapandisha majini ya kichaga. Najaribu kumtuliza hatulii, naombeni mnisaidieni kwani nampenda sana na ninamuhitaji maishani na sikupanga kumuumiza moyo
 
Dah.. pole saana!... kuwa muwazi zaidi kwa atakaye fuataia.... pia jaribu mbembeleza atatulia
 
pole sana mzee, hapo pazito, ushauri ni kwamba mtafute mtu ambaye ni trustworthy na ambaye gf wako anamweshimu na kumuamini, ajitaidi kumtuliza hasira. N.B tumia njia hii baada ya kuona kuwa njia zote ulizotumia zimeshindwa kufanikiwa kabisa, kwanini? sababu kuu ni kuwa mambo ya mapenzi mara nyingi wahusika ndio uweza kuyamaliza matatizo wenyewe ndani kwa ndani.
 
Ishu yako imenikumbusha mbali.
Hao watoto amewakuta asipanic sana. Wangekuwa wamezaliwa wakati mshaanza mahusiano ingekuwa mbaya zaidi.
Mwambie ulimficha ukihofu kuwa atakuacha na wewe unampenda, ukweli umejulikana hujui ufanyaje kwahyo mwamuzi ni yeye ila unajutia kwa ulichofanya.
Uwe mpole wakati unaongea.
 
Nina girlfriend wangu ambaye amekuwa ni mchumba wangu ila huenda kuanzia sasa uchumba umeisha baada ya kugundua kuwa nimemdanganya.
Nilipokuwa chuo nilizaa na wanawake wawili tofauti si unajua tena mambo ya ushamba.
Baada ya kupata kazi nikapata mchumba ambaye ndiye huyu sasa. Tuna mwaka mmoja na nusu na kwa kipindi hicho chote sikuwahi kumweleza kuwa nina watoto wawili. Yeye alikuwa anajua kuwa ninao wawili. Moto wake si mdogo, kavunja vyombo vyote kabatini, kavunja dressing table, kavunja coffee table yaani ni kasheshe, binti kapandisha majini ya kichaga. Najaribu kumtuliza hatulii, naombeni mnisaidieni kwani nampenda sana na ninamuhitaji maishani na sikupanga kumuumiza moyo

Hebu fafanua hapo kwenye rangi Mkuu
 
Ishu yako imenikumbusha mbali.
Hao watoto amewakuta asipanic sana. Wangekuwa wamezaliwa wakati mshaanza mahusiano ingekuwa mbaya zaidi.
Mwambie ulimficha ukihofu kuwa atakuacha na wewe unampenda, ukweli umejulikana hujui ufanyaje kwahyo mwamuzi ni yeye ila unajutia kwa ulichofanya.
Uwe mpole wakati unaongea.

Bonge la mbinu, asante sana.
 
pole sana mzee, hapo pazito, ushauri ni kwamba mtafute mtu ambaye ni trustworthy na ambaye gf wako anamweshimu na kumuamini, ajitaidi kumtuliza hasira. N.B tumia njia hii baada ya kuona kuwa njia zote ulizotumia zimeshindwa kufanikiwa kabisa, kwanini? sababu kuu ni kuwa mambo ya mapenzi mara nyingi wahusika ndio uweza kuyamaliza matatizo wenyewe ndani kwa ndani.

asante kaka ingekuwepo batani ya thanks ningekugongea
 
Kazi kweli kweli. Watoto wawili ni wengi kweli ukizingatia familia za kisasa wanahitaji watoto wawili hao hao basi. Sasa umemchanganya maana tayari una wawili. Maanake yeye akiongeza wawili maisha yatakuwa magumu! Ila nachomshangaa mdada kwa nini anavunja vitu ndani? Mimi nami ningevunja uchumba ila vitu vyako wala nisingeharibu. Nadhani anachosikitika ni aibu kwa kuwa labda ushatoa mahali atapata wakati mgumu kueleza ndugu na jamaa what happened. Watoto si wabaya kwa kuwa uliwazaa kabla ya kumfahamu yeye na ni obvious watu wanakuwa na wapenzi kabla ya kuoa ila wengi wana bahati hawawapi wasichana ujauzito. Issue ni kuwa umeharibu mipango yake ya maisha kwani nadhani atakuwa alishajipangia kuzaa watoto wawili na labda mshawahi kuzungumzia mnahitaji watoto wangapi kumbe wewe tayari unao wawili.

Mimi nina mfano wa jamaa alioa akiwa ameshazaa mtoto wa kiume. yeye hakuficha ila wife aisee hana amani kabisa kwa kuwa yeye ana girls tu hivyo anawasiwasi jamaa aki dead mali atamwandikia mtoto wake wa nje ya ndoa. Kaazi kweli kweli.
 
bwana weee yeye alijua kuwa nina mtoto mmoja kumbe ninao wawili

Sasa nimekuelewa. Akishatulia halafu mkae chini umuombe samahani kwa kumdanganya kisha umfahamishe kwamba unampenda sana na bado unapendelea kuendelea kuwa naye ili mkijaaliwa muweze kufunga pingu za maisha.
 
bwana weee yeye alijua kuwa nina mtoto mmoja kumbe ninao wawili

haaa haaa! Hee!
Ninacheka ati kama ni mazuri nacheka hatua alochukua ya kuanza kuvunja samani za ndani aah! Anatumia mfumo wa kizamani sana ule wa 'Machines vandalizing' enzi zile za workers movt. Luddism kama sijakosea.
Si angelikuadhibu muhusika hapo hapo ili amalize hasira zake.
Pole sana ndugu yangu tupo wengi wenye 'misala' ya aina yako na wengine ishakwisha na tunaugulia, japo yupo jamaa yangu hapo (namhifadhi) yeye anao kama wako huo na mbaya zaidi ye alipiga hatrick nje ya uwanja na kibaya zaidi ameongeza kitu kingine wakati yupo uwanjani (offside).
Najua naye ipo siku atakuja kuomba ushauri juu ya hiyo mimba ya nje baada ya kuoa afanyaje.
Pole ndugu yangu, japo kama walivyoshauri jamaa hapa ni kumtafuta mtu wanaeheshmiana na mkeo ili aweze kumtuliza.
Usijali ndugu yangu ndio matokeo ya kupanda mbegu ya Magugu.
Jipe moyo yatakwisha na kwa niaba ya wanaJf tuko pamoja nawe ktk kipindi hiki cha sekeseke.
 
wazimu huo wa kula ugali kwa ndimu,kwani hao watoto ni wadogo kuliko umri wa uhusiano wenu au.
 
Kagundua mwenyewe

kwa siku chache zijazo kasheshe utaona tu..
lakini kama kweli anakupenda na kuanza ku build
ile trust tena hataenda popote..
ila cha moto utakiona sababu kagungua mwenyewe..

ila kwanini we hukumwambia ukweli
na ulikuwa unaelewa kabisa hili ni bomu lililo expire??
 
Ulipofikia kanivunjia vitu nikahisi tu wa kili mi 1 alivunja kila kitu mpaka tv,deck hadi vitanda na alitaka kuchoma nyumba tena ya kupanga majirani wakamwahi, wanapenda jumla na hawapendi uongo,pole sana kuwa mpole atakusamehe.
 
Kuvunja vitu ni kuppenda, wivu au hasira? Sioni uhusinao kati ya uharibifu wa mali na kupenda. watu wa hivyo ni wabaya sana kwani jua wazi maisha ya ndoa ugomvi wa hapa na pale ni part na parcel. Sasa atakuwa anakutia hasara kila siku. mkigombana anavunja vioo vya gari. Kesho anavunja TV. Mtaendelea kweli. I hate that. My colleague had a similar problem. Mkewe wivu mbaya. Yaani kila siku wanaanza kununua vitu upya ndani. Mara utasikia wife kachoma moto nguo. Mara wife kavunja vioo vya gari. Taabu kweli kweli.

Ulipofikia kanivunjia vitu nikahisi tu wa kili mi 1 alivunja kila kitu mpaka tv,deck hadi vitanda na alitaka kuchoma nyumba tena ya kupanga majirani wakamwahi, wanapenda jumla na hawapendi uongo,pole sana kuwa mpole atakusamehe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom