Utetezi wangu wa Mhe. Sophia Simba dhidi ya Ukosoaji usio wa haki

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Nikiri ya kwamba nimesikitishwa na kushangazwa sana na baadhi ya ukosoaji wa Mhe. Simba kufuatia mahojiano yangu naye siku chache zilizopita. Kilichonisikitisha zaidi ni jinsi gani baadhi yetu tuna angalia vitu ambavyo si vya msingi na kuviacha vya msingi; kilichonishangaza zaidi ni jinsi gani wengine wamekuwa wa kali kiasi cha wao wenyewe kuwa kile wanachomtuhumu Mhe. Simba.. arrogance!

Katika mahojiano yangu na watu mbalimbali (kama Dr. Migiro, Dr. Salim, na wengineo) sijawahi kujaribu kumtetea mtu yeyote kwa majibu yake. Hata hivyo katika hili la Mhe. Simba nimeona kilele cha kebehi na kina cha parapanda ya unafiki wa uongo. Wengi wamemhukumu Mhe. Sofia kwa ukali ambao haukustahili na umeenda zaidi ya ukosoaji wa kumjenga mtu!

Kwa hawa nina ujumbe ufuatao: Sikiliza!

BONYEZA HAPA KUSIKILIZA
 
Mzee mwenzangu Mwanakijiji you really have a point........however, sidhani kama waliomshambulia Simba waliangalia Jinsia yake kama ulivyosema ktk utetezi wako........kama wako waliomshambulia kutokana na jinsia yake hao wamefilisika akili kabisa......

........Otherwise tuko pamoja ktk utetezi mkuu
 
Du! Mwanakijiji umekasirika mzee, punguza Jaziba...

siyo kukasirika inaitwa passion. Najua watu wamezoea lugha ya kubembelezana na kuoneana haya.. kuna wakati wake siyo huu. Laiti tungekuwa na watu wenye passion kwenye mambo wanayoyafanya to the point ya kuonekana wamechukizwa.
 
dakika 15 si nyingi...

Sawa baba;

Ila umezunguka-zunguka weee, wakati ujumbe wako ulikua straight, true and very important kwetu watanzania (wote!).... They always say, "be short, clear and straight to the point"
 
Last edited:
sijahoji uhuru wa watu kutoa maoni, nimeyahoji maoni yenyewe na kuyaonesha kuwa hayana msingi!

Kumbuka na mtu katoa maoni kutokana na mtazamo wake anavyo ona yeye.
Maoni siku zote hayakoselewi ila yanapembuliwa unachagua pumba na mchele.
 
Kumbuka na mtu katoa maoni kutokana na mtazamo wake anavyo ona yeye.
Maoni siku zote hayakoselewi ila yanapembuliwa unachagua pumba na mchele.

hapana.. maoni yanabakia ya binafsi mawazoni; yakitolewa basi yana haki ya kuchambuliwa kukosolewa, kusahihishwa na wakati mwingine kuonesha kuwa hayana msingi. Lakini pia maoni yanaweza kuungwa mkono kama hoja zake zinakubalika.

Na unaposema kuwa yanapembuliwa "unachagua pumba na mchele" utaweza vipi bila kufanya ukosoaji. NI ukosoaji unaweza kukufanya uone zipi ni pumba na upi mchele.
 
Unajua Mkjj kinachoonekana hapa ni kwamba huyu mama ameonesha kiwango kilicho chini zaidi hata ya "Sarah Palin" yaani mimi ninachokiona hapa si jinsia bali ni kumkabidhi mtu aliye na uwezo mdogo wa uchambuzi majukumu makubwa kama ya kuisimamia TAKUKURU na UWT(Usalama).

Mimi ninachokiona hapa Mkjj ni kwa wewe kusafisha njia ya kupata nafasi nyingi zaidi za kuwahoji hawa viongozi vinginevyo watakuogopa wewe, Ila kwa mtazamo huo tupo ukurasa mmoja lazima uoneshe balancing, kwamba wewe upo fair.

Nina kuhakikishia usingefanya hivi unavyofanya mama Simba asingekubali tena kuongea na wewe in the future kwa kuogopa kuanikwa uwelewa wake mdogo na watu. Na kwa style hiyo utawapata wengi sana wa kuwahoji, maana watajisikia wapo katika mikono salama. "kudos Mkjj"
 
siyo kukasirika inaitwa passion. Najua watu wamezoea lugha ya kubembelezana na kuoneana haya.. kuna wakati wake siyo huu. Laiti tungekuwa na watu wenye passion kwenye mambo wanayoyafanya to the point ya kuonekana wamechukizwa.[/quote]

Nimejaribu mimi kuchokonoa passion za watu na Miafrika Ndivyo Tulivyo matokeo yake nikawa public enemy number one! Lol......
 
no comment..
 
inabidi uwe mkali kidogo halafu tell it to their/our face without flinching!
 
Mwanakijiji,

..hakukuwa na ulazima kwa Sophia Simba kutumia redio yako kuwakandia wagombea wenzake.

..halafu mbona uwezo wake wa kujieleza na kuchambua hoja unatofautiana sana na kiwango cha elimu na uzoefu anaojisifia kuwa nao, pamoja na taaluma yake ya uanasheria?

..she did not come across kama msomi. pia nina mashaka kwa umahiri ule ataweza kuvutia wasomi wowote wa maana huko UWT.

..wingu la kampeni za rushwa na ufisadi ktk uchaguzi wa UWT ni zito mno.

..ingefaa kama ungemuuliza Sophia Simba ametumia fedha kiasi gani, na amezitoa wapi.

NB:

..hawa kina mama walipaswa kuwa na midahalo kadhaa mbele ya wapiga kura wao.

..gazeti la raia mwema linaripoti kwamba wagombea walijieleza mbele ya wapiga kura kwa dakika kama tano kila mmoja na hakuna maswali yoyote waliyoulizwa. baada ya hapo wajumbe walipiga kura.

..pia kuna habari kwamba fedha zilikuwa zikigawiwa kwa wajumbe waliokuwa wakienda msalani.
 
Back
Top Bottom