'Usisome Hapa'

Oct 22, 2010
78
0
Linapokuja suala la kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo (ama hata mambo mengine yenye matokeo hasi kwa watoto) wazazi wengi huwa hawawi wazi kwa watoto wao kiasi cha kutosha kuwaonesha wazi wazi madhara ya kujihusisha na ngono katika umri mdogo. Wanasema tu, 'usifanye hivi, usifanye vile' nk. Watoto wengi, kwa udadisi wa kutaka kujua ubaya ama uzuri wa kufanya ama kutofanya walichokatazwa kufanya na wazazi wao wameishia kuharikiwa na kupoteza ndoto za muda mrefu za maisha yao lakini yote ni sababu wazazi hawakuwa wazi kiasi cha kutosha kuwapa msimamo thabiti katika kujenga maisha yao. Mara nyingi watoto hufanya kile walichokatazwa kufanya iwapo sababu za kufanya ama kuto fanya hazikuwekwa wazi. Tujitahidi sana kutoa sababu za msingi tunapokataza watoto kufanya kitu fulani chenye matokeo hasi ili kuwaepusha na matatizo yanayoweza kuwapata pindi wanapoamua kujitafutia sababu za kwa nini wafanye ama wasifanye walichoambiwa wasifanye. Tena tufanye hivyo at the right time! Waharifu wa kwanza wa mtoto ni wazazi! Unadhani kuna sababu ya msingi kuwaficha watoto ukweli wa mambo kwa dunia ya leo? Kumbuka, asiyefunzwa na mamaye, ulimwengu utamfunza!
 
Sasa kama unataka tusisome umeandika ya nini?Haya mie huyo natoka bila kusoma maana nafuata masharti ya mganga!
 
Uliandika heading baada ya kunywa piwa nini?

Piwa means Gongo, si ajabu aliipata hii kabla ya kuchagua heading. Halafu wakati anaandika ujumbe wenyewe gongo ikwa imeshaisha kichwani. Nami napita tu kwa mujibu wa heading.
 
Mimi nimepitiliza mpaka hapa kwenye nafasi hii na nimeamua kukuomba utubadilishie hako kaneno USISOME HAPA!Ili tuweze kusoama kwa amani na kuchangia,pia ingefaa zaidi utueleze kwa kwa namna gani ulifikiria kutuambia tusisome wakati umeandika maelezo ambayo yanatakiwa yasomwe.
 
PJ Mbavu zangu pls!au alidamkia valuu maana nayo haitaki mchezo na juu hili!!

I'm so sorry, I have tried to change 'edit' but without much success. Hata hivyo, kama great thinkers nilitegemea mtaelewa point yangu ni ipi. Once again I'm sorry.
 
Msiogope 'great thinkers' maana yangu ilikuwa simple tu. Mara nyingi unapomzuia mtu kufanya kitu na kama hukumpa maelezo ya kutosha kwa nini atii onyo lako basi kutokana na udadisi lazima atafanya ili tu kujiridhisha mwenyewe ubaya ama uzuri wa kutii ama kutotii. Ni kweli nimeandika usisome, wapo baadhi wamesoma siwalaumu kwa sababu sikutoa sababu ya kwa nini wasisome. Nilitaka tujifunze kutoka makosa tunayofanya kwa kuto kutoa maelezo ya kutosha. Nashukuru kwa Great, great Thinkers wachache walionielewa. Hongereni sana.
 
Back
Top Bottom