mi nahisi anamuandaa RIZ1
sasa nani aliyekwambia 2015 ccm itafanya free and fair elections. africa nchi zenye free and fair elections ni ghana, botswana na zambia.2015 Pakiwa na free and fair election kwa mara ya kwanza RAIS Tz atatoka chama cha upinzani! nimutazamo tu.
Waitara,Sikuwahi kujua kuwa nawe huwa una mawazo ya kihafidhina. Pole WildCard. Kuundoa utawala mbovu kama wa CCM hauhitaji katiba mpya. Hata kwa katiba iliyopo CCM wanaweza kuondoka. Hivyo vyombo vya dola unavyovizungumzia ni vipi? Watawala waliondolewa sehemu zingine haikuhitaji katiba mpya. Inahitajika mikakati endelevu, sera imara na mbadala, kukubalika kwa watu, basi. The rest will have to follow...si suala la kumsubiri Said Mwema au wenzake...
kaka nipo na wewe bega kwa bega lakini je hiyo katiba itapatikana?na isipopatikana unahisi nini kitatokea,kwa sababu watanzania ni waoga lakini sio kama zamani huoni dalili za nchi kuvurugika ziko wazi sana.nasema hivi kwa sababu hakuna nchi ambayo wananchi wake walizaliwa wanapenda fujo ila udhalimu ndio ulisababisha.usishangae siku moja tz ikalipuka niamini aka dalili zinaonekana wazi.sio kwa upinzani tu kuichafua nchi hata chama tawala peke yake mwenendo wake ni wa kuichafua nchi hatupo salama sisi kama taifa.historia ni mama wa yote.siku njema.Waitara,
Kwa namna vyombo vya DOLA vilivyo hakuna namna upinzani utatangazwa kuwa umeshinda hata kama utakuwa umeshinda kweli. Chukua mfano mdogo tu wa uchaguzi wa Urais wa Zanzibar. Kule CCM haijashinda tangu mwaka 1995 na haitashinda hata kwa chaguzi nyingine tano zijazo. Tunataka KATIBA MPYA itusaidie kunyoosha baadhi ya mambo yafuatayo:-
-Ituwekee taasisi zenye nguvu na huru kabisa katika UTENDAJI na MAAMUZI yake kama vile TUME YA UCHAGUZI;
-Iweke wazi mgawanyo wa madaraka wa MIHIMILI mitatu ya DOLA;
-Iweke mifumo mizuri ya kuwapata wagombea kuanzia ndani ya vyama;
Kimsingi chaguzi tulizofanya tangu mwaka 1995 ni maigizo tu. Uhalisia wa kuchaguana haupo. Kwa kuwa wewe umeamua kujiajiri kwenye SIASA unajua taabu mnayoipata hata kuupata UDIWANI tu kwa mfumo katili wa sasa.
Busara iliyotumika kuamua tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi itatumika pia kutupatia KATIBA MPYA kama ile ya jirani zetu KENYA. Hili hata Kikwete mwenyewe litamjengea heshima ya aina yake baada ya kuvurunda sana kwenye URAIS wenyewe.kaka nipo na wewe bega kwa bega lakini je hiyo katiba itapatikana?na isipopatikana unahisi nini kitatokea,kwa sababu watanzania ni waoga lakini sio kama zamani huoni dalili za nchi kuvurugika ziko wazi sana.nasema hivi kwa sababu hakuna nchi ambayo wananchi wake walizaliwa wanapenda fujo ila udhalimu ndio ulisababisha.usishangae siku moja tz ikalipuka niamini aka dalili zinaonekana wazi.sio kwa upinzani tu kuichafua nchi hata chama tawala peke yake mwenendo wake ni wa kuichafua nchi hatupo salama sisi kama taifa.historia ni mama wa yote.siku njema.
hatuwezi kuacha kumchagua mtu kwa sababu eti ndugu yake ni kiongozi wa ngazi ya juu ili mradi tu anasifa za kuchaguliwa. Kuwa mke wa rais ama mtoto wa rais siyo kikwazo, lakini isizidi kama ambavyo cdm wamezoea.