Halafu kwani usomi ni nini? Mtu unaweza ukawa msomi bila kujua kiingereza? Hapa nikiwa na maana msomi unayejua lugha moja tu, Kiswahili. Au usomi ni lazima mtu uwe unajua kiingereza tena kile kama cha Pundit....heheheh.....
Usomi siyo kujua kiingereza.Ingawa kiingereza ni lugha rasmi ya pili Tanzania lakini bado wabongo wengi tuna fikra za kitumwa kwamba anayejua kiingereza ndiye msomi na ndiyo maana hata na wao viongozi wanaona ujiko kuchomekea kiingereza kwenye mazungumzo ili waonekane wasomi na wengi wanaofanya hivyo usomi wao hua una mashaka.Ndiyo maana msomi aliyeelimika kama Dr.Migiro huwezi mkuta akafanya huu upuuzi.