Elections 2010 Utafiti: CHADEMA 74% Igunga, kama uchaguzi ungefanyika leo

Huku Igunga CCM haina chao,wamechanganyikiwa thus why hata mitume kumi na wawili 12 wameshindwa kwenda.
 
WANAZUONI wa Kiislamu nchini wameipa siku tatu Chadema Taifa kulaani kitendo cha wafuasi na viongozi wake kulidhalilisha vazi tukufu la hijab na kumwomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, kwa kumvua sitara yake.

Wamesema iwapo chama hicho kitapuuza kufanya hivyo na kupita muda huo wanazuoni hao na Waislamu wataiona Chadema kama chama chenye sera na madhumuni ya kuhujumu Uislamu na Waislamu wa Tanzania na kuhimiza Waislamu kukiepuka kama ukoma.

Kauli hiyo iko kwenye tamko la Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (HAY-AT) lililosomwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Umoja huo, Shehe Sherali Hussein Sherali na kusema siku tatu hizo zilianza jana.

Wanazuoni hao zaidi ya 10 wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Shehe Suleimani Kilemile, walitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari na kusema baada ya hapo umoja huo utakaa na kutafakari hatua stahiki za kukabiliana na dharau hizo na kuelekeza Waislamu cha kufanya.

Sherali alisema ifahamike, kwamba shambulio lolote dhidi ya hijab ni dhidi ya Uislamu na Waislamu wote, haliwezi kuvumilika na watakabiliana na yeyote anayetaka kuidhalilisha amri ya hijab iliyo katika Quran sura ya 33:59.

"Tunataka ifahamike, kwamba yeyote atakayelidharau vazi la hijab kwa kauli au vitendo, atakuwa amewachokoza Waislamu na sisi kamwe hatukubali hilo liendelee na kukaa kimya, tutachukua hatua stahiki na ikibidi tutalazimika kuondoa munkari kwa mikono yetu wenyewe, kama dini yetu inavyotuelekeza," alisema.

Aliongeza kuwa wanalaani na kupinga kitendo kilichofanywa na wanaodaiwa kuwa wafuasi na viongozi wa Chadema kumvua nguo Mkuu huyo wa Wilaya na kumwacha bila sitara.

Alisema Kimario ni Mwislamu anayefuata mafundisho ya Uislamu yanayomtaka kila
mwanamke ajisitiri kwa vazi la hijab, hivyo kumvua ni kumdhalilisha kwa wanajamii kama mwanamke wa Kiislamu, mama mwenye watoto na kiongozi wa Serikali.

Tumetafakari tukio hili kwa undani na tunalichukulia kama shambulio la wazi na la makusudi dhidi ya mafundisho yetu na dini ya Kiislamu, yanayomtaka kila mwanamke aliyevunja ungo, kujisitiri kwa kuvaa vazi la hijab," alisema Sherali.

Aliwaomba Watanzania wote, wanaharakati wa asasi za kijamii na wa haki za binadamu, viongozi wa vyama vya siasa na wa dini zote, kulaani na kupinga unyanyasaji huo wa kijinsia na kidini unaokwenda kinyume na Katiba ya nchi na utamaduni wa Watanzania wa kuheshimiana.

"Tumesikitishwa na ukimya wa asasi za kijamii zinazodai kutetea haki za binadamu na za wanawake, kutolaani kitendo hiki cha mwenzao kudhalilishwa kijinsia, kuendelea kukaa kimya kunatulazimisha kuwaona wanafiki na ndumilakuwili juu ya madai yao ya kutetea wanawake," alisisitiza.

Alisema wanaitaka Serikali ilitafakari kwa kina tukio hili la kudhalilishwa mwanamke Mwislamu, akilitumikia Taifa kama mmoja wa viongozi wake, kukaa kimya kutatoa tafsiri hasi juu ya jinsi inavyolichukulia tukio hilo na kuitaka kuwachukulia hatua kali wahusika.

Wanawake Waislamu Katika hatua nyingine, kikao cha wanawake Waislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee Jumapili, wanawake walilaani tukio hilo.

Kikao hicho chini ya Mwenyekiti wake Fatma Juma, kiliwataka wanawake na wapenda amani wote kulaani kitendo hicho cha udhalilishaji wanawake.

Walisema kitendo hicho kimeonesha dharau, si tu kwa Uislamu, bali hata kwa madhehebu mengine na kinaweza kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini hivi sasa.

Tamko la kikao hicho, lilisema litaanza kusambazwa katika misikiti yote Ijumaa, ili Waislamu waelewe namna walivyoguswa na kusononeshwa na tukio hilo.

Shura ya Maimamu
Habari zaidi zilizopatikana zilisema Shura ya Maimamu nayo itakutana hivi karibuni kujadili tukio hilo la mwanamke wa Kiislamu kuvuliwa hijab.

Mbali ya kukutana huko, Shura hiyo itaandaa maandamano ya kupinga kitendo hicho ambacho wamekitafsiri kuwa ni matusi dhidi ya Uislamu.

Katibu wa Shura ya Maimam, Shehe Ponda Issa Ponda, jana alithibitisha kuwapo kwa ajenda hiyo.

Akizungumza na gazeti hili jana alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa Chadema kimekosa utu, ustaarabu, uungwana na maadili mema na kinapaswa kukemewa na wapenda amani wote nchini, bila kujali itikadi zao, kwani kikiachwa kitazidi kukomaa na kuonekana ni
jambo la kawaida katika jamii.

Akizungumzia kadhia hiyo, Katibu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini (Baraza Kuu), Shehe Ramadhan Sanze, naye alisema taasisi yake inaungana na wanaolaani tukio hilo .
Masaburi feki ya kichina yakiwa kazinii!
 
Tatizo kubwa ni kwamba kura zilishapigwa na zipo tayari kwenye maboksi zikisubiri siku ya kuhesabiwa. Ulinzi mkali sana unahitajika, vinginevyo wizi ni ule ule tu.
 
Mchaga bana..
Kila saa unawaza kuibiwa!
 
jamani tuache ushabik na tufuate uhalisia tusije pata viongozi wa magazetin na kwenye mitandao
sama hani kama nitakuwa nime harm mind ya mtu lakn hatahivyo uhalisia si ndo unapreveil ? thenks kama utafiti ulifanyika kweli na kwa makini kwa kuzingatia mfumo au kanuni za kiutafiti. ASANTE!
 
WANAZUONI wa Kiislamu nchini Tanzania (HAY-AT)........ lililosomwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Umoja huo, Shehe Sherali Hussein Sherali na kusema siku tatu hizo zilianza jana.
Chama kinaitwa HAYATI hahahahaaaa, angalau wangekiita MAREHEMU.
 
Mimi najua watu tupo online kujua yanayojiri..Chadema hatudanganyani..Ahsante kwa utafiti huu ambao unawapa pressure wana Magamba..Wanaopinga ni wanatumia Masaburi yao bila kujua watendalo..Peoplessss....Powerrrr...
 
kama unabisha mioe leo nimeenda kwenye mikutano miwili kwanza ccm na ili chadema, ukweli ccm itaangukia pua tena vibaya sana . Nadhani mie nilivyoona leo mjini ccm 30 % chadema 59%
 
Leopold Mahona (CUF) ....................................................................................................................4% (37 votes)

Joseph Kashindye (CHADEMA).......................................................................................................88% (758 votes)

Peter Kafumu (CCM).......................................................................................................................6% (50 votes)

Said Makeni (DP)...............................................................................................................................................1% (7 votes)

Lazaro Ndageya (UMD)..............................................................................................................0% (2 votes

John Maguma (SAU).........................................................................................................................1% (7 votes)

Total votes: 861

source:Mwanahalisi
 
Magazeti yenyewe TANZANIA DAIMA LA MBOWE, NA MWANA HALISI ANTHONY KOMU
CHADEMA-subirini matokeo ndio mtajua kama chadema wanaigunga hawaitaki kuwamwagia tindikali muwamwagie na kura wawape?
Aliyetumwagia tindikali inaonekana unawafaham. Csi ndo wanaigunga na CDM tunaichagua utake usitake.
Kama na wewe una magamba njoo Igunga tukuvue.
 
WANAZUONI wa Kiislamu nchini wameipa siku tatu Chadema Taifa kulaani kitendo cha wafuasi na viongozi wake kulidhalilisha vazi tukufu la hijab na kumwomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, kwa kumvua sitara yake.

Wamesema iwapo chama hicho kitapuuza kufanya hivyo na kupita muda huo wanazuoni hao na Waislamu wataiona Chadema kama chama chenye sera na madhumuni ya kuhujumu Uislamu na Waislamu wa Tanzania na kuhimiza Waislamu kukiepuka kama ukoma.

Kauli hiyo iko kwenye tamko la Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (HAY-AT) lililosomwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Umoja huo, Shehe Sherali Hussein Sherali na kusema siku tatu hizo zilianza jana.

Wanazuoni hao zaidi ya 10 wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Shehe Suleimani Kilemile, walitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari na kusema baada ya hapo umoja huo utakaa na kutafakari hatua stahiki za kukabiliana na dharau hizo na kuelekeza Waislamu cha kufanya.

Sherali alisema ifahamike, kwamba shambulio lolote dhidi ya hijab ni dhidi ya Uislamu na Waislamu wote, haliwezi kuvumilika na watakabiliana na yeyote anayetaka kuidhalilisha amri ya hijab iliyo katika Quran sura ya 33:59.

“Tunataka ifahamike, kwamba yeyote atakayelidharau vazi la hijab kwa kauli au vitendo, atakuwa amewachokoza Waislamu na sisi kamwe hatukubali hilo liendelee na kukaa kimya, tutachukua hatua stahiki na ikibidi tutalazimika kuondoa munkari kwa mikono yetu wenyewe, kama dini yetu inavyotuelekeza,” alisema.

Aliongeza kuwa wanalaani na kupinga kitendo kilichofanywa na wanaodaiwa kuwa wafuasi na viongozi wa Chadema kumvua nguo Mkuu huyo wa Wilaya na kumwacha bila sitara.

Alisema Kimario ni Mwislamu anayefuata mafundisho ya Uislamu yanayomtaka kila
mwanamke ajisitiri kwa vazi la hijab, hivyo kumvua ni kumdhalilisha kwa wanajamii kama mwanamke wa Kiislamu, mama mwenye watoto na kiongozi wa Serikali.

Tumetafakari tukio hili kwa undani na tunalichukulia kama shambulio la wazi na la makusudi dhidi ya mafundisho yetu na dini ya Kiislamu, yanayomtaka kila mwanamke aliyevunja ungo, kujisitiri kwa kuvaa vazi la hijab,” alisema Sherali.

Aliwaomba Watanzania wote, wanaharakati wa asasi za kijamii na wa haki za binadamu, viongozi wa vyama vya siasa na wa dini zote, kulaani na kupinga unyanyasaji huo wa kijinsia na kidini unaokwenda kinyume na Katiba ya nchi na utamaduni wa Watanzania wa kuheshimiana.

“Tumesikitishwa na ukimya wa asasi za kijamii zinazodai kutetea haki za binadamu na za wanawake, kutolaani kitendo hiki cha mwenzao kudhalilishwa kijinsia, kuendelea kukaa kimya kunatulazimisha kuwaona wanafiki na ndumilakuwili juu ya madai yao ya kutetea wanawake,” alisisitiza.

Alisema wanaitaka Serikali ilitafakari kwa kina tukio hili la kudhalilishwa mwanamke Mwislamu, akilitumikia Taifa kama mmoja wa viongozi wake, kukaa kimya kutatoa tafsiri hasi juu ya jinsi inavyolichukulia tukio hilo na kuitaka kuwachukulia hatua kali wahusika.

Wanawake Waislamu Katika hatua nyingine, kikao cha wanawake Waislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee Jumapili, wanawake walilaani tukio hilo.

Kikao hicho chini ya Mwenyekiti wake Fatma Juma, kiliwataka wanawake na wapenda amani wote kulaani kitendo hicho cha udhalilishaji wanawake.

Walisema kitendo hicho kimeonesha dharau, si tu kwa Uislamu, bali hata kwa madhehebu mengine na kinaweza kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini hivi sasa.

Tamko la kikao hicho, lilisema litaanza kusambazwa katika misikiti yote Ijumaa, ili Waislamu waelewe namna walivyoguswa na kusononeshwa na tukio hilo.

Shura ya Maimamu
Habari zaidi zilizopatikana zilisema Shura ya Maimamu nayo itakutana hivi karibuni kujadili tukio hilo la mwanamke wa Kiislamu kuvuliwa hijab.

Mbali ya kukutana huko, Shura hiyo itaandaa maandamano ya kupinga kitendo hicho ambacho wamekitafsiri kuwa ni matusi dhidi ya Uislamu.

Katibu wa Shura ya Maimam, Shehe Ponda Issa Ponda, jana alithibitisha kuwapo kwa ajenda hiyo.

Akizungumza na gazeti hili jana alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa Chadema kimekosa utu, ustaarabu, uungwana na maadili mema na kinapaswa kukemewa na wapenda amani wote nchini, bila kujali itikadi zao, kwani kikiachwa kitazidi kukomaa na kuonekana ni
jambo la kawaida katika jamii.

Akizungumzia kadhia hiyo, Katibu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini (Baraza Kuu), Shehe Ramadhan Sanze, naye alisema taasisi yake inaungana na wanaolaani tukio hilo .
unajaribu kuhamisha watu kwenye mada,pili inaonyesha upunguani kwa hao mashehe ubwbwa,yaani sasa wanataka kuandamana kwa ajili ya hijabu na wala si mahakama ya kadhi,mtatumiwa sana na ccm kama ifanyavyo condom baada ya mechi hutupwa,kama ilivyokua kadhi baada ya kura mkachenjiwa,waislam elimikeni kama wakristo huwezi kuta huu upuuz
 
Na hapo bado CHADEMA hawajafungua gala lake. Tunasubiria kwa shauku kubwa kusikia Cdm wameshusha 'CONVOY' yake iliyosheheni silaha za maangamizi. I mean kina Wenje, Kiwia, Selasini, Mnyika, Mdee, Lema, Sugu, Silinde, Nyerere, na makamanda wengine. Hakika Igunga hapatatosha. Magamba lazima watawehuka.

Jana nilikutana na Kamanda ZITTO maeneo ya Ubungo Plaza nafikiri alikuwa akihudhuria vikao fulani pale maana kulikuwa na magari ya mabalozi kadhaa pale nje. Nikamuuliza vipi kamanda upo hapa mida hii wakati Uwanja wa mapambano IGUNGA hujasikika??? Akaniambia kuwa yeye anatakiwa kuwa IGUNGA wiki ya mwisho ya kampeni ili kumalizia kila kitu. Nikamwambia akusanye silaha zote nzito nzito kwenda kumaliza kazi. Hivyo wananchi wa IGUNGA wajiandae ngoma ndio kwanza haijakolea!!!!!!!!!
 
CHADEMA waende kule ambako kuna udhaifu fulani ili kuimarisha zaidi na kukaaa huko Kijijini na kuona tunakuwa washindi na Mungu atasaidia kabisa katika hili
 
Jana nilikutana na Kamanda ZITTO maeneo ya Ubungo Plaza nafikiri alikuwa akihudhuria vikao fulani pale maana kulikuwa na magari ya mabalozi kadhaa pale nje. Nikamuuliza vipi kamanda upo hapa mida hii wakati Uwanja wa mapambano IGUNGA hujasikika??? Akaniambia kuwa yeye anatakiwa kuwa IGUNGA wiki ya mwisho ya kampeni ili kumalizia kila kitu. Nikamwambia akusanye silaha zote nzito nzito kwenda kumaliza kazi. Hivyo wananchi wa IGUNGA wajiandae ngoma ndio kwanza haijakolea!!!!!!!!!

ha ha ha ha haaa, amekudanganya sana, Zitto hawezi kukanyaga Igunga hata kwa bunduki
 
Back
Top Bottom