Gwalihenzi
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 5,125
- 1,300
Akili yako mbovu kweli kweli, kwani ulifanya juhudi gani kuwa mzanzibar? au wazazi walifanya juhudi gani kukuzaa wewe wakiwa huko zanzibar?Kwa sasa Wazanzibari hawaangalii kufa kwa CUF wala CCM zaidi wanajikita katika kuisimika Jamuhuri ya watu wa Zanzibar iliyo huru kabisa! Mutake musitake kuingia kwa CUF ndani ya Serikali hapa Zanzibar mambo yamekua tofauti kwa mustakabali wa Zanzibar, Wazanzibari na Uzanzibari! Sio siri Raia wengi wamepatwa na hamu na shauku kubwa hususan katika kutaka kuikomboa Zanzibar iliyo huru! Nyinyi leteni majungu yenu munavyopenda ila ipo siku historia itakuja kuwasuta. Leo saa 10 jioni tunawaalika muhudhurie Lumumba muje mushuhudie jinsi Wazanzibari walivyokua wamoja kwa sasa, tofauti na Tawala zote zilizopita. Zanzibar Daima Mbele. Am proud to be Zanzibari! Watanganyika mwaka huu imekula kwenu, kilichobaki kwenu ni kupika majungu tu dhidi ya Wazanzibari. Nchi kwanza mambo mengine baadae. Vyama vinakuja na kuondoka lakini Zanzibar ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo!