Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,850
- 12,086
Twaweza, JamiiForums, The Union of Tanzania Press Clubs (UTPC), Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) na Media Institute of Southern Africa Tanzania Chapter (MISATan) kwa pamoja wanatarajiwa kuzindua Ripoti ya Sauti za Waaandishi, leo Februari 16, 2024.
Ripoti hiyo inatarajiwa kujadili Uzoefu na Maoni ya Waandishi wa Habari nchini #Tanzania kuhusu Sekta ya Vyombo vya Habari, lengo likiwa ni kutoa taarifa (data) zilizopatikana kutokana na utafiti uliyofanyika kati ya Septemba na Novemba 2023.
Sauti za Wananchi ni utafiti wa Simu za Mkononi wa kwanza Barani Afrika unaotoa data za Kisayansi kuhusu maoni na uzoefu wa raia kuhusu masuala mbalimbali ya Utawala.
Waandishi wa habari hubeba jukumu kubwa katika jamii. Husaidia wananchi kupata taarifa za matukio muhimu, hufanya kazi kama mlezi kuhakikisha wale wenye nguvu wanawajibishwa Pamoja na kutoa nafasi kwa vyombo vyao vya Habari kurahisisha mazungumzo ya kitaifa kwa kutoa jukwaa (na kipaza sauti) kwa raia kusikilizwa.
Hivyo, uzoefu na maoni ya waandishi wa habari ni muhimu sana. Je, waandishi wa habari wana aina gani ya hali ya ajira? Je, wanajisikia wanaweza kuishi vizuri, na je, wameridhika na kazi zao? Mara ngapi wanakabiliwa na vitisho na unyanyasaji kama matokeo ya kazi yao, na kutoka kwa nani? Wanahisi vipi kuhusu uhuru wa vyombo vya habari kwa kanuni, na kwa vitendo? Na ni matarajio gani wanayo kwa mustakabali wa taaluma yao nchini Tanzania?
Muhtasari huu unawasilisha matokeo ya utafiti wa waandishi wa habari, wahariri na bloga 1,202 wanaofanya kazi nchini Tanzania. Kikundi hiki kilianzishwa kutoka kwenye maktaba za wanachama wa vyama mbalimbali vya vyombo vya habari, hasa Chama cha Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), pamoja na Chama cha Wanawake wa Vyombo vya Habari Tanzania (TAMWA), Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika Tanzania (MISA-Tan), JamiiForums na Baraza la Wahariri Tanzania (TEF). Mahojiano yalifanyika kwa simu kati ya Septemba 23 na Novemba 7, 2023.
Muhtasari wa matokeo muhimu:
- Wengi wa waandishi wa habari hawana ajira za kudumu
- Wengi wa waandishi wa habari wanasema ni vigumu kuishi vizuri kutokana na uandishi wa habari
- Wengi wa waandishi wa habari wameridhika na kazi yao ya sasa, ingawa wengi wao hawatopenda waatoto wao kujihusisha na kazi hiyo.
- Waandishi wa habari wa kike wanahisi hawatendewi haki ikilinganishwa na wenzao wa kiume
- Nusu ya waandishi wa habari wamewahi kutishwa, kuteswa au kushambuliwa wakati fulani
- Waandishi wa habari wanawatuhumu maafisa wa serikali kama chanzo kikuu cha vitisho kwa kazi yao
- Waandishi wa habari wanakiri umuhimu wa kuchunguza ukweli wa mambo kabla ya kuripoti, lakini kwenye baadhi ya mambo huwa hawafanyi hivyo
- Waandishi wa habari wanatambua sana ufisadi ndani ya vyombo vya habari
- Waandishi wa habari wanakubaliana kwa kanuni kwamba vyombo vya habari vinapaswa kuwa huru kutoka udhibiti wa serikali, lakini wanakubali mipaka katika hali maalumu
- Wengi wa waandishi wa habari wanahisi kuwa vyombo vya habari nchini Tanzania havina uhuru mwingi wa kufanya kazi kwa uhuru
- Waandishi wa habari wanachukulia baadhi ya mada kuwa hazipaswi kujadiliwa
- Waandishi wa habari wanachukulia changamoto za kiuchumi kuwa kizuizi kikubwa kwa uhuru wa vyombo vya habari
- Waandishi wa habari nchini Tanzania wanatarajia mabadiliko mengi katika miaka 5-10 ijayo, lakini kwa ujumla wanatazamia madadiliko hayo kwa matumaini
- Wengi wa waandishi wa habari wanategemea jukumu la waandishi wa habari kubadilika, lakini si kupungua.
Michango ya Washiriki kwenye Mada
Aidan Eyakuze (Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza)
- Sheria ziwalinde wanahabari na sio kuwatisha ili wasiibue ukweli. Nafasi ya Waandishi wa Habari katika jamii ni muhimu, sisi sote tunapaswa kufanya kila tuwezalo kuwalinda na kuwastawisha
CAG Mtaafu, Ludovick Utouh
- Mzingira duni ya Uchumi ni moja ya sababu ya mazingira ya Rushwa kuendelea katika Tasnia ya Uandishi wa Habari
- Asisitiza Waandishi wa Habari kuwa na uelewa wa masuala ya Sheria za Ajira kwa kuwa ajira zote zipo chini ya Muongozo wa Sheria za Nchi ili kuweza kupata haki wanazostahili. Amesema, "Nawasikitikia Wanahabari ambao hawapo kwenye Mikataba ya Ajira kwa kuwa hii inawafanya kuwa 'vulnerable' kwa Waajiri wao".