Waandishi wa Habari Simiyu watangaza kutofanya kazi na DC Bariadi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Tamko,
Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) imesikitishwa na kuuzunishwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani humo, Simon Simalenga cha kuwafukuza kwa dhihaka kwenye kikao cha Ushauri cha Wilaya (District Consultative Council -DCC), waandishi wa habari saba wa vyombo mbalimbali vya habari waliokwenda kuchukuwa taarifa kwenye kikao hicho, kilichofanyika Februari 19,2024, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Waandishi hao wa habari ambao wamefikisha taarifa rasmi kwa uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari simiyu (Simiyu Press Club) kulalamikia kitendo hicho, wamesema kitendo alichofanya mkuu huyo wa wilaya si tu kimewafedhehesha waandishi wa habari pamoja na tasnia ya habari, bali kinakiuka Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayohimiza uhuru wa mtu kutoa na kupata taarifa.

Halikadhalika, kitendo hicho kilichofanywa na Mkuu Wilaya Bw. Simalenga kuwafukuza waandishi wa habari tena kwa lugha isiyokuwa na staha, kinakinzana na sheria ya haki ya kupata taarifa ya mwaka 2016.

DC Simalenga alinukuliwa akisema: “MMEKUJA KUFANYA NINI HAPA, NILIWAAMBIA MSIALIKE WAANDISHI WA HABARI, NANI ALIALIKA TENA? WAANDISHI WA HABARI TOKENI NJE NA MILANGO YA UKUMBI IFUNGWE," mwisho wa kunukuhu.

Rekodi zinaonesha kuwa, hii siyo mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kufanya vitendo hivyo, ambapo mara ya kwanza aliwatolea maneno ya kudhalilisha viongozi wa SMPC, ambao ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wetu.

Kutokana na hali hiyo, Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) kwanza inatangaza kulaani kitendo cha udhalilishaji kilichofanywa na DC Simalenga kwa waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu.

Pili, Uongozi wa SMPC na waandishi wake inatangaza rasmi kuanzia leo 20 Februari,2024,hautafanyakazi na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Peter Simalenga.

Tatu, tunaiomba Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoa tamko juu ya tukio hilo.

Hivyo basi, tunawaomba viongozi mbalimbali na wananchi ndani ya Mkoa wa Simiyu, kuwaheshimu waandishi wa habari pale wanapotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, na kuepuka kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji, ubaguzi, udhalilishaji na ukikwaji wa sheria.

Imetolewa na Uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC).

20 FEBRUARI,2024.
 
Sasa nyie waandishi wa Bariadi mtaripoti nini Cha maana kwa wananchi kama hamtafanya kazi na huyo DC?.Au ndiyo tusubiri habari za Gamboshi?
 
Vitu vingin sio vya kupublicize ndo mana akawaondoa
Angetumia lugha ya staha mzee mwenzangu ,
Alafu nikueleze kitu waandishi wa habari wakitaka wakufanye malaika unakua malaika ,wakitaka uwe shetani unakua jini alilotupiwa mayele kabisaaa🤣
 
Asisahau kama hao waandishi wa habari wanaweza waka sababisha akakosa huo ukuu wa wilaya kwa kutoa taarifa yake moja tuu ya hovyo, wakiamua uishi kama shetani wanaweza kabisa
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Tamko,
Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) imesikitishwa na kuuzunishwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani humo, Simon Simalenga cha kuwafukuza kwa dhihaka kwenye kikao cha Ushauri cha Wilaya (District Consultative Council -DCC), waandishi wa habari saba wa vyombo mbalimbali vya habari waliokwenda kuchukuwa taarifa kwenye kikao hicho, kilichofanyika Februari 19,2024, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Waandishi hao wa habari ambao wamefikisha taarifa rasmi kwa uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari simiyu (Simiyu Press Club) kulalamikia kitendo hicho, wamesema kitendo alichofanya mkuu huyo wa wilaya si tu kimewafedhehesha waandishi wa habari pamoja na tasnia ya habari, bali kinakiuka Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayohimiza uhuru wa mtu kutoa na kupata taarifa.

Halikadhalika, kitendo hicho kilichofanywa na Mkuu Wilaya Bw. Simalenga kuwafukuza waandishi wa habari tena kwa lugha isiyokuwa na staha, kinakinzana na sheria ya haki ya kupata taarifa ya mwaka 2016.

DC Simalenga alinukuliwa akisema: “MMEKUJA KUFANYA NINI HAPA, NILIWAAMBIA MSIALIKE WAANDISHI WA HABARI, NANI ALIALIKA TENA? WAANDISHI WA HABARI TOKENI NJE NA MILANGO YA UKUMBI IFUNGWE," mwisho wa kunukuhu.

Rekodi zinaonesha kuwa, hii siyo mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kufanya vitendo hivyo, ambapo mara ya kwanza aliwatolea maneno ya kudhalilisha viongozi wa SMPC, ambao ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wetu.

Kutokana na hali hiyo, Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) kwanza inatangaza kulaani kitendo cha udhalilishaji kilichofanywa na DC Simalenga kwa waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu.

Pili, Uongozi wa SMPC na waandishi wake inatangaza rasmi kuanzia leo 20 Februari,2024,hautafanyakazi na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Peter Simalenga.

Tatu, tunaiomba Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoa tamko juu ya tukio hilo.

Hivyo basi, tunawaomba viongozi mbalimbali na wananchi ndani ya Mkoa wa Simiyu, kuwaheshimu waandishi wa habari pale wanapotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, na kuepuka kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji, ubaguzi, udhalilishaji na ukikwaji wa sheria.

Imetolewa na Uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC).

20 FEBRUARI,2024.
Waongo hao, usiwaamini waandishi wa habari wa Tanzania ni waongo njaa zao zinawaponza, walimsaliti mwandishi mwenzao marehemu Mwangoka alipouawa, wakawa upande wa wauaji! Walishindwa hata kukemea na kupaza sauti zao wakiogopa kuzikosa bahasha za khaki.
 
Kama Simalenga amefanya hayo basi atakuwa amesahau mapema kwamba na yeye ni zao la Vyombo vya habari.

Kabla hajateuliwa Kwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya alikuwa ni Mtumishi kutoka Clouds Media Group

Ni busara ajitokeze kuomba radhi Wanahabari wenzake
 
Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) imesikitishwa na kuuzunishwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani humo, Simon Simalenga cha kuwafukuza kwa dhihaka kwenye kikao cha Ushauri cha Wilaya (District Consultative Council -DCC), waandishi wa habari saba wa vyombo mbalimbali vya habari waliokwenda kuchukuwa taarifa kwenye kikao hicho, kilichofanyika Februari 19,2024, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.​
Simalenga, Chalamila - wote Wanyalukolo toka Iringa.

Labda walikulia kwenye nyumba ambayo wazazi walikuwa wakiuza ulanzi, wakaanza kunywa wakiwa wadogo, na leo ndio tunaona matokeo!

Ugimbi unaharibu sana akili ya watoto.
 
Daaaaah huyu jamaa hua ana shida gani kwani?! Ana matukio tatanishi sana na hua yanaisha kimya kimya watu wakidhani anaonewa, ipo siku wanaomtetea nao watachoka sasa. Sema siwezi kushangaa sana maana kipindi yuko kaole kama Muigizaji yeye na mwenzake Mtunisi walikua na kauli za dharau sana enzi hizo akijulikana kama Dimera. Alikua anapenda kucheza position za Boss yuko Ofsini na kauli zake always zilikua za dharau sana kwa clients na watu wa chini yake japo yale yalikua maigizo tu. Hiki kinachoendelea kwake sasa hivi ni reflection tu ya jinsi alivyo
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Tamko,
Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) imesikitishwa na kuuzunishwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani humo, Simon Simalenga cha kuwafukuza kwa dhihaka kwenye kikao cha Ushauri cha Wilaya (District Consultative Council -DCC), waandishi wa habari saba wa vyombo mbalimbali vya habari waliokwenda kuchukuwa taarifa kwenye kikao hicho, kilichofanyika Februari 19,2024, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Waandishi hao wa habari ambao wamefikisha taarifa rasmi kwa uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari simiyu (Simiyu Press Club) kulalamikia kitendo hicho, wamesema kitendo alichofanya mkuu huyo wa wilaya si tu kimewafedhehesha waandishi wa habari pamoja na tasnia ya habari, bali kinakiuka Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayohimiza uhuru wa mtu kutoa na kupata taarifa.

Halikadhalika, kitendo hicho kilichofanywa na Mkuu Wilaya Bw. Simalenga kuwafukuza waandishi wa habari tena kwa lugha isiyokuwa na staha, kinakinzana na sheria ya haki ya kupata taarifa ya mwaka 2016.

DC Simalenga alinukuliwa akisema: “MMEKUJA KUFANYA NINI HAPA, NILIWAAMBIA MSIALIKE WAANDISHI WA HABARI, NANI ALIALIKA TENA? WAANDISHI WA HABARI TOKENI NJE NA MILANGO YA UKUMBI IFUNGWE," mwisho wa kunukuhu.

Rekodi zinaonesha kuwa, hii siyo mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kufanya vitendo hivyo, ambapo mara ya kwanza aliwatolea maneno ya kudhalilisha viongozi wa SMPC, ambao ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wetu.

Kutokana na hali hiyo, Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) kwanza inatangaza kulaani kitendo cha udhalilishaji kilichofanywa na DC Simalenga kwa waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu.

Pili, Uongozi wa SMPC na waandishi wake inatangaza rasmi kuanzia leo 20 Februari,2024,hautafanyakazi na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Peter Simalenga.

Tatu, tunaiomba Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoa tamko juu ya tukio hilo.

Hivyo basi, tunawaomba viongozi mbalimbali na wananchi ndani ya Mkoa wa Simiyu, kuwaheshimu waandishi wa habari pale wanapotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, na kuepuka kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji, ubaguzi, udhalilishaji na ukikwaji wa sheria.

Imetolewa na Uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC).

20 FEBRUARI,2024.
Halafu na wewe mwandishi wa habari unaandikaje "Kuuzunishwa?"
 
Daaaaah huyu jamaa hua ana shida gani kwani?! Ana matukio tatanishi sana na hua yanaisha kimya kimya watu wakidhani anaonewa, ipo siku wanaomtetea nao watachoka sasa. Sema siwezi kushangaa sana maana kipindi yuko kaole kama Muigizaji yeye na mwenzake Mtunisi walikua na kauli za dharau sana enzi hizo akijulikana kama Dimera. Alikua anapenda kucheza position za Boss yuko Ofsini na kauli zake always zilikua za dharau sana kwa clients na watu wa chini yake japo yale yalikua maigizo tu. Hiki kinachoendelea kwake sasa hivi ni reflection tu ya jinsi alivyo
Tangu lini msanii akaacha usanii? Nafasi ya ukuu wa wilaya imeshushwa sana hadhi na haya mapopoma ya CCM
 
Hako kajamaa kipindi kalipokuwa Songwe kuna shughuli fulani iliwahi kutukutanisha sasa wakati wa chakula eti analeta uboss anamtuma demu wangu akampakulie chakula kisa demu wangu yupo naye ofisi moja , kwa mara ya kwanza niliona ni jinsi gani unaweza kuuwa bila kukusudia , nilimkanya demu mbele ya wajumbe na mbele yake kuwa sitaki huo upumbavu alafu nikamkata jicho moja kali bwana Simalenga , akatizama chini .
Ila akaikumbuka hii sura maana kabla hajawa mkuu wa wilaya akiwa Clouds aliwahi kuja ofisi mojawapo akanikuta nilimzingua kinyama maana alikuja kuleta ushubwada tu .
 
Back
Top Bottom