Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
- Thread starter
- #21
Mwanakijiji,
..hakukuwa na ulazima kwa Sophia Simba kutumia redio yako kuwakandia wagombea wenzake.
that is the problem.. hakuwakandia wagombea wenzake!
..halafu mbona uwezo wake wa kujieleza na kuchambua hoja unatofautiana sana na kiwango cha elimu na uzoefu anaojisifia kuwa nao, pamoja na taaluma yake ya uanasheria?
Kila mtu ana kipaji chake siyo wote wanaweza kujenga hoja hivi au vile. Nakuambia ukipata nafasi ya kuzungumza na watu mbalimbali ambao unaweza kusema ni wasomi katika ujengaji wao wa hoja inasikitisha. Siyo wao tu hata hapa JF kuna watu wanajenga hoja za ajabu kweli, the reasoning is flawed soo are the conclusions.. lakini wenyewe wanaamini kuwa ni wasomi!
Nimegundua kuwa nasikiliza zaidi mtu anachomaanisha kuliko ufundi wake wa kujenga hoja kwani ni wachache sana wanaweza kujenga hoja kisomi katika mazungumzo ya kawaida!
..she did not come across kama msomi. pia nina mashaka kwa umahiri ule ataweza kuvutia wasomi wowote wa maana huko UWT.
Mtu anaweza kuzungumza kwa namna yeyote kutegemea na mazungumzo. Mama Sophia hakuwa anatoa lecture au mhadhara wa kisomi, yalikuwa ni mazungumzo yenye mlengo wa kisiasa tu. Inaonekana amewavutia watu wa kutosha hadi kupata kura za kumfanya awe Mwenyekiti.
..wingu la kampeni za rushwa na ufisadi ktk uchaguzi wa UWT ni zito mno.
hilo yeye mwenyewe kalikiri.. (ukimsikiliza vizuri)
..ingefaa kama ungemuuliza Sophia Simba ametumia fedha kiasi gani, na amezitoa wapi.
Hiyo ya "ninge" ni 20/20. I agree though.
NB:
..hawa kina mama walipaswa kuwa na midahalo kadhaa mbele ya wapiga kura wao.
Hiyo ndiyo point yake kuwa hawakupimwa mbele ya wapiga kura zaidi kuandikwa kwenye udaku tu na malumbano yao. Kwanini chombo cha habari chochote hakikudhamini mdahalo fulani? I'm tempted now to host mdahalo wa wagombea wa Mbeya Vijijini!!
..gazeti la raia mwema linaripoti kwamba wagombea walijieleza mbele ya wapiga kura kwa dakika kama tano kila mmoja na hakuna maswali yoyote waliyoulizwa. baada ya hapo wajumbe walipiga kura.
Well, sasa watu hawakuwauliza maswali yoyote walitarajia nini? Labda na wenyewe walikuwa na ugumu wa kujenga hoja kisomi!
..pia kuna habari kwamba fedha zilikuwa zikigawiwa kwa wajumbe waliokuwa wakienda msalani.
Hili siku hizi kuna watu wamelikubali, lilikuwepo kwenye UVCCM ambapo hadi mkuu wa wilaya moja alikuwa anatumika na mtoto wa kigogo mmoja! Nani atamfunga paka kengele!?